Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Yawezekana nayo imepikwa,kama ya mbowe ilipikwa ktk vyombo vya habari vingi tena kwa masaa kadhaa tu hii itashindikana nini kupikwa?

Harafu nahoja nyingine Kama kweli polisi wametumwa kukipa ushindi ccm kwanini hawakutumia hii advantage ya kupigwa mtikila kukamata wafuasi wa chadema mvua?

Kwasababu alisema JK na Ditto walikumbatiana.
 
Kwasababu alisema JK na Ditto walikumbatiana.

wepi waliotungua jiwe ndio walisema jk na ditto wamekumbatiana ama unataka kusema jk ametuma watu wakamtungue??

Swali hujajibu
swali ni hili kwanini kama hao polisi wametumwa kwenda kuibeba ccm hawakutumia fursa hiyo ya mtikila kutunguliwa kuwakandamiza wanachama wa chadema??
Na badala yake wamekamata viongozi wa chama kilichowatuma??
 
Katika uchaguzi mdogo unao endelea hivi sasa Tarime kuna mengi ya kujifunza.La msingi hata hivyo ni hili la CCM kutumia nguvu nyingi kupita kiasi.Tumeshuhudia bwana Steven Wasira akitumia hata gari la serikali kufanyia kampeini na hatimaye kuonywa.Tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa ngazi za juu kabisa wa CCM wakiongeza nguvu katika suala zima la kampeini.Na katika hali isiyo ya kawaida kabisa, hata Mtikila amekuwa 'drafted' kuongeza nguvu na hati za kupigia kura za CCM zinauzwa hovyo mitaani,ushahidi wa kijana yule aliyekamatwa mtaani ni dhahiri.Kwangu mimi hii ni ishara tosha kwamba CCM hawakubaliki tena na wako tayari kutumia mbinu zozote, hata chafu, kufanikisha adhma yao ya kupata kiti cha Tarime.Kama wangekuwa wanakubakika nguvu hizi zisingekuwa za lazima.Lakini ninalojiuliza mimi ni kwamba wanataka kumuongoza nani hasa,na wanachong'ang'nia ni nini?CCM wameshapoteza 'credibility'
kwa wananchi na hawaaminiki tena kabisa.Ni vema wakalitambua hilo na wakapisha wengine ambao wana nia ya kweli ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania.CCM wanakotupeleka siko,tunawaomba kwa nia njema kabisa waondoke.
 
Yawezekana nayo imepikwa,kama ya mbowe ilipikwa ktk vyombo vya habari vingi tena kwa masaa kadhaa tu hii itashindikana nini kupikwa?

Harafu nahoja nyingine Kama kweli polisi wametumwa kukipa ushindi ccm kwanini hawakutumia hii advantage ya kupigwa mtikila kukamata wafuasi wa chadema mvua?
Imepikwa? kauli kaitoa msemaji mwenyewe wa polisi utasemaje kuwa habari ya kupikwa? Labda utuambie kuwa huyo Polisi ndio kapikwa!
 
Mkuu Field Marshal,

Maneno mazito hayo.Kuna wakati huwa naona CCM na vibaraka wake wamedharau wannchi mpaka inabidi ku-apply mechanization.Wananchi inabidi muwe na ujasiri kupapambana na dhuluma yoyoyte inayosababishwa na Dola.Kama CCm itatumia dola vibaya ili kupata madaraka,basi mimi nitaungana na wananchi watakaokua wanakabiliana na hiyo hali.Ukandamizaji uwe mwiko.

Nguvu ya umma itumike kukabiliana na matumizi mabaya ya dola,hilo nitalikubali ikiwa gharama ya kupata haki ni lazima kupapambana.
 
Imepikwa? kauli kaitoa msemaji mwenyewe wa polisi utasemaje kuwa habari ya kupikwa? Labda utuambie kuwa huyo Polisi ndio kapikwa!

Hukunielewa.

mimi nasema ile ya kukamata wanachama wake na wa ccm na skendo la kupikwa kwanini isiwe hivyo?? kama la mbowe lilipikwa??
 
Hukunielewa.

mimi nasema ile ya kukamata wanachama wake na wa ccm na skendo la kupikwa kwanini isiwe hivyo?? kama la mbowe lilipikwa??
mkamap nimekuelewa ila habari ndio hiyo,
Mkuu umelisikia hilo la kukamatwa mtu ndani ya ofisi ya CCM akinunua shahada za kupigia kura? nadhani hata hili laweza kuwa la kupika?
 
mkamap nimekuelewa ila habari ndio hiyo,
Mkuu umelisikia hilo la kukamatwa mtu ndani ya ofisi ya CCM akinunua shahada za kupigia kura? nadhani hata hili laweza kuwa la kupika?

ehe
sijasikia mkuu ehe nani aliyemkamata? makomandoo wa chadema AMA makomandoo wa ccm yani polisi na takuru??
 
ehe
sijasikia mkuu ehe nani aliyemkamata? makomandoo wa chadema AMA makomandoo wa ccm yani polisi na takuru??
Mkuu commandos wa Chadema nafikiri ni sera zao hivyo Chadema hawawezi kukamata mtu. Vyombo vyote vya habari leo hii vimetoa mpaka picha ya mtuhumiwa. Msemaji wa Polisi keshadhibitisha hilo kutokea.
 
Mkuu commandos wa Chadema nafikiri ni sera zao hivyo Chadema hawawezi kukamata mtu. Vyombo vyote vya habari leo hii vimetoa mpaka picha ya mtuhumiwa. Msemaji wa Polisi keshadhibitisha hilo kutokea.

Sasa imekua je? CCM wakamkamata CCM mwezao?? mbona sielewi mkuu.

Maana hapo mwanzo tuliambiwa ccm yani polisi wamejazwa huko kuisaidia ccm makamba ishinde SASA huko ccm polisi ndio wanaisaidia ccm makamba ama inaku
je hiyo??
 
Imetolewa mara ya mwisho: 29.09.2008 0035 EAT

Mwanafunzi abambwa akiuza shahada

Na Richard Mwaikenda, Tarime

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Rebu wilayani Tarime amekamatwa kwa tuhuma za kuuza shahada tano za kupigia kura ikiwemo ya kwake mwenyewe.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Oparesheni Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Bw. Venance Tossi katika mkutano na waandishi wa habari ilisema mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Mahemba Daudi (1 alikamatwa saa nne asubuhi alipokwenda kuuza shahada hizo katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Tarime.

Bw. Tossi alisema baada ya vijana wa CCM kumkamata, walimfikisha kituo cha Polisi ambako alifunguliwa shitaka la jinai la kutaka kuuza shahada kinyume cha sheria.

"Tumemhoji mtuhumiwa kujua shahada zimemfikiaje, mpaka sasa nimeshatuma timu ya wapelelezi kufuatilia ili tujue nani walimtuma au kama zimeibwa," alisema Kamanda Tossi na kuongeza kwamba "Endapo itabainika, basi yeye pamoja na watakaohusishwa na tukio hilo watapelekwa haraka mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria."

Alipoulizwa kuwa kijana huyo ni mfuasi wa chama gani, Kamanda Tossi alijibu kuwa kazi ya Jeshi la Polisi si kujua hilo bali kwa vile shahada si mali ya chama chochote, ila cha muhimu ni kuwakamata watu wote wanaofanya biashara hiyo ya kuziuza kwani ni kosa la jinai.

"Anayeuza shahada na anayenunua wote wanafanya kosa la jinai, wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria, hivyo tunatoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo watamwona yeyote akiuza shahada," alisema Kamanda Tossi.

Kamanda Tossi alisema kabla ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilikuwa halijapata taarifa kutoka chama chochote kulalamikia biashara ya uuzaji shahada.

Naye George John anaripoti kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Zitto Kabwe amedai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) Bw. Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw, Yusuf Makamba wanachofanya Tarime ni usanii kwani chama hicho hakina rekodi ya maendeleo wilayani humo kwa zaidi ya miaka 40 tangu nchi ipate uhuru.

Akihutubia mkutano wa kampeni jana kwenye uwanja wa Shule ya msingi Nyamisangura, Bw. Kabwe alisema miaka miwili ambayo CHADEMA imeongoza halmashauri ya wilaya hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupata hati safi.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutolewa elimu bure ,kuimarishwa miundombinu ya barabara, zahati na mambo mengine.

" Makamba anapaswa ajibu fedha wanazolipiwa wanafunzi leo zimetoka wapi wakati huu wa CHADEMA na wakati wa CCM zilikuwa wapi?" Alihoji Bw. Kabwe.

Alieleza kusikitishwa na sera za CCM alizodai zimewafanywa Watanzania kukalia madini lakini yananufaisha watu wa nje kutokana na mikataba mibovu.

Alisema CHADEMA na wabunge wengine wa upinzani hawakubaliani na hali hiyo na wako tayari kufa ili Watanzania wanufaike na rasilimali zao.

"Wananchi wa Tarime kutupa moyo, chagueni upinzani ili uzidi kushughulikia EPA, Buzwagi na ufisadi mwingine," alisema Bw. Kabwe.

Katika mkutano huo, Bw. Kabwe alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema kumkamata mara moja, Bw. Makamba kwa kauli yake kwamba ameandaa vijana kushughulikia CHADEMA .

Alisema kauli hiyo ni sawa na kuanzisha jeshi ndani ya nchi. Alidai CCM imekuwa ikiwatumia Polisi lakini inasikitisha kwamba askari hao wanalipwa mishahara midogo kuliko nchi yoyote duniani huku viongozi wakizidi kuneemeka na kupanuka pengo kati ya masikini na matajiri.

Alilitaka Jeshi la Polisi pia kumkamata Mchungaji Mtikila kwa kile alichodai kueneza uongo kuwa CHADEMA ilihusika na kifo cha Wangwe.

Pia Bw. Zitto alimtaka Spika wa Bunge kuunda tume kuchunguza kifo hicho kwani alidai pamoja na uchunguzi wa Polisi kuhusu kifo hicho, CCM imezidi kuing'ang'ania CHADEMA kuwa imehusika na kifo hicho na kutumia suala hilo kama 'kete'muhimu katika kampeni zake.
 
Mmmmh atajifunza na huo ulimi wake nadhani alisahau kwamba ulimi uliponza kichwa.
 
Ni muhimu kufahamu kwamba Tarime ni mahali ambapo Mafisadi wanapatumia kutaka kujisafisha, na wanasema kwamba ufisadi uko mjini tena Dar pekee na kwamba Igunga, Monduli, Bariadi na Tarime hawajui ufisadi ni nini kwa hiyo watahakikisha wanashinda Tarime ili kuthibitisha maneno yao
 
Kwahiyo una maana gani ya kwamba wameigiza kumkamata huyo kijana ama chadema walimtungua Mtikila na polisi wakawakamata wafuasi wake ili kuhakikisha kua polisi wanafanya kazi bila kujali itikadi ya chama.

Mimi kinachonishangaza ni kua vyama vingine vyote hata vifanye nini ni maigizo Lakini chadema hongera nyingi wakati nao ni BIG ZERO.
 
mkamap unaweza ku save muda ukasoma na kuacha ama ungoje siku ukiwa na hoja nzito utaibuka maana inaonekana umechoka sasa unaelekea kupigana .Tujadili hoja ambayo ndiyo mada kuu na si kudivert issues
 
mkamap unaweza ku save muda ukasoma na kuacha ama ungoje siku ukiwa na hoja nzito utaibuka maana inaonekana umechoka sasa unaelekea kupigana .Tujadili hoja ambayo ndiyo mada kuu na si kudivert issues
Lunyungu,
Umemjibu vema Mkamap. Unajua yuko nje ya nchi anasoma huyu na mambo yanayoendelea hapa Tz hajui anadakia hoja tu huyu. Asubiri akimaliza shule aje aingie kwenye chama cha majambazi waendeleze.
 
Kwa hiyo hoja inadakiwa je? mkuu

Vyama vyote ni Majambazi CCM,CHADEMA,DP ,CUF nk,

Mimi nionavyo nina ona huruma watanzania wezangu kwa kutaka kuingizwa mkenge mwingine kwamba chadema ni mbadala.

CCM hovyo kama walivyo hovyo CHADEMA na DP,CUF na wengine.

kuendelea kuweka mategemo kwa vyama hivyo mnapoteza wakati tu SANASANA mnachofanya ni kuwapa MAFISADI yani wenyeviti wa vyama hivyo ulaji.
 
mkamap unaweza ku save muda ukasoma na kuacha ama ungoje siku ukiwa na hoja nzito utaibuka maana inaonekana umechoka sasa unaelekea kupigana .Tujadili hoja ambayo ndiyo mada kuu na si kudivert issues

Na fahamu hujakosea hilo jina ila umeandika makusudi kabisa

Eti kwa akili hii kweli hawa ni viongozi wa chama mbadala ??
 
Tehe Tehe, kho, nimefurahi sana huyu jamaa kutandika jiwe la kisogo. Natamani lingekuwa la jicho angekoma kuwa kuwadi wa Ufisadi.

majitaka.JPG
 
Na fahamu hujakosea hilo jina ila umeandika makusudi kabisa

Eti kwa akili hii kweli hawa ni viongozi wa chama mbadala ??

mkamap mimi unasema ? Nakuomba ubadili mwelekeo tujikite kwenye hoja na si vioja nk .Please
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom