Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Hii inaweza kuwa na maana kubwa sana, ambayo usipotumia kichwa na kukipa kazi kichwa chako hutaelewa na kuona kama huu uliofanyika ni uhuni.
MAUMIVU YA KICHWA HUANZA POLEPOLE

Naomba wajuzi wa sheria wanieleze kuhusu yafuatayo:

1. Je, fulana au kofia unayopewa na chama cha siasa ni mali yako ama vipi ?
2. Ukiacha kuwa mwanachama na hutaki tena kuivaa unatakiwa ufanye nini ?
3. Ukiwa na nguo halafu ukawa huitaki tena je una haki kuivua, kuitupa na hata kuichoma ?
4. Ukiamua kuitupa kwenye dampo je, hapo umefanya kosa ?
5. Kitu ambacho hukihitaji tena kinakuwa uchafu - sasa uchafu hufanywa nini. Je ni kosa kutupa, kufukia na hata kuchoma uchafu ?
6. Je ukiitupa kwenye dampo halafu ikaja kuchomwa kama uchafu wowote mwingine, nani atashtakiwa - wewe ama halmashauri ?
7. Je, ukiigawa kwa ndugu yako na akaivaa anaweza kukamatwa ?
8. Je, fulana na kofia ni takrima na kama ni hivyo inaruhusiwa kisheria?
 
Nawashauri mumuonee huruma MASATU. Kazi ya kulinda NGOME KUU ya MFUMO FISADI chini ya TABAKA NYANG'AU la kina Rostam and company unlimited sio ndugu jamani...

Chonde muone huruma jamani MASATU wetu.....

Tanzanianjema
 
Siku tutaikumbuka sisiemu kwa waliyoifanyia Tanzania miaka yote hiyo baada ya Mwl. Nyerere kututoka. Hii ni Idd wamswalie mtume. Kama wanaiba hadi wakati wa mfungo wa ramadhani yaani mwezi mtukufu wa toba, hii ni ajabu na kweli kama si waabudu mashetani na wachawi kwani hata toba hawafanyi kama yaliyosemwa ni kweli?
 
Kada aiweka pabaya CCM Tarime (Mwananchi)
Na Mussa Juma, Tarime

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), ambacho bado kinahaha kutatua mgogoro baina ya makundi mawili kwenye kampeni zake za ubunge na udiwani wilayani Tarime, sasa kitalazimika kufanya kazi ya ziada zaidi baada ya kada wake kukishutumu kwa kuteua 'Wa-Dar es salaam' kuongoza kampeni za ubunge wa jimbo la Tarime badala ya wazawa wa eneo hilo.

Kada huyo, Mwita Waitara, ambaye aliwahi kuvuliwa ukatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Tanga baada ya kutaka viongozi waliojiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, wavuliwe pia uanachama wa CCM, alikuwa akizungumzia kitendo cha CCM kumuondoa kwenye timu ya kampeni na nafasi yake kuchukuliwa na Hiza Tambwe kwa madai kuwa ni mzungumzaji mzuri.

"Ni vizuri vyama vya siasa vikawaachia watu wa Tarime wamchague mbunge wanayemtaka badala ya kulazimishwa," alisema Kada Waitara, ambaye sasa amehamishiwa makao makuu ya UV-CCM jijini Dar es salaam lakini jana alitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa msaidizi wa mwenyekiti wa UV-CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya G Five mjini hapa, Waitara alisema siasa za makada waliohamia CCM siku za karibuni kutoka vyama vya upinzani-Hiza na Shaibu Akwilombe- hazina nguvu kwa sasa na kwamba kutumia kifo cha mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Chacha Wangwe kwenye kampeni ni udhaifu mkubwa.

Siasa za Tarime si kama za Dar es Salaam," alisema kada huyo ambaye alisema bayana kuwa nafasi yake UV-CCM ni kama ya ukarani kwenye ofisi ya Mwenyekiti Emmanuel Nchimbi, hailingani na elimu yake ya chuo kikuu.

"Hapa kuna watu wamezaliwa wanajeshi bila ya kujiunga na jeshi... sasa ni muhimu sana watu wa Tarime wenyewe waachiwe kuchagua mbunge wao na hawa polisi ambao wamefurika hapa mjini wapelekwe kwenye mapigano ya koo.?p>

Waitara alisema ari yake kwenye kampeni hizo za kumpigia debe Cristopher Kangoye kuwania ubunge wa jimbo la Tarime imeshuka kutokana baada ya Nchimbi kumuondoa kwenye wadhifa wake kwenye timu ya kampeni.

Mimi ni mkazi wa hapa Tarime ni nitaendelea kukaa hapa na hata kama nikiondolewa kwenye kampeni za CCM wala sina wasiwasi kwani hata sasa wenzangu CCM wananiita eti mimi karani wa Nchimbi kweli roho inaniuma sana,?alisema Waitara.

Waitara pia alikituhumu chama hicho kwa kutumia fedha kwenye kampeni akisema haamini kama mbinu hizo zitasaidia.

"Mimi sina fedha lakini nilikuja hapa kugombea ubunge wa jimbo hili na nikashika nafasi ya tatu katika kura za maoni za CCM, lakini nilikubali matokeo na kumuunga mkono Kangoye," alisema.

Kuhusu tuhuma dhidi ya mafisadi walio kwenye chama hicho, Waitara suala hilo limekuwa kero kubwa kwenye kampeni zinazoendelea Tarime.

Waitara alisema ni lazima watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM wachukuliwe hatua ili kurejesha imani ya wananchi katika chama hicho.

Alisema bado anaamini kuwa aliyekuwa mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe alikuwa ni mtetezi mkubwa wa wananchi wa wilaya hiyo hasa katika masuala ya unyayasaji unaofanywa kwenye migodi ya Nyamongo, katika biashara za mipakani na maslahi ya wananchi wa Tarime kwa ujumla.

Mimi kama mkazi wa Tarime nitamuunga mkono wakati wote mgombea ambaye atashinda na kuendeleza yale aliyokuwa akitenda Chacha bila kujali anatoka chama kipi," alisema.

"Na atakayechaguliwa hatawatetea wananchi na hasa wanaodhulumiwa kwenye migodi ya Nyamongo na wengine, nitampinga.?p>

Kauli ya Waitara itaifanya CCM iangalie upya mwenendo wake kwenye kampeni hizo baada ya makundi kuibuka mapema kutokana na mgombea wa sasa, Kangoye kutoungwa mkono na kundi la mgombea aliyeshindwa na Wangwe, Christopher Gachuma, ambaye anaona kinara wa kundi linalomuunga mkono Kangoye, Kisyeri Chambili alimsaliti baada ya kutopita kwenye kura za maoni mwaka 2005.

Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alikanusha kuwepo kwa makundi hayo akisema kuwa CCM ionaendelea vizuri na kampeni zake.

Nani kakwambia kuna mgawanyiko sisi tupo vizuri na tunaendelea na kampeni na hata muda huu (jana mchana) nipo kwenye kampeni na mgombea wetu,?alisema Makamba na kukata simu yake na mkononi.

Katika uchaguzi huo mdogo ambao utafanyika Oktoba 12, vyama vya CCM na Chadema ndivyo vinapambana vikali kurithi kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wa Chadema, Chacha Wangwe.

Chadema imemsimamisha mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime, Charles Mwera kutetea kiti chao.
 
Chadema watabiri uchaguzi Tarime kuvurugika (Mwananchi)
Na Kizitto Noya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuna dalili za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Tarime kuvurugika kwa kuwa kampeni chafu zimezidi.

Chama hicho kimelitupia lawama jeshi la polisi kikieleza kuwa ndilo linalochangia kuvuruga kampeni za uchaguzi huo kikilituhumu kukiuka maadili na kuanza kusaliti dhamana ya kulinda amani.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema jana kuwa polisi wanaolinda amani jimboni Tarime wameanza kukiuka maadili na kujiingiza katika siasa.

"Hizi ni dalili mbaya kwa hatma ya uchaguzi kwani polisi ambao ndio walitakiwa kulinda amani na kuzuia uhalifu, wameanza kujiingiza kwenye siasa," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema hayo alipokuwa akizungumzia tukio la polisi kukamatwa akijaribu kununua kadi za Chadema katika kampeni za uchaguzi huo zinazoendelea jimboni humo.

"Sisi (CHADEMA) tunaamini huu ni mkakati maalum ambao tulishaanza kuupigia kelele tangu zamani kwani tulijua mapema kuwa watu wamepanga kutuhujumu,".

Alisema polisi aliyekamatwa akinunua kadi za CHADEMA ni sehemu ya mkakati huo kwani hakuna maelezo ya kuridhisha yakakayotolewa na jeshi la polisi kuhalalisha tukio hilo.

"Huyo ni askari mmoja tu ambaye tumemfahamu kwa kuwa amekamatwa, kama huo ni mchezo wao kuna askari wangapi ambao hawakukamatwa na bado wanaendelea na kazi hiyo," alihoji.

Alisema CHADEMA ina taarifa ya siri kwamba wapinzani wao wamepanga kuwahujumu na tukio hilo ni sehemu na hujuma hiyo iliyokwishaanza kwa staili mbalimbali.

Dk Slaa ameeleza hayo wakati tayari jeshi la polisi likiwa limezungumzia tukio la askari wake kukamatwa akinunua kadi za Chadema na kusema alifanya hivyo kama sehemu ya kazi yake.

Kiongozi wa Kikosi cha Operesheni Maalum ya jeshi hilo jimboni Tarime, Venance Tossi aliliambia gazeti hili juzi kuwa askari huyo ni wa kikosi chake ambaye alikuwa katika kazi maalum ya kikachero.

"Huyu ni askari wetu wa kikundi maalum cha intelligency aliyekuwa kazini. Sasa huwezi kuwatambua polisi wote na ndio maana alikamatwa,". alisema Kamanda Tossi.

Alisema mawazo yaliyojengeka kwamba askari huyo alilenga kufanya hujuma katika uchaguzi huo sio sahihi kwani alikuwa kazini na kukamatwa kwake ni ajali ya uwajibikaji.

"Ni vema nikwambie ukweli ili msiandike uongo. Huku tuna vikosi vingi sana ambavyo vinafanya kazi tofauti wengine wako kwenye sare na wengine wanavaa kiraia. huyo ni askari wetu, alikuwa kazini," alisema.

Septemba 29 mwaka huu askari polisi wa Kikosi cha Oparesheni Maalum, kinachoongozwa na Kamanda Venance Tossi, alikamatwa akiwa katika jaribio la kununua kadi 20 za uanachama wa Chadema.

Tukio hilo lilifanyika siku moja baada ya mwanafunzi wa kidato cha tatu kukamatwa kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) akisaka mteja wa kununua shahada za kupigia kura.

Matukio hayo mawili pia yametanguliwa na vituko vingi, kejeli, kurushiana maneno makali, mapambano na kupakana matope baina ya wagombea na wafuasi wa vyama vya siasa katika kampeni hizo za kumrithi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe.

Emmanuel Zacharia, ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Fujo (FFU) kutoka mkoani Arusha, akiwa miongoni mwa polisi 400 waliomwagwa wilayani Tarime kwa ajili ya oparesheni maalum ya kidemokrasia na kuzuia mapigano baina ya koo, alikamatwa juzi kwenye ofisi za Chadema akijaribu kununua kadi.

Imedaiwa kuwa askari huyo alienda kwenye ofisi za Chadema zilizoko Mtaa wa Saronge, kitongoji cha Serengeti majira ya saa 8:00 na kutaka kuonana na maofisa wa chama hicho kwa madai kuwa anataka kununua kadi za uanachama.

Hata hivyo kitendo chake cha kuomba kadi nyingi, kiliwastua wengine na hivyo hata kabla ya kutimiza azma yake, walinzi maalum wa Chadema, maarufu kama Blue Guard, walimchunguza na kubaini kuwa ni polisi.

"Baada ya kuingia ofisini, kijana huyo alionekana kuwa na wasiwasi, kitu ambacho kilitupa mashaka pia na tukamuweka chini ya ulinzi," alisema mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema, Dk. Ben Kapwani ambaye alisema hata baada ya kumbana askari huyo aligoma kutaja sababu za kununua kadi hizo

Kiti cha ubunge wa Tarime na udiwani wa kata ya Tarime Mjini kimekuwa wazi baada ya Chacha Wangwe aliyekuwa akishikilia viti hivyo vyote kufariki kwa ajali ya gari alipokuwa akisafiri kwa gari binafsi kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Lakini utata umezingira kifo chake kutokana na baadhi kuamini kuwa kilitengenezwa, kiasi cha mazishi yake kucheleweshwa ili kusubiri uchunguzi wa mganga kutoka Kenya, ambaye aliondoa utata kuwa mbunge huyo wa Chadema hakupigwa risasi kama ilivyodhaniwa.

Hata hivyo, utata wa kifo chake umeibuliwa tena kwenye kampeni na kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alijikuta akipigwa jiwe alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara akisema Wangwe aliuawa na Chadema.
 
Nawashauri mumuonee huruma MASATU. Kazi ya kulinda NGOME KUU ya MFUMO FISADI chini ya TABAKA NYANG'AU la kina Rostam and company unlimited sio ndugu jamani...

Chonde muone huruma jamani MASATU wetu.....

Tanzanianjema

Mkuu Tanzanianjema,

Vp tena mbona unakwenda personal hivyo? of all people basi hata wewe?... au ndio hoja zimeisha sasa
 
Zitto: Siogopi kukamatwa

na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na kushtushwa na matamshi yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba dhidi yake.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Kigali nchini Rwanda, alilokwenda kwa shughuli za kibunge, Zitto, mmoja wa wanasiasa vijana machachari, alisema matamshi ya Kolimba si ya kiongozi wa kiserikali bali ya kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Zitto ambaye hata baada ya kuwasiliana kwa simu na gazeti hili aliandika majibu yake kwa maandishi, alisema tishio la Kolimba la kutaka akamatwe akimhusisha na kosa la kuchoma moto fulana za kampeni za CCM halina nguvu zozote kisheria.

Alisema ili kuonyesha namna asivyotishwa na tamko hilo la mkuu wa wilaya, Zitto alisema atakaporejea Tarime kwa ajili ya kuendelea na kampeni kesho, hatasubiri kukamatwa, bali yeye mwenyewe atajipeleka polisi.

'‘Nipo Rwanda kwa shughuli za kibunge. Nitarudi Tarime Ijumaa. Huyo DC wa Tarime anaongea kama kada wa CCM. Sitasubiri polisi waje kunikamata, nitakwenda mwenyewe ili wanikamate," alisema Zitto kwa kujiamini.

Mbali ya hilo, mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema anaamini hakufanya kosa lolote ambalo linaweza kumtia hatiani hata kusababisha akamatwe.

'‘Nimefanya kosa gani la kukamatwa au anatishia. Ajue mimi siogopi chochote na ninasimama katika haki," alisema Zitto katika ujumbe wa maandishi alioutuma katika gazeti hili baadaye jana.

Akielezea kuhusu tukio lililosababisha DC huyo afikie hatua ya kutaka akamatwe, Zitto alisema, walichofanya vijana wa CHADEMA ni kuchoma moto fulana zao walizopewa na CCM na si bendera za chama hicho ambazo kimsingi husajiliwa kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa.

'‘Vijana walichoma fulana zao walizopewa na CCM. Hawakuchoma bendera ya CCM. Fulana hizo si nembo za CCM, kwani hazina hatimiliki na wala funala hazisajiliwi kwa msajili," alieleza Zitto katika maandishi yake.

Mbali ya hilo, alisema iwapo atakuta vijana waliochoma fulana hizo wamekamatwa atafanya kila linalowezekana kuwatoa ndani, kwani hatua hiyo ni ya kionevu.

Mwanasiasa huyo alisema vitisho hivyo vya DC Kolimba ni kielelezo kwamba, CCM sasa imefikia hatua ya kuanza kutumia maofisa wa serikali kutafuta ushindi kwa nguvu Tarime.

Alieleza pia kwamba, katika sheria za uchaguzi, mkuu wa wilaya hana mamlaka yoyote ya kuingilia mwenendo wa kampeni kama anavyojaribu kufanya Kolimba.

'‘Sio tu sijachoma fulana, bali pia hata hao vijana waliochoma kama wamekamatwa nitaenda kuwatoa polisi, kwani ni uonevu. CCM sasa wameamua kutumia maofisa wa serikali kutaka ushindi kwa nguvu. DC hana mamlaka yoyote katika uchaguzi. Yeye anatafsiri sheria za uchaguzi kama nani?

'‘Hebu aonyeshe sehemu ya sheria ya uchaguzi inayomtaja DC. Asihusike kabisa na uchaguzi kwani sheria ya uchaguzi haimtambui. Ametumwa na Makamba anaropoka, hanijui tu. Ahesabu siku zake za u-DC, kwani naona amechoka kazi. Hili ndilo tatizo la watu walioomba kura kwa wananchi na kisha kukataliwa, halafu wakapewa u-DC. wanakuwa watu wa kujipendekeza," alisema Zitto akimwelezea Kolimba ambaye amepata kuwa mbunge kabla ya kushindwa katika kura za maoni baadaye.

Wakati Zitto akitoa maelezo yake hayo, viongozi wa CHADEMA walioko Tarime, jana waliwasilisha malalamiko yao dhidi ya Kolimba kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Tarime (OCD), Constantine Massawe.

Mbali ya hilo, CHADEMA katika malalamiko yao, walimtaka OCD huyo kumhoji Kolimba kuhusu matamshi yake kwamba chama hicho kilikuwa kimeingiza vijana wa kundi la Mungiki kutoka nchini Kenya kwa nia ya kuvuruga uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa CHADEMA, Msafiri Mtemelwa, alisema DC Kolimba anao wajibu wa kutoa maelezo ya kuridhisha juu ya matamshi hayo.

"Huyu mtu anaonekana amekurupuka katika matamshi yake ya juzi, ikiwa ni pamoja na kuamuru kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama chetu, Zitto Kabwe, na hili la kuwepo kundi la Mungiki ambalo anaonekana kufahamu mahali lilipofikia na shughuli linayofanya mjini hapa.

"Ameagiza pia kukamatwa kwa Zitto huku akitambua fika kuwa hana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria na asiingilie kampeni," aliongeza Mtemelwa.
 
Kampeni Tarime: CCM wageukana

na Kulwa Karedia, Tarime
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoko Tarime imeanza kusambaratika baada ya mmoja wa makada na viongozi wa chama hicho kuwageuka na kuwashambulia wenzake hadharani.

Hatua ya kada huyo ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga, Mwita Mwikwabe Waitara, imesababisha kuibuka kwa hali ya kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa chama hicho walioko hapa kwa ajili ya kampeni za ubunge na udiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya G Five jana, Waitara alieleza kushangazwa kwake na propaganda za baadhi ya wanasiasa wanaotumia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe kama turufu ya kupata ushindi.

Huku akijua kwamba, kifo cha Wangwe kimekuwa kikitumia na chama chake na baadhi ya viongozi wa upinzani kama Christopher Mtikila, katika kujinadi, Waitara alisema wananchi wa Tarime wanahamu ya kusikia sera ambazo zitawasaidia kuwaletea maendeleo.

Mbali ya hilo, kada huyo wa CCM alieleza kushangazwa kwake pia na juhudi zinazofanywa na chama fulani cha siasa ambacho hakukitaja za kutumia vitisho na nguvu za Jeshi la Polisi na fedha kuwatisha raia kwa lengo la kumhalalishia mgombea wao ushindi.

Waitara ambaye alionekana moja kwa moja kukilenga chama chake, aliwataka viongozi wa kisiasa walioko Tarime kupiga kampeni na kuwapa uhuru wananchi wa jimbo hilo kuchagua mgombea wanayemtaka bila ya kutumia shinikizo lolote.

"Siridhishwi na mwenendo wa kampeni zinazoendelea katika uchaguzi huu mdogo hapa Tarime, ambako kunaonekana kuwepo na ushawishi wa chama fulani lazima kishinde kwa kutumia fedha na nguvu za Jeshi la Polisi, hatua ambayo itawaathiri zaidi wananchi wa Tarime na si mtu mwingine yeyote," alisema Waitara.

Akizungumza kwa kujiamini huku akisisitiza kwamba yuko tayari kukabiliana na matokeo yoyote kutoka ndani ya chama chake, Waitara alisema anaamini kuwa mshindi wa ubunge lazima awe yule mwenye uwezo wa kusimama na kuwatetea wana Tarime bila kujali anatoka CCM au Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika hatua nyingine, mwana CCM huyo alifikia hatua ya kuwaonya makada wenzake wa chama hicho waliopo Tarime kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, akisema wanapaswa kufanya hivyo wakijua kwamba wananchi wa jimbo hilo si kama wale wa Dar es Salaam na kwingineko, kwani wanao uelewa mkubwa wa mambo.

"Kuna timu ya wana CCM ambao wamekuwa hapa kwa ajili ya kuwanadi wagombea wao, napenda kuwatahadharisha kwamba siasa za Tarime si kama zile za Dar es Salaam...hapa watu wanauelewa mkubwa wa hali ya hapa Tarime," alisema Waitara.

Kada huyo wa CCM ambaye hivi karibuni alikuwa miongoni mwa viongozi wa UVCCM waliosimama kidete kumtetea Nape Nnauye ndani ya Baraza Kuu la jumuiya hiyo ya CCM, alieleza pia kusikitishwa kwake na hatua ya chama hicho kumuondoa katika eneo kubwa la kampeni na nafasi yake kuchukuliwa na Tambwe Hizza.

Kuhusu uamuzi huo, Waitara ambaye alieleza kushangazwa na uamuzi huo ambao alidai ulichukuliwa kwa maelezo kwamba, Tambwe, mmoja wa makada vipenzi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yussuf Makamba, alikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza kuliko yeye.

"Huu ni mkakati wa kutaka kunimaliza kisiasa, kwani haiwezekani nikashushwa kwenye gari na nafasi yangu kupewa Hizza, kwa madai kuwa eti anajua kujieleza vizuri. Sasa nimehamishiwa Kata ya Nyandoto kwa ajili ya kupiga kampeni," alisema Waitara kwa masikitiko.

Katika hatua ambayo inaonyesha dhahiri kukerwa na mwenendo wa ndani wa CCM, Waitara aliwahimiza wananchi wa Tarime kutoyumbishwa na kumchagua mbunge ambaye atakuwa mstari mbele kutetea mambo yote yaliyokuwa yanapiganiwa na marehemu Chacha Wangwe, kwani kufanya hivyo kutakuwa njia pekee ya kumuenzi.

"Napenda kuwaambia kwamba jambo kubwa ambalo sasa linawakabili wana Tarime ni kumchagua mbunge ambaye atasimama kidete kutetea na kulinda mambo yote aliyotetea marehemu Wangwe, yakiwamo ya wananchi kufukuzwa kwenye mgodi wa dhahabu wa Nyamongo, wananchi kukamatwa ovyo na kupigwa na wafanyabiashara katika mpaka wa Sirari," alisema Waitara.

Katika hatua nyingine, CHADEMA imemtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime (OCD), Constantine Massawe, kumhoji Mkuu wa Wilaya ya Tarime Stanley Kolimba kuhusu matamshi yake kwamba chama hicho kimeingiza vijana wa kundi la Mungiki kutoka nchini Kenya kwa nia ya kuvuruga uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12.

Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa, amewaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha viongozi wa chama hicho na Jeshi la Polisi mjini hapa kilichofanyika ofisini kwa OCD, kuwa Kolimba anawajibika kutoa ufafanuzi wenye maelezo ya kutosha juu ya matamshi hayo.

"Huyu mtu anaonekana amekurupuka katika matamshi yake ya juzi, ikiwa ni pamoja na kuamuru kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama chetu Zitto Kabwe, na hili la kuwepo kundi la Mungiki ambalo anaonekana kufahamu mahali lilipofikia na shughuli linayofanya mjini hapa," alisema Mtemelwa.

"Ameagiza pia kukamatwa kwa Zitto huku akitambua fika kuwa hana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria na kumuonya kuwa asiingilie uchaguzi," aliongeza Mtemelwa.

Kikao hicho kati ya OCD na viongozi wa CHADEMA, kiliwashirikisha pia mgombea ubunge wa CHADEMA, Charles Mwera na Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa chama hicho, Benson Kigaila, ambapo undani wa kilichojadiliwa hakikuweza kujulikana mara moja
 
Date::10/1/2008
Kada aiweka pabaya CCM Tarime
Na Mussa Juma, Tarime

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), ambacho bado kinahaha kutatua mgogoro baina ya makundi mawili kwenye kampeni zake za ubunge na udiwani wilayani Tarime, sasa kitalazimika kufanya kazi ya ziada zaidi baada ya kada wake kukishutumu kwa kuteua 'Wa-Dar es salaam' kuongoza kampeni za ubunge wa jimbo la Tarime badala ya wazawa wa eneo hilo.

Kada huyo, Mwita Waitara, ambaye aliwahi kuvuliwa ukatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Tanga baada ya kutaka viongozi waliojiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, wavuliwe pia uanachama wa CCM, alikuwa akizungumzia kitendo cha CCM kumuondoa kwenye timu ya kampeni na nafasi yake kuchukuliwa na Hiza Tambwe kwa madai kuwa ni mzungumzaji mzuri.

"Ni vizuri vyama vya siasa vikawaachia watu wa Tarime wamchague mbunge wanayemtaka badala ya kulazimishwa," alisema Kada Waitara, ambaye sasa amehamishiwa makao makuu ya UV-CCM jijini Dar es salaam lakini jana alitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa msaidizi wa mwenyekiti wa UV-CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya G Five mjini hapa, Waitara alisema siasa za makada waliohamia CCM siku za karibuni kutoka vyama vya upinzani-Hiza na Shaibu Akwilombe- hazina nguvu kwa sasa na kwamba kutumia kifo cha mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Chacha Wangwe kwenye kampeni ni udhaifu mkubwa.

“Siasa za Tarime si kama za Dar es Salaam," alisema kada huyo ambaye alisema bayana kuwa nafasi yake UV-CCM ni kama ya ukarani kwenye ofisi ya Mwenyekiti Emmanuel Nchimbi, hailingani na elimu yake ya chuo kikuu.

"Hapa kuna watu wamezaliwa wanajeshi bila ya kujiunga na jeshi... sasa ni muhimu sana watu wa Tarime wenyewe waachiwe kuchagua mbunge wao na hawa polisi ambao wamefurika hapa mjini wapelekwe kwenye mapigano ya koo.”

Waitara alisema ari yake kwenye kampeni hizo za kumpigia debe Cristopher Kangoye kuwania ubunge wa jimbo la Tarime imeshuka kutokana baada ya Nchimbi kumuondoa kwenye wadhifa wake kwenye timu ya kampeni.

“Mimi ni mkazi wa hapa Tarime ni nitaendelea kukaa hapa na hata kama nikiondolewa kwenye kampeni za CCM wala sina wasiwasi kwani hata sasa wenzangu CCM wananiita eti mimi karani wa Nchimbi kweli roho inaniuma sana,” alisema Waitara.

Waitara pia alikituhumu chama hicho kwa kutumia fedha kwenye kampeni akisema haamini kama mbinu hizo zitasaidia.

"Mimi sina fedha lakini nilikuja hapa kugombea ubunge wa jimbo hili na nikashika nafasi ya tatu katika kura za maoni za CCM, lakini nilikubali matokeo na kumuunga mkono Kangoye," alisema.

Kuhusu tuhuma dhidi ya mafisadi walio kwenye chama hicho, Waitara suala hilo limekuwa kero kubwa kwenye kampeni zinazoendelea Tarime.

Waitara alisema ni lazima watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM wachukuliwe hatua ili kurejesha imani ya wananchi katika chama hicho.

Alisema bado anaamini kuwa aliyekuwa mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe alikuwa ni mtetezi mkubwa wa wananchi wa wilaya hiyo hasa katika masuala ya unyayasaji unaofanywa kwenye migodi ya Nyamongo, katika biashara za mipakani na maslahi ya wananchi wa Tarime kwa ujumla.

“Mimi kama mkazi wa Tarime nitamuunga mkono wakati wote mgombea ambaye atashinda na kuendeleza yale aliyokuwa akitenda Chacha bila kujali anatoka chama kipi," alisema.

"Na atakayechaguliwa hatawatetea wananchi na hasa wanaodhulumiwa kwenye migodi ya Nyamongo na wengine, nitampinga.”

Kauli ya Waitara itaifanya CCM iangalie upya mwenendo wake kwenye kampeni hizo baada ya makundi kuibuka mapema kutokana na mgombea wa sasa, Kangoye kutoungwa mkono na kundi la mgombea aliyeshindwa na Wangwe, Christopher Gachuma, ambaye anaona kinara wa kundi linalomuunga mkono Kangoye, Kisyeri Chambili alimsaliti baada ya kutopita kwenye kura za maoni mwaka 2005.

Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alikanusha kuwepo kwa makundi hayo akisema kuwa CCM ionaendelea vizuri na kampeni zake.

“Nani kakwambia kuna mgawanyiko sisi tupo vizuri na tunaendelea na kampeni na hata muda huu (jana mchana) nipo kwenye kampeni na mgombea wetu,” alisema Makamba na kukata simu yake na mkononi.

Katika uchaguzi huo mdogo ambao utafanyika Oktoba 12, vyama vya CCM na Chadema ndivyo vinapambana vikali kurithi kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wa Chadema, Chacha Wangwe.

Chadema imemsimamisha mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime, Charles Mwera kutetea kiti chao.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Lunyungu,

Mwenyewe umeona hapa jinsi watu wanavyokuja na matusi badala ya hoja. Naona mkuu Masatu ameamua kula nao sahani moja.

Wengine hatuamini hizo sera za jino kwa jino, kwahiyo wache watukane wanavyotaka lakini
siwezi kuacha kuchangia na wala sitajiingiza kwenye hayo matusi.

Mkuu,

Kama huamini sera za jino kwa jino mbona unazishabikia? Acha usanii bro,tumeshakushtukia.

Katika maelezo yako hapo juu,hoja iko wapi mkuu? kwi kwi kwi!
 
CCM waanza kugeukana,he he he sasa sijui wasuluhishane au wapige kampeni.

Pia,mimi sitaki vurugu lakini kama jeshi la polisi limeshindwa kumdhibiti Mtikila kwa sababu anafanya mambo ya kuinufaisha CCM na kuihujumu chadema,basi ni bora wananchi wa Tarime wamdhibiti kwa kumchukulia hatua kali zaidi.Mtu mmoja hawezi kuwa source ya machafuko huku polisi wakimsimamia tu hivi hivi.

Unajua sometimes wananchi wanalazimishwa kuchukua sheria mkononi,sasa na ni bora wamtungue tena.Pathetic reverend,to hell with him!
 
Mkuu Lunyungu,

Hii habari imeshawekwa kule kwenye thread ya wagombea na uchaguzi.hata hivyo shukrani
 
mpaka hizi kampeni ziishe tutaona mengi. na kwa wanaosoma alama za nyakati huu ni mwanzao tu ngoma ni 2010
 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na kushtushwa na matamshi yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba dhidi yake.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Kigali nchini Rwanda, alilokwenda kwa shughuli za kibunge, Zitto, mmoja wa wanasiasa vijana machachari, alisema matamshi ya Kolimba si ya kiongozi wa kiserikali bali ya kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Zitto ambaye hata baada ya kuwasiliana kwa simu na gazeti hili aliandika majibu yake kwa maandishi, alisema tishio la Kolimba la kutaka akamatwe akimhusisha na kosa la kuchoma moto fulana za kampeni za CCM halina nguvu zozote kisheria.

Alisema ili kuonyesha namna asivyotishwa na tamko hilo la mkuu wa wilaya, Zitto alisema atakaporejea Tarime kwa ajili ya kuendelea na kampeni kesho, hatasubiri kukamatwa, bali yeye mwenyewe atajipeleka polisi.

‘‘Nipo Rwanda kwa shughuli za kibunge. Nitarudi Tarime Ijumaa. Huyo DC wa Tarime anaongea kama kada wa CCM. Sitasubiri polisi waje kunikamata, nitakwenda mwenyewe ili wanikamate,” alisema Zitto kwa kujiamini.

Mbali ya hilo, mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema anaamini hakufanya kosa lolote ambalo linaweza kumtia hatiani hata kusababisha akamatwe.

‘‘Nimefanya kosa gani la kukamatwa au anatishia. Ajue mimi siogopi chochote na ninasimama katika haki,” alisema Zitto katika ujumbe wa maandishi alioutuma katika gazeti hili baadaye jana.

Akielezea kuhusu tukio lililosababisha DC huyo afikie hatua ya kutaka akamatwe, Zitto alisema, walichofanya vijana wa CHADEMA ni kuchoma moto fulana zao walizopewa na CCM na si bendera za chama hicho ambazo kimsingi husajiliwa kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa.

‘‘Vijana walichoma fulana zao walizopewa na CCM. Hawakuchoma bendera ya CCM. Fulana hizo si nembo za CCM, kwani hazina hatimiliki na wala funala hazisajiliwi kwa msajili,” alieleza Zitto katika maandishi yake.

Mbali ya hilo, alisema iwapo atakuta vijana waliochoma fulana hizo wamekamatwa atafanya kila linalowezekana kuwatoa ndani, kwani hatua hiyo ni ya kionevu.

Mwanasiasa huyo alisema vitisho hivyo vya DC Kolimba ni kielelezo kwamba, CCM sasa imefikia hatua ya kuanza kutumia maofisa wa serikali kutafuta ushindi kwa nguvu Tarime.

Alieleza pia kwamba, katika sheria za uchaguzi, mkuu wa wilaya hana mamlaka yoyote ya kuingilia mwenendo wa kampeni kama anavyojaribu kufanya Kolimba.

‘‘Sio tu sijachoma fulana, bali pia hata hao vijana waliochoma kama wamekamatwa nitaenda kuwatoa polisi, kwani ni uonevu. CCM sasa wameamua kutumia maofisa wa serikali kutaka ushindi kwa nguvu. DC hana mamlaka yoyote katika uchaguzi. Yeye anatafsiri sheria za uchaguzi kama nani?

‘‘Hebu aonyeshe sehemu ya sheria ya uchaguzi inayomtaja DC. Asihusike kabisa na uchaguzi kwani sheria ya uchaguzi haimtambui. Ametumwa na Makamba anaropoka, hanijui tu. Ahesabu siku zake za u-DC, kwani naona amechoka kazi. Hili ndilo tatizo la watu walioomba kura kwa wananchi na kisha kukataliwa, halafu wakapewa u-DC. wanakuwa watu wa kujipendekeza,” alisema Zitto akimwelezea Kolimba ambaye amepata kuwa mbunge kabla ya kushindwa katika kura za maoni baadaye.

Wakati Zitto akitoa maelezo yake hayo, viongozi wa CHADEMA walioko Tarime, jana waliwasilisha malalamiko yao dhidi ya Kolimba kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Tarime (OCD), Constantine Massawe.

Mbali ya hilo, CHADEMA katika malalamiko yao, walimtaka OCD huyo kumhoji Kolimba kuhusu matamshi yake kwamba chama hicho kilikuwa kimeingiza vijana wa kundi la Mungiki kutoka nchini Kenya kwa nia ya kuvuruga uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 12.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa CHADEMA, Msafiri Mtemelwa, alisema DC Kolimba anao wajibu wa kutoa maelezo ya kuridhisha juu ya matamshi hayo.

“Huyu mtu anaonekana amekurupuka katika matamshi yake ya juzi, ikiwa ni pamoja na kuamuru kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama chetu, Zitto Kabwe, na hili la kuwepo kundi la Mungiki ambalo anaonekana kufahamu mahali lilipofikia na shughuli linayofanya mjini hapa.

“Ameagiza pia kukamatwa kwa Zitto huku akitambua fika kuwa hana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria na asiingilie kampeni,” aliongeza Mtemelwa.
 
hajafanya kosa aogope nini? Waliochoma bendera za ccm ni wanachama na si yeye
 
Tarime ina historia nadhani Kolimba kalewa sana pesa za wale jamaa wa mgodini .Alikaa hapa Mabiti kichwa maji aliishia Mahakamani na sasa yeye nadhani anacheza na moto .Hivi kazi za wakuu wa Wilaya na Mkoa ni zipi hasa ?
 
Mkuu Ben asante nilikuwa sijaiona .Samahani maana inaonekana nimekurupuka jamani mnisamehe .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom