Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mtanzania,

Uko right, but ninachopinga ni hii kasumba ya watu kutaka first hand information na wanapogundua kwamba wao walikua wrong kutokana na hawakuwa na back up data nzuri bado wanaendelea na misimamo yao.Yaani kasumba ya aina hii haitakaa ijenge hata siku moja.

Dr. Slaa alishalaani hizo vurugu,nadhani hata mkuu FMES alihisi labda kuna kipengele hasa kile cha kulaani hizo vurugu watu walishindwa au kwa makusudi waliamua kutokiona katika maelezo ya Dr. Slaa,ikabidi akiweke separately but ilishangaza kuona bado kuna watu wamegoma kubadili walicho nacho akilini.

Je,mkuu ulitaka Dr.slaa alaaani tu hizo vurugu bila kuongelea makosa aliyofanya Dr.Mvungi? Is this not a doble standard?

Mazingira ya vurugu za CCM kule Kiteto ilikua ni tofauti kabisa na ya huko Tarime.Hilo hasa ndilo kosa kubwa sana la wanasiasa wengi hapo nyumbani,hawana uwezo wa kusoma saikolojia ya audience.Na hili suala la CCM kutumia vyombo vya dola lina mwisho wake,Very soon watakoma kama walivyokoma kunyonya ziwa la mama.

Sisi ndio wananchi tunaolipa kodi za kuwalipa hao FFU wanaotumika against sisi,ipo siku watakabiliana na action movement wakidhani wanakuja kuwanyanyasa walalahoi maanake hata matumizi ya FFU kwa interest zao imeshahalalishwa hadi kufikia hatua wanawita vijana wao.Ila jambo moja la msingi hata hao FFU inafaa watambue kwamba wao ni sehemu ya Tanzania na ni ndugu zetu.Vuguvugu la kimapinduzi au Radical Changes hata siku moja halitashindwa na vyombo vya dola.Historia inasema hivyo,ni ukweli mchungu kwa wengine but that is the fact!

Ben,

Ni kweli Dr. Slaa kalaani hizo vurugu, lakini kusema Dr. Mvungi alaumu ulimi wake mwenye na wala sio hao wananchi waliompiga mawe inaondoa kabisa kule kulaani alikofanya.

Huwezi kuchanganya hayo mambo mawili kwa pamoja.

Ana haki ya kumlaumu Dr. Mvungi kuongea maneno ya uwongo lakini hana haki kumwambia kupigwa kwake ajilaumu mwenyewe.

Naheshimu mchango wa Dr. Slaa kwenye haya mapambano ila kama mwanasiasa na kiongozi
ni muhimu kutokuchanganya hayo mambo mawili. Hata mtu akikosea dawa sio kupigwa.

Je CCM wakivamia mkutano wa CHADEMA na kuwapiga viongozi kwa visingizo vya kwamba mlikuwa mnawatukana kwamba ni mafisadi, je mtafanya nini? Mtalaani?

Nimesoma ujumbe wa Dr. Slaa mara nyingi na bado naondoka na hisia ile ile ya kwamba anahalalisha kupigwa kwa Dr. Mvungi kwa kisingizio cha kwamba alikuwa anahutubia uongo. Kulaani kwa mwanzoni inakuwa kama machozi ya mamba.
 
Ni kweli kabisa. Dk Slaa amekuwa mstari wa mbnele kusisitiza utawala wa sheria. Hata kama Dk Mvungi aliwatukana Chadema, hawakustahili kuchukua shseria mkononi kama walivyofanya, wawe ni wafuasi, wapenzi au wanachama
 
Ben,

Ni kweli Dr. Slaa kalaani hizo vurugu, lakini kusema Dr. Mvungi alaumu ulimi wake mwenye na wala sio hao wananchi waliompiga mawe inaondoa kabisa kule kulaani alikofanya.

Huwezi kuchanganya hayo mambo mawili kwa pamoja.

Ana haki ya kumlaumu Dr. Mvungi kuongea maneno ya uwongo lakini hana haki kumwambia kupigwa kwake ajilaumu mwenyewe.

Naheshimu mchango wa Dr. Slaa kwenye haya mapambano ila kama mwanasiasa na kiongozi
ni muhimu kutokuchanganya hayo mambo mawili. Hata mtu akikosea dawa sio kupigwa.

Je CCM wakivamia mkutano wa CHADEMA na kuwapiga viongozi kwa visingizo vya kwamba mlikuwa mnawatukana kwamba ni mafisadi, je mtafanya nini? Mtalaani?

Nimesoma ujumbe wa Dr. Slaa mara nyingi na bado naondoka na hisia ile ile ya kwamba anahalalisha kupigwa kwa Dr. Mvungi kwa kisingizio cha kwamba alikuwa anahutubia uongo. Kulaani kwa mwanzoni inakuwa kama machozi ya mamba.

Hata kiteto walipigwa watu baada ya kukiita CCM chama cha mafisadi.Lakini hawakusema wazilaumu ndimi zao.

KTK utawala wa sheria huwezi mtu kumwita FISADI,MWIZI kama sheria haijathibitisha kua jamaa ni mwizi ama fisadi.

Wala MVUNGI kukandia wana siasa wenzake ni kosa la kawaida kabisa ktk uwanja wa siasa.

Ni sawa kusema KAKA na MDOGO wake walio ktk mechi na wako timu pinzani ,basi mdogo ana ambaa ambaa ktk winga kufunga bao na kaka mtu anatokea anampiga ile KITU double engine,Harafu baada ya mchezo watu wanamshambulia kaka mtu .
 
Mgawanyiko wa upinzani hautokani na ubaya wao. Unatokana na jinsi ambavyo zoezi la kuwachonganisha na kuwadhoofisha linavyofanywa na CCM. Kama wakifanikiwa kuepuka mbinu za CCM basi watakuwa salama. Lakini ipo kazi kubwa.

Nawatia moyo CHADEMA kusonga mbele. Hata kama kuna ghiliba kubwa namna gani bado nafasi ya kushinda ipo. Tarime sio wajinga wa kubebwa hovyo na rushwa na kuuza shahada zao za kupigia kura.

SONGENI MBELE CHADEMA MTASHINDA.
 
Mkuu KAMENDE,

Pokea zako tano.Maneno adimu sana hayo.Ubarikiwe sana mkuu.
 
Mtanzania,
Ilikuwa lazima na chanzo cha watu kufanya vurugu kijulikane ili iwe angalizo kwa watu wengine wawaeleze wapiga makusudio yao sio kuleta uchochezi kama alivyofanya Dr Mvungi.
 
• Polisi yazuia mkutano wa CHADEMA Tarime

*Ulipangwa kufanyika leo, wao waapa kuufanya

Na George John, Tarime

JESHI la Polisi wilayani Tarime mkoani Mara limepiga marufuku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya mkutano wake ulipangwa kufanyika mjini hapa leo.

Kwa mujibu wa barua ya Polisi ya Septemba 6 yenye kumbukumbu TAR/A.14/13/B/VOL.V/132 kwenda kwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Polisi imekataa kufanyika mkutano huo kutoka na machafuko yanayoendelea wilayani humo.

Taarifa hiyo ya Polisi iliyosainiwa na Bw. Costantino Masawe ambaye ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya na nakala yake kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, polisi ilieleza kuwa mkutano huo hautaweza kufanyika kwa vile wilaya hiyo inakabiliwa na mapigano ya koo nne za kabila la Wakurya.

"Nakujulisha kuwa kutokana na hali mbaya ya wilaya yetu kuwa na mapigano ya kikabila kati ya koo za Wanchari na Warechoka na Wahunyaga na Wamera, nguvu ya ulinzi imeelekezwa huko na pia tunazoezi la usimamizi wa mtihani ...kutokana na sababu hizo kibali cha kufanya mkutano huo hakitatolewa kutokana na uhaba wa askari, " ilisema sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo iliongeza kuwa Polisi wataruhusu kufanyika mikutano hiyo baada ya hali amani na utulivu kurejea wilayani humo.

Hata hivyo CHADEMA imepinga hatua hiyo ya Polisi na kusisitiza kuwa mkutano huo utafanyika kama ilivyopangwa kwa maelezo kuwa chama hicho hakijawahi kufanya mkutano na kuvuruga amani bali waliomba kibali hicho kwa mujibu wa taratibu.

Katika barua yao ya kupinga hatua hiyo ya Jeshi la Polisi yenye kumbukumbu CDM/KW/UCH/VOL.1/043/08 iliyosaniwa na Bw. Chacha Okong'o na nakala zake kupelekwa kwa viongozi wakuu wa CHADEMA ,wamesema sababu zilizotolewa na Polisi hazina msingi wa kuzuia mkutano huo.

"Ni vizuri kuzingatia vyama vya siasa vinavyotaka kufanya mkutano wa hadhara ama maandamano ya amani haviombi kibali Polisi kufanya hivyo isipokuwa vinatoa taarifa ya maandishi ya saa 48 kabla ya kufanya hivyo,"ilisema sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo ya CHADEMA ilidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Septemba 3 mwaka huu kilifanya mkutano wake kutafuta mgombea ubunge na Polisi walitoa ulinzi huku mkuu huyo wa Polisi akiwepo mwenyewe kwenye mkutano huo wakati mapigano hayo yakiendelea na kuhoji, iweje leo CHADEMA izuiwe kwa kisingizio cha vurugu zinazoendelea ?

Septemba 5, CHADEMA kupitia kwa Katibu wake wa Wilaya Bw. Joseph Anthon ilitoa taarifa Polisi kuwajulisha kuwepo mkutano huo Septemba leo katika uwanja wa mpira mjini Tarime kwa lengo la kutoa elimu ya uraia.

Wakati huo huo watu 12 wamepitishwa na vyama vyao kugombea nyadhifa za ubunge na udiwani katika kata ya Tarime mjini na jimboni Tarime.

Waliomba na kupitishwa na vyama vyao baada ya kupigiwa kura za maoni katika vikao vya vyama hivyo vilivyofanyika kwa nyakati na siku tofauti mjini hapa.

Mwanachama wa CCM aliyechaguliwa kuombea kiti cha ubunge katika Jimbo la Tarime ni Bw. Ryoba Kangoye ambaye katika uchaguzi huo alipata kura 586 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Bw. Nyambari Nyangwine aliyepata kura 326.

CCM pia ilimchagua mfanyabiashara maarufu mkoani Mara, Bw. Peter Zakaria, kugombea kiti cha udiwani katika kata ya Tarime Mjini baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 198 dhini ya Bw. Bomani Kituho aliyepata kura 15.

Kwa upande wa CHADEMA, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Bw. Charles Mwera, alichaguliwa kugombea ubunge baada ya kupata kura 28 akifuatiwa na Bw. Job Chacha aliyepata kura 11.

Katika nafasi ya udiwani, CHADEMA ilimpitisha, Bw. John Heche aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 12 dhidi ya Bw. Stephen Kisengewa (kura 2).

NCCR-Mageuzi kiliwapitisha Bw. Enock Haruni kugombea kiti cha ubunge na Bw. David Wangwe (Osama) ambaye ni ndugu wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, kugombea kiti cha udiwani kata ya Tarime Mjini.

Chama cha Wananchi (CUF) kiliwapitisha, Bw Job Kerario kugombea ubunge wa Jimbo hilo na Bw. John Rotente kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha udiwani.

Hata hivyo, vikao vya Taifa vya vyama hivyo ndivyo vyenye maamuzi ya mwisho juu ya mwanachama anayefaa kugombea ubunge wakati vikao vya ngazi ya mkoa, vitatoa maamuzi ya mwisho kwa wagombea udiwani.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wagombea wote wanatakiwa kufanya kampeni za uchaguzi huo kati ya Septemba 14 na Oktoba 11, kabla ya uchaguzi, Oktoba 12 mwaka huu.

Nafasi za ubunge Jimbo la Tarime na udiwani katika Kata ya Tarime Mjini ilibaki wazi baada ya kifi cha mbunge wa zamani marehemu Wangwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Julai 28, mwaka huu, eneo la Pandambili, Kongwa mkoani wa Dodoma akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam.
 
Wakuu,

Hivi CHADEMA wakifanya mkutano na ikatokea vurugu ni nani Wa kulaumiwa?
Kuna wale wakuu wangu wenye allergy na double standards kwenye siasa sasa hili la polisi kuwazuia CHADEMA huku wakiruhusu CCM siku mbili kabla tena kwa kutoa full support ya ulinzi mnaonaje hapa?

Halafu vipi huyo bwana Mwera anakubalika kiasi gani huko Tarime?
 
Hivi teuzi za CHADEMA zinakuwaje? Mbona jamaa kachaguliwa kwa kura chache sana? Inaelekea wanachagua watu wachache sana na kwa kuwa huyo Mwera ni Mwenyekiti wa halmashauri nadhani alikuwa na nafasi kubwa kupita. Zile mbwembwe za mwandishi habari, pia yule dada ina maana wameshindwa?

CCM wanatumia vyombo vya dola kushinda uchaguzi. Hapo tatizo sio amani wala usalama, wanatumia manguvu kuzuia mikutano ya CHADEMA.

Siasa za Afrika ni kama boxing, kumtoa mtu aliyeko madarakani inabidi umtwange knock out, vinginevyo majaji watampendelea bingwa tu.

Ndio maana ni muhimu mno kushirikiana vyama vyote kupambana na CCM kama wanataka ushindi. Ukitegemea kuishinda CCM kwa asilimia 55, jua haitoshi. Inatakiwa kuwe na matarajio ya zaidi ya asilimia 70 ili hata wakiiba bado washindwa kuziba hiyo tofauti.
 
Mkuu,hapo ndipo amani inapovurugika,kwani watawala hawapendi sisi kuleta mabadiliko kwa njia ya amani.
 
Wakuu,

Hivi CHADEMA wakifanya mkutano na ikatokea vurugu ni nani Wa kulaumiwa?
Kuna wale wakuu wangu wenye allergy na double standards kwenye siasa sasa hili la polisi kuwazuia CHADEMA huku wakiruhusu CCM siku mbili kabla tena kwa kutoa full support ya ulinzi mnaonaje hapa?

Halafu vipi huyo bwana Mwera anakubalika kiasi gani huko Tarime?

BEN,
Yaani unadhani CCM wamelala????Katika mambo yanayowanyima usingizi, basi uchaguzi mdogo wa Tarime umewashika pabaya.Ila kutokana na jinsi wanavyojua kutumia mbinu mbalimbali chafu na safi kushinda sasahivi ni kama vile askari aliyepo msituni tayari kwa vita.
Marehemu chacha wangwe alishinda ubunge wa tarime kwasababu kuu tatu:
1. Wananchi wa tarime walikuwa wamechoka kuwakilishwa na Mbunge bubu Kisyeri chambiri pamoja na majigambo ya ukooo wao like Enock aliyekuwa m/kiti wa ccm mkoa na wengineo.
2. Wananchi wa tarime walikuwa wamechoshwa na unyanyasaji wanaofanyiwa na wakwapuaji wa mgodi wa nyamongo(north mara gold mine)
3. Wanachinchi wa Tarime walikuwa wanahitaji kiongozi atakayeshirikaiana nao katika kutetea maslahi yao ndipo wakalazimika kumchagua marehemu chacha wangwe kwa kuwa ni mtu aliyekuwa akifahamika na kuaminika kwa misimamo yake isiyoyumba!

Kwahiyo ni dhahiri kuwa ccm wamefanya makusudi kumsimamisha Ryoba Kangoye ambaye alichuana na Chambiri 2005 na kushindwa ingawa wananchi wengi walionekana kumkubali.
Lakini pia kufuatia ushindi wa marehemu chacha wangwe na jinsi alivyoanza mara moja kutetea maslahi ya wanatarime tangu aingie bungeni, CHADEMA ilizidi kupata wafuasi wengi sana Tarime.Na kuanzia hapo CCM ilianza kujipanga kuirudisha Tarime mikononi mwake.
Nimalizie kwa kusema tu kwamba suala la Polisi kuwazuia chadema kufanya mkutano wao leo, ni mkakati maalum wa ccm kuimaliza chadema na wao washinde uchaguzi. Sasa kama kuna mtu anaamini kuwa Polisi wamekwenda kutuliza mapigano ya warenchoka vs waanchari na wahunyaga vs wamera anajidanganya!CHADEMA watakapotia mguu tu uwanjani ndipo weatajua kuwa Polisi wapo wengi sana tena hayo mapigano ni kisingizio tu. Wanaopigana sasahivi wametulia hiyo vurugu ilikuwa wiki iliyopita!
Nawashauri chadema watafute mbinu mbadala kukabiliana na ccm na sio kubishana na polisi, wananchi na wapiga kura wao watumia bure na kuwapa turufu ccm.
Mbona Tundu Lisu yuko tarime siku nyingi tu, kwani chadema hawana njia mbadala ya kufanya kampeni hadi iwe mkutano wa hadhara?
Mnakumbuka kauli ya Msekwa kule kiteto?!!!!
NARROW & BROAD CASTING CAMPAIGN!??
 
Basi mkuu hapo ndipo uzalendo wa diplomasia unaponishinda.Nimeisoma lakini bado kuna mazingira mengine inabidi ni-compromise na hii professional.Ina maana kwa mtaji huu mabadiliko kwa njia ya amani ni ngumu,CCM wasilzimishe hali ya machafuko.Kama ktk jimbo la tarime tu hawako tayari kuachia mamlaka,itakuaje kuhusu kuachia ikulu? CCM sasa inabidi wakue bwana,lazima waanguke kwa njia ya amani wasitake kulazimisha njia mbadala
 
Nina amini kuwa CCM ndiyo wenye dola kama watajaribu kufanya mchezo mchafu basi mtarajie mengi kujiri, naomba hilo liwe masikioni mwenu, tunajua watajitahidi kufanya wanaloweza, ila wajue maisha ya watanzania wa Tarime bado yako mikononi mwao.

Sisi kama wanatarime tunajua kuwa kupiga kura ni haki yetu ya msingi kikatiba na hivyo hatutegemei kuona tukipotosha na chochote kile, hii ikiwa ni pamoja na kujiepusha kupokea rushwa za vyama,

Tutamuhitaji kiongozi bora na si vingivevyo, mwenye uwezo wa kututetea watanzania
 
Dr Slaa,

Ushirikiano wa vyama ndio m-mesha uzika rasmi? if thats the case u can just forget abt winning Tarime
Masatu,
Sembuse ungelijua ninayoyajua sasa! Kwa bahati mbaya si tabia ya Chadema kwa unafiki wa aina yeyote ile. Tukishindwa Tarime ni kwa sababu nyingine wala si kwa kuachana na Ushirikiano. Nimeeleza kwingineko kuwa sasa tunaushahidi wa wazi. Hatuna sababu ya kuwa na ushirikiano na watu ambao usiku wanatuchoma visu.

Nimesema tuna video recording ya Mwenyekiti mmoja wa Ushirikiano, aliyemwita Mhariri wa Gazeti, tena linalomilikiwa na tuliyemtaja katika Listi ya Ufisadi, na "wakatunga" story ya Mbowe kuangusha Sherehe Tarime baada ya kupata Taarifa ya kifo. Unahitaji ushahidi gani zaidi! Mwenye macho na masikio haambiwi! Ni wakati sasa watanzania wakaelezwa kwa uwazi aina ya vyama tulivyonavyo hapa Tanzania.

Kuna Chama sasa hivi kimepewa fedha kwenda Tarime, na mtawasikia na kuwaona siku chache zijazo. Chadema huwa hatusemi bila kuwa na ushahidi mnajua. Tutatoa yote wakati ukifika. Lakini ujue kuwa hakuna sababu kujilazimisha katika ndoa ambayo umethibitisha kabisa haiwezekani.

Tungetaka kuweka ki theolojia tungeliiweka, lakini labda si mahali pake. Kwa kifupi hizi ni zile ndoa ambazo hata kwa wakatoliki zinakuwa "dissolved" kwa kuwa ni null and void Ab initio.
 
...its about time sasa na hakuna haja ya kufanya mambo nusu nusu,kama ushahidi upo weka mbele & make the case, wananchi wanapenda honest & straightalk na mtasaidia sana kukua kwa demokrasi na hakuna atakaye accuse mnafanya for political gain, huu ndio wakati wa kuweka kila kitu nje full force na sisi tutasaidia kuzi forward na kuzibandika kwenye youtube ili wananchi wajue ukweli na hata siku ya uchaguzi wawe clear wana vote upande gani.
 
Tutatoa yote wakati ukifika.

Mh.Dr. Slaa,
Kwanini msiyaseme sasahivi? kwani mnaogopa nini kama ushahidi mnao?

Isije ikatokea bahati mbaya mkakosa ushindi ndipo mkaanza kutueleza hayo mnayoyajua ambayo ama kwa hakika ni mambo ambayo yananuia kukiangusha chama chenu.

Ni vizuri kuweka wazi kwa wanachama wenu, wapenzi wa demokrasia na hata mashabiki wenu, yawezekana ikasaidia kubaini hila za ccm na washirika wake na hivyo wote kwa pamoja mkajipanga na kuhakikisha kuwa mnashinda.

Suala la msingi hapa ni ushindi kwanza hayo mengine ni mazungumzo baada ya habari.Hivi hamjifunzi kutokana na uzoefu mliopata Tunduru na Kiteto? au huko hamkujifunza kitu?Wekeni ma,bo hadharani mapema kama kuna mbinu yoyote chafu ijulikane na watu wajipange mapema kukabiliana nayo.

Nadhani utakuwa umenielewa mheshimiwa.
 
MWITA MARANYA

Mkuu kama watauweka ushaid hapa jamvini mapema, mbinu mbadala zitabuniwa na hivyo kuwapa kazi nzito kuzibaini, nadhani tuwape muda kisha wakati ukitimu watafanya hivyo, tunajua tunaelewa Sisiemu wanaweza kufanya wanaloweza hapa Tarime ila wawe makini, na kwa hilo wanajua.
 
kumekucha tarime siyo, ntawashangaa sana wananchi wa tarime kwenda kuichagua ccm wakati ikiwa kama serikali imeshindwa kucontrol vita za huko tarime, ni afadhali wagome kupiga kura kabisa kuliko kuichagua ccm.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom