Mtanzania heshima yako,
Jambo la msingi la kuzingatia katika suala la mapigano ya hizi koo Mbili Warenchoka vs Wanchari, ni matokeo ya serikali kushindwa kuwalinda wanachi wake na kuwapatia usalama.Ugomvi wa hawa watu kwa sehemu kubwa umejikita katika historia.Na kwa bahati mbaya sana, inawezekana serikali inajua ama kutojua ni kuwaachia madaraka makubwa ya maamuzi wazee,wakurya tunawaita wazee wa kimila.
hawa wazee wanaheshimika sana na kuogopwa sana. Kwa mfano wakitangaza kuwa leo hakuna kwenda shambani hakuna mtu anyeweza kukiuka maagizo hayo.Kwahiyo basi inapotokea wezi kutoka ukoo mmoja wakaiba mifugo (sanasana ng'ombe) kutoka upande wa pili, kawaida kuna kitu tunaita kufuatilia nyayo(hapa hupigwa yowe ili wanaume wote wajitokeze na kwenda kuwatafuta hao ng'ombe walioibiwa).
Sasa katika kufuatilia hiyo nyayo ikiingia katika kijiji cha ukoo mwingine hapo ndipo balaa linaapoanzia. Mara nyingi hutokea nyayo ikifika upande wa pili hawa wafuatiliaji huzuiwa kuendelea na zoezi lao au kukuta kuwa baada ya kufika upande wa pili nyayo zimetawanyika kwa maana ya kwamba ng'ombe wamegawanywa.
Kinachotokea hapo walioibiwa huijulisha polisi kwa upelelezi na hatua nyingine.Lakini kwa uzoefu polisi hawafanikiwi kuwarudisha ng'ombe walioibwa,na hivyo basi wazee wa kimila huwataka vijana walipize kisasi kwakuwa haiwezekani ng'ombe wao waende hivihivi.Hapo sasa ndipo mapigano yamekuwa yakijirudia kila kukicha.Ni vizuri kujua kuwa mgawanyo wa vijiji mwaka 1974 wakati wa operation vijiji, kila ukoo wa kikurya ulipangiwa kijiji/vijiji vyake. Kwa maana kwamba wahunyaga, wamera, wanchari, warenchoka,watimbaru,wanyabasi,wairege,wajaluo n.k kila watu wanaishi katika vijiji vyao wenyewe.
Kwa ufupi niseme tu kwamba nimejaribu kuwapa picha kamili wale wasioifahamu tarime jinsi tunavyoishi.
Kwa maoni yangu serikali inabeba lawama zote kwa sababu zifuatazo:
1. Imeshindwa kupeleka polisi maeneo hayo muda wote ili kukomesha mlipuko wa mapigano ya kila mara na badala yake imejaza polisi eneo la nyamongo katika mgodi wa north mara ili kulinda maslhi ya wakwapuaji wa barrick.Na hapo ndipo makali yao yanapoonekana.Ukionekana tu unakaribia uzio wa barrick ni kipigo tu.
2.Imeshindwa kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa utawala wa sheria na badala yake kuwaachia wazee wa kimila ambao hakuna upande utakao kubali kushindwa daima dumu!