Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Katika hali ya kuashiria kuwepo na kutokubalika kwa CHADEMA huko Tarime, Kamati maalumu ya Ushindi ya CHADEMA iliyokutana jana usiku imepanga kutumia njia ya chama cha CUF waliyoitumia kulipata jimbo la mji mkongwe huko Zenj.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo wa siri ambae amepewa jukumu la kukusanya vijana ili kuleta vurugu katika kila mkutano wa kampeni wa vyama vingine alinukuliwa akisema hayo wakati akiwashawishi baadhi ya vijana wa kata ya makoroboi huko Mwanza.

Mpango mzima utaanza kwa kuifanyia fujo kubwa chama cha DP ambacho kinategemewa kuanza kampeni zake mapema wiki ijayo. Zaidi imefahamika njia itakayotumika ni kuandika mabango ya kejeli, kutumia mawe fimbo na mapanga kwa wananchi ambao watakuwa wanakwenda kwenye mikutano ya kampeni.

Hadi hivi sasa kuna juhudi kubwa inayofanywa ya kuwaunganisha vijana hao wa Mwanza na baadhi ya vijana wa Tarime ili kufanikisha harakati hizo za kuleta vurugu.
 
kibunango! mkuu acha kuwapotosha wana JF walio mbali na Mwanza. Vijana wa Mabatini, Mirongo na Pasiansi walioandaliwa na CCM kwa ajili ya kwenda Tarime walikuwa hajui nini kina endelea zaidi ya kuambiwa kuna mshiko wa 20,000/ kila mmoja. Kwa taarifa yako baada ya kusikia fedha aliyopewa Makamba wameshtuka na sijui wataamua nini maana wameshtukiawanavyo fanywa wajinga.Kama kuna wakumpiga Mtikila basi ni kauli zake za kuchanganya mambo na si Chadema.Ila narudia ,Watarime walishasahau na kumshukuru Mungu kwa msiba wa Wangwe (RIP) kama Mtikila anaona hiyo ni ajenga ,mwache aende nayo.ATAWAKUMBUKA MABWANA ZAKE kwa yatakayomkuta. Njaa ukiiendekaza wenda shimoni
 
Hapa tukumbushane kwa hilolinawezekana kufanyika nakumbuka katika miaka sio ya zamani wakti Dr salmin amour juma akiwa rais wa zanzibar wakati wa uchaguzi john malichela alikuwa akihutubia kule tanga na kuwambia vijana nendeni zanznibar mkafanye fujo na kusema kuwa hapa sikumbuki alitumia chama au serekali itakulindeni haitasahauli hilo kuna msemo usemao Mtenda husahau mtendewa hasahau.nawaombea salama na Mungu awaepushie ndugu zetu wa Tarime sahari CCM kama ndio wamepanga hilo
 
Jana niliona jinsi ambavyo Chadema walizindua kampeni, nilifurahi sana. Nikiwa kama mwanachama mfu wa CCM ambaye mwaka huu nimeamua kutolipia kadi yangu kutokana na chama kuwa Dodoki na kuiacha misingi ya kupigania masilahi ya wakulima na wafanyakazi nawaomba wananchi wa Tarime wasiukumbatie ufisadi na kukipa chama changu cha CCM kura.

Mlioko huko hebu tupatieni updates juu ya nini kinajili huko
 
Ile ndoa ya upinzani iko wapi? kwani hapo ndio naona upinzani umeanza kurudi nyuma kwani muungano wa upinzani na kuweka mgombea mmoja ilikuwa tishio kwa ccm.
 
Nafikiri pia tuangalie mbali zaidi kwenye uchaguzi mkuu ujao ili tupate wabunge wengi wa upinzani ili kuiamsha serikali katika majukumu yake na hapo ndio tutaanza kushughulikia matatizo yetu. Ombi kwa wanaJF wenye uwezo wa kugombea ubunge wajitokeze ili tuikomboe nchi yetu kwani tuliko fikishwa ni mbali sana kwani kila yeyote anayetoa kauli ya kukemea maovu huwa anafanyiwa mizengwe na kutolewa kwenye uongozi.
 
Uchaguzi Tarime Itakuwa ni Baraka au Mgawanyiko Zaidi kwa Wanamageuzi?

Chacha Wangwe alikuwa ni mpiganaji ambaye hakuwa mnafiki. Historia yake tokea NCCR na baadaye CHADEMA ilikuwa wazi kuwa aliwapinga CCM lakini pia hakuacha kuwapinga viongozi wenzake ndani ya chama chake kama wakipotoka. Hiii ndio moja kati ya sifa nilizompendea Wangwe, licha ya elimu yake ya wastani.

Hivi sasa kwenye vyama vyetu vyote, CCM na vya upinzani, kumezuka tabia ya kuwepo vikundi vya 'elites' (mitandao) ambavyo huonekana kuwa na sauti ya mwisho kwenye kila kinalochokea ndani ya hivyo vyama. Jambo hili ni hatari sana kwa siasa changa za Tanzania kwani linauwezo wa kukomaa. Mifano ya hivi karibu tuliyoiona ndani ya CCM na CHADEMA ambayo imewaathiri wanasiasa chipukizi wenye mitizamo tofauti na viongozi wao, ni kionjo tu cha picha iliyojificha ndani yake.

  • Ndani ya CCM upendeleo umekuwepo siku nyingi lakini haujawahi kufikia kiasi cha kuwanyonga vijana wanaopinga ubadhilifu, kama ilivyokuwa kwa Nape Mnauye. Lowassa, Malecela walipingwa na Mwalimu miaka ya nyuma kwa sababu ya kupenda kwao rushwa na madaraka lakini hata wao hawakuchinjwa hadharani kama ilivyokuwa kwa Nape Mnauye.
  • Chadema nao tumeona wakati Chacha Wangwe alipopingania mabadiliko ndani ya CHADEMA, mwenyekiti wake, Mbowe, na karibu uongozi mzima wa CHADEMA ukamgeuka na hata kumwita kuwa ni kibaraka wa CCM, Rostam Aziz na hata yeye mwenyewe kuitwa fisadi. Hii ni hali inayoogopesha sana kwani kuna uwezekano mkubwa kwa vyama vyetu kutekwa nyara na vikundi vya kibinafsi vyenye nia tofauti na kuijenga nchi. Kujitenga kwa CHADEMA na wanamageuzi wengine ni dalili mojawapo ya tamaa zilizopo.
Hivyo, hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa jimbo la Tarime, jimbo ambalo Wangwe aliliwakilisha kwa jasho na hatimaye kwa damu yake, licha ya upinzani mkali toka kwa CCM na hata kwa viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, matokeo ya huo uchaguzi yatakuwa na tafsiri nyingi kwa wanamageuzi. Kubwa ambazo nimeonelea nizidokeze ni hizi zifuatazo;
  1. Kama CHADEMA wakishinda, Je yale aliyokuwa akipigania marehemu Wangwe yatakuwa ndio yamekoma ?
    [*]Kama CHADEMA wakilipoteza hili jimbo, Je watabadilika na kujichunguza zaidi ndani ya chama chao kama alivyojaribu kupendekeza marehemu Wangwe?
    [*]CHADEMA wakishinda/ wakishindwa, Je msimamo wao wa kutoshirikiana na vyama vingine vya upinzani utabadilika? Je muungano wa vyama unaojumuisha CHADEMA ndio utakuwa ndio mwisho wake?

---------------------
 
Hivi CHADEMA wakishindwa itakuwa ni furaha kwa wapinzani wengine au CCM tu?
 
Hivi CHADEMA wakishindwa itakuwa ni furaha kwa wapinzani wengine au CCM tu?

Wakati wananchi wa Tarime wamezingirwa na mamia ya polisi walioletwa na serikali "kutuliza fujo na kulinda amani", na wakati ambao wananchi wa Tarime wanakabiliwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kemikali za sumu toka kwa makampuni ya madini kumwagwa kwenye vyanzo vya maji Tarime,

na wakati ambao watu wa Tarime wanajiuliza ni nani atasimamia haki zao ili wanufaike na madini ambayo walilazimika kupisha wageni (wenye vyombo vya kisasa na nguvu ya serikali) kuchimba "kwa ufanisi"..... na wakati .... kukiwa na mambo mengi yanayowakabili wananchi wa Tarime,

Wewe unachoona ni ushindi wa kisiasa (furaha) wa vyama vya siasa Tanzania....

Ama kweli hii ni bongo... kila mtu anafikiri na kujali ya kwake kwanza.
 
Mkuu Magabe,
Nakubaliana na wewe kuwa matatizo ya Tarime ni mengi na ni muhimu tukayaongelea ili yatatuliwe, lakini uchaguzi hautatui matizo wakati huo huo, na ndo maana bado yapo matatizo mengine mengi yanayowasibu waTZ nchi nzima ingawa wameshafanya chaguzi.

La muhimu pamoja na kupata mwakilishi ni kuelewa kuwa matokeo ya uchaguzi Tarime yatakuwa na impact kubwa kwenye mwelekeo wa upinzani nchini. Ndio maana sikutaka kujifungia katika kujadili tu yale yaliyopo bali kuangalia mbele zaidi kwa yanayoweza kutuathiri zaidi.
 
Unavyosema yale ambayo yanaweza kukuathiri zaidi (kushinda/kushindwa kwa upinzani au vyama vya siasa) kuwa ni bora kuliko wananchi wa Tarime ambao kwa sasa wako katika hatari kubwa sana kiafya kutokana na kemikali zinazomwagwa kwenye vyanzo vyao maji, na wana wasiwasi mkuu kutokana na namba kubwa ya polisi "wanaotuliza fujo", huku hali yao ya maisha ikizidi kuwa ngumu kutokana na mwenendo wa uchumi wa Tarime na Tanzania,

Katika hili mkuu wangu sikuelewi kabisa, ila baada ya kutumia muda mrefu kusoma posts zako zote hapa JF, kwa sasa nimejenga picha nzuri zaidi ya kile unachopenda wewe kukiona kikitokea Tanzania (na hapa JF). Asilimia kubwa sana ya posts zako hapa inahusu mambo fulani tu ambayo yanakutafsiri zaidi.

Good luck mkuu na juhudi zako hizo za kujua yale yatakayokuathiri zaidi.

Asante!
 
Nafikiri you are making a mountain out of nothing in deed. Polisi sio adui unless uwe mhalifu au watumiwe vibaya na viongozi. Taarifa nilizosoma leo ni kuwa Tarime sasa ni shwari, ikiwa na maana kuwa polisi wamefanya kazi yao vizuri, ukiachilia mbali suala la CHADEMA kukataliwa uwanja.

Hilo la maji kuchafuliwa kama ni kubwa kiasi unavyolipigia kelele, basi sijui kwa nini wanasiasa na viongozi wa Tarime, ambayo iko chini ya CHADEMA, wasingechukua hatua au hata kuandaa maandamano kwenye huo mgodi mpaka waache wanachofanya, simple as that. Hili ni suala la kiutendaji na sio la kampeni.

Ndio maana nikakudokeza kuwa tuangalie matokeo ya uchaguzi Tarime yatakavyobadili sura ya siasa za Tanzania hasa kwa wanamageuzi. Let's stick on this.
 
Uchaguzi Tarime Itakuwa ni Baraka au Mgawanyiko Zaidi kwa Wanamageuzi?

Chacha Wangwe alikuwa ni mpiganaji ambaye hakuwa mnafiki. Historia yake tokea NCCR na baadaye CHADEMA ilikuwa wazi kuwa aliwapinga CCM lakini pia hakuacha kuwapinga viongozi wenzake ndani ya chama chake kama wakipotoka. Hiii ndio moja kati ya sifa nilizompendea Wangwe, licha ya elimu yake ya wastani.

Hivi sasa kwenye vyama vyetu vyote, CCM na vya upinzani, kumezuka tabia ya kuwepo vikundi vya 'elites' (mitandao) ambavyo huonekana kuwa na sauti ya mwisho kwenye kila kinalochokea ndani ya hivyo vyama. Jambo hili ni hatari sana kwa siasa changa za Tanzania kwani linauwezo wa kukomaa. Mifano ya hivi karibu tuliyoiona ndani ya CCM na CHADEMA ambayo imewaathiri wanasiasa chipukizi wenye mitizamo tofauti na viongozi wao, ni kionjo tu cha picha iliyojificha ndani yake.

  • Ndani ya CCM upendeleo umekuwepo siku nyingi lakini haujawahi kufikia kiasi cha kuwanyonga vijana wanaopinga ubadhilifu, kama ilivyokuwa kwa Nape Mnauye. Lowassa, Malecela walipingwa na Mwalimu miaka ya nyuma kwa sababu ya kupenda kwao rushwa na madaraka lakini hata wao hawakuchinjwa hadharani kama ilivyokuwa kwa Nape Mnauye.
  • Chadema nao tumeona wakati Chacha Wangwe alipopingania mabadiliko ndani ya CHADEMA, mwenyekiti wake, Mbowe, na karibu uongozi mzima wa CHADEMA ukamgeuka na hata kumwita kuwa ni kibaraka wa CCM, Rostam Aziz na hata yeye mwenyewe kuitwa fisadi. Hii ni hali inayoogopesha sana kwani kuna uwezekano mkubwa kwa vyama vyetu kutekwa nyara na vikundi vya kibinafsi vyenye nia tofauti na kuijenga nchi. Kujitenga kwa CHADEMA na wanamageuzi wengine ni dalili mojawapo ya tamaa zilizopo.
Hivyo, hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa jimbo la Tarime, jimbo ambalo Wangwe aliliwakilisha kwa jasho na hatimaye kwa damu yake, licha ya upinzani mkali toka kwa CCM na hata kwa viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, matokeo ya huo uchaguzi yatakuwa na tafsiri nyingi kwa wanamageuzi. Kubwa ambazo nimeonelea nizidokeze ni hizi zifuatazo;
  1. Kama CHADEMA wakishinda, Je yale aliyokuwa akipigania marehemu Wangwe yatakuwa ndio yamekoma ?
    [*]Kama CHADEMA wakilipoteza hili jimbo, Je watabadilika na kujichunguza zaidi ndani ya chama chao kama alivyojaribu kupendekeza marehemu Wangwe?
    [*]CHADEMA wakishinda/ wakishindwa, Je msimamo wao wa kutoshirikiana na vyama vingine vya upinzani utabadilika? Je muungano wa vyama unaojumuisha CHADEMA ndio utakuwa ndio mwisho wake?

---------------------
Nadhani unaweza kujijibu mwenyewe, ukirejea post zako nyingi unazopost humu, mtizamo wa post zako jinsi Tanzania inavyostahili kuendelea kubaki na mfumo wa kifisadi uliopo, si dhani kuwa upinzani ukishinda au ukishindwa kuna impact, hasa kwa kuzingatia Watanzania wengi hawakupata nafasi ya kuerevuka na hata pale ilipotokea kidogo, bado wanaendelea kufufishwa. Unategemea nini kama miaka 5 ya kwanza ya Mkapa alipokuwa rais sehemu zote zilizokuwazimchagua wabunge wa upinzani walitengwa kama wahaini! Ukitaka kamuulize hata Sumaye
 
Labda kwa kuingilia kidogo katikati ya mjadala huu, nani kwa wenye data anafikiriwa anaweza kuwa mpambanaji wa kuwasaidia wana Tarime na ana sifa zipi ambazo zinaweza kuwakomboa kiuongozi na kimaadili?
 
Ukimaanisha miongoni mwa wagombea wote wa ubunge Tarime ama?
 
CCM yaikingia kifua serikali kwa ufisadi
Faraja Mgwabati, Tarime
Daily News; Sunday,September 21, 2008 @20:06

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema serikali yake inalishughulikia suala la ufisadi kwa vitendo tofauti na wapinzani ambao wamekuwa wakipiga kelele tu, lakini hawachukui hatua yoyote.

Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Pius Msekwa alisema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Kata ya Nyanungu katika Kijiji cha Itiryo wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Tarime ambazo zilianza Jumapili iliyopita.

Msekwa alisema wapinzani wamekuwa wakikituhumu chama hicho kuwa kina ufisadi wakati wao, pia wana ufisadi ndani ya vyama vyao na akasema bora CCM inapambana na ufisadi kwa vitendo, lakini wapinzani hakuna wanalofanya.

'Kama alivyosema Rais bungeni, fedha za EPA… zinarudishwa ni sawa na jambazi akiiba ng'ombe, zinarudishwa kwanza ng'ombe ndipo jambazi anashughulikiwa," alisema Msekwa.

Katika mkutano ambao ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho wakiwamo mawaziri, Msekwa alisema baadhi ya vyama vya upinzani kuna ufisadi mkubwa, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, lakini badala yake wanabaki kulalamika ufisadi, ufisadi, ufisadi.

Msekwa ambaye naye aliungana na viongozi wengine wa CCM kwamba walifanya makosa mwaka 2005 kwa kumsimamisha mgombea asiyekubalika, alisema safari hii CCM itashinda kwa sababu chama hicho kina wanachama wengi kuliko wapinzani.

Alisema kama wanachama wote watakipigia chama hicho kura, wapinzani hawatakuwa na chao hivyo ushindi wao unategemea CCM. Alisema sasa wamemleta Ryoba Kangoye, mgombea ubunge ambaye amechujwa na chama hicho na anakubalika.

Aliahidi kutatua kero wanayopata wananchi wanaoishi karibu na mbuga ya Serengeti ambao wamekuwa wakikamatwa na kutozwa faini kubwa wanapoingiza mifugo eneo la hifadhi hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba alianza kwa kusema wananchi wasifanye makosa ya kumlinganisha Katibu wa CCM na wa Chadema (Dk. Wilbroad Slaa) kwa sababu yeye ni katibu wa chama tawala, ni vitu viwili tofauti.

"Msinifananishe mimi na Dk. Slaa, mkifanya hivyo ni sawa na kufananisha mlima na kichuguu, sisi ndiyo tunaongoza serikali na hao wana nini," aliuliza na kuendelea, "Wala msimfananishe Mwenyekiti wa CCM (Rais Jakaya Kikwete) na wa Chadema (Freeman Mbowe)."

Alisema katika kumchagua mgombea, inabidi wananchi hao waangalie sifa nne ambazo ni chama anachotoka mgombea, elimu, asiyependa ukabila na awe mcha Mungu.

"Msimchague Mbunge ambaye hata Ikulu hakujui, Rais hamjui na hata kwenda Ikulu anaona aibu," alisema Makamba na kushangiliwa na viongozi wa chama hicho.

Viongozi waliohudhuria uzinduzi huo ni Mbunge wa Serengeti na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. James Wanyancha, Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Mkoa, Issa Machibya, Mbunge wa Rorya, Profesa Sarungi, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Ofisa wa Idara ya Propaganda Tambwe Hiza na Mbunge wa Afrika Mashariki, Didas Masaburi.

Wengine ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Christopher Gachuma, John Komba na Profesa Samwel Wangwe ambaye ni kaka wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe.

Naye Mjumbe wa NEC, Stephen Wassira alizungumza kwa hisia kwamba wananchi hao wasifanye makosa ya kuchagua Chadema kwa sababu ni chama cha watu wawili, Edwin Mtei na Philemon Ndesamburo.

Aliwaambia wakazi hao kuwa mwaka 2005 Tarime walimpigia kura Mbowe wa Chadema kwa kura 30,000, lakini hawajapewa hata kiti kimoja cha ubunge maalumu, bali wabunge wote wa Viti Maalumu wamepewa kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.

"Mnajua kilichotokea Kenya baada ya umoja kwisha? Wenzetu walipigana na hatutaki hapa umoja uishe," alisema Wassira na kuongeza kuwa anashangaa kuna watu wanajiita wapo upinzani kata hiyo.

"Msimchague mtu anayetangatanga na hana jipya, kazi yake kulalamika tu. Lazima mjue kwamba mtu mnayemchagua atawaletea maendeleo na huyo ni Kangoye."
Mgombea wa ubunge, Kangoye alielezea mambo mengi ambayo ameshafanya kama vile kuchangia vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Sh milioni 600, elimu na akaahidi kusaidia kuleta umeme katika kata hiyo.

"Naomba tarehe 12 mwezi ujao, mnikopeshe kura zenu niwalipe maendeleo," alisema na kuongeza kuwa atashirikiana na serikali kutatua tatizo la wananchi wanaokaa karibu na mbuga endapo atachaguliwa.

Katika mkutano huo, pia mdogo wake, marehemu Wangwe, Keba Wangwe aliendelea kutoa shutuma za kwamba Chadema wanahusika na kifo cha kaka yake.

Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, alifariki dunia usiku wa Julai 28, mwaka huu kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma; katika kifo ambacho hadi leo mazingira yake yanaendelea kukoroga vichwa vya watu wengi nchini.

Wanachama 50 wa vyama vya upinzani walirudisha kadi na 157 wapya walipewa kadi mpya za uanachama.
 
Karibuni wanachama wapya.....!
 
*Familia: Wangwe alichomwa singe kisogoni (Gazeti la Majira)
*Yadai pia alivunjwa taya, mbavu tatu

Na George John,Tarime

WAKATI uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe ukiendelea, familia ya mwanasiasa huyo imeibuka na kutamka hadharani kuwa ndugu yao aliuawa kwa kuvunjwa mbavu tatu, taya, kunyongwa na kuchomwa singe kisogoni.

Kaka wa marehemu Wangwe, Bw. Keba Wangwe, alitangaza hayo jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge Jimbo la Tarime, zilizohudhuriwa pia na ndugu mwingine wa familia hiyo, Profesa Samwel Wangwe.

Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Itiryo, Kata ya Nyanungu ambayo ni ngome kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na nyumbani kwa mgombea ubunge wa chama hicho,Bw. Charles Mwera

Bw. Keba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime kwa miaka 10 na kitaaluma ni mwanasheria, alisema familia baada ya kusita kukubali uchaguzi uliofanywa huko Dodoma, yeye na Prof. Wangwe walilazimika kufungua jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu na kubaini mauji hayo ya kinyama.

Alidai kuwa familia hiyo itazidi kuilaumu CHADEMA kuwa huenda ilihusika na mauji hayo ya ndugu yao kutokana na kushindwa kufika kumzika na hata kutoa mkono wa pole kwa mbunge huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

"CHADEMA wametufanya familia kuota upara, hadi sasa hawajaja hata kutoa mkono wa pole kwa familia pamoja na kwamba walichangisha rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali hazijafika, leo tena wanatuomba kura?Si wakati wake,"alisema Bw. Keba huku akichanganya lugha na kuufanya umati huo kuinamisha vichwa.

Katika hatua nyingine, Makamu Mweyekiti wa CCM, Tanzania Bara Bw. Pius Msekwa alisema kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe na watuhumiwa wote watashughulikiwa bila kukurupuka.

Alisema baada ya kubainika kuwepo wizi huo, serikali imechukua hatua za kuhakikisha fedha za EPA zinarejeshwa mara moja kabla ya kuwafikisha mahakamani wahusika hao bila kukurupuka.

"Suala la EPA ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe, Serikali ya CCM inapambana kwa vitendo kwa kurejesha kwanza fedha na baadaye hatua nyingine za kisheria zitafuta si kama wapinzani wanavyotaka tukamate watu kisha hela zetu zipotee,"alisema Bw. Msekwa.

Hata hivyo Bw. Msekwa, alikiri kuwa kushindwa kwa CCM katika chaguzi mbalimbali za ubunge na udiwani kunatokana na makosa yanayosabishwa na chama kuteua wagombea wasiokubalika kwa wapiga kura.

Alisema kutokana na CCM kugundua makosa hayo, imekuwa makini kuteua wagombea kwa kufuata maoni ya wananchi na ndivyo ilivyofanya kwa mgombea wao jimboni humo, Bw. Christopher Kangoye.

Aliishutumu CHADEMA na kudai kwamba ni chama cha kikabila kisicho na sera za kuongoza Watanzania na kimejaa ufisadi ambao unawanufaisha viongozi wa juu huku wanachama wake wakitumiwa kama daraja.

"Sisi tunapambana na ufisadi kwa dhati lakini wenzetu wanasema bila vitendo, ndani ya CHADEMA kuna ufisadi ambao hauelezeki ...tumewapa wilaya miaka miwili, wamefanya nini? Wamekula hela zote za miradi ya maendeleo tena mkiwapa hii iliyobaki, hamtapata kitu chagueni chama chenye sera nzuri,"alikipigia debe chama chake.

Alisema tangu mfumo wa vyama vingi ukubaliwe nchini CCM,imezidi kukubalika kwa wananchi kutokana na sifa, sera na umakini wake kushughulikia hoja na matatizo ya wananchi ukilinganisha na wapinzani ambao sasa wanakubalika kwa asilimia 12 tu nchi nzima.

Kwa upande wake akizungumza kabla ya kumkaribisha Bw. Msekwa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alitamba kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi huo mdogo kwa madai kuwa CCM ndiyo yenye serikali inayoweza kushughulikia matatizo ya wananchi wa Tarime na si wapinzani.

"Msinilinganishe mimi na Slaa (Dkt. Wilbrod -Katibu Mkuu wa CHADEMA) kufanya hivyo ni sawa na kulinganisha kichuguu na Mlima Kilimanjaro. Eti kuna watu wanamfananisha Rais Jakaya Kikwete na Mbowe ( Freeman -Mwenyekiti wa CHADEMA), hapana ! Kufanya hivyo mnakosema, Kikwete ni Rais wa nchi Mbowe ni mtu wa kutangatanga hata hana Ikulu kama sisi,"alitamba Bw. Makamba.

Aliwataka wananchi hao kumchagua, Bw. Kangoye kwani ni mtu makini mwwenye upeo anayeweza kutatua shida zao kwa haraka tofauti na wapinzani na kwamba ameoa mke mzuri mwenye mvuto wa kuwa mke wa mbunge.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bw. Stephen Wasira aliibeza CHADEMA kuwa ni chama cha kikabila na kinaendeshwa kama kampuni ya watu wachache.

Alisema uchaguzi wa Oktoba 12 ndicho kipimo cha watu wa Tarime kupata maendeleo na kuonya kuwawakishindwa kutumia nafasi hiyo, wataijutia kwa muda mrefu.

Naye Bw. Kangoye alisema mipango ya maendeleo katika jimbo hilo aliianza mapema kwa kununua vifaa vya hospitali vyenye thamani ya sh. mil. 600 kabla ya kufikiri kugombea ubunge na endapo wananchi watamchagua, watashirikiana vyema kufanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimboni humo.

"Nilianza zamani kuchukizwa na umasikini wa wananchi wa Tarime na kuleta miradi hapa, mimi siombi kuchaguliwa ili niwaletee maendeleo bali kazi hii nilishaianza mapema mniwezeshe tu niendeleze hayo yote ili Tarime ya neema iwezekane,"alisema Bw. Kangoye

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho na kupambwa na kundi la sanaa la TOT.
 
Mabomu ya machozi yarushwa Tarime

na Mwandishi Wetu

POLISI mjini hapa, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioonyesha dalili za kutaka kushambuliana wakati wakirejea kwenye mikutano yao ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge mjini hapa.

Katika kampeni za jana, CCM ilikuwa ikihutubia katika Kata ya Mjini Tarime ambapo pia ilizindua rasmi kampeni za mgombea wake wa udiwani, Peter Zacharia.

Dalili za kuwapo kwa vurugu, zilionekana tangu wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM ambapo kada mmoja wa chama hicho, aliyejulikana kwa jina moja la Omary Msungu, alimwagiwa maji ya pilipili na kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anayedaiwa kuwa ni mfuasi wa CHADEMA.

Hali hiyo ilisababisha vurugu, kwani polisi walimshika kijana huyo na kutaka kumfikisha katika kituo cha polisi huku wafuasi hao wa upinzani, wakijaribu kumnasua mwenzao kutoka katika makucha ya polisi.

Mkutano huo ulipomalizika na magari ya msafara wa mgombea wa CCM katika uwanja huo kuondoka, walikutana ana kwa ana na wafuasi wa vyama vingine vya upinzani na kutaka kushambuliana ndipo polisi walipolazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba aliwataka wananchi hao kutomchagua mgombea wa CHADEMA, kwa madai kuwa chama hicho hakina bajeti ya kuendeshea nchi, hivyo hawatapata maendeleo kwa haraka.

Pia Makamba alitumia nafasi hiyo kuwalaumu wabunge wa upinzani, hususan wa CHADEMA, kwamba wamekuwa wakosoaji wakubwa wa bajeti na kugomea kuipitisha, hivyo hawajui namna gani maendeleo yanaweza kuletwa.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, alisema kuwa ametumwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kwenda Tarime kuona kama wapinzani wanafanya fujo, hivyo amethibitisha hali hiyo na jana jioni angemwambia rais.

Kwa upande wa CHADEMA, jana mkutano wake ulihudhuriwa na maelfu ya watu, ambapo viongozi wao walitamba kuwa jimbo hilo ni lao na hawana sababu ya kulikosa.

Waliwataka wanachama wao kuacha kuogopa vitisho vya dola, kwani njia pekee ya kuepukana na mkono wa dola ni kufuata sheria na kujiepusha na vurugu.

Kwa kifupi, vyama vya CCM na CHADEMA ndivyo vyenye ushindani mkubwa katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe, kufariki dunia kwa ajali ya gari, akitokea mjini Dodoma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom