Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
kumekucha tarime siyo, ntawashangaa sana wananchi wa tarime kwenda kuichagua ccm wakati ikiwa kama serikali imeshindwa kucontrol vita za huko tarime, ni afadhali wagome kupiga kura kabisa kuliko kuichagua ccm.

Acha hizo weweee!wananchi wa Tarime wasipige kura ili ccm wajitwalie jimbo kibwege namna hiyo?kama ni ushauri basi huu wako ni ushauri mbaya kuliko kitu chochote.

hivi we hujui kuwa ccm na ZANU PF ya mugabe ngoma droo!au umesahau jinsi mugabe alivyojitangazia ushindi wa kishindo baada ya Tsvangirai kujitoa?

Suala la msingi ni kuhakikisha kuwa mgombea wa upinzani atakayeonekana anakubalika na anafaa kuwawakilisha wanatarime apewe full support ili ashinde uchaguzi.

Kugoma kupiga kura ni sawa na kumsusia nguruwe shamnba la mihogo!kama hujui ubaya wa kumsusia nguruwe shamba la mihogo kawaulize MDC ya zimbabwe.

kwa ajili ya ku-maintain idadi ya wabunge wa upinzani bungeeni lazima tushirikiane ili jimbo la tarime liendelee kuwa mikononi mwa chama cha upinzani na wala sio kwa mafisadi!
 
Wakuu,

Mimi naomba somo, samahani kama nimetoka nje ya hoja hii. Hivi kwanini hizo koo nne zinapigana?

Je juhudi zote za kuleta amani zimenishindikana na kwanini?

Inasikitisha inapoonekana watu wanapigana na kuuana, serikali inaona mambo kama business as usual.

Watu wa Tarime hivi na ushujaa wenu wote wa kuleta mabadiliko, mnashindwa kutatua tofauti zenu wenyewe?

Onyesheni mapinduzi na uzalendo wenu kwa kutenda haki na kuleta amani kwa wananchi wenzenu wa Tarime.

Ukimpiga panga ndugu yako wa Tarime huku unasema utaleta umoja wa TZ wapi na wapi? Umoja unaanzia nyumbani.

Akina Mwita leteni mabadiliko ya kweli Tarime.
 
Isayamwita,

Kiteto mungeliweka gogo pia labda lingeshinda. Ndio maana CCM wanashinda kirahisi, kuna watu wanashindwa hata kukubali the reality na matokeo yake badala ya kutafuta mbinu za kupambana na CCM wanabaki kushinda kwenye vijiwe wakiamini CCM wataanguka.

Sitashangaa CCM wakishinda Tarime safari hii hasa kama Prof. Wangwe ndiye atakuwa mgombea wao.

Hata kama CCM itamsimamisha Prof. Wangwe still watakuwa na kazi yz ziada ya kuwashawishi watu wa TARIME. Kumbukeni aliye lala usimwammshe ukimwamsha utalala wewe, sasa hivi watu wa Tarime wanataka ripoti zote mbili za Madaktari zitolwe ili wajue Mpendwa wao walikufaje halafu eti kwa sababu ni KAKA MTU ndio wam,pitishe kiurahisi hivyo...

Ushauri wa bure kwa Prof. Wange aachane na siasa afundishe wananchi ambao ni taifa linalotegemewa huu mchezo mchafua anao taka ku uanza utamweka pabaya...
TARIME wanauchungu wa nduguzao waliokamatwa na hawajulikani walipo eti walivamia mgodi wa NORTH MARA wakati mpigania haki wao akiendleza libeneke WAKAMZIMA hii dhambi ya kumzima haitaisha.. NATAMANI MZUKA WAKE UWATOKEE WOTE WALIOHUSIKA NA KIFO CHAKE HADI WATAKAPO JITANGAZA HADHARANI! RIP CHACHA WANGWE
 
Wakuu,

Mimi naomba somo, samahani kama nimetoka nje ya hoja hii. Hivi kwanini hizo koo nne zinapigana?
Je juhudi zote za kuleta amani zimenishindikana na kwanini?

Inasikitisha inapoonekana watu wanapigana na kuuana, serikali inaona mambo kama business as usual.

Watu wa Tarime hivi na ushujaa wenu wote wa kuleta mabadiliko, mnashindwa kutatua tofauti zenu wenyewe?

Onyesheni mapinduzi na uzalendo wenu kwa kutenda haki na kuleta amani kwa wananchi wenzenu wa Tarime.

Ukimpiga panga ndugu yako wa Tarime huku unasema utaleta umoja wa TZ wapi na wapi? Umoja unaanzia nyumbani.

Akina Mwita leteni mabadiliko ya kweli Tarime.

Serikali yetu haiwajibiki kwa wananchi, wao mradi wanatawala na kupata ulaji tu. Tarime kumekuwa na vita vya koo kati ya Warenchoka na Waanchari kwa muda mrefu, ati serikali imeshindwa kuwapatanisha! Hivi karibuni vimeibuka vita kati ya koo mbili nyingine (nje ya watani wa jadi-Walenchoka Vs Waanchari) lakini serikali inafanya kazi kigoigoi kukoomesha vita hivyo.

Maalbino wanauawa Serikali inabweka tu kama Mbwa koko! Mwandishi asiyekuwa hata na ujuzi wa Kishushushu kama Usalama wa Taifa na CID-Polisi anafanikiwa kuwajua Wauaji, ati Serikali (yenye mkono mrefu) inashindwa kuwakamata! Wapemba walipoisimamia Serikali cha moto walikiona!

Yaani provided maslahi ya Watawala hayaguswi, piganeni na uaneni lakini mkigusa asali yao tu moto utawaakia.
.
Tuendelee na Mada ya Ubunge Tarime hilo umeshajibiwa
 
Mdogo wa Wangwe aihama CHADEMA

*Agombea udiwani NCCR-Mageuzi

Na Gaudence Massati

ALIYEKUWA Mratibu wa uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani Tarime David Wangwe 'Osama' amejitokeza kuwania nafasi ya udiwani wa Kata ya Tarime mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.

Akizungumza kwenye ofisi za gazeti hili jijini Dar es Salaam jana Wangwe ambaye ni mdogo wa aliyekuwa diwani wa kata hiyo na Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe, alisema kuwa ameamua kuwania nafasi hiyo ili kuziba kikamilifu pengo lililoachwa na kaka yake.

Wangwe alisema, hata hivyo amelazimika kuihama CHADEMA na kwenda NCCR-Mageuzi baada ya kuona chama hicho kimeanza kupoteza uelekeo uliojengwa na wanachama wake kwa nguvu na muda mwingi wilayani Tarime.

"Mimi nilikuwa mratibu wa uchaguzi Chadema wilayani Tarime kwa miaka minne, tumefanya kazi kubwa kukijenga chama kule, lakini sasa naona kinapoteza muelekeo na malengo yake kwa wananchi wa Tarime, imani imepungua,"alisema Wangwe.

Alisema kuwa alichukua fomu za kuwania nafasi hiyo Septemba 4, mwaka huu na kwamba iwapo chama chake kitampitisha atahakikisha anashirikiana kikamilifu na wana Tarime kuhakikisha kata hiyo muhimu inabaki kambi ya upinzani.

Uchaguzi huo mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu unakuja kufuatia kifo cha Chacha Wangwe aliyekuwa diwani wa kata ya Tarime mjini na mbunge wa jimbo la Tarime kilichotokea kwa ajali ya gari hivi karibuni.
 
Wakuu,

Mimi naomba somo, samahani kama nimetoka nje ya hoja hii. Hivi kwanini hizo koo nne zinapigana?

Je juhudi zote za kuleta amani zimenishindikana na kwanini?

Inasikitisha inapoonekana watu wanapigana na kuuana, serikali inaona mambo kama business as usual.

Watu wa Tarime hivi na ushujaa wenu wote wa kuleta mabadiliko, mnashindwa kutatua tofauti zenu wenyewe?

Onyesheni mapinduzi na uzalendo wenu kwa kutenda haki na kuleta amani kwa wananchi wenzenu wa Tarime.

Ukimpiga panga ndugu yako wa Tarime huku unasema utaleta umoja wa TZ wapi na wapi? Umoja unaanzia nyumbani.

Akina Mwita leteni mabadiliko ya kweli Tarime.

Mtanzania heshima yako,

Jambo la msingi la kuzingatia katika suala la mapigano ya hizi koo Mbili Warenchoka vs Wanchari, ni matokeo ya serikali kushindwa kuwalinda wanachi wake na kuwapatia usalama.Ugomvi wa hawa watu kwa sehemu kubwa umejikita katika historia.Na kwa bahati mbaya sana, inawezekana serikali inajua ama kutojua ni kuwaachia madaraka makubwa ya maamuzi wazee,wakurya tunawaita wazee wa kimila.

hawa wazee wanaheshimika sana na kuogopwa sana. Kwa mfano wakitangaza kuwa leo hakuna kwenda shambani hakuna mtu anyeweza kukiuka maagizo hayo.Kwahiyo basi inapotokea wezi kutoka ukoo mmoja wakaiba mifugo (sanasana ng'ombe) kutoka upande wa pili, kawaida kuna kitu tunaita kufuatilia nyayo(hapa hupigwa yowe ili wanaume wote wajitokeze na kwenda kuwatafuta hao ng'ombe walioibiwa).

Sasa katika kufuatilia hiyo nyayo ikiingia katika kijiji cha ukoo mwingine hapo ndipo balaa linaapoanzia. Mara nyingi hutokea nyayo ikifika upande wa pili hawa wafuatiliaji huzuiwa kuendelea na zoezi lao au kukuta kuwa baada ya kufika upande wa pili nyayo zimetawanyika kwa maana ya kwamba ng'ombe wamegawanywa.

Kinachotokea hapo walioibiwa huijulisha polisi kwa upelelezi na hatua nyingine.Lakini kwa uzoefu polisi hawafanikiwi kuwarudisha ng'ombe walioibwa,na hivyo basi wazee wa kimila huwataka vijana walipize kisasi kwakuwa haiwezekani ng'ombe wao waende hivihivi.Hapo sasa ndipo mapigano yamekuwa yakijirudia kila kukicha.Ni vizuri kujua kuwa mgawanyo wa vijiji mwaka 1974 wakati wa operation vijiji, kila ukoo wa kikurya ulipangiwa kijiji/vijiji vyake. Kwa maana kwamba wahunyaga, wamera, wanchari, warenchoka,watimbaru,wanyabasi,wairege,wajaluo n.k kila watu wanaishi katika vijiji vyao wenyewe.

Kwa ufupi niseme tu kwamba nimejaribu kuwapa picha kamili wale wasioifahamu tarime jinsi tunavyoishi.

Kwa maoni yangu serikali inabeba lawama zote kwa sababu zifuatazo:

1. Imeshindwa kupeleka polisi maeneo hayo muda wote ili kukomesha mlipuko wa mapigano ya kila mara na badala yake imejaza polisi eneo la nyamongo katika mgodi wa north mara ili kulinda maslhi ya wakwapuaji wa barrick.Na hapo ndipo makali yao yanapoonekana.Ukionekana tu unakaribia uzio wa barrick ni kipigo tu.

2.Imeshindwa kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa utawala wa sheria na badala yake kuwaachia wazee wa kimila ambao hakuna upande utakao kubali kushindwa daima dumu!
 
Mwita,

Asante sana kwa taarifa za ndani. Inasikitikisha sana pale serikali inapofikia hatua ya kuliacha tatizo liendelee.

Hapa duniani hakuna tatizo lisilo na solution, muhimu ni wahusika kufanya juhudi za wazi. Kama ANC na Makaburu waliongea na amani kupatikana, je kweli sisi tunashindwa kuwafanya watu wetu tena wa wilaya moja wafikie makubaliano?

Hapo kuna mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, wabunge, jeshi la polisi nk. Kweli wote wameshindwa kuona umuhimu wa kuzuia vifo vya raia wetu?

Afrika wakati mwingine tunasikitisha sana.
 
..binafsi nimesikitika kwamba Dada Esther Matiko hakupewa nafasi na Chadema kugombea Ubunge wa Tarime.

..umefika wakati tuwathamini dada zetu na kuwapa nafasi za Uongozi.

Mwita Maranya,

..lakini Jeshini na Polisi si kuna Wakurya wengi tu. sasa hao hawatachanganyikiwa na kujiingiza kwenye mapigano ya koo?

..lawama zinapaswa kwenda kwa wana Tarime pia manaake inaelekea kuna ka-element ka kupenda vurugu na magomvi.
 
Jokakuu,
Serikali inao uwezo wa kukomesha mapigano ya koo za wakurya tarime na watu tukasahau kabisa habari ya warenchoka vs wanchari.

Nikufahamishe tu kwamba kabila la wakurya limeenea kwa kiwango kikubwa katika wilya za Tarime, Serengeti na Bunda. Musoma wapo lakini wachache kulinganisha na wilaya nyingine.

Mwishoni mwa miaka ya 80 hadi 90 kulikuwa na mapigano makali sana wilayani serengeti kati ya koo za wakira + warenchoka vs wanyabasi + watimbaru.

Mapigano hayo yalidumu kwa muda mrefu na yaliendelea kushika kasi hadi yakaanza kuwagusa ukoo wa wangoreme, yakavuka hadi kwa wairege(hawa wako tarime).Sababu kubwa ya mapigano haya ilikuwa ni wizi wa mifugo hasa ng'ombe(kwa asili wakurya ni wafugaji) na hadi leo ndio shughuli kubwa wanayoifanya pamoja na kilimo.

Lakini ilipofikia mahali serikali ikaamua mapigano hayo yalikoma hadi leo hakuna suala la mapigano ya koo za wakurya. Na wizi wa mifugo kwa kiasi kikubwa sana umedhibitiwa. Hiyo iliwezekana kwani serikali ilipeleka serengeti kikosi maalum(inasemekana walikuwa ni wanajeshi) kilichoongozwa na kamanda mmoja aliyejulikana sana kama KUBIHA(naambiwa sasahivi amestaafu utumishi wa umma lakini amepata ajira ICTR Arusha). Walipita kijiji kimoja hadi kingine. Kwakuwa walikuwa na majina ya wezi sugu, walipofika tu walianza kuwashughulikia wezi kwanza kama mwezi mzima hivi,wakatajana wote waliokuwa wakishirikiana kuendesha wizi wa ng'ombe na wakakamatwa na kushughulikiwa kisawasawa.

Baada ya hapo kila kijiji kiliitisha mkutano na zikapigwa kura za siri kuwabaini wezi wa mifugo.Waliotajwa na kubainika kuhusika na wizi huo walikabidhiwa mikononi mwa hicho kikosi cha kazi, kikawashughulikia hadi wakanyooka.

Jambo jingine la msingi wazee wa kimila hawakuendelea kuwa na nguvu za maamuzi kama awali.Ingawa suala la utawala bora na utawala wa sheria na kuzingatiwa kwa haki za binadamu wilayani serengeti si wa kuridhisha lakini hakuna tena mapigano ya koo za wakurya na sasahivi serengeti inakuja juu vizuri kimaendeleo.

Narudia kauli yangu kuwa serikali haijatekeleza wajibu wake ipasavyo katika kulinda usalama wa raia wake na mali zao.
 
Mwita,

Nakubaliana na lawama zako kwa serikali lakini pia kama alivyosema JokaKuu, wananchi pia mmeshindwa kutimiza wajibu wenu kama raia.

Tusisubiri wakati wote mpaka serikali ndio ije itutatulie matatizo yetu. Inatakiwa hata sisi wananchi tusiruhusu ujinga kama huo kusumbua raia wema. Tunaweza kutatua tatizo na kisha tukaiwajibisha serikali kupitia uchaguzi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Nashangaa hayo mapigano yapo miaka na miaka, inatakiwa ifike mahali wananchi wenyewe ambao ndio mnadhurika mseme enough is enough na kuandaa taratibu za kudumu za kushughulikia matatizo hayo.
 
Mtanzania,
Pamoja na mapigano hayo kuwa ni ya ukoo mmoja dhidi ya mwingine,ukweli ni kuwa hawa wezi wa ng'ombe hawana uadui hata kidogo!wao wanawasiliana kama kawaida na ndio wanopeana 'deal' za kuibiana ng'ombe.

Mwizi mrenchoka akifanikisha wizi kutoka upande wake,kinachofuata ni mwizi munchari kufanikisha wizi kutoka upande wao na kumpa mwenzake wa upande wa pili.

Na mara nyingi ng'ombe wanaoibwa huvushwa na kwenda kuuzwa nchi jirani hususan umasaini,(ikumbukwe vijiji hivi viko mpakani mwa nchi yetu).Kuna sehemu moja hapo nchi jirani(NAROK kama naikumbuka vizuri) ni maarufu sana kwa ununuzi wa ng'ombe wa wizi kutoka Tanzania.

Mara nyingi hawa wezi wana utaratibu wa kuwagawia wazee wa kimila ng'ombe na wao huchinja na kula nyama huku wakijipongeza na kuwasifu vijana kwa kazi nzuri.Kwa asili mkurya sio mtu wa kukubali kushindwa kirahisi.Ukimshinda leo,kesho atajaribu kulipa kisasi na keshokutwa hadi atakaporidhika na hususan kunapokuwa na msukumo wa maagizo ya wazee wa kimila ambao ndio wenye 'final say' hapo hakuna kushindwa.Nilisema hapo mwanzo kuwa haya mapigano yana mkono wa historia na yana mkono wa wananchi wenyewe kama jamii lakini pia yana mkono wa serikali kama mhimili wa amani na usalama wa watu hawa.

Huyo kamanda niliyemtaja hapo juu aliyeendesha operation kali wilayani serengeti mwaka 1990 kwa kipindi cha miezi kati ya mitatu hadi sita hivi na wizi wa mifugo ukaisha matokeo yake mapigano yakaisha. Ilifikia kipindi wezi wenyewe wakawa wanajisalimisha wenyewe,tena kipindi hicho watu wengi walikuwa wanamiliki silaha za moto ambazo hawakuzipata kihalali. Watu walikuwa wanasalimisha bunduki wenyewe kwa kuhofia mkono wa kamanda KUBIHA.

Labda nitoe ushauri mwingine kwa serikali yetu,labda imtafute tena bwana Kubiha imkabidhi hiyo kazi naamini anaweza kumaliza hizo vurugu kabisa na ikabaki historia.
 
Hakika kumekucha, hawa askari mbona wengi jamani huku Tarime? nadhani kila askari atakabiliana na raia mmoja, hawa fanya fujo uone(FFU) MBONA WAMEMWAGWA HADI TUNASHINDWA PA KUHEMEA? hapa ipo kazi, kazi tunayo, kweli ushindi ni wa CCM kwa mtindo huu, lakini hatutakufa moyo tutaendelea hadi kieleweke.

Nadhani hii imefanyika kwa makusudi tu ili tuogope lakini ....., haki itasimama.
 
Wala usiwe na shaka wakwetu,

Hiyo ya kumwaga FFU ni kawaida ya CCM wanapohisi uwezekano wa kupata ushindi ni mdogo sana.Wanajua kuwa tarime ni vigumu wao kupata ushindi kihalali, kwahiyo lazima watumie mabavu ili kujitangazia ushindi.

Lakini hakuna haja ya kukata tamaa, muhimu ni kuendelea kuhamasishana na hatimaye siku ya uchaguzi watu wajitokeze kwa wingi kumchagua mwakilishi atakayekuwa na jeuri ya kutetea maslahi ya wanatarime. Kuchagua ccm ni kuchagua kuzika maslahi ya wanatarime.Mbunge kutoka ccm hawezi kuwakilisha maslahi ya wananchi,atawakilisha maslahi ya ccm. Kwani katiba yao (ccm) haiwaruhusu kutetea maslahi ya nchi bali mafisadi!

Ukitetea maslahi ya nchi wanaku-NAPE! Eti kwa utovu wa nidhamu!
 
Isaya Mwita said:
Kwa asili mkurya sio mtu wa kukubali kushindwa kirahisi.Ukimshinda leo,kesho atajaribu kulipa kisasi na keshokutwa hadi atakaporidhika na hususan kunapokuwa na msukumo wa maagizo ya wazee wa kimila ambao ndio wenye 'final say' hapo hakuna kushindwa.

Isaya Mwita,

..mzizi wa hili tatizo ni huo utamaduni ulioelezea hapo na mimi nimeunukuu.

..umeeleza kwamba miaka ya 90 mlipatiwa askari na nguvu za dola zikasimamisha mapigano. mlitakiwa wananchi muendeleze amani na ujirani mwema wenyewe kuanzia hapo.

..leo hii ukija kulalamika kwa serikali, ni kana kwamba ulitarajia FFU wawe stationed huko milele na milele amina.

..Spirit ya kutokukubali kushindwa mnapaswa muielekeze masuala yenye kuleta maendeleo, siyo kuwarudisha nyuma.

..nina mashaka sana kama nguvu za dola zinaweza kuwaletea amani. dola inaweza kugawa dawa kuzuia milipuko kama kipindupindu, lakini kama wananchi wenyewe hawazingatii kanuni za usafi na afya basi gonjwa hilo halitaondoka ktk jamii husika.

..ushauri wangu kwa wana-Tarime ni kuzingatia kanuni za USALAMA na UJIRANI MWEMA.
 
Salaam tokea Tarime .Mambo si shwari na CCM sasa wameamua kufanya yale yaliyo tegemewa .Nimeshuhudia Tossi leo na kikao kikubwa hapa Tarime na Kova anategemea kutinga muda wowote ili kuhakikisha CCM wanapata jimbo hili .Hii ni baada ya wana Tarime kumkataa Kangoye Ryoba ambaye anabebwa na Makamba na Gachuma ambao wamesema ni mtu wao na lazima apite .Wana Tarime wanasema wana imani na Charle Mwela baada ya CCM kumkataa kipenzi wao Nyambali Nyangwire .Ukweli upo maana Dodoma kumekuwa kimya kwa siku 2 hadi jioni hii walipo amua kumoa Kangoye wa TRA kisa yeye na gachuma ni damu damu na Makamba yeye ni omba omba anajua chake cha juu kiko wazi .

Jeshi la Polisi linafanya kufuru sasa maana leo pekee wameletwa 300 na wiki hii wanategemea wengine 600 zaidi kwa jina la vurugu za kikabila lakini ukweli ni kwamba jimbo la Tarime lirudi CCM ndiyo nia yao .JK na Mwema yetu macho na tuna waangalia kwa makini sana .Chadema bado wana uwezo mkubwa wa kulitwaa jimbo hili kwa mujibu wa uchunguzi wangu na imekuwa tishio hadi Tossi na Kova kuaminiwa kuja kulirudisha jimbo .
 
Lunyungu unachemka! hivi kuna tatizo gani vyombo vya ulinzi na usalama kuwepo hapo ilhali hali ya Tarime ni tete? If anything hiyo ni blessing na uhakika wa usalama acha spin zako
 
Lunyungu unachemka! hivi kuna tatizo gani vyombo vya ulinzi na usalama kuwepo hapo ilhali hali ya Tarime ni tete? If anything hiyo ni blessing na uhakika wa usalama acha spin zako

Wewe nani kakwambia hali ya Tarime ni tete? Ni yale yale ya Mbowe kufukuzwa na mapanga na mikuki.
 
Masatu am right here na naijua hali halisi hakuna cha utete wala nini .Mnatumia maneno haya kila siku kuhalalisha mambo ya kipuuzi .Hali tete inaanza leo wakati muhimu kama huu ? Kova Dar anamwachia nani ?Tossi umeona mambo yake ? Mbona tuko Tarime hatuoni vurugu wala kufukuzana badala yake kuona polisi wamevalia kijeshi muda wote na kuranda mitaani ? kuna vurugu ipi hapa kwa muda huu na imeanza lini ?
 
Mvungi alijitakia mwenyewe. Huu ugomvi wa Wanyanchare sijui na akina nani wale umekuwepo muda mrefu tu mbona FFU hawakupelekwa. Sasa wakati uchaguzi mdogo unapokaribia ndipo mnapeleka jeshi la CCM?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom