Nyinyi si ndio wapagazi waaminifu wa RA.
Keep taking tablets.....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyinyi si ndio wapagazi waaminifu wa RA.
Mtanzania,
Uko right, but ninachopinga ni hii kasumba ya watu kutaka first hand information na wanapogundua kwamba wao walikua wrong kutokana na hawakuwa na back up data nzuri bado wanaendelea na misimamo yao.Yaani kasumba ya aina hii haitakaa ijenge hata siku moja.
Dr. Slaa alishalaani hizo vurugu,nadhani hata mkuu FMES alihisi labda kuna kipengele hasa kile cha kulaani hizo vurugu watu walishindwa au kwa makusudi waliamua kutokiona katika maelezo ya Dr. Slaa,ikabidi akiweke separately but ilishangaza kuona bado kuna watu wamegoma kubadili walicho nacho akilini.
Je,mkuu ulitaka Dr.slaa alaaani tu hizo vurugu bila kuongelea makosa aliyofanya Dr.Mvungi? Is this not a doble standard?
Mazingira ya vurugu za CCM kule Kiteto ilikua ni tofauti kabisa na ya huko Tarime.Hilo hasa ndilo kosa kubwa sana la wanasiasa wengi hapo nyumbani,hawana uwezo wa kusoma saikolojia ya audience.Na hili suala la CCM kutumia vyombo vya dola lina mwisho wake,Very soon watakoma kama walivyokoma kunyonya ziwa la mama.
Sisi ndio wananchi tunaolipa kodi za kuwalipa hao FFU wanaotumika against sisi,ipo siku watakabiliana na action movement wakidhani wanakuja kuwanyanyasa walalahoi maanake hata matumizi ya FFU kwa interest zao imeshahalalishwa hadi kufikia hatua wanawita vijana wao.Ila jambo moja la msingi hata hao FFU inafaa watambue kwamba wao ni sehemu ya Tanzania na ni ndugu zetu.Vuguvugu la kimapinduzi au Radical Changes hata siku moja halitashindwa na vyombo vya dola.Historia inasema hivyo,ni ukweli mchungu kwa wengine but that is the fact!
Ni kweli Dr. Slaa kalaani hizo vurugu, lakini kusema Dr. Mvungi alaumu ulimi wake mwenye na wala sio hao wananchi waliompiga mawe inaondoa kabisa kule kulaani alikofanya.
Nimesoma ujumbe wa Dr. Slaa mara nyingi na bado naondoka na hisia ile ile ya kwamba anahalalisha kupigwa kwa Dr. Mvungi kwa kisingizio cha kwamba alikuwa anahutubia uongo. Kulaani kwa mwanzoni inakuwa kama machozi ya mamba.
Ben,
Ni kweli Dr. Slaa kalaani hizo vurugu, lakini kusema Dr. Mvungi alaumu ulimi wake mwenye na wala sio hao wananchi waliompiga mawe inaondoa kabisa kule kulaani alikofanya.
Huwezi kuchanganya hayo mambo mawili kwa pamoja.
Ana haki ya kumlaumu Dr. Mvungi kuongea maneno ya uwongo lakini hana haki kumwambia kupigwa kwake ajilaumu mwenyewe.
Naheshimu mchango wa Dr. Slaa kwenye haya mapambano ila kama mwanasiasa na kiongozi
ni muhimu kutokuchanganya hayo mambo mawili. Hata mtu akikosea dawa sio kupigwa.
Je CCM wakivamia mkutano wa CHADEMA na kuwapiga viongozi kwa visingizo vya kwamba mlikuwa mnawatukana kwamba ni mafisadi, je mtafanya nini? Mtalaani?
Nimesoma ujumbe wa Dr. Slaa mara nyingi na bado naondoka na hisia ile ile ya kwamba anahalalisha kupigwa kwa Dr. Mvungi kwa kisingizio cha kwamba alikuwa anahutubia uongo. Kulaani kwa mwanzoni inakuwa kama machozi ya mamba.
Mgawanyiko wa upinzani hautokani na ubaya wao. Unatokana na jinsi ambavyo zoezi la kuwachonganisha na kuwadhoofisha linavyofanywa na CCM. Kama wakifanikiwa kuepuka mbinu za CCM basi watakuwa salama. Lakini ipo kazi kubwa.
Nawatia moyo CHADEMA kusonga mbele. Hata kama kuna ghiliba kubwa namna gani bado nafasi ya kushinda ipo. Tarime sio wajinga wa kubebwa hovyo na rushwa na kuuza shahada zao za kupigia kura.
SONGENI MBELE CHADEMA MTASHINDA.
Kisiki cha CHADEMA sio CUF,NCCR wala TPL bali ni CCMSONGENI MBELE CHADEMA MTASHINDA.
Wakuu,
Hivi CHADEMA wakifanya mkutano na ikatokea vurugu ni nani Wa kulaumiwa?
Kuna wale wakuu wangu wenye allergy na double standards kwenye siasa sasa hili la polisi kuwazuia CHADEMA huku wakiruhusu CCM siku mbili kabla tena kwa kutoa full support ya ulinzi mnaonaje hapa?
Halafu vipi huyo bwana Mwera anakubalika kiasi gani huko Tarime?
Wakuu,
Hivi CHADEMA wakifanya mkutano na ikatokea vurugu ni nani Wa kulaumiwa?
Kuna wale wakuu wangu wenye allergy na double standards kwenye siasa sasa hili la polisi kuwazuia CHADEMA huku wakiruhusu CCM siku mbili kabla tena kwa kutoa full support ya ulinzi mnaonaje hapa?
Halafu vipi huyo bwana Mwera anakubalika kiasi gani huko Tarime?
Masatu,Dr Slaa,
Ushirikiano wa vyama ndio m-mesha uzika rasmi? if thats the case u can just forget abt winning Tarime
Masatu,
Sembuse ungelijua ninayoyajua sasa! Kwa bahati mbaya si tabia ya Chadema kwa unafiki wa aina yeyote ile. Tukishindwa Tarime ni kwa sababu nyingine wala si kwa kuachana na Ushirikiano. Nimeeleza kwingineko kuwa sasa tunaushahidi wa wazi. Hatuna sababu ya kuwa na ushirikiano na watu ambao usiku wanatuchoma visu.
Nimesema tuna video recording ya Mwenyekiti mmoja wa Ushirikiano, aliyemwita Mhariri wa Gazeti, tena linalomilikiwa na tuliyemtaja katika Listi ya Ufisadi, na "wakatunga" story ya Mbowe kuangusha Sherehe Tarime baada ya kupata Taarifa ya kifo. Unahitaji ushahidi gani zaidi! Mwenye macho na masikio haambiwi! Ni wakati sasa watanzania wakaelezwa kwa uwazi aina ya vyama tulivyonavyo hapa Tanzania.
Kuna Chama sasa hivi kimepewa fedha kwenda Tarime, na mtawasikia na kuwaona siku chache zijazo. Chadema huwa hatusemi bila kuwa na ushahidi mnajua. Tutatoa yote wakati ukifika. Lakini ujue kuwa hakuna sababu kujilazimisha katika ndoa ambayo umethibitisha kabisa haiwezekani.
Tungetaka kuweka ki theolojia tungeliiweka, lakini labda si mahali pake. Kwa kifupi hizi ni zile ndoa ambazo hata kwa wakatoliki zinakuwa "dissolved" kwa kuwa ni null and void Ab initio.
Tutatoa yote wakati ukifika.
Mh.Dr. Slaa,
Kwanini msiyaseme sasahivi? kwani mnaogopa nini kama ushahidi mnao?
Isije ikatokea bahati mbaya mkakosa ushindi ndipo mkaanza kutueleza hayo mnayoyajua ambayo ama kwa hakika ni mambo ambayo yananuia kukiangusha chama chenu.
Ni vizuri kuweka wazi kwa wanachama wenu, wapenzi wa demokrasia na hata mashabiki wenu, yawezekana ikasaidia kubaini hila za ccm na washirika wake na hivyo wote kwa pamoja mkajipanga na kuhakikisha kuwa mnashinda.
Suala la msingi hapa ni ushindi kwanza hayo mengine ni mazungumzo baada ya habari.Hivi hamjifunzi kutokana na uzoefu mliopata Tunduru na Kiteto? au huko hamkujifunza kitu?Wekeni ma,bo hadharani mapema kama kuna mbinu yoyote chafu ijulikane na watu wajipange mapema kukabiliana nayo.
Nadhani utakuwa umenielewa mheshimiwa.