Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Ndugu IGP Mwema

Leo vijana wako msafara wa magari takribani ishirini wamefanya patrol Tarime na kukamata zaidi ya vijana hamsini kwa sababu za kisiasa. Na wengine wamekamata mpaka pikipiki na mali zao nyingine. Vijana wako, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu watanzania, wanakubali kutumika kisiasa kwa kuwa tu wanapata chakula toka kwa tajiri anayeitwa Zakaria ambaye pia anagombea udiwani kwa CCM Tarime. Naandikia ujumbe huu wa wazi uchukue hatua za haraka. Nami siku chache zijazo naelekea huko huko Tarime. Mtukamate wote mujaze mahabusu na magereza yote huko. Uchaguzi utakapokishwa, dhana nzima ya polisi jamii ambayo umekuwa ukihubiri itakuwa umepotea.

Wako katika ujenzi wa Taifa

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana-Taifa
0754694553
JJ
 
Hivi IGP Mwema huwa anasoma hizi posts hapa JF? Nilitegemea uwasiliane nae kwanza kwa barua ama simu, kisha utubandikie hapa reaction yake, kama ni nzuri tumpongeze, kama ni mbaya tushirikiane kuendelea kumpigia kelele hadi achukue hatua ya kuridhisha.
 
IGP ni taasisi si mtu
 
Ukisoma gazeti la Mtanzania la leo, ukurasa wa kwanza "Kampeni zazidi kunoga Tarime" utaona Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa anasema,

"Wakati nakuja (tarime), rais (Kikwete) alinituma kuangalia kama kweli kuna fujo au la, lakini tangu niwasili wilayani hapa yamekuwapo matukio ya fujo. Nilipokuwa naingia Tarime, msafara wangu ulizomewa na kurushiwa mawe. Leo (jana) usiku nitamjulisha hali halisi ilivyo, na ifahamike yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, kwa hiyo atampa maagizo Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo msije mkajuta."

Leo asubuhi saa 5.20, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, akiwa katika jengo la CRDB Bank Tarime, aliendewa na maofisa wa polisi wakiwa na vijana wa FFU na muda mfupi wakaondoka na kuanza kamata kamata.

Wakati huo dereva wa polisi aitwaye Constantino jana alipakia viloba vya mchele, kuku na kuni nyumbani kwa mgombea wa CCM.

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa DP, anayejiita Mchungaji, Christopher Mtikila, yuko eneo la Sirari akisambaza vipeperushi vinavyosema kwamba Mbowe kamuua Wangwe, anafanya hivyo akiwa analindwa na polisi.

Watu wana ushahidi hadi wa picha za matukio hayo.

Nini maana ya yote haya yanayotokea:

-Kama Taifa tunakoelekea ni kubaya na tutarajie maafa ama machafuko huko.
-Tujiandae kutokea pengine mabaya zaidi ya yaliyotokea Pemba mwaka 2001, wakati huo Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi, kama ilivyo sasa Kikwete yuko nje ya nchi.
_Kuna kila sababu kwa wapenda amani kote nchini kukemea mara moja vitendo vichafu vinavyofanywa na CCM.
 
Nashukuru. Nilitegemea ungeuliza, kwanini hukumpigia simu au kumtumia SMS wakati una namba yake? Nilitarajia uniulize kwani umeandika ujumbe wa wazi!

Nashukuru HALISI amenielewa na kuanza kuchukua hatua. Mjadala mwema

JJ
 
Ukisoma gazeti la Mtanzania la leo, ukurasa wa kwanza "Kampeni zazidi kunoga Tarime" utaona Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa anasema,

"Wakati nakuja (tarime), rais (Kikwete) alinituma kuangalia kama kweli kuna fujo au la, lakini tangu niwasili wilayani hapa yamekuwapo matukio ya fujo. Nilipokuwa naingia Tarime, msafara wangu ulizomewa na kurushiwa mawe. Leo (jana) usiku nitamjulisha hali halisi ilivyo, na ifahamike yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, kwa hiyo atampa maagizo Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo msije mkajuta."

Leo asubuhi saa 5.20, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, akiwa katika jengo la CRDB Bank Tarime, aliendewa na maofisa wa polisi wakiwa na vijana wa FFU na muda mfupi wakaondoka na kuanza kamata kamata.

Wakati huo dereva wa polisi aitwaye Constantino jana alipakia viloba vya mchele, kuku na kuni nyumbani kwa mgombea wa CCM.

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa DP, anayejiita Mchungaji, Christopher Mtikila, yuko eneo la Sirari akisambaza vipeperushi vinavyosema kwamba Mbowe kamuua Wangwe, anafanya hivyo akiwa analindwa na polisi.

Watu wana ushahidi hadi wa picha za matukio hayo.

Nini maana ya yote haya yanayotokea:

-Kama Taifa tunakoelekea ni kubaya na tutarajie maafa ama machafuko huko.
-Tujiandae kutokea pengine mabaya zaidi ya yaliyotokea Pemba mwaka 2001, wakati huo Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi, kama ilivyo sasa Kikwete yuko nje ya nchi.
_Kuna kila sababu kwa wapenda amani kote nchini kukemea mara moja vitendo vichafu vinavyofanywa na CCM.

Mpendwa napenda kukueleza kuwa nchi si muda mrefu itakuwa out of control, na kila mmoja anajua kuwa Kikwete haiwezi kabisa hali inayokuja kuikabili nchi siku za karibuni, huenda ndiyo maana anasafiri san. Lakini tuko katika wakati wa mabadiliko. Wataalamu wanaita Paradigm shift, toka katika hali ya kubweteka na kukubali kila kitu kuelekea katika democracia ya kweli na uwazi katika utendaji, na ili hali hii itokee ni lazima machafuko yaje.

Mimi si nabii wala mtoto wa nabii lakini nchi inakwenda kwenye machafuko na mauaji makubwa, lakini hilo halina budi litokee kama kweli Tanzania patakuwa mahali bora pa kuishi baadaye. Watanzania sasa wanatafuta uhuru wao, ndiyo maana unasikia migomo kila mahali na kila kukicha, na mara tu utasikia maandamano ya kila siku na muda utasikia watu wakiuuawa na polisi na damu itakapoanza kumwagika ndipo ukombozi wa Mtanzania dhidi ya mafisadi wa ccm utakapowadia.

Hivyo Watanzania myaonapo haya inueni vichwa vyenu juu maana ukombozi wenu umekaribia. Katika mapambano kama haya kamwe usitegemee kukosa wasaliti kama Mtikila, Mbatia, Mrema, Mvungi nk. hawa ni wasaliti na kama ukichunguza kwa undani sana utagundua kuwa wako kwenye payrol ya mafisadi.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.
 
Hawa watu wanakamatwa hewani? leteni picha!!!!!! Maneno tu inaonekana siasa; yaani watu karibu hamsini, magari na pikipiki vyote vikamatwe na hakuna mwenye picha ya vitendo hivyo? Picha zinasema elfu!
 
Wanaoripoti wako huku (mbali) Haiyumkini picha zitafuata muda sio mrsfu! Vuta subira.
 
Hawa watu wanakamatwa hewani? leteni picha!!!!!! Maneno tu inaonekana siasa; yaani watu karibu hamsini, magari na pikipiki vyote vikamatwe na hakuna mwenye picha ya vitendo hivyo? Picha zinasema elfu!

Picha za nini mkuu, kama si kweli IGP akanushe. Yale ya Zanzibar yamehamia Tarime, nguvu na vitisho. Akishinda mgombea wa upinzani atatangwa wa ccm kisha polisi watamwagwa mitaani tusikie fyoko fyoko.
 
Picha zinasema maneno mengi na zinatumia lugha nyingi. Ni sawa na mtu anasema "fulani ananunua kadi za kupigia kura" na hadi leo huyo fulani hajawahi kujitokeza au kuwekwa mtego wa kukamatwa wanunuzi n.k Sasa sitaki kuamini kuwa hakuna mtu anayeweza kutega mtego wa namna hiyo.

Sisemi vitendo hivyo vya Polisi havipo (nawajua polisi wetu) ninachosema ili kuweza kuleta outrage and outcry; show the world the pictures!!
 
Hawa watu wanakamatwa hewani? leteni picha!!!!!! Maneno tu inaonekana siasa; yaani watu karibu hamsini, magari na pikipiki vyote vikamatwe na hakuna mwenye picha ya vitendo hivyo? Picha zinasema elfu!

Inasikitisha mwananzuoni kama Mwanakijiji kudai ushahidi wa picha ili kuamini kwamba kuna fujo. Kauli ya Msekwa mwenyewe inakueleza kwamba kuna fujo na kamata kamata. Kama watu wameshuhudia wasiseme kwasababu hawana picha? Matukio mangapi yanapelekwa mahakamani na kupatiwa hukumu bila watu kuwa na ushahidi wa picha?

La msingi hapa ni wewe kuelewa na kuamini kwamba hali huko Tarime ni tete. Yote haya yanachangiwa na siasa za mabavu za CCM. Hiyo kamata kamata, fujo, Wasira kutumia gari la serikali kwenye kampeni, shahada za kupiga kura za wapinzani kununuliwa na CCM ni sehemu tu ya hali tete. Tutarajie mabaya zaidi. Hasa hili la Mtikila kutumiwa na CCM kumpaka Mbowe na Silaa matope kwa kuwahusisha na kifo cha Wangwe.

Mwanakijiji ningeomba utusaidie kumuomba Mtikila ushahidi wa picha!!
 
Ndugu IGP Mwema

Leo vijana wako msafara wa magari takribani ishirini wamefanya patrol Tarime na kukamata zaidi ya vijana hamsini kwa sababu za kisiasa. Na wengine wamekamata mpaka pikipiki na mali zao nyingine. Vijana wako, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu watanzania, wanakubali kutumika kisiasa kwa kuwa tu wanapata chakula toka kwa tajiri anayeitwa Zakaria ambaye pia anagombea udiwani kwa CCM Tarime. Naandikia ujumbe huu wa wazi uchukue hatua za haraka. Nami siku chache zijazo naelekea huko huko Tarime. Mtukamate wote mujaze mahabusu na magereza yote huko. Uchaguzi utakapokishwa, dhana nzima ya polisi jamii ambayo umekuwa ukihubiri itakuwa umepotea.

Wako katika ujenzi wa Taifa

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana-Taifa
0754694553
JJ

Mnyika,
  1. Hivi JF ni chombo cha habari au ndio CHADEMA inapotolea matangazo yake? Mbona chama kikubwa namna hii kinafanywa kuwa kama kikundi tu cha mitaani au chama cha wanafunzi?
  2. Imejulikanaje kuwa waliokamatwa wamekamatwa kwa sababu za kisiasa na sio vurugu au ubovu katika utendaji wa jeshi letu la polisi? Hebu tupe ushahidi ili tusione kuwa ni malalamishi tu ya kisiasa.
Nakubaliana na Mwjj kuwa kama kuna ushahidi, picha, video n.k. zitolewe, katika kuwafahamisha wana JF na sio kama ujumbe kwa IGP.

Halafu, unless tufahamishwe kuwa kuna uhusiano wa kimaslahi kati ya JF na CHADEMA, otherwise JF isitumiwe kutolea matamko ya vyama vya kisiasa kwa serikali. Tukifanya hivyo tusije tukalalamika JF ikija kuvamiwa tena.
 
Inasikitisha mwananzuoni kama Mwanakijiji kudai ushahidi wa picha ili kuamini kwamba kuna fujo. Kauli ya Msekwa mwenyewe inakueleza kwamba kuna fujo na kamata kamata. Kama watu wameshuhudia wasiseme kwasababu hawana picha? Matukio mangapi yanapelekwa mahakamani na kupatiwa hukumu bila watu kuwa na ushahidi wa picha?

La msingi hapa ni wewe kuelewa na kuamini kwamba hali huko Tarime ni tete. Yote haya yanachangiwa na siasa za mabavu za CCM. Hiyo kamata kamata, fujo, Wasira kutumia gari la serikali kwenye kampeni, shahada za kupiga kura za wapinzani kununuliwa na CCM ni sehemu tu ya hali tete. Tutarajie mabaya zaidi. Hasa hili la Mtikila kutumiwa na CCM kumpaka Mbowe na Silaa matope kwa kuwahusisha na kifo cha Wangwe.

Mwanakijiji ningeomba utusaidie kumuomba Mtikila ushahidi wa picha!!

Hivi nimetumia neno "ushahidi" mahali popote pale; umesikia nimesema kwamba Mnyika anadanganya au hayo aliyodai kutokea hayajatokea. Soma usikurupuke ili uelewe ni kwanini nimeuliza picha. Ukifikiria vizuri utakumbuka kuwa ni baada ya mimi kupata picha za watumishi wa Chadema kupigwa na Polisi kule Kiteto ndiyo kelele zilipigwa na hatimaye kutuma ujumbe mzito toka makao makuu!

fikiri kabla ya kurusha madongo!
 
Nimefikiria na kutafakari sana kabla ya "kurusha dongo". Naona hapa unajaribu tu kukimbia hoja. La msingi ni kwamba huamini thread ilivyoelezea hali ya kamata kamata na fujo huko Tarime. Kwa maneno yako mwenyewe ukasema "Leteni picha". Hii mimi ndio nimeiita wewe kudai "ushahidi". Why would you ask for pictures kama sio kutaka kuamini yale yalioandikwa? Na picha ndio ushahidi wenyewe unaoutaka wewe ili kuweza kuamini. Kauli yako imekuwa ya kejeli kidogo. Kwamba huamini watu na pikipiki wanaweza kukamatwa kwa wingi tena kwa wakati mmoja.

Picha zitakuja tu usiwe na wasiwasi bwana Tomaso. Just be patient mate!
 
Yanayoendelea Tarime yanatisha na nimekuwa naandika hapa kwa muda sasa. Kitendo cha Polisi (na sasa jeshi litahusishwa baada ya kauli za viongozi wa CCM kuwa Kikwete ni amiri jeshi mkuu na sasa ameambiwa kuwa Tarime kuna fujo) kuja kwa mamia Tarime na kuigeuza Tarime kama Baghdadi ni cha kukemewa na wapenda amani wote Tanzania.

Wito wa mzee mwanakijiji wa kuwa na picha ni wa muhimu sana ila pia ifahamike kuwa polisi wanakamata yeyote anayeonekana na kamera au kurekodi matukio na kuunganisha na wale wanaitwa "waleta fujo Tarime".

Makamba, Msekwa, Wassira, na viongozi wakuu wa ccm wakiondoka Tarime baada ya "Ushindi" wao kwenye chaguzi za Tarime (ubunge na udiwani), watakuwa wameacha makovu na matatizo makubwa kwa wakazi wa Tarime ambayo yatachukua miaka mingi sana kuyatibu na kuyatatua.
 
Ndugu IGP Mwema

Leo vijana wako msafara wa magari takribani ishirini wamefanya patrol Tarime na kukamata zaidi ya vijana hamsini kwa sababu za kisiasa. Na wengine wamekamata mpaka pikipiki na mali zao nyingine. Vijana wako, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu watanzania, wanakubali kutumika kisiasa kwa kuwa tu wanapata chakula toka kwa tajiri anayeitwa Zakaria ambaye pia anagombea udiwani kwa CCM Tarime. Naandikia ujumbe huu wa wazi uchukue hatua za haraka. Nami siku chache zijazo naelekea huko huko Tarime. Mtukamate wote mujaze mahabusu na magereza yote huko. Uchaguzi utakapokishwa, dhana nzima ya polisi jamii ambayo umekuwa ukihubiri itakuwa umepotea.

Wako katika ujenzi wa Taifa

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana-Taifa
0754694553
JJ

Asante Mnyika kwa hii habari, natumaini IGP akisoma hii habari uliyomtumia na akipata kinachoandikwa hapa atajua kuwa wengi hawafurahii kinachoendelea Tarime.

Hivi ushindi wa uchaguzi za ubunge na udiwani tu vina gharama kiasi gani?
Yaani CCM na majimbo yote waliyonayo hawawezi kuwaachia watu wa Tarime wakafanya chaguzi hizi kwa amani bila kubughudhiwa na kunyanyaswa na hao wanaotakiwa kulinda amani Tarime?

Hii nchi tunaelekea wapi? yaani madini ya Tarime na nguvu ya makampuni ya madini kwenye serikali yamefikia hatua ya kutumia mamia ya polisi kwenye hili suala muhimu kabisa kwenye demokrasia ya nchi?

Hii ni aibu kabisa kwa serikali na waendeshaji/wasimamizi wa uchaguzi.
 
Mpendwa napenda kukueleza kuwa nchi si muda mrefu itakuwa out of control, na kila mmoja anajua kuwa Kikwete haiwezi kabisa hali inayokuja kuikabili nchi siku za karibuni, huenda ndiyo maana anasafiri san. Lakini tuko katika wakati wa mabadiliko. Wataalamu wanaita Paradigm shift, toka katika hali ya kubweteka na kukubali kila kitu kuelekea katika democracia ya kweli na uwazi katika utendaji, na ili hali hii itokee ni lazima machafuko yaje.

Mimi si nabii wala mtoto wa nabii lakini nchi inakwenda kwenye machafuko na mauaji makubwa, lakini hilo halina budi litokee kama kweli Tanzania patakuwa mahali bora pa kuishi baadaye. Watanzania sasa wanatafuta uhuru wao, ndiyo maana unasikia migomo kila mahali na kila kukicha, na mara tu utasikia maandamano ya kila siku na muda utasikia watu wakiuuawa na polisi na damu itakapoanza kumwagika ndipo ukombozi wa Mtanzania dhidi ya mafisadi wa ccm utakapowadia.

Hivyo Watanzania myaonapo haya inueni vichwa vyenu juu maana ukombozi wenu umekaribia. Katika mapambano kama haya kamwe usitegemee kukosa wasaliti kama Mtikila, Mbatia, Mrema, Mvungi nk. hawa ni wasaliti na kama ukichunguza kwa undani sana utagundua kuwa wako kwenye payrol ya mafisadi.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.

Kwenye highlight;Mrema kamsaliti nani ni nani huyo/hao walioko kwenye hiyo payroll ya mafisadi?
 
Jamani huku tuelekeako kuna tisha jama! Yaani pesa mwana haramu, mtu anageuka kuwa kama roboti bila hata kutumia akili ya kuzaliwa? we unaambiwa kamata mtu tu bila sababu yoyte unatekeleza tu!!!

Hivi majeshi yetu kwanini wasitumie akili na kuwa huru kukataa kukiuka miiko yao ya kazi? nijuavyo wameapa kulinda raia na mali zao si kulinda maslahi ya kikundi cha watu wachache, kwanini wanapo ambiwa kitu ambacho si shahihi nao wasikatae?

Majeshi yetu matuangusha kwa kukubali kuwa vibaraka badala ya kusimama na kutetea haki kwa kadri ya viapo vyenu! Damu itakayo mwagiga itakuwa juu yenu milele.
 
Wiki iliyo pita nilikuja hapa na kusema maneno .Akaja Masatu na kundi lake wakasema tuache polisi walinde Nchi .Mie nilipenya kwenye kikao chao na mkakati wao umekuwa ni CCM kushinda Tarime .Tossi ndiye kinara akisaidiwa na mtu anaitwa Anaclet .

Tarime vijana wanasema watahubiri upendo na kwamba hawa taanza vurugu ila wataachia polisi uacha .Mwema anajua sana .Msekwa anajua kwamba wanatumia Ubabe .Wasira anajua wanacho kipanga .Lowasa anawajua watu wa Tarime na hakuwapenda hadi anaondoka madarakani kwa wizi wake ,JK anaijua Tarime vyema maana yeye aliwahi kwenda kutaka kutetea Halmashauri akabwagwa kwa aibu na pesa zake .

Tarime ni Iraq ndugu zanguni.Mniamini kabisa.Kuna maafa na watu watakufa kwa jina la CCM kutwa jimbo .Tambwe , Makamba , JK , Msekwa they care nothing about people life but power na kuendeleza wizi na Ubabe .RPC wa Mara ni mbabe akisaidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara .Tarime itaweka historia na baada ya Uchaguzi mtasikia mengi .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom