Dr.W.Slaa: Ben na wana JF
1. Nimefuata mjadala kwa karibu sana. Nadhani tatizo ni kuwa wengi wame react kwenye kilichokuwa posted kwenye thread hii na hawakusoma aliyoyasema Dr. Mvungi, ambayo hajayakanusha. We need to be scientific in our approach to issues.
i) Kauli ya Dr. Mvungi niliyoijibu ilitoka kwenye TBCl, Daily News na Mtanzania ya September, 4th, 2008. Dr. Mvungi hajakanusha.
2) Dr. Mvungi ametoa pia Kauli kali dhidi ya "Chadema" kama Chama. Dr. Mvungi ni msomi aliyebobea anapaswa kujua tofauti kati ya Mashabiki, na Wanachama wa Chadema, na Chadema anayoituhumu na kutaka imwombe msamaha.
3) Dr. Mvungi amenukuliwa akisema " Chama cha Ushindani kimekiri kuwa hakitaki washindani wengine wawepo, hivyo vyama vingine vitoweke kibaki chenyewe tu na chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Upinzani kiitwacho CHADEMA, kimetumia hoja ya mawe badala ya kudhihirisha demokrasia". Haya ni maneno mazito, hasa yanapotoka kwa msomi. Ni hatari, na yakiachwa hivi hivi, ndiyo Taifa hili linapelekwa korongoni na wanasiasa wa aina hii.
4. Dr. Mvungi anatakiwa atamke Chadema imekiri wapi, na kwa njia gani? na wapi? Dr. Mvungi anatakiwa aeleze umma wa Tanzania ni wapi Chadema imesema haiwataki wapinzani au vyama vingine? Wananchi wanaosoma magazeti lakini si wachambuzi wanaelewa nini? Siasa ni Sayansi na si udanganyifu ndio maana Chadema haiko tayari kuvumilia upotoshwaji wa aina hii.
4) Dr. Mvungi angekuwa mkweli angelieleza ni katika hatua ipi alipigwa mawe, na neno gani alikuwa amelitamka lililoamsha hasira ya Wananchi. Anataka kumdanganya na kumpotosha nani?
5) Kauli ya Dr. Slaa imetanguliwa na kulaani watu, wananchi wanaochukua sheria mikononi mwao na kuwa sikubaliani na mashabaki au wanachama kupiga watu.
6. Nilichoeleza ni kuwa Dr. Mvungi akumbuke kwenye nchi jirani watu wameenda msituni kutokana na kauli za viongozi na wanasiasa.
7. Nikakemea viongozi wote wanaotumia vibaya ndimi zao, kama Dr. Mvungi. Nikaeleza kuwa "uvumilivu una mwisho" na mtu akashawishika kuchukua hatua baada ya kuwa provoked kwa kiasi alichofanya Dr. Mvungi, asilalamike wala kumtafuta mchawi ila aulaumu ulimi wake.
8. Haya ndiyo niliyoyasema on the basis of statements za Dr. Mvungi.
Mheshimiwa Dr. Slaa,
Mkuu Mtanzania,
Heshima yako tena bro, Dr. Slaa amesema wazi kwenye kifungu cha 5 kwamba amelaani kwanza vitendo hivyo, halafu hii habari ya muanzisha mada tuliyoletewa inaonekana kuwa haikuwekwa yote, tuliwekewa yale tu mtoa mada aliyoyataka tuamini, lakini kwa maelezo ya Dr. Slaa hapo juu ni clear kuwa tumechezewa, labda tu umuombe radhi Dr. Slaa kwa kumshambulia bila ya kuwa na ukweli wote kuhusu original habari yenyewe, au?
Kwa sababu kwa maneno ya Dr. slaa sio hata clear kama Mvungi alipigwa hayo mawe!