Mkuu weeee acha tu mambo ya ndoa haya na siasa mmmmmhh shemeji yenu nadhani yupo na akina Makamba ile sura ya Muungwana ilimchanganya, ana matenge na vilemba vya CCM ila huwa havai nadhani alipewa kwenye kampeni za 2005.....nadhani amegundua nadharia ya KASI MPYA, NGUVU MPYA NA ARI MPYA ni utopia....
Usiendelee kuwa Kichwangumu, results ndivyo zilivyo.Zimethibitika.
Wasu,Hongera sana Chadema.Mimi sijasema lolote
Update: Kwa taarifa za kuaminika nilizozipata, Chadema wamefanya vizuri sana kwenye Kata ya Kemambo yenye vijiji: Nyangoto, kewanja, matongo, mrito na Kerende. Pia na Tarime mjini. Kwenye kata ya Kemambo, kwa mfano, Chadema wame-sweep kwa average ya 90%+. Nitazidi kuwapatia updates.
Kaka
kama unataka kutuharibia siku ulegeee. tumeshasahu huku tunasherehekea tu
Mkuu, niwaharibie nin tena? Mimi natoa updates tu, maana kuna watu walikuwa wanauliza % kwa kila kata.
Ama kweli maajabu ya Mussa haya!..
Nitawapongeza sana viongozi wa Chadema kwa kazi ngumu waliyoifanya kuhakikihsa ushindi umepatikana... Hongera..
Pia sina budi kumshukuru Kikwete na Utawala wake (ktk swala hili moja) kuchukua hatua moja mbele ktk kuhakikisha demokrasia inakomaa Tanzania kwani binafsi nilikuwa nasubiri habari za mauaji yatakayo fuata baada ya CCM kutangaza ushindi.
Itanichukua muda mrefu kuweza kumeza funda hili maanake domo langu wazi mwaaaaaa!
Hongereni sana CHADEMA!pongezi kwa wana tarime!
Mwanakijiji,
Ndio maana nimesema kuwa watu wanaanza kutambua polepole kuwa CCM ni kapu ambalo limefumka kwenye makalio yake. I believe this is a harbinger of things to come.
Mkidhania kuwa Chadema imeshinda Tarime kwa sababu ya kazi ngumu iliyofanywa na viongozi wake itakuwa mnamiss point nzima ya ushindi wa Tarime. Kilichofanywa na viongozi ni wazi kina nafasi kubwa na isiyoweza kuondolewa, lakini ushindi wa Chadema Tarime ulitokana na watu kuikataa CCM zaidi kuliko kuikubali Chadema zaidi.
Wana Tarime walikuwa na kila sababu ya kuikimbia Chadema na kuikana (kama ukizingatia habari na porojo zilizokuwa zimetengenezwa kwa muda). Kama wana Tarime wangesikiliza maneno ya "nani alimuua Wangwe" ni wazi kuwa wangeikimbia Chadema. Kama yale ya Mbowe nusura kupigwa kule Tarime wakati wa msiba yangekuwa ni ya kuaminika watu wangeona kweli Tarime wamechukizwa na Chadema. Ukizingatia mgongano wa maneno kati ya marehemu Wangwe na Mbowe na pia uongozi mzima wa Chadema ni wazi kuwa Tarime walikuwa na kila sababu ya kutoichagua Chadema na kuijaribu tena CCM. Hawakufanya hivyo. Why?