Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
*Familia: Wangwe alichomwa singe kisogoni (Gazeti la Majira)
*Yadai pia alivunjwa taya, mbavu tatu

Na George John,Tarime

WAKATI uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe ukiendelea, familia ya mwanasiasa huyo imeibuka na kutamka hadharani kuwa ndugu yao aliuawa kwa kuvunjwa mbavu tatu, taya, kunyongwa na kuchomwa singe kisogoni.

Kaka wa marehemu Wangwe, Bw. Keba Wangwe, alitangaza hayo jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge Jimbo la Tarime, zilizohudhuriwa pia na ndugu mwingine wa familia hiyo, Profesa Samwel Wangwe.

Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Itiryo, Kata ya Nyanungu ambayo ni ngome kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na nyumbani kwa mgombea ubunge wa chama hicho,Bw. Charles Mwera

Bw. Keba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime kwa miaka 10 na kitaaluma ni mwanasheria, alisema familia baada ya kusita kukubali uchaguzi uliofanywa huko Dodoma, yeye na Prof. Wangwe walilazimika kufungua jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu na kubaini mauji hayo ya kinyama.

Alidai kuwa familia hiyo itazidi kuilaumu CHADEMA kuwa huenda ilihusika na mauji hayo ya ndugu yao kutokana na kushindwa kufika kumzika na hata kutoa mkono wa pole kwa mbunge huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

"CHADEMA wametufanya familia kuota upara, hadi sasa hawajaja hata kutoa mkono wa pole kwa familia pamoja na kwamba walichangisha rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali hazijafika, leo tena wanatuomba kura?Si wakati wake,"alisema Bw. Keba huku akichanganya lugha na kuufanya umati huo kuinamisha vichwa.

Katika hatua nyingine, Makamu Mweyekiti wa CCM, Tanzania Bara Bw. Pius Msekwa alisema kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe na watuhumiwa wote watashughulikiwa bila kukurupuka.

Alisema baada ya kubainika kuwepo wizi huo, serikali imechukua hatua za kuhakikisha fedha za EPA zinarejeshwa mara moja kabla ya kuwafikisha mahakamani wahusika hao bila kukurupuka.

"Suala la EPA ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe, Serikali ya CCM inapambana kwa vitendo kwa kurejesha kwanza fedha na baadaye hatua nyingine za kisheria zitafuta si kama wapinzani wanavyotaka tukamate watu kisha hela zetu zipotee,"alisema Bw. Msekwa.

Hata hivyo Bw. Msekwa, alikiri kuwa kushindwa kwa CCM katika chaguzi mbalimbali za ubunge na udiwani kunatokana na makosa yanayosabishwa na chama kuteua wagombea wasiokubalika kwa wapiga kura.

Alisema kutokana na CCM kugundua makosa hayo, imekuwa makini kuteua wagombea kwa kufuata maoni ya wananchi na ndivyo ilivyofanya kwa mgombea wao jimboni humo, Bw. Christopher Kangoye.

Aliishutumu CHADEMA na kudai kwamba ni chama cha kikabila kisicho na sera za kuongoza Watanzania na kimejaa ufisadi ambao unawanufaisha viongozi wa juu huku wanachama wake wakitumiwa kama daraja.

"Sisi tunapambana na ufisadi kwa dhati lakini wenzetu wanasema bila vitendo, ndani ya CHADEMA kuna ufisadi ambao hauelezeki ...tumewapa wilaya miaka miwili, wamefanya nini? Wamekula hela zote za miradi ya maendeleo tena mkiwapa hii iliyobaki, hamtapata kitu chagueni chama chenye sera nzuri,"alikipigia debe chama chake.

Alisema tangu mfumo wa vyama vingi ukubaliwe nchini CCM,imezidi kukubalika kwa wananchi kutokana na sifa, sera na umakini wake kushughulikia hoja na matatizo ya wananchi ukilinganisha na wapinzani ambao sasa wanakubalika kwa asilimia 12 tu nchi nzima.

Kwa upande wake akizungumza kabla ya kumkaribisha Bw. Msekwa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alitamba kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi huo mdogo kwa madai kuwa CCM ndiyo yenye serikali inayoweza kushughulikia matatizo ya wananchi wa Tarime na si wapinzani.

"Msinilinganishe mimi na Slaa (Dkt. Wilbrod -Katibu Mkuu wa CHADEMA) kufanya hivyo ni sawa na kulinganisha kichuguu na Mlima Kilimanjaro. Eti kuna watu wanamfananisha Rais Jakaya Kikwete na Mbowe ( Freeman -Mwenyekiti wa CHADEMA), hapana ! Kufanya hivyo mnakosema, Kikwete ni Rais wa nchi Mbowe ni mtu wa kutangatanga hata hana Ikulu kama sisi,"alitamba Bw. Makamba.

Aliwataka wananchi hao kumchagua, Bw. Kangoye kwani ni mtu makini mwwenye upeo anayeweza kutatua shida zao kwa haraka tofauti na wapinzani na kwamba ameoa mke mzuri mwenye mvuto wa kuwa mke wa mbunge.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bw. Stephen Wasira aliibeza CHADEMA kuwa ni chama cha kikabila na kinaendeshwa kama kampuni ya watu wachache.

Alisema uchaguzi wa Oktoba 12 ndicho kipimo cha watu wa Tarime kupata maendeleo na kuonya kuwawakishindwa kutumia nafasi hiyo, wataijutia kwa muda mrefu.

Naye Bw. Kangoye alisema mipango ya maendeleo katika jimbo hilo aliianza mapema kwa kununua vifaa vya hospitali vyenye thamani ya sh. mil. 600 kabla ya kufikiri kugombea ubunge na endapo wananchi watamchagua, watashirikiana vyema kufanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimboni humo.

"Nilianza zamani kuchukizwa na umasikini wa wananchi wa Tarime na kuleta miradi hapa, mimi siombi kuchaguliwa ili niwaletee maendeleo bali kazi hii nilishaianza mapema mniwezeshe tu niendeleze hayo yote ili Tarime ya neema iwezekane,"alisema Bw. Kangoye

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho na kupambwa na kundi la sanaa la TOT.

Wanaccm, chonde chonde chonde... msituletee mambo ya ukabila Tarime. Elezeni sera zenu na sio mambo ya kikabila, na ya kifo cha Wangwe ambayo mlikataa kuunda tume huru kuyachunguza.

Tanzania hii sijui tunaelekea wapi, yaani kama Msekwa, Makamba na Wassira wote wanaleta pumba hivi kwenye mkutano wa siasa, je nini kitegemewe toka kwa mgombea mwenyewe?

Ushauri kidogo tu kwenu wanaccm, watu tusio na vyama Tarime tunahitaji mtu ambaye atasimamia maslahi ya Tarime lakini wakati huo huo akiunganisha Tarime na makabila mengine Tanzania. Mnakoelekea huku sio kuzuri.

Chonde chonde Makamba... muogope MUNGU
 
*Familia: Wangwe alichomwa singe kisogoni (Gazeti la Majira)
*Yadai pia alivunjwa taya, mbavu tatu

Na George John,Tarime

WAKATI uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe ukiendelea, familia ya mwanasiasa huyo imeibuka na kutamka hadharani kuwa ndugu yao aliuawa kwa kuvunjwa mbavu tatu, taya, kunyongwa na kuchomwa singe kisogoni.

Kaka wa marehemu Wangwe, Bw. Keba Wangwe, alitangaza hayo jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge Jimbo la Tarime, zilizohudhuriwa pia na ndugu mwingine wa familia hiyo, Profesa Samwel Wangwe.

Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Itiryo, Kata ya Nyanungu ambayo ni ngome kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na nyumbani kwa mgombea ubunge wa chama hicho,Bw. Charles Mwera

Bw. Keba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime kwa miaka 10 na kitaaluma ni mwanasheria, alisema familia baada ya kusita kukubali uchaguzi uliofanywa huko Dodoma, yeye na Prof. Wangwe walilazimika kufungua jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu na kubaini mauji hayo ya kinyama.

Alidai kuwa familia hiyo itazidi kuilaumu CHADEMA kuwa huenda ilihusika na mauji hayo ya ndugu yao kutokana na kushindwa kufika kumzika na hata kutoa mkono wa pole kwa mbunge huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

“CHADEMA wametufanya familia kuota upara, hadi sasa hawajaja hata kutoa mkono wa pole kwa familia pamoja na kwamba walichangisha rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali hazijafika, leo tena wanatuomba kura?Si wakati wake,”alisema Bw. Keba huku akichanganya lugha na kuufanya umati huo kuinamisha vichwa.

Katika hatua nyingine, Makamu Mweyekiti wa CCM, Tanzania Bara Bw. Pius Msekwa alisema kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe na watuhumiwa wote watashughulikiwa bila kukurupuka.

Alisema baada ya kubainika kuwepo wizi huo, serikali imechukua hatua za kuhakikisha fedha za EPA zinarejeshwa mara moja kabla ya kuwafikisha mahakamani wahusika hao bila kukurupuka.

“Suala la EPA ni wizi kama ulivyo wizi wa ng'ombe, Serikali ya CCM inapambana kwa vitendo kwa kurejesha kwanza fedha na baadaye hatua nyingine za kisheria zitafuta si kama wapinzani wanavyotaka tukamate watu kisha hela zetu zipotee,”alisema Bw. Msekwa.

Hata hivyo Bw. Msekwa, alikiri kuwa kushindwa kwa CCM katika chaguzi mbalimbali za ubunge na udiwani kunatokana na makosa yanayosabishwa na chama kuteua wagombea wasiokubalika kwa wapiga kura.

Alisema kutokana na CCM kugundua makosa hayo, imekuwa makini kuteua wagombea kwa kufuata maoni ya wananchi na ndivyo ilivyofanya kwa mgombea wao jimboni humo, Bw. Christopher Kangoye.

Aliishutumu CHADEMA na kudai kwamba ni chama cha kikabila kisicho na sera za kuongoza Watanzania na kimejaa ufisadi ambao unawanufaisha viongozi wa juu huku wanachama wake wakitumiwa kama daraja.

“Sisi tunapambana na ufisadi kwa dhati lakini wenzetu wanasema bila vitendo, ndani ya CHADEMA kuna ufisadi ambao hauelezeki ...tumewapa wilaya miaka miwili, wamefanya nini? Wamekula hela zote za miradi ya maendeleo tena mkiwapa hii iliyobaki, hamtapata kitu chagueni chama chenye sera nzuri,”alikipigia debe chama chake.

Alisema tangu mfumo wa vyama vingi ukubaliwe nchini CCM,imezidi kukubalika kwa wananchi kutokana na sifa, sera na umakini wake kushughulikia hoja na matatizo ya wananchi ukilinganisha na wapinzani ambao sasa wanakubalika kwa asilimia 12 tu nchi nzima.

Kwa upande wake akizungumza kabla ya kumkaribisha Bw. Msekwa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Yusuf Makamba alitamba kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi huo mdogo kwa madai kuwa CCM ndiyo yenye serikali inayoweza kushughulikia matatizo ya wananchi wa Tarime na si wapinzani.

“Msinilinganishe mimi na Slaa (Dkt. Wilbrod -Katibu Mkuu wa CHADEMA) kufanya hivyo ni sawa na kulinganisha kichuguu na Mlima Kilimanjaro. Eti kuna watu wanamfananisha Rais Jakaya Kikwete na Mbowe ( Freeman -Mwenyekiti wa CHADEMA), hapana ! Kufanya hivyo mnakosema, Kikwete ni Rais wa nchi Mbowe ni mtu wa kutangatanga hata hana Ikulu kama sisi,”alitamba Bw. Makamba.

Aliwataka wananchi hao kumchagua, Bw. Kangoye kwani ni mtu makini mwwenye upeo anayeweza kutatua shida zao kwa haraka tofauti na wapinzani na kwamba ameoa mke mzuri mwenye mvuto wa kuwa mke wa mbunge.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bw. Stephen Wasira aliibeza CHADEMA kuwa ni chama cha kikabila na kinaendeshwa kama kampuni ya watu wachache.

Alisema uchaguzi wa Oktoba 12 ndicho kipimo cha watu wa Tarime kupata maendeleo na kuonya kuwawakishindwa kutumia nafasi hiyo, wataijutia kwa muda mrefu.

Naye Bw. Kangoye alisema mipango ya maendeleo katika jimbo hilo aliianza mapema kwa kununua vifaa vya hospitali vyenye thamani ya sh. mil. 600 kabla ya kufikiri kugombea ubunge na endapo wananchi watamchagua, watashirikiana vyema kufanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimboni humo.

“Nilianza zamani kuchukizwa na umasikini wa wananchi wa Tarime na kuleta miradi hapa, mimi siombi kuchaguliwa ili niwaletee maendeleo bali kazi hii nilishaianza mapema mniwezeshe tu niendeleze hayo yote ili Tarime ya neema iwezekane,”alisema Bw. Kangoye

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho na kupambwa na kundi la sanaa la TOT.
 
Mabomu ya machozi yarushwa Tarime (Tanzania Daima)

na Mwandishi Wetu

POLISI mjini hapa, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioonyesha dalili za kutaka kushambuliana wakati wakirejea kwenye mikutano yao ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge mjini hapa.

Katika kampeni za jana, CCM ilikuwa ikihutubia katika Kata ya Mjini Tarime ambapo pia ilizindua rasmi kampeni za mgombea wake wa udiwani, Peter Zacharia.

Dalili za kuwapo kwa vurugu, zilionekana tangu wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM ambapo kada mmoja wa chama hicho, aliyejulikana kwa jina moja la Omary Msungu, alimwagiwa maji ya pilipili na kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anayedaiwa kuwa ni mfuasi wa CHADEMA.

Hali hiyo ilisababisha vurugu, kwani polisi walimshika kijana huyo na kutaka kumfikisha katika kituo cha polisi huku wafuasi hao wa upinzani, wakijaribu kumnasua mwenzao kutoka katika makucha ya polisi.

Mkutano huo ulipomalizika na magari ya msafara wa mgombea wa CCM katika uwanja huo kuondoka, walikutana ana kwa ana na wafuasi wa vyama vingine vya upinzani na kutaka kushambuliana ndipo polisi walipolazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba aliwataka wananchi hao kutomchagua mgombea wa CHADEMA, kwa madai kuwa chama hicho hakina bajeti ya kuendeshea nchi, hivyo hawatapata maendeleo kwa haraka.

Pia Makamba alitumia nafasi hiyo kuwalaumu wabunge wa upinzani, hususan wa CHADEMA, kwamba wamekuwa wakosoaji wakubwa wa bajeti na kugomea kuipitisha, hivyo hawajui namna gani maendeleo yanaweza kuletwa.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, alisema kuwa ametumwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kwenda Tarime kuona kama wapinzani wanafanya fujo, hivyo amethibitisha hali hiyo na jana jioni angemwambia rais.

Kwa upande wa CHADEMA, jana mkutano wake ulihudhuriwa na maelfu ya watu, ambapo viongozi wao walitamba kuwa jimbo hilo ni lao na hawana sababu ya kulikosa.

Waliwataka wanachama wao kuacha kuogopa vitisho vya dola, kwani njia pekee ya kuepukana na mkono wa dola ni kufuata sheria na kujiepusha na vurugu.

Kwa kifupi, vyama vya CCM na CHADEMA ndivyo vyenye ushindani mkubwa katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe, kufariki dunia kwa ajali ya gari, akitokea mjini Dodoma.
 
Wanaccm, chonde chonde chonde... msituletee mambo ya ukabila Tarime. Elezeni sera zenu na sio mambo ya kikabila, na ya kifo cha Wangwe ambayo mlikataa kuunda tume/kamati/ushirika wa polisi/wapepelezi/wana usalama huru kuyachunguza.

Tanzania hii sijui tunaelekea wapi, yaani kama Msekwa, Makamba na Wassira wote wanaleta pumba hivi kwenye mkutano wa siasa, je nini kitegemewe toka kwa mgombea mwenyewe?

Ushauri kidogo tu kwenu wanaccm, watu tusio na vyama Tarime tunahitaji mtu ambaye atasimamia maslahi ya Tarime lakini wakati huo huo akiunganisha Tarime na makabila mengine Tanzania. Mnakoelekea huku sio kuzuri.

Chonde chonde Makamba... muogope MUNGU
 
Aliwataka wananchi hao kumchagua, Bw. Kangoye kwani ni mtu makini mwenye upeo anayeweza kutatua shida zao kwa haraka tofauti na wapinzani na kwamba ameoa mke mzuri mwenye mvuto wa kuwa mke wa mbunge.

Hayo niliyonukuu hapo juu inadaiwa ni maneno ya Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM "akimpigia debe" mgombea wa CCM huko Tarime. Kama hizo ndizo sifa za kumnadi mgombea, yaani nimechoka vibaya! Sijui hii tutaita nini?
 
Kwenye kampeni zenye ushindani mkubwa chochote kinawezwa kusemwa...
 
POLISI mjini hapa, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walioonyesha dalili za kutaka kushambuliana wakati wakirejea kwenye mikutano yao ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge mjini hapa.

Katika kampeni za jana, CCM ilikuwa ikihutubia katika Kata ya Mjini Tarime ambapo pia ilizindua rasmi kampeni za mgombea wake wa udiwani, Peter Zacharia.

Dalili za kuwapo kwa vurugu, zilionekana tangu wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM ambapo kada mmoja wa chama hicho, aliyejulikana kwa jina moja la Omary Msungu, alimwagiwa maji ya pilipili na kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anayedaiwa kuwa ni mfuasi wa CHADEMA.

Hali hiyo ilisababisha vurugu, kwani polisi walimshika kijana huyo na kutaka kumfikisha katika kituo cha polisi huku wafuasi hao wa upinzani, wakijaribu kumnasua mwenzao kutoka katika makucha ya polisi.

Mkutano huo ulipomalizika na magari ya msafara wa mgombea wa CCM katika uwanja huo kuondoka, walikutana ana kwa ana na wafuasi wa vyama vingine vya upinzani na kutaka kushambuliana ndipo polisi walipolazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba aliwataka wananchi hao kutomchagua mgombea wa CHADEMA, kwa madai kuwa chama hicho hakina bajeti ya kuendeshea nchi, hivyo hawatapata maendeleo kwa haraka.

Pia Makamba alitumia nafasi hiyo kuwalaumu wabunge wa upinzani, hususan wa CHADEMA, kwamba wamekuwa wakosoaji wakubwa wa bajeti na kugomea kuipitisha, hivyo hawajui namna gani maendeleo yanaweza kuletwa.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, alisema kuwa ametumwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kwenda Tarime kuona kama wapinzani wanafanya fujo, hivyo amethibitisha hali hiyo na jana jioni angemwambia rais.

Kwa upande wa CHADEMA, jana mkutano wake ulihudhuriwa na maelfu ya watu, ambapo viongozi wao walitamba kuwa jimbo hilo ni lao na hawana sababu ya kulikosa.

Waliwataka wanachama wao kuacha kuogopa vitisho vya dola, kwani njia pekee ya kuepukana na mkono wa dola ni kufuata sheria na kujiepusha na vurugu.

Kwa kifupi, vyama vya CCM na CHADEMA ndivyo vyenye ushindani mkubwa katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe, kufariki dunia kwa ajali ya gari, akitokea mjini Dodoma.

TANZANIA DAIMA
 
Hivi vyama hakuna njia nyingine ya kuelezea kampeni zao hadi wazihusishe na marehemu?Aliyekufa kafa na haki yake iko Mola.Familia nayo wameingizwa mjini kwa kurubuniwa na wanasiasa,wakati Prof mwenyewe alitamkia umati kuwa wamejiridhisha chacha(R.I.P) amekufa kwa ajali,leo huyu mwingine anatoa tuhuma nzito nzito na hawa wana usalama wako kimya.PROF amekaa kimya maana anajua akisema kitu kitamrudi ndipo akamsukumia huyu mwingine.

Halafu Mgosi Makamba anasema CHADEMA hawana bajeti ya kuendesha nchi,hivi hizo fedha za nchi ni mali ya sisiem au kodi za wananchi?empty words!
 
single D;

Tunapokuwa na watu kama wewe hapa tanzania ni hatari sana, yaani munaishia kubwabwaja tu, hakuna lolote mnalofanya kuhakikisha kuwa mnapambana na hawa mafisadi, nawambieni kweli kuwa ninyi nyo hapa jamvini ni wapiga kelele tu.

Niliwaambia siku zile kuwa tuwe na mjadala mpana wa kumshauri Mbowe ajiweke pembeni(ajiuzulu) ili CCM wakose mshiko, wewe single D; ile hoja haukuwahi kuichangia hata siku moja, single D; nadhani wewe ni mfuata mkumbo tu hauna mtizamo wa kisiasa kwa siku za usoni.

single D; unadhani mafisadi watakuwa tayari kuicha nchii hii? single D;unadhani watakuwa tayari kuachia utawala?laiti tungeweza kumshauri Mbowe ajiweke pembeni na tukafanya marekebisho ndani ya chama hiki
(CHADEMA) Kwani kwa sasa ndicho chenye sura ya kitaifa hakika tungepiga hatua
 
... marekebisho ndani ya chama hiki
(CHADEMA) Kwani kwa sasa ndicho chenye sura ya kitaifa hakika tungepiga hatua
Pemba mna wanachama wangapi, kuna matawi mangapi ya chadema na mna ofisi ngapi huko Pemba?
 
Last edited:
Pemba mna wanachama wangapi, kuna matawi mangapi ya chadema na mna ofisi ngapi huko Pemba?

kibunango;

Hapa ni lazima uelewe kuna mgawanyo wa region, kuna sehemu sera za chama furani zinakubalika na kuna sehemu nyingine hazikubaliki, sasa unapojadili pemba ni wazi unajua kazi hiyo CUF imeimaliza, sasa kama kuna haja ya kufanya hivyo hilo ni lingine Mkuu.

Tukijielekeza na kutambua kuwa vita yetu ni ipi hapo yaweza kuwa rahisi kuishinda na kama tutaendelea kupigana vikumbo na kuvutia kwako, kwangu pakavu ......., hapo itatuchukua miaka 50 zaidi kuupata upinzani wa kweli huku bara.

kibunango; NAOMBA UFUMBUE MACHO, ACHA FIKRA ZAKO HIZO ZILIZOCHAKAA,hapa hatujadili kwa kuona ni nani bora ila tunajadili ili tuweze kujinasua toka mikononi mwa mafisadi
 
Hivi vyama hakuna njia nyingine ya kuelezea kampeni zao hadi wazihusishe na marehemu?Aliyekufa kafa na haki yake iko Mola.Familia nayo wameingizwa mjini kwa kurubuniwa na wanasiasa,wakati Prof mwenyewe alitamkia umati kuwa wamejiridhisha chacha(R.I.P) amekufa kwa ajali,leo huyu mwingine anatoa tuhuma nzito nzito na hawa wana usalama wako kimya.PROF amekaa kimya maana anajua akisema kitu kitamrudi ndipo akamsukumia huyu mwingine.

Halafu Mgosi Makamba anasema CHADEMA hawana bajeti ya kuendesha nchi,hivi hizo fedha za nchi ni mali ya sisiem au kodi za wananchi?empty words!
Nimefarijika sana kwa maneno yako,nafikiri wanajf tuwashauri wanasiasa wetu wawe wanatumia neno walipakodi.Hili likirudiwa mara kwa mara litajenga uelewa kwa wananchi kuwa fedha zinazopitishwa kwenye bajeti ni kodi waliyolipa hivyo kuondoa dhana potofu iliyojengeka kuwa ni fedha ya serikali.Hii itapunguza kelele za wanasiasa wenye kutumia midomo kuishi badala ya fikra(Makamba Type).
 
single D;

Tunapokuwa na watu kama wewe hapa tanzania ni hatari sana, yaani munaishia kubwabwaja tu, hakuna lolote mnalofanya kuhakikisha kuwa mnapambana na hawa mafisadi, nawambieni kweli kuwa ninyi nyo hapa jamvini ni wapiga kelele tu.

Niliwaambia siku zile kuwa tuwe na mjadala mpana wa kumshauri Mbowe ajiweke pembeni(ajiuzulu) ili CCM wakose mshiko, wewe single D; ile hoja haukuwahi kuichangia hata siku moja, single D; nadhani wewe ni mfuata mkumbo tu hauna mtizamo wa kisiasa kwa siku za usoni.
single D; unadhani mafisadi watakuwa tayari kuicha nchii hii? single D;unadhani watakuwa tayari kuachia utawala?laiti tungeweza kumshauri Mbowe ajiweke pembeni na tukafanya marekebisho ndani ya chama hiki
(CHADEMA) Kwani kwa sasa ndicho chenye sura ya kitaifa hakika tungepiga hatua

Very crooked views which cannot be made straight,hivi wewe huwa unachangia kila hoja inayoletwa hapa jamvini?Hapa hatutafuti nani zaidi ya mwingine wala kujionyesha nani anachangia kila hoja!What is this lacking?Tunapopambana hatuonyeshi silaha zote kwa adui,kwa hiyo kama unafanya hivyo pole sana,you are striving after wind.Sijawahi kufuata mkumbo katika siasa na wala sina haja ya kufuata Mkumbo.
 
Jamani nisaidieni, hivi Makamba ana eleimu gani? Siku zote nikimsikiliza huwa napata kichefuchefu! CCM katika Karne hii bado inakumbatia viongozi ambao upeo wao ni mdogo sana. Ingekuwa nchi hii ina watu wanaopima maneno na hata kuwasilisha malalamiko mahakamani nadhani makamba angekuwa keko au nyumbani kwake akiliam nyanya!
 
Jobo umesema kweli, leo asubuhi nimeshikilia mbavu zangu nilipokuwa nikisikia upupu alo kuwa akiutoa makamba! jamani hivi hata kama hujasoma hata ule utu uzima hautoshi jama kukufanya uongee yenye mantiki?

Lakini si yeye tu, Hata Msekwa naye kanishangaza kwa hizo kauli zake kwamba kikwete ni amiri jeshi kamtuma amwambie kama kuna vurugu tarime na sasa anaenda kumwambia ipo, kwahiyo akiwa amiri jeshi kazi yake ni kuamrisha majeshi yatwange watu pasipo sababu?

Ushauri wangu ni kwamba unapoenda kwenye kampeini ukubali yote mawili, ukisema yenye maana ukashangailiwa furahi lakini ukimwaga upupu wa chagua msomi mwenye mke mzuri ni halali yako uzomewe, na usitishie nyau!
 
Binafsi sina tatizo lolote na mgombea wao lakini hawa viongozi wanatutia kichefuchefu. Halafu Tume ya Uchaguzi inakaa kimya wakisikia maneno ya kibaguzi yakitolewa. Serikali inatumia mali za wananchi katika kampeni kwa jina la viongozi wa chama. Seriakali inatoa ulinzi na mambo mengine kwa ajili ya CCM lakini vyama vingine vinaachwa kama watoto yatima. Sijui ni kwanini bado mzee Makame anaendelea kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, kwani hakuna Watanzania wengine wenye uwezo wa kuwa hapo?
 
Very crooked views which cannot be made straight,hivi wewe huwa unachangia kila hoja inayoletwa hapa jamvini?Hapa hatutafuti nani zaidi ya mwingine wala kujionyesha nani anachangia kila hoja!What is this lacking?Tunapopambana hatuonyeshi silaha zote kwa adui,kwa hiyo kama unafanya hivyo pole sana,you are striving after wind.Sijawahi kufuata mkumbo katika siasa na wala sina haja ya kufuata Mkumbo.

Isayamwita ana ajenda yake ambayo anajua sana kuichomeka kila apatapo nafasi, lakini Singe D, ukianza tu majibizano naye, mjadala utahamia huko. Nadhani kwa ushauri anaweza kuendeleza hiyo mada yake ya Mbowe mahali pale pale, watu wakimfuata ataendelea nao, na wale watakaopuuza kama Singe D, wataingia katika mijadala inayowavutia, huo ndio uhuru wa JF si kulazimishana ndio maana hata Invisible halazimishi watu kujadili doc kubwa na muhimu alizoweka kuhusu Bank M na Debt Gate wakati ni mada kubwa na muhimu na yeye ana uwezo wa kuiweka juu isitoke,

Tuendelee "kupingana bila kupigana"
 
Niko Tarime .Yale niliyo yasema siku chache nyuma ndiyo haya .Uharamia wa wazi wazi upo Tarime .Leo kuna kila aina ya gari za polisi na FFU Tarime .Serikali yote iko Tarime hata kama JK hajaingia .Msekwa kasema katumwa na JK kuona kama wapinzani wanaleta vurugu .Ngoma hii bado nzito na CCM wanacheza na kutumia ukabila .Prof Wangwe anajivua nguo.Hawezi kumeza maneno yake ,why waone mbavu kisiri wakae kimya ? Wanataka sisi tuwaamini ?

Nasema Chache Wangwe aachwe alikuwa na mapenzi na Tarime na si Prof .Wangwe mwenye mapenzi na pesa ya walipa kodi na CCM yake .

CCM waeleze juu ya Barrick na unyama wao Nyamongo , na shjida nyingi za wana Tarime .

Mkono wa pole leo wanau usema ? Hivi si hao hao walio taka kumpiga Mbowe ? Chadema wapi walitaka wafike ? Hivi akina Zitto si Chadema ? Au walitaka Mbowe na leo wanamtumia yeye kama sababu ?

Niko Tarime na Tossi anachemka na vijana wake , nia ni kuona CCM wana twaa Jimbo.

Matumizi haya mabaya ya madaraka hadi lini ?
 
Niko Tarime .Yale niliyo yasema siku chache nyuma ndiyo haya .Uharamia wa wazi wazi upo Tarime .Leo kuna kila aina ya gari za polisi na FFU Tarime .Serikali yote iko Tarime hata kama JK hajaingia ....
Kamanda ujaacha tu zuga zako...
 
Niko Tarime .Yale niliyo yasema siku chache nyuma ndiyo haya .Uharamia wa wazi wazi upo Tarime .Leo kuna kila aina ya gari za polisi na FFU Tarime .Serikali yote iko Tarime hata kama JK hajaingia .Msekwa kasema katumwa na JK kuona kama wapinzani wanaleta vurugu .Ngoma hii bado nzito na CCM wanacheza na kutumia ukabila .Prof Wangwe anajivua nguo.Hawezi kumeza maneno yake ,why waone mbavu kisiri wakae kimya ? Wanataka sisi tuwaamini ?

Nasema Chache Wangwe aachwe alikuwa na mapenzi na Tarime na si Prof .Wangwe mwenye mapenzi na pesa ya walipa kodi na CCM yake .

CCM waeleze juu ya Barrick na unyama wao Nyamongo , na shjida nyingi za wana Tarime .

Mkono wa pole leo wanau usema ? Hivi si hao hao walio taka kumpiga Mbowe ? Chadema wapi walitaka wafike ? Hivi akina Zitto si Chadema ? Au walitaka Mbowe na leo wanamtumia yeye kama sababu ?

Niko Tarime na Tossi anachemka na vijana wake , nia ni kuona CCM wana twaa Jimbo.

Matumizi haya mabaya ya madaraka hadi lini ?

Mkuu Lunyungu inasikitisha sana kuona yote haya yanatendeka Tzania yetu. Labda kwa mtazamo wako unaonaje uelekeo ukoje pamoja na nguvu na vitisho vyote hivyo? je vinawajaza hofu wana Tarime wabadii msimamo wao? tupe data mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom