Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mtikila anaponzwa na Fedha za Rostam. Alikopeshwa akashindwa kulipa, sasa yawezekana ameambiwa malipo yake ni kwenda kuibomoa Chadema huko Tarime kwa mbinu zozote zile.
Kwa kipigo hicho, anafanya malipo halali ya kuchukuwa fedha za fisadi!!

Kama anao ushahidi kuwa Chadema ndio walihusika na mauaji ya Wangwe, basi mahali sahihi pa kuutoa ni mahakamani maana kesi hiyo tayari ipo!
 
Katika nchi huru - kila mtu ana uhuru wa kusema/kuongea - sasa walitaka asiseme anayoyajua yeye?? Hao vijana wakamatwe na kuhojiwa kwani ujasiri wa kumpiga mtu mawe unatokana na nguvu iliyoko nyuma ya mpiga mawe - kama sio shetani basi rushwa/hongo au???????
 
Katika nchi huru - kila mtu ana uhuru wa kusema/kuongea - sasa walitaka asiseme anayoyajua yeye?? Hao vijana wakamatwe na kuhojiwa kwani ujasiri wa kumpiga mtu mawe unatokana na nguvu iliyoko nyuma ya mpiga mawe - kama sio shetani basi rushwa/hongo au???????

na hiyo nguvu aliyonayo Mtikila inatoka wapi kama si kwa mafisadi? Kwani t5umesahau jinsi alivyotumiwa kummaliza Sumaye kila kukicha Press Conference.

Huyu ni Mganga njaa tu na siku moja atakuja kulipia usaliti wake kwa WaTZ.
 
Lakini alionywa mapema asiende na gia ya kifo cha Chacha sasa kama ameingia kwa gia hiyo basi ndo mshahara wake....kwa nini asinge anza na sera za kummaliza Rostam?? angeenza na gia ile kuwa zile milioni 3 kesha lipa angefagiliwa...
 
...anacheza na poti? safi sana atie akili na aachane na siasa zake za kujenga chuki!!!
 
Wananchi walipandwa na hasira na kuwaomba polisi wamkamate kwa kufanya uchochezi lakini polisi wakamuacha aendelee kusema na kugawa makaratasi yenye maneno yake kuwa Mbowe, Mengi, Ndesa, Slaa, Mnyika na Zitto ndio waliopanga na kumuua Chacha Wangwe kwa kutuma vijana wamchome Kisu na baadaye kumpiga na nyundo. Hapo ndipo wananchi wakamgeukia na kumpiga mawe

..............habarindiyohiyo

Nimesoma waraka wa Mtikila aliotaja watu mbalimbali nikiwemo. Suala la majina yetu kuchafuliwa ni suala la madai. Kila aliyechafuliwa ana haki na uhuru wa kufungua au kutofungua kesi. Lakini kwa yoyote ambaye amesoma kwa ukamilifu waraka wake atakubaliana nami kuwa kuna madai ya kijinai ambayo kama tunajamhuri halali inayolinda utawala wa sheria itachukua hatua za haraka. Masuala ya jinai hayasubiri mtu binafsi kushtaki ni kazi ya jamhuri. Lakini ushauri wangu ni kuwa pamoja na hatua zozote zitakazochukuliwa ni vyema pia akapimwe akili. Nampa pole sana kwa madhila yaliyompata. Naamini vyombo vya dola vitachukua hatua mapema. Kadiri vyombo vya dola vinavyokaa kimya vinapunguza imani kwa wananchi na hatimaye wananachi wanajenga utamaduni wa kuchukua hatua wenyewe. Huu ni utadamuni wa cynicism ambao taratibu unaanza kumea katika taifa letu. Kosa moja halipaswi kuhalalisha kosa lingine lakini tukumbuke kuwa kosa moja linaweza kuzaa makosa mengine, kwa kutaka au kutokutaka.

Nawatakia mjadala mwema

JJ
 
Mtikila atakuwa alikwisha waandaa watu wa first-aid. He must have anticipated this reaction, and perhaps expected the worse




Hehehehe

Leo nimejikuta nacheka tu... This reminds me mswahili...

Yangu mimi macho!



Sijaelewa kwa nini watu wanasema Mtikila ameponzwa. Huko aliko akisoma magazeti atakuwa anacheka tu.

Mwenzetu anajipongeza na kutupia jicho kwenye the next item on the TODO list.



.
 
Lakini alionywa mapema asiende na gia ya kifo cha Chacha sasa kama ameingia kwa gia hiyo basi ndo mshahara wake....kwa nini asinge anza na sera za kummaliza Rostam?? angeenza na gia ile kuwa zile milioni 3 kesha lipa angefagiliwa...
Sidhani kwamba kusema Chadema wamemuua Wangwe pekee kunatosha kuwapa wananchi sababu za kumpa kura mgombea wa DP (Chama cha Mtikila)
Hilo hata yeye mwenyewe Mtikila analijua dhahiri. Sasa watu makini lazima wajiulize kwa nini anatumia nguvu nyingi na vipeperushi kwa hoja hiyo ya kifo cha Wangwe? sio bure ila kuna sababu tena nzito inayomfanya Mtikila akubali kuhatarisha maisha yake kuzungumza hayo ilihali alishaonywa asiyasemee Tarime.
Nilikuwa ninamheshimu sana Mtikila katika mapambano dhidi ya ufisadi na mengi ambayo yanaenda kombo hapa Bongo, ila kama itadhibitika kuwa matendo anayofanya sasa ni kununuliwa,kulipa fadhila ili afutiwe deni/madeni aliyokopa kwa mafisadi na mengine ya aina hiyo, basi atakuwa amejivua nguo hadharani yeye mwenyewe, na nitamdharau sana.
 
I do! He should stop poking his nose in other people's businesses.

Uhuru wa kuongea upo wapi sasa? Wanasiasa haiwezekani wakaongea kile watu wote wanafurahia kwani mtazamo wa mambo kwa watu wote si sawa. Kupigwa kwa Mtikila ni kukosekana kwa kupewa ulinzi madhubuti wa Polisi. Ni aibu kama Polisi hawatawakamata waliofanya hilo tendo.
Walioudhiwa wangeweza ondoka na kumwacha anaongea peke yake KAMA kichaa, hio ndio adhabu poa.
Kimsingi kama tutapenda kua na utawala wa kisheria TZ, si uungwana kuunga mkono kupigwa kwa Mtikila pamoja na kumchumkia kwako.
Wasipowajibishawa na kuadhibiwa wakosaji, si muda mrefu watu watapigwa kwa kusema hata kwa mambo yale tuyaonayo poa.
 
Jamani tusiwe wajinga wa kupumbazwa na mtu huyu kwa sababu tu amebeba jina la Uchungji..
Hivikweli mtu na akili zako unaweza kusimama mbele ya watu ktk mkutano na kutoa accusation kama hizo?.. Hivi kweli kuna kiongozi yeyote nchini anaweza kusimama na kusema kiongozi wa CCM fulani ndiye aliyemuua fulani tena jimbo la CCM na ukategmea kutoka salama!...
jamani huyu Mtikila hazimtoshi, kama kiongozi nilitegemea angekuwa akifikiria kwanza na pengine labda naye tuseme huyo mtu anayemwandikia speech zake ni mwendawazimu zaidi...Yaani hata hainingii akilni kabisa kwa kiongozi kuweka madai mazito kama haya kwenye kampeni badala ya kuyapeleka ktk vyombo vya Usalama....
Saizi yake kabisa waliompiga mawe sio viongozi wa Chadema ila ni wananchi wenye hasira! inawezekana kabisa kuwepo vijana wa CCM na vyama vingineyo... Kwani mwizi siku zote hapigwi mawe na mtu yule aliyeibiwa peke yake.. hupigwa mande!
 
...hivi gorofa la mtikila litaisha lini angalau aache huu usaliti ??..maana ni njaa tu inamsumbua....siamini kama huyu ni mtikila tuliyekuwa tunapigwa mabomu kwa ajili yake tukiwa university..tuliyembeba nkrumah....aliyesababisha watu wapate mzuka mara ya kwanza pale jangwani......

..alipokopa kwa rostam alisema alihitaji pesa za kumalizia kibanda chake.....mdomo umemsaidia mtikila kujenga gorofa kubwa...tatizo la kuifanyia gorofa lake finishing ....linamponza,....kama tujuavyo ukiwa na mfanyakazi akiumia kazini unahitaji kumfidia ...SASA MTIKILA KAUMIA AKIWA KAZINI ...NADHANI WALIOMTUMA NI BUSARA WAKIMFIDIA ILI AMALIZIE GOROFA LAKE....NANI AJUAYE KABDA AKISHAMALIZIA JUMBA LAKE ANAWEZA KURUDIA UZALENDO WAKE WA ZAMANI....HIVI KARIBUNI PIA WALIMPA MERCDES BENZ ...anayotembelea ..hasa baada ya kutembea kwa miguu hadi kukaribia kumaliza viatu vyake vyote.....baada ya lile guruwe lake kuwa juu ya mawe kwa karibu miaka kumi...
 
Unajua taifa likifika mahali sheria hazifuatwi kama sisi Tanzania, basi ni haki ya wananchi kuchukua sheria mikononi, kwa sababu Mtikila alitakiwa kuchukuliwa sheria tayari kwa kusema maneno ambayo hayana ushahidi,

Sasa kwa sababu maneno yake yanawafurahisha baadhi ya mafisadi, basi hakuna sheria angesema maneno hayo dhidi ya rais, au Mwalimu, ungesikia kuna sheria ya kumbana Mtikila lakini kwa sababu anasema dhidi ya Chadema na ni wakati wa uchaguzi, basi oooh hakuna sheria ya kumbana, sasa wananchi mlitaka wafanye nini? Tena wananachi wenyewe wa Tarime?

Piga mawe na fimbo, maana huyu walijua hata kumzomea tu haitoshi kama waliwafanyia viongozi wa CCM,

Wananchi wa Tarime tuko pamoja hapo!
 
Jamani Huyu Mchungaji feki ni yuleyule aliekuwa anamnyoshea RA vidole kumbe kahongwa Shs milioni 3 au zaidi. Sasa kaambiwa asizirejeshe ila atafute namna ya kukichafua chadema pamoja na watu fulani fulani ambao wanachonga saana kuhusu RA.
Matapeli wa siasa hiyo ndio dawa yao. Wanafikiri watanzania wataendelea kudanganywa tu!!!
 
Kitendo cha Mtikila kutaka kumwaga sumu ya chuki miongoni mwa Watanzania hakipaswi kuchukuliwa kwa uzito mdogo. Kipindi cha nyuma watu walimjengea imani kubwa kuwa ni mtetezi wa haki za wanyonge lakini imegundulika kuwa alivyokuwa anachukuliwa ndivyo sivyo. Gharama ya kusimamia uongo ni kubwa mno na kila achumae kwa njia dhambi malipo yake yatakuwa kwa njia ya dhambi.

Mtikila alifanya matatizo ya Watanzania kuwa ndio mtaji wake. Kitendo cha kusimama majukwaani mchana kutukana watu halafu jua likizama kuwafuata nyumbani kuchukua kitu kidogo kitamgharimu na kitamtesa maisha yake yote. Anajifanya kuwa ni mcha Mungu kumbe rohoni mwake ni amejaa unafiki, udhalimu na ulaghai mkubwa. Kama mchungaji na mtu wa Mungu hupaswi kuwagawa watu kwa kutoa mahubiri ya chuki. Anayoyafanya sasa ni maelekezo/masharti kwa yale aliyofanyiwa kwenye giza. Mdomoni ananena machukizo ya rushwa ilhal rohoni anajua maisha yake yamesimama kwa utegemezi wa rushwa. Anaowsema sasa wamekataa kushiriki udhalimu wake.

MTIKILA UMEMUASI NA KUMFANYIA DHIHAKA MUNGU WAKO, KAUNGAME UPATE HURUMA NA URUDI KWENYE KUNDI LA WACHA WAKE. KUMBUKA ADHABU YA UOVU UTAIPATA HAPA HAPA DUNIANI.

"WANA TARIME MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA KUWATANGULIA MFANYE UCHAGUZI WA AMANI NA MPATE VIONGOZI WAADILIFU NA WACHA MUNGU"
 
Mzee Mwanakijiji,

Hutakiwi kuwa genius kujua hilo katika mtililiko huu. Ni sawa na kule Kiteto wala hatukutakiwa kuwa genius kujua vijana wa CCM walipiga viongozi wa CHADEMA.

Hivi lile tendo la Kiteto la watu kupigwa vibaya ulitetea vipi ndugu Mtanzania ?Maana hapa unawaka sana na lile unalisemeaje ?Maneno ya Makamba na Msekwa na matumizi ya polisi unayasemeaje ?
 
Si tuliambiwa kuwa Makamba alimwahidi 50 million akafanye kazi ya kuwamaliza CHADEMA. Huo mshiko ni mkubwa na kuufanyia kazi inahitajika atoke jasho la damu.
Ndiyo hayo yaliyomkuta, na nina uhakika aliyatarajia.
Kupigwa mawe anafurahia maana anafanya justification ya dau la 50m. Yupo kazini huyo.
 
sawa kabisaa, watanzania ndo sasa wanaamka, bila friction hakuna fikra mpya, kwa hiyo mawe, rungu ni friction, muda si mrefu makamba naye yatamsibu, hakuna atakayezungumza utumbo eti ccm ni kiboko ya mafisadi nk, tunaelekea kwenye upande chanya.

vijana amkeni wakati ni huu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom