Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Heshima mbele, mkuu unataka hata kunifundisha kiswahili mkuu?...Kiswahili safi tunaposema watu wa sehemu fulani wamelala haina maana wamelala usingizi isipokuwa wamelala kiakili...They can see but their minds are shut!.. ndio Ujinga huo kuu...Haiwezekani kuwa unaposema watu wamelala hauna maana ya Ujinga kwani kulala kiakili ni Ujinga na ndio maana wazungu wanachukua mali zao bila wao kufahamu....

No, that's ya own definition, Bob. Go back and read my original thread/replies. I kindly ask you to stop twisting my words to trying to justify your own prejudice.

Na kwabahati mbaya Barricks wamechukua mali kibao sasa ndio mnaamka..Yaani ujinga umewatoka..kwa hiyo binafsi siku zote mtu yeyote anayetumia.

No mkuu, watarime wameamka siku nyingi sana. Ila nadhani tatizo ni kwako ambaye umekuwa hu-pay close /enough attention kuhusu kilichokuwa kikiendelea huko Tarime tangu '98, wazungu walipoanza utafiti...

Kuhusu Tarime mkuu wangu wala usinambie kitu nimekuwa sehemu hizo toka mdogo nikienda Ikizu kwa jamaa zangu. hata mwaka jana nilikuwepo na kama unakumbuka nilitoa hoja moja kuhusiana na Miwa. Kwa nini Ukivuka mpaka tu kuingia kenya utaona mashamba makubwa ya miwa hali upande wa Tanzania hakuna kitu kabisa yaani pori...Na nikatoa pendekezo linalohusiana na sehemu hiyo... Kwa hiyo naposema zipingi hoja yenu nina maana kwamba Watanzania wote tumehsa amka hatujalala tena na vizuri sana issue hii imepata watu wanaoweza kuisimamia ikiwa wabunge wetu wameshindwa. Ni harakati ambazo zimeanzishwa na Mkurya ma wakurya lakini ziwe na mtazamo zaidi ya mipaka ya Tarime kama Kenyatta na Wakikuyu walivyopigania haki za Wakenya..Ilianzia wapi na kwa maslahi ya nani isiwe sababu ya kuzuia harakati hizi..

Naelewa mkuu. Expertisee yako kuhusu mambo ya Tarime [all this 'miwa' thing] is superb!

...hadi sasa hivi mnaachamwanya mkubwa sana wa CCM kujibu mapigo yetu tena kwa viabaya sana kuliko hata madai ya Zanzibar ambo inajulikana hapo awali ilikuwa nchi yenye mamlaka yake...
Kuhusiana na uwanja wa ndege unataka kunambia hao wachimbaji wadogo ndio watakuwa na ndege zao zikiruka kwenda nje kuuza hizo dhahabu au?..Hivi kweli unaelewa ukubwa wa investment ya dhahabu na vitu vinavyohusiana na uchimbaji...

He he he...!! Sasa umeamua kunichekesha mkuu! I think sasa ni bora tu tukaiachia hii issue hapa maana naona umeishiwa point...
 
Ni aibu kwa mtanzania kuwa na mawazo mabovu kama hayo.Kwanza ni uaini wenyewe hawajaacha kupigana mpaka sasa

Oh, really? kuna 'uhaini' gani kuhusu kile ambacho watarime wanachodai [I mean, autonomous status]? Hivi kwani ni uhaini kuwa na utofauti wa kimawazo na watu wengine?Please, fafanua kidogo hapo...
 
Oh, really? kuna 'uhaini' gani kuhusu kile ambacho watarime wanachodai [I mean, autonomous status]? Hivi kwani ni uhaini kuwa na utofauti wa kimawazo na watu wengine?Please, fafanua kidogo hapo...

Gustanza_The;

Pole sana my brother, hapa utapata shida sana, hawa jamaa ni wagumu sana wa kuelewa na hata ukiwaelimisha ni wepesi wa kusahau. Gustanza_The; laiti ungevuta hisia zako zikakukumbusha ile miaka ya 87- 94, mji wetu wa tarime ulikua kwa sababu ya dhahabu hiyo ya pale Nyamongo, nakumbuka 91 na mimi nilijongea pale hakika nikajikuta nikiboresha kipato changu.

Gustanza_The; naweza kuilaumu sana serikali yetu kwa wakati ule kwani haikutoa mwongozo katika sera ya madini, lakini ninakumbuka sana watu wa mkoa huo(Mara) wote tulinufaika na dhahabu ile.

Matajiri wote walio matajili hadi leo pale Tarime wengi wao walipata itajiri wao toka ndani ya uchimbaji wa dhahabu ile,jambo la kushangaza tangu hawa wawekezaji wamejikita hapa nyumbani, mji wetu kwa sasa umedolola, tunapata kipato kutokana na biashara za hapa Mpakani na kilimo kisichokuwa na tija.

Gustanza_The; hakika tusingekuwa na ugomvi na serikali yetu kama hawa wawekezaji wangekuwa wanailipa serikali yetu kodi ya kutosha, ila tunachukizwa na huo MRAHABA WA 3%, NA KIBAYA ZAIDI HAWA JAMAA WANA DHARAU, NA HAPA NDIPO TUTAPIGANA HAKI YETU MPAKA KIELEWEKE.
 
LISSU YUPO TARIME NA HII NI SIKU YA NNE , watu wanaenda kisayansi zaifdi kuliko kukurupuka.
 
Ondoeni hisia kuwa ukoo wa wangwe unanguvu za kisiasa tarime, mvurugano ndani ya ccm tarime ulidhoofisha nguvu za ccm kwa sasa hali hiyo haipo.

Chadema TLP NCCR badala ya kupoteza muda na tarime wahangaikie jimbo la mwibara na biharamulo ambayo kwa uhakika nimali ya upinzani lakini sio tarime.
 
Gustanza_The said:
What you [JokaKuu] fail to grasp here ni kwamba, endapo kama madai ya Tarime yatakubaliwa, then hiyo AIRSPACE itakuwa chini ya Tarime, brother! I kindly suggest kwamba: rudi tena kasome encyclopedia yako upya juu ya nini maana ya neno "AUTONOMOUS."

Gustanza_The,

..sijayasoma kwa undani mapendekezo ya wana Tarime, but i dont think autonomy wanayoitaka itajumuisha mpaka masuala ya airspace.

..ikifikia mpaka kudai kuwa na airspace basi labda tutakuwa tunazungumzia "Jamhuri ya Watu wa Tarime."
 
Nataka kuungana na Isaya Mwita juu ya Prof .Wangwe .The guy is a personal friend to JK na ana kiburi cha ajabu sana na hakubaliki hata katika hali ya kawaida .Kama CCM wanataka kuona ukweli huu basi wamweke na wategemee kura za huruma .watapata kura za huruma kama Lowasa ataenda kuomba msamaha wakurya kwa kejeli kwao na kuwaondoa mafisadi migodini .Vinginevyo sina imani kwamba hapa Tarime CCM can penetrate .
 
Gustanza na Wenzako,

Tuchulie kwamba mimi sielewi maana kamili ya msemo usemao - Watu wengine wamelala..kama ulivyosema hiyo ni definition yangu naomba yako bila kurudi nyuma...
Kisha nakuomba unambie kwa nini unasema WaTarime waliisha amka siku nyingi!..
Tukimaliza hapo na watu wote wakakubali maana yako sintakuwa na zaidi....
 
Gustanza na Wenzako,
Tuchulie kwamba mimi sielewi maana kamili ya msemo usemao - Watu wengine wamelala..kama ulivyosema hiyo ni definition yangu naomba yako bila kurudi nyuma...

Kwa definition yako: kulala usingizi = ujinga. Mimi nakataa kuwa sikusema hivyo. Naweza nika-argue kwamba maintaning the status quo = kulala usingizi. Now, take for example, neocon. Some of its members are very smart people! However, ukija kwenye suala zima la national security, approach yako imejengeka kwenye msingi kwamba: first bomb,then ask questions later [i.e all threats must be confronted by force]. Haimanishi kwamba wao ni wajinga [hapana], ila wanadhani kuwa hii ndiyo approach sahihi, and diplomasia ni upotezaji wa muda tu... And kwanini wanaamini hivyo? Coz strategy hii ilifanikiwa kumtia adabu Hitler miaka hiyo...

On the other hand, liberals wao wanaweka emphasis zaidi kwenye diplomasia, na kwao utumiaji wa force unakuja as a last resort. And they sincerely believe that. So kwa upande wangu, naweza nikasema kuwa neocon bado wamelala usingizi, maana bado hawajakubaliana na fact kwamba dunia ya sasa sio ile ya mwaka 1914.

Now, tukirudi tena kwenye issue ya wanatarime—wao wameamua kuwa, for now, it's good for them to go all alone kwasababu wanaamini kuwa—bado wananchi wa sehemu zingine za Tanzania wamelala usingizi. In other words, bado wana-embrace more of the same [status quo]. CCM, CCM, CCM, CCM, CCM.

Kisha nakuomba unambie kwa nini unasema WaTarime waliisha amka siku nyingi!...

Hili nimelizingumzia tena na tena. KWAHIYO KAMA BADO HUJANIELEWA SIDHANI HATA KAMA NIKITUMIA NATURAL TERM OF MY LIFE EXPLAINING TO YOU THE SAME THING OVER AND OVER ITAKUBADILI THINKING YAKO NA KUKUFANYA UAFIKIANE NAMI.

Tukimaliza hapo na watu wote wakakubali maana yako sintakuwa na zaidi....

No, hata kama watu wote wasipokubali/afiki/elewa/unga mkono kuhusu suala hili; mimi msimamo wangu uko palepale: I support citizens of Tarime on this matter [Autonomous Status] 110%.
 
Hao wanaotaka kujinyakulia Uhuru kutoka kwa Mkoloni CCM ,wanayaweza mapambano wasije wakayakuta wale waComoro ,halafu wacheni kulinganisha na Zanzibar ,maana hata Juzi mlimsikia mkubwa wao akitoa heshima kwa kusema Zanzibar ni nchi.
Ila kama Zanzibar ingelikuwa ipo sehemu kama za Kitarime basi naamini kabisa kungekuwa na gorila war.
 
Gustanza_The,
Mkuu maelezo yako yote mkuu umerudi pale pale..
Ujinga ni kutofahamu ambako ndiko kunamfanya mtu asikubaline na facts kunatokana na kutokuwa na elimu fulani...Yote haya mkuu wangu ni Akili imelala wala sio macho...huwezi kutokubaliana na kitu ambacho akili yako ama elimu yako inakwambia tofauti..
Huo mfano wa neocon mkuu hakuna mahala popote ktk misahafu yote ya tafsiri inayoweza kusema watu wenye mtazamo huo ama maamuzi hayo huwa wamelala..Hapana mkuu maadam wanalishughulikia swala pamoja na kwamba ni njia tofauti haina maana kuwa wamelala hakuna kiswahili cha nanma hiyo..

Mtu aliyelala ni yule ambaye hashughulikii kitu ambacho kipo wazi kabisa...unajaribu kupotosha lakini hata hivyo mkuu Ujinga sio tusi la nguoni isikupe homa sana.. hapa JF ni mahala ambapo tunajaribu kufuta Ujinga yaani kutoa hizo tongo machoni..Ujinga unafutika mkuu na ndio moja ya malengo ya nchi yetu, ni sawa na Umaskini unaweza kuwachusha watu unapotakwa lakini hauna maana mbaya zaidi unless sio ukweli.. Kifupi napinga watu kulala (ujinga) kwa sababu nina hakika makabila mengine wanafahamu fika kinachowakuta lakini nguvu ya dola imekuwa nzito kwao na wamekosa mshikamano toka kwa Watanzania wengine.. Bulyanhulu mkuu walikufa watu zaidi ya 100 unafikiri walikuwa wakifanya nini! au kwa sababu walifukiwa na hayo magreda ndio maana unasema walikuwa wamelala! kwi kwi kwi!

Mkuu hata mwenye tongo machoni hawezi kuitwa kipofu pamoja na kwamba tongo zina sound vibaya...na hazipendezi.
Hata hivyo, kila la kheri nawatakia mwanzo mzuri na tutakuja yazungumza pindi mkifika kituo cha kwanza -Chalinze!...
 
Mwingine toka CCM alimezea mate jimbo la Tarime
Na Steven William, Muheza

WAKATI vuguvugu la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime likiendelea kupamba moto, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Mwikabe Mwita Waitara, amejitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na marehemu Chacha Wangwe.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa juzi, Waitara, mwenye shahada ya ualimu wa sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam, alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kutaka kuitumia elimu yake kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii yaliyopo katika jimbo hilo.

''Kikubwa zaidi kilichonisukuma kuamua kugombea ni utajiri na fursa nyingi zilizopo katika jimbo hilo, lakini katika kipindi kirefu, jimbo limekosa mwakilishi mahiri anayeweza kuwa kiunganishi kati ya wananchi na serikali ili kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi,'' alisema.

Waitara ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) mwaka 2005/06, aliongeza kusema kuwa moja ya matatizo makubwa yaliopo katika jimbo hilo ni migogoro ya mara kwa mara na mapigano ya koo ambayo utatuaji wake unahitaji umakini mkubwa.

Alisema kuwa wananchi wengi wa jimbo hilo ni wakulima wa zao la kahawa, lakini wamekuwa wakikosa soko la uhakika kutokana na chama cha ushirika kufa na hivyo mazao hayo kununuliwa na walanguzi huku wakulima kubaki maskini, jambo ambalo alisema atalitafutia ufumbuzi.

“Wakinipa fursa ya kuongoza jimbo la Tarime, ninaamini nitaleta mabadiliko kukabiliana changamoto mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo ambazo zinakwamisha maendeleo ya wananchi, aliongeza kusema Waitara.

Alieleza kuwa anatarajia kuchukua fomu za kugombea ubunge wa Tarime Agosti 29 mwaka huu na kwamba ana imani kuwa atapata nafasi ya kuwakilisha jimbo hilo.

Umoja wa Vijana wa CCM wilayani Muheza, umempongeza katibu huyo wa vijana wa mkoa kwa kitendo chake cha kutaka kugombea ubunge Tarime.

Katibu wa Vijana wilaya ya Muheza, Gerald Mwadalu, katika mkutano wa Baraza Kuu la Vijana wilaya uliofanyika juzi katika Ukumbi wa Tate Pub Plus, alisema uamuzi wa Waitara wanauunga mkono na watashirikiana naye atakapohitaji msaada wao.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Muheza, Peter Jambele, ambaye aliupongeza umoja wa vijana wilayani hapa kwa kufanya kazi nzuri katika umoja huo bila kutetereka na kuwatakia heri wana CCM waliogombea nafasi za uongozi katika jumuiya zao.
 
Badilisha heading yako huyu sio rais wa Daruso ila aliwahi kuwa .Kuweka hivyo unapotosha wasomaji.
 
MK,

Inaonekana unamfahamu vizuri huyo kijana.ama back coz now Mjadala kuhusu uchaguzi umeanza kuwa mzito...

Tuambie Je anaweza kuiangusha CHADEMA kama akipita?
 
MK,

Inaonekana unamfahamu vizuri huyo kijana.ama back coz now Mjadala kuhusu uchaguzi umeanza kuwa mzito...

Tuambie Je anaweza kuiangusha CHADEMA kama akipita?

Kupita kwale lutategemea mabo makubwa mawili

1. Mgombea atakayesimamishwa na CHADEMA anakubalika kwa kiasi gani

2. Mgombea wa CCM anapata support kiasi gani kutoka Juu.

But jamaa ni aggresive kiaina naweza sema anashabihiana kwa karibu sana na Marehemu chacha, kwa wanaomfahamu watakubaliana nami.

Pia jamaa alimpa support sana Chacha(RIP) wakati wa uchaguzi 2005.

Ila kama mgombea wa chadema atakua strong, jamaa Historia yake ya uongozi wa Daruso inaweza kumuwekea doa kwani ni mtu fulani asiye na misamamo wa kisisasa "Political Opportunist" but anawa2 fulani wa uliokuwa "mtandao" wanomuunga mkono na inasemekana hata hiyo nafasi alonayo kwa sasa huko Tanga wao ndo walimtafutia.

Kwangu mimi ni mtu ambaye haaaminiki na ni vigumu kuweka dhamana juu yake. Ni mlafi sana wa hela naweza sema ni m2 ambaye "hana simile" na hela
 
Mwingine toka CCM alimezea mate jimbo la Tarime
Na Steven William, Muheza

WAKATI vuguvugu la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime likiendelea kupamba moto, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Mwikabe Mwita Waitara, amejitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na marehemu Chacha Wangwe.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa juzi, Waitara, mwenye shahada ya ualimu wa sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam, alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kutaka kuitumia elimu yake kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii yaliyopo katika jimbo hilo.

''Kikubwa zaidi kilichonisukuma kuamua kugombea ni utajiri na fursa nyingi zilizopo katika jimbo hilo, lakini katika kipindi kirefu, jimbo limekosa mwakilishi mahiri anayeweza kuwa kiunganishi kati ya wananchi na serikali ili kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi,'' alisema.

Waitara ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) mwaka 2005/06, aliongeza kusema kuwa moja ya matatizo makubwa yaliopo katika jimbo hilo ni migogoro ya mara kwa mara na mapigano ya koo ambayo utatuaji wake unahitaji umakini mkubwa.

Alisema kuwa wananchi wengi wa jimbo hilo ni wakulima wa zao la kahawa, lakini wamekuwa wakikosa soko la uhakika kutokana na chama cha ushirika kufa na hivyo mazao hayo kununuliwa na walanguzi huku wakulima kubaki maskini, jambo ambalo alisema atalitafutia ufumbuzi.

“Wakinipa fursa ya kuongoza jimbo la Tarime, ninaamini nitaleta mabadiliko kukabiliana changamoto mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo ambazo zinakwamisha maendeleo ya wananchi, aliongeza kusema Waitara.

Alieleza kuwa anatarajia kuchukua fomu za kugombea ubunge wa Tarime Agosti 29 mwaka huu na kwamba ana imani kuwa atapata nafasi ya kuwakilisha jimbo hilo.

Umoja wa Vijana wa CCM wilayani Muheza, umempongeza katibu huyo wa vijana wa mkoa kwa kitendo chake cha kutaka kugombea ubunge Tarime.

Katibu wa Vijana wilaya ya Muheza, Gerald Mwadalu, katika mkutano wa Baraza Kuu la Vijana wilaya uliofanyika juzi katika Ukumbi wa Tate Pub Plus, alisema uamuzi wa Waitara wanauunga mkono na watashirikiana naye atakapohitaji msaada wao.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Muheza, Peter Jambele, ambaye aliupongeza umoja wa vijana wilayani hapa kwa kufanya kazi nzuri katika umoja huo bila kutetereka na kuwatakia heri wana CCM waliogombea nafasi za uongozi katika jumuiya zao.

CCM bwana .Waitara once again is missing the point hapa .Elimu si kipimo cha Uongozi .Hebu angalia ma Prof walioko CCM na Tanzania ilipo sasa .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom