Gustanz_The, Mkuu naona bado kabisa hujatumia hekima ktk kuwasilisha hoja yako kwani hapa unachojaribu kujenga ni tofauti ya Tarime na Zanzibar..Kifupi mimi sioni tofauti kabisa kwani matumizi ya hili neno yanaweza kuwa na mapana sawa kabisa na madai ya Zanzibar.
Nijuavyo mimi Zanzibar wanachofanya ni kudai -The ability to govern herself (Zanzibar) hii habari ya kudai NCHI itakuwa haina maana kama swala la sovereign as a Country halipo ili wapate kujitawala wao. Sasa ktk confusion ya hiyo self governing ndipo wanapokuja na visa kuwa PM hana madaraka Visiwani..Hivyo usidanganywe na kichwa cha habari ambacho sisi hapa tunakitungia tunzi za kufikiria tu kuwa hao viongozi wana uroho ama tamaa ya madaraka lakini ukweli bado hawa jamaa wana seek Zanzibar self identity and concerption of rights ambayo mimi naona zina fall under autonomy...
Mkuu hapa nitatafautiana na wewe kidogo. Natambua kuwa unaamini kabisa unachokizungumza hapa, ila I think unachanganya matumizi ya haya maneno mawili [autonomous & secession]. Penginepo tu niyatofautishe kwa ufupi ili tunapoendelea huko mbele, ufahamu bayana ni kipi Tarime wanachodai.
First, an autonomous region/county/community is a region/county/community with
special powers of self-rule. Emphasis zaidi kwenye neno 'special power' coz
Autonomy is not
independence. Chukulia kwa mfano People's Republic of China. China ina autonomous regions kibao kiasi kwamba kuna hadi counties ambazo zina 'special power'/uwezo wa kutunga sheria na ku-run mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na central government ya Beijing. Lakini haimanishi kuwa hizo regions/counties haziitambui serikali ya Beijing kuwa ndiyo yenye absolute power inapokuja kwenye masuala makubwa kama vile masuala ya kijeshi, foreign policy, etc...
While
secession is simply the withdrawal of a State from the national Union. Hiki ndicho wazinzibar wanachokidai.
..lakini bob ikiwa Tanzania nzima hali ndio hiyo na kama nilivyosema hapo awali madai ya Tarime sio sehemu ya indiginous ambao pengine kutokana na utawala huu wametengwa na kunyanyaswa tofauti na wakazi wa Chalinze, Kinyerezi au Monduli ambao wanachanua unafikira huyo JK ama Pinda ataweza kuyaona vipi?..madai yenu yanahusiana na wazungu wawekeshaji (wageni) na upana wa madai kama yenu hayakuanza wala kukomea Tarime..Isipokuwa hali halisi ya yale yaliyotangulia kama Bulyanhulu, Tarime na kkwingineko kote yanaweza kujenga hoja nzito zaidi na kwamba sasa hivi wananchi wamechoka!
Penginepo labda umesoma original thread kwa haraka, and/or hukuwa na muda wa kutosha ku-digest kile ambacho TCAG (Tarime Citizens Action Group) wanachokidaicoz ukisoma original thread vizuri, hakuna sehemu inayozungumzia issue ya indiginous kama kigezo cha wao kudai "autonomous status." Ila naelewa point yako hapa ni nini mkuu: I think wewe umechukulia autonomus communities mathalani za sehemu kama Spain ambazo typically zinahuisha minority group(s) ambazo ni tofauti na majority group(s) uka-conclude kwamba autonomous regions/communities zote zinaangukia kwenye kundi hilo la indiginous peke yake [which is not true].
Mkuu, Pamoja na dharau zako za makabila mengine lakini kummbuka tu huwezi kuweka chandarua kuzuia mbu wakati kumekwisha kucha! Usiku mzima umekung'ata leo waja shtuka jua la adhuhuri! hao wazungu toka wameingia na kuwekesha tena wamepewa ardhi hiyo hadi siku madini yatakapo kwisha...Mlikuwa wapi siku zote hali mlisoma yaliyowakuta Bulyanhulu!
Mkuu, inaelekea hujui kabisa historia ya wakazi wa Tarime vs upingaji wa makampuni ya kigeni!! Hawa jamaa (watarime) wamekuwa wakipinga hizo kampuni za uchimbaji wa madini tangu kipindi cha mkoloni. Usidhani kwamba Barick ndio watu wa kwanza kutia mguu Tarime. Kuna makampuni mengi sana yamejaribu siku za nyuma nakushindwa vibaya mno kutokana na fierce resistence waliyoipata toka kwa local citizens. Hata hao Barick (kipindi hicho bado ikiitwa East Africa Gold Mine) waliwahi ku-face the same resistance mpaka pale walipowaweka sawa RC, DC, RPC, na viongozi wengine wakubwa wa ngazi za juu [mkoa/kitaifa ] ambao baada ya kunyweshwa Safari lager, ghafla wakaanza kutumia deadly force ili kuhakikisha kuwa mzungu anachimba dhahabu ya Tarime apendavyo whether watarime watake ama wasitake. Mathalani, itakumbukwa kuwa mwaka 94/95 (kama sikosei) kulikuwa na uprise ya nguvu huko Nyamongo, Tarime kiasi kwambwa FFU ndio waliokuja kutuliza hiyo uprise. Na hata baada ya hiyo uprise kuwa imezimwa, bado kumeendela kuwa na sporadic uprising ambazo zimekuwa zikiendela ila nisema tu media za kibongo hazijawapa enough attention watu wa Tarime. So next time usijenge hoja kama huna hard evidence za ku-back hoja yako.
...Haiwezekani hata kwa kufikiria kuwa Tarime wanaweza kupata sheria fulani ya madini tofauti na wilaya nyinginezo ati kwa sababu watu wa huko Chalinze wamelala..mtapewa nyinyi dose mpate kulala kama wengine ili kazi isiwe ngumu zaidi. Ni rahisi kuwalaza Tarime kuliko kuwaamsha Watanzania wote...
That's what I call "spirit of defeatism." What you just don't know is that Tarime People are very resillient. Just because watu wa wilaya zingine wamelala usingizi, haimanishi kuwa watu wa Tarime nao watalala usingizi wakipatiwa hicho unachokiita "dose."