Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Haya mambo watu wanajifanya kumlaumu Mtikila hawajui kibao kinaweza geuka.

Mtikila KASEMA na anayeona hatendewi haki angechukua vipeperushi hivyo akatinga navyo mahakamani

Sitoshangaa na siku zaja
Pale DR SLAA atakapobondwa mawe kwa kuwaita jamaa MAFISADI maana atakua naye ni mchochezi.
Ama siku hiyo mtasema ambaye hakupendezwa na maneno yake angeenda polisi na mahakamani??
 
Yule mchungaji matata anayeitwa Mtikila, hivi pundwe amepelekwa hospitali kulazwa na kushonwa nyuzi baada ya kupigwa mawe na wananchi wenye hasira. Mtikila alipata dhahama hiyo baada ya kuhutubia kuwa Mbowe na CHADEMA yake ndio waliomuua Chacha Wangwe.

.......ndiyohiyo

Akome,huyu naye amezidi kutapatapa na kauli zisizo na manufaa yoyote sanasana kuleta chuki na uhasama ktk jamii.Mtikila amefeli kama mwanasiasa anachotakiwa kukubali ni kuwa siasa sio uwanja wake atafute njia nyigine ya kujipatia umaarufu na ulaji. Asipoangalia next time sio mawe tena; atapigwa na vingine ambavyo vitamgharimu maisha yake. Sippendi na wala sijawahi kupenda uchochezi wa Mtikila, in the name of politics.
Shame on you the so called Mchungaji Mtikila, your game theory is way below standard.
 
M.M. MKJJ

Unaonaje utusaidie kufanya mahojiano na mkuu wa polisi wa eneo hilo tujue kilichojiri huko Tarime.
 
Hivi huyu jamaa yuko relevant kweli? Kuna mtu anayemsikiliza siku hizi? Na chama chake vipi? Kipo au kipo jina tu? Halafu ni mchungaji wa kanisa gani huyu Mtikila?
Yes Indeed, ni mchungaji na chama chake ni DP Kipo hadi huko Visiwani
 
Macho_Mdiliko,

Mengi anaingia vipi hapa especially katika siasa??

GM ... Mengi anamiliki vyombo vya habari ... na kuna wanasiasa ambao wanaona vyombo vyake vya habari vinawawekea kauzibe....
 
Mtanzania mie si mwana CCM wala CHADEMA, lakini maneno aliyoongea Mtikila na kugawa yale makaratasi yamenistua sana. Nafkiri hata wanaCCM wengi yamewastua, au mwezetu? Yale yale ya Simba Vs Yanga?

Sasa si wampeleke mahakamani? Msimamo wangu juu ya Wangwe niliutoa siku ile ile anakufa kwamba ile ni ajali. Kama kuna mtu anachochea vurugu au anasema uwongo basi polisi au hao waliotuhumiwa waende mahakamani. Sheria ndivyo inavyosema na wala sio kupiga watu.

Vurugu zote zinaanzia na mambo madogo kwa kuwatumia hao vijana wasio na kazi mitaani, mwisho wake ni nchi nzima kuangamia. Lazima tulaani vurugu zozote zile.
 
Huyu mtikila sawa na mpinzani wa zimbabwe sawa na mrema lipumba na wengine wengi waliowahi kupigwa katika harakati zao za kisiasa wanapigwa vichwani je tukiwapa uongozi vichwa vitafanyakazi tena jamani ?
 
Ni Mtikila huyu bingwa wa kupeleka kesi mahakamani,Ni Mtikila amemwomba rais alete Scotlandyard wachunguze kifo cha Wangwe (RIP) ??? Leo anatangaza wauwaji wa Wangwe (RIP)kwenye mkutano ??? Kama tayari anajua nani alimuua Wangwe (RIP) kwanini aanze kutoa majina ya wauaji wakati hata ombi lake la kuchunguza halijatekelezwa ? Nadhani Mtikila ana matatizo.
Nafikiri polisi kwa kutomkamata Mtikila wamefanya vema na waendelee kunyamaza dhidi ya waliomtandika kwani Extrajudicial itakuwa balanced....
Watu wanataka kujua nini watatendewa na mbunge mtarajiwa,Mtikila anaenda kuwakumbusha majonzi ya Mbunge wao kwa kuwapa taarifa zisizo na ushahidi (Nasema hazina ushahidi kwa sababu ni mhusika mwenyewe aliyeomba scotlandyard waje wachunguze angekuwa na ushahidi kwa Hulka ya Mtikila angekuwa tayari kwa DP kama sio kwa Majaji.
Namwombea apone haraka....
 
Mtikila ana hoja,inawezekana kweli CHADEMA wamemuua Wangwe.Who knows? hakuna haja ya kumpiga mawe aitwe adhibitishe.Basi
 
Huyu mtikila sawa na mpinzani wa zimbabwe sawa na mrema lipumba na wengine wengi waliowahi kupigwa katika harakati zao za kisiasa wanapigwa vichwani je tukiwapa uongozi vichwa vitafanyakazi tena jamani ?
Na wewe ule udhibitisho wa tuhuma za mama Kilango umeishia wapi?

Unamsema mwenzio
 
1. Kusema mtu amemuua mwingine ni kosa la jinai. Mwenye wajibu wa kufungua kesi ni jamhuri. Sio Mbowe, Mengi, Slaa, Mnyika wala Zitto. Hivyo, polisi wamkamate Mtikila.

2. Kusema kwamba asishushwe jukwaani apelekwe mahakamani nayo ni kituko kwa kuwa akishtakiwa leo kesi itaisha mwaka 2009 wakati uchaguzi wa Tarime ni Oktoba 12 mwaka 2008.

Huyu ndiye Mtikila, aliyefungwa jela kwa kusema CCM wamemuua Kolimba na aliyeshtakiwa kwa kuita maiti ya Nyerere kuwa ni MZOGA.

.......habarindiyohiyo
 
1..

.......habarindiyohiyo

Kusema mtu amemuua mwingine ni kosa la jinai. Mwenye wajibu wa kufungua kesi ni jamhuri. Sio Mbowe, Mengi, Slaa, Mnyika wala Zitto. Hivyo, polisi wamkamate Mtikila.
HIYO SIO MARA YA KWANZA KWA YEYE KUTOA TUHUMA KAMA HIZO HUYO KICHWA CHAKE KIMEPIGWA SANA SASA AMESHACHOKA HANA UWEZO WA KUFIKIRIA KAMA BINADAMU WA KAWAIDA , APELEKWE AKAPIMWE AKILI KWANZA

2. Kusema kwamba asishushwe jukwaani apelekwe mahakamani nayo ni kituko kwa kuwa akishtakiwa leo kesi itaisha mwaka 2009 wakati uchaguzi wa Tarime ni Oktoba 12 mwaka 2008.
UNA UHAKINA NA UNAYOSEMA ? HATA IKIISHA MWAKA 3000 SI USHAHIDI BADO HAUJAKAMILISHWA ?

Huyu ndiye Mtikila, aliyefungwa jela kwa kusema CCM wamemuua Kolimba na aliyeshtakiwa kwa kuita maiti ya Nyerere kuwa ni MZOGA

HUKO JELA WALIMGONGA SANA KICHWA CHAKE KAMA MORGAN WA ZIMBABWE HANA AKILI SAWA HUYU TUSIHANGAIKE NAE
 
Inaonekana siasa za nchi ya Tanzania zinakwenda kubaya, watu wamefikia kutokujali maisha wala mustakabali wa Taifa kuanzia upinzani mpaka walioko madarakani, wanachojali ni kupata madaraka kwa njia yoyote ile iliyo mbele yao.

Wasifikirie matatizo ya Somalia, Sierra Leone, Liberia, Burundi, Rwanda etc hayawezi kufika Tanzania......kuna siku kama watu hawatakaa chini na kujirudi yatafika yaliyowafika wenzetu halafu tutakaoumia ni sisi walalahoi tusioweza kukimbilia ulaya na marekani.
 
Mkuu Mtikila anafaidika kutokana na fedha aliyopewa na hao mabwana zake... Amepewa contract ya kuwachafua Mengi, Mbowe na Slaa.

I hope that is not the case; maana hadi mtu kurushiwa mawe itakuwa ni fedha ya kutosha kweli; on the other hand, sasa akiwa amelazwa hospitali atafanyaje kazi hiyo ya uchafuzi? On the other hand, je akitoka na kusema kuwa amesema kweli ndio maana amepigwa mawe na kuwa ukweli unauma si atajipatia mashabiki zaidi. On the other hand, inakuwaje kama kweli anachosema ndicho anachoamini kweli na hajatumwa na mtu yeyote? on the other hand.. (how many hands do I have..?)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom