Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Kuna taarifa kwamba helikopta za CCM hazijakaguliwa wala kulipiwa kodi. Chadema waliambiwa wazi kwamba hawawezi kupitia Sirari kwa kuwa hakuna Airport ya kuweza kukaguliwa na watu wa TRA na idara nyingine lakini CCM wamepitia Sirari bila kukaguliwa. Inawezekana hata hizo fedha za kulipia gharama zinaweza kurudi kiulaini kama haijakaguliwa
 
Msimamo wangu uko pale pale.
CHADEMA wapuuzi kama walivyo CCM.
CHADEMA wanatumia fedha za posho kuruka na upuuzi mtupu wakati wapuuzi wengine CCM wanatumia EPA kuruka na chopper.
Tatizo lako Ben bado hujanielewa na hutokaa unielewe .

Msimamo wangu ni ule ule CHADEMA na CCM ni wote bomu hawana sera zozote na kuendelea kutegemea CHADEMA eti chama mbadala LABDA mbadala ktk kuendeleza ufisadi.

Hizi posho ndizo zinaishia makao makuu kwa deni baada ya uchaguzi,mtaendelea lini.mkimaliza hapo mtalipa deni la helkopita hiyo mpaka 2010,Na 2010 mtakopa tena mpae na helkopita mkimaliza hapo mtalipa deni hadi 2015 na 2015 mtakopa tena.Mtakiendeleza lini ninyi hicho chama.



Aaa wapi,huna msimamo wowote.Hata kichaaa husimama barabarani magari yanakopita,akiaambiwa toka anasema msimamo wake ni huo huo.Kwi kwi kwi!


Naona umekuja na jipya kukiri CCM ni wapuuzi.Tafadhali usiwasingizie CHADEMA,we are very strategic,si afadhali CHADEMA wanaokopa na kufanya kazi kulipa kuliko CCM wanaoiba kutoka hazina ya walalahoi? For you it seems it makes sense! CHADEMA NI CHAMA MBADALA kwa hiyo kutoka Kukataa chama cha mafisadi na wezi (CCM) na ku-opt chama cha wakopaji kama ulivyodai wewe (CHADEMA) ni hatua kubwa sana,wewe huoni hilo?


Kwa mara nyingine nimekufunga bonge la bao 7-0
 
Wote wanatakiwa watupatie gharama walizotumia kwenye huu uchaguzi na wapi walipata hizo pesa. I wish our foreign donors come forth and twist their hands to demand the breakdown of their shameless spendings. How come that our major parties spend lavishly in a minor election with no regard to the stinking poverty our people are facing?

Nadhani unaongelea CCM maanake huo ndiyo utamaduni wa CHADEMA kuweka wazi matumizi ya fedha za kampeni.Immediately after 2005 election,CHADEMA declared the campaign expenses.Ilikua rahisi sana kwenye check and balance lakini CCM hadi leo hawajafanya hivyo.Kiambie hicho chama cha mapinduzi kitupe matumizi na kiasui cha fedha kilichotumika.

Kubwajinga,Mkamap,Mtanzania,fisadi mtoto,Gembe, Kibunungo na Masatu ulizeni gharama za kampeni ya chama chenu tangia 2005,au mnaogopa kufukuzwa uanachama maanake mnaweza kuwa mnaogopa yaliyomkuta Nape.

Si kulilia CHADEMA tu hapa huku mkishindwa kuhoji chama Chenu
 
Helikopta ya Mbowe yabomoa CCM Tarime
2008-10-09 12:31:04
Na Mashaka Mgeta, Tarime


Joto la kampeni za kusaka kiti cha ubunge jimbo la Tarime likiwa limepanda kuelekea upigaji kura Jumapili ijayo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya kada wake, Mwita Mwikwabe Waitara, kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Waitara ambaye alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga, kisha akajitosa kwenye kinyang\'anyiro cha uchaguzi huo mdogo akitafuta tikiti ya CCM kuteuliwa kuwa mgombea na kuambulia nafasi ya tatu, alianza kampeni dhidi ya CCM jana na kuonya kwamba chama hicho kinakaribia mwisho kwa kuwa kinakimbiwa na vijana.

Kada huyo aliyegoma uhamisho wa kwenda kuwa Katibu Muyeka wa Mwenyekiti wa UVCCM, alianza kuonyesha dalili za kuichoka CCM wiki iliyopita alipofanya mkutano na waandishi wa habari na kudai kwamba kampeni za chama hicho Tarime zilikuwa zimekosa mwelekeo, na kuwataka wanachi kumchagua mbunge yeyote hata kama ni wa Chadema.

Waitara awali alikuwa akimdadi mgombea wa CCM Tarime, Christopher Kangoye, lakini alilalalamika kuenguliwa rasmi na nafasi yake kuchukuliwa na watu aliosema wametoka makao makuu Dar es Salaam, lakini wasiojua siasa za Tarime.

Waliotoka makao makuu ni pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda, Tambwe Hiza.

Waitara jana alisema amefikia hatua ya kujiengua CCM kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa Chadema katika Jimbo la Tarime, Charles Mwera, uliofanyika mjini Sirari, wilayani hapa.

Katika mkutano huo, Waitara alikabidhi kadi yake ya UVCCM namba 572182 na kadi ya CCM namba AL 1216241 kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Akitangaza uamuzi wake huo, Waitara alisema amejiondoa CCM kutokana na kushindwa kuvumilia vitendo vya dhuluma na unyanyasaji wanavyofanyiwa wakazi wa Tarime anakotoka yeye.

``Wananchi Tarime wanapigwa sana na polisi, wananyanyaswa kutokana na shinikizo la CCM. Nimeshindwa kuvumilia kuwa ndani ya chama kinachonyanyasa baba zangu, mama zangu, dada zangu na kaka zangu, hivyo, nimeamua kutoka,`` alisema Waitara.

Aliongeza kuwa kujiondoa kwake CCM ni sehemu ya falsafa ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kusema kwamba: ``CCM si baba yangu wala mama yangu.``

Hata hivyo, Waitara aliionya CCM kuhusu kuchukia harakati za vijana wanaotaka kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho, akisema kwamba hali hiyo inasababisha vijana wengi wakichukie chama hicho.

``Ukiona chama kinachochukia vijana kinawapenda na kuwakumbatia wazee peke yao, chama hicho kinaenda kufa. Hivyo, CCM nayo inakwenda kufa,`` alisema Waitara.

Alisema yeye ni miongoni mwa watu walionufaika na fedha zilizotolewa na CCM katika kampeni zinazoendelea Tarime, lakini yuko tayari kufa kuwatetea wananchi maskini walio wengi jimboni humo.

``Sisi watu wa Tarime ni wanaharakati, hatuogopi kutetea haki zetu, nipo tayari kufia Tarime nikimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mwera,`` alisema Waitara.

Kampeni za jana za Chadema, zilifanywa na helikopta yenye namba 5Y-HSN iliyowasili mchana na kutua kwenye Uwanja wa Sabasaba, mjini Tarime.

Wakati helikopta hiyo ikitua, watu waliokuwa wakisikiliza mkutano wa kampeni za mgombea udiwani katika Kata ya Tarime Mjini kwa tiketi ya CCM, Peter Zakaria, kwenye uwanja wa Menonite, waliondoka katika mkutano huo na kuikimbilia helikopta hiyo.

Helkopta hiyo ilikuwa imewachukua Mbowe, Mwera, Waitara na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, ambao walifanya mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mogabiri, kabla ya kufanya mkutano mjini Sirari, mpakani na Kenya.

Akihutubia mkutano huo, Mbowe aliwataka wananchi wa Tarime wasimame imara kutetea haki yao kwenye uchaguzi kwani kazi ya kuondoa watu kwenye utawala ni ya hatari kwa wanaharakati wanaoshiriki.

NEC yaonya polisi wasio na namba Tarime

Nayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeonya kuhusu kuwepo askari polisi wanaoshiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime, bila kuwa na namba za jeshi hilo kwenye sare zao.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, alisema hayo jana, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari mjini hapa.

Jaji Makame, Mkurugenzi wa NEC, Rajab Kiravu, na maofisa wengine wa Tume hiyo, waliwasili jana mjini hapa, kushuhudia mwenendo wa kampeni na uchaguzi wa udiwani na ubunge jimboni humo.

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka vyama vya upinzani, hususan Chadema, wakilalamikia kuwepo askari polisi wasiokuwa na namba kwenye sare zao.

Jaji Makame alisema kwa mujibu wa sheria zilizopo, askari polisi hapaswi kutekeleza majukumu yake, bila kuwa na namba za kijeshi.

``Nitashangaa sana kama kuna askari mwajiriwa wa polisi aliyevaa sare hana namba,`` alisema na kumwagiza Msimamizi wa uchaguzi huo, Trasias Kagenzi, kufuatilia na kupata ufumbuzi wa kadhia hiyo.

Kwa mujibu wa sheria namba 1 ya mwaka 1985, polisi ni miongoni mwa wadau wanaosimamia uchaguzi nchini.

Jaji Makame alisema askari polisi anapaswa kuwa nje ya chumba cha kupigia kura kwa ajili ya ulinzi na kusimama nyuma ya mtu wa mwisho baada ya muda wa kupiga kura kufikia ukomo.

Mtikila amvulia kofia Mbowe Naye Mwenyekiti wa DP, Christopher Mtikila, amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anaheshimika kama `Mungu-mtu` kwa wakazi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Mtikila alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia mapokezi makubwa aliyoyapa Mbowe, alipowasili mjini hapa kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani, utakaofanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mtikila alisema inashangaza kuona, licha ya wakazi wa Tarime wakiwemo wafuasi wa Chadema kupigwa na vyombo vya dola, walipokuwa katika harakati za kumpokea Mbowe, bado walijitokeza kwa wingi kumlaki mwanasiasa huyo.

Mtikila amekuwa akimtuhumu Mbowe na watu wengine, kuwa walihusika katika mipango ya kumuua aliyekuwa Mbunge wa Tarime (Chadema), marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

Kauli hiyo, ilisababisha hasira kwa wakazi wa Tarime baada ya Mtikila kurejea hoja hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Starehe hivi karibuni, na hivyo kusababisha kupigwa mawe na kujeruhiwa kichwani.

Licha ya Mtikila viongozi na makada wa vyama vya CCM na NCCR-Mageuzi, wamekuwa wakiitumia hoja hiyo katika mikutano ya kampeni za uchaguzi huo, na kujikuta wakinusurika kupigwa ama kuzomewa.

``Ninawashangaa hawa watu Tarime, sijui wamelishwa nini na Mbowe, walipigwa, lakini bado wanaenda kumpokea Mbowe,?wanamfanya Mbowe kama Mungu-mtu,`` alisema.

Hata hivyo, Mtikila aliukejeli umati wa watu waliomlaki Mbowe, na kusema uliwahusisha wahuni wanaovuta bangi na kunywa pombe haramu ya gongo.

Kwa upande mwingine, Mtikila alidai kuwa DP, NCCR-Mageuzi na CCM, vinatekeleza mpango wa kuhakikisha Chadema inashindwa katika uchaguzi huo.

Alidai kuwa wameamua kuwa na mpango huo kwa sababu matumizi ya fedha za umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo wilayani Tarime, zinafujwa na uongozi wa halmashauri hiyo inayoongozwa na Charles Mwera, ambaye pia ni mgombea ubunge kupitia Chadema.

Alisema nakala ya matumizi ya fedha hizo, iliwasilishwa kwake na NCCR-Mageuzi kupitia kwa maofisa wa serikali ya CCM ambao hata hivyo hakuwataja.

``CCM na NCCR-Mageuzi wanazungumza kuhusu ukweli huu? wenzetu NCCR walishaanza, tunachotaka ni kuwatendea haki wananchi wa Tarime,`` alidai.

Waziri adai polisi wako ngangari Tarime

Naye Simon Mhina anaripoti kuwa serikali imesema Jeshi la Polisi limejizatiti vilivyo kuhakikisha uchaguzi mdogo wa Tarime unafanyika kwa amani na kusisitiza kwamba halitasita kutumia nguvu iwapo wanasiasa watachochea fujo kwa kisingizio cha demokrasia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki, alisema suala la kampeni za uchaguzi huo pamoja na upigaji kura kukamilika kwa amani, bila mabomu limo mikononi mwa wanasiasa.

Hatuwezi kuachia vurugu yo yote, hatuwezi kukubali kuona watu waovu wanafurukuta, tunataka uchaguzi ufanyike kwa amani, alisema.



SOURCE: Nipashe
 
Ni Mwita Mwikabwe, aliyeshtukia mchezo kuwa wamemtosa katika kugombea ubunge wa Tarime kama alivyotarajia, kwasababu ya fedha zilivyomwagwa.

Mbaya zaidi, hakutarajia kilichotokea, as alidhani watampa hata ukurugenzi wa kampeni huko Tarime, wakamtosa tena, wakampa Tambwe Hizza.

Kama hiyo haitoshi, Mwikabwe wetu akaanza kushambulia timu ya kampeni ya CCM jinsi ilivyokuwa ikitumia agenda ya kifo cha Wangwe kama nyenzo, akawaponda sana kama 'alivyoozoea kuongea wakati ule akihamasisha migomo pale UDSM'.

Wakamshtukia. Wakaona huyu anataka kuwa Nape Nauye, ndani ya hii hii miezi miwili, hapana! Wakaamua kucheza tena ka-game. Bosi wake, Nchimbi, akamwita na kumwambia aende makao makuu ya UVCCM, amepatiwa kazi ya kufanya huko, ahame sasa kutoka Tanga kama katibu wa umoja huo wa vijana.

Rais mstaafu huyo wa DARUSO akawashtukia, akagomea hiyo ofa, akisema ni sawa na kwenda kuwa mtumishi wa kumletea chai Nchimbi. Akasema yeye ni msomi, tena ana shahada ya ualimu kutoka chuo maarufu Afrika, na duniani pia.

Hapa tukashtuka. Tukaanza kushangaa kuwa Waitara kakumbuka leo kuwa ni msomi?!Alikuwa wapi!! Mbona hakwenda moja kwa moja kwenye ajitra yake alipohitimu, akaonja chungu wanayopata walimu! mafao hewa, mishahara ya chini, na kila aina ya rabsha zinazowafanya wapange migomo isiyotekelezeka hatahivyo kwa kutishiwa kila leo na ahadi hewa za serikali yetu 'smart'!

Sawa. Kama aliamua kwenda kuwapigania wanyonge kwa kutumia siasa tu na si taaluma yake(kutoenda kwenye ualimu hata akaanzia ukatibu wa wilaya wa CWT), kwa usomi wake huo kweli, hakuyakumbuka machungu ya pale chuoni, KWELI KWELI AKADHANI URAHISI NI KWENDA UVCCM?

Tuna mashaka na huo uamuzi. Tukisema alitaka madaraka na kujinufaisha binafsi bila kuonja chungu ya wapiganaji halisi kama kina:

-Mnyika-aliyepokonywa ushindi pale ubungo,
-Zitto-alieonja machungu ya kufukuzwa bungeni na mgomo wa UDSM wa 2003 kugomea kuanzishwa bodi ya mikopo-akiwa Secretary General(Waziri mkuu wa DARUSO) ulivyomtesa
-Tweve, aliyekuwa chachu ya mgomo wa 2003 pia, lakini ndo wameenda kusomeshwa na CHADEMA na kuwa nguzo ya propaganda za kupambana na ufisadi
-Mrema, aliyekuwa waziri mkuu hapo DARUSO wakati Mwita akiwa Rais, jinsi alivyoenda mapema CHADEMA, na ndio wapanga mikakati myema ya kuokoa nchi hii na ufisadi.

Si hao tu;Wapo kina Mdee, Suzan Lymo, huwezi amini wote hawa walikuwa wanafunzi wa Mwikabwe katika Siasa. Tuseme mwalimu wao huu aliwasaliti? kisa, tamaa ama! Sasa jana ndio KAINGIA CHADEMA RASMI na kukabidhiwa kadi na kamanda Mbowe, tuseme alichelewa ama? je atailipa nini jamii aliyochelewa kuitumikia? Je aiombe radhi?Ndio, yametimia, lakini alikuwa wapi?
Tuna wasiwasi na maamuzi yake haya!

Samahani Mkuu 2003 Zitto alikua keshamaliza Chuo
Tweve hajapelekwe soma uingereza na Chadema.
Mdee na Suzan wote walimaliza chuo kabla ya mwita sidhani kama ni sahihi kuwaita wanafunzi wa Mwikabe.
Nadhani ucheki vizuri vitabu vyako vya kumbukumbu.
 
Helikopta ya Mbowe yabomoa CCM Tarime
2008-10-09 12:31:04
Na Mashaka Mgeta, Tarime


......

Hata hivyo, Mtikila aliukejeli umati wa watu waliomlaki Mbowe, na kusema uliwahusisha wahuni wanaovuta bangi na kunywa pombe haramu ya gongo.

Kwa upande mwingine, Mtikila alidai kuwa DP, NCCR-Mageuzi na CCM, vinatekeleza mpango wa kuhakikisha Chadema inashindwa katika uchaguzi huo.

....


``CCM na NCCR-Mageuzi wanazungumza kuhusu ukweli huu? wenzetu NCCR walishaanza, tunachotaka ni kuwatendea haki wananchi wa Tarime,`` alidai.

....


SOURCE: Nipashe

Huyu Mtikila mpuuzi kweli na anaaibisha nafasi ya uchungaji katika jamii ya watanzania. Yaani wananchi wa Tarime kwa maelfu ni wavuta bangi na wanywa gongo.

Huu ndio upuuzi nimekuwa naukataa hapa over and over again, kudharau na kudhalilisha wananchi wa Tarime kwa faida za kisiasa ni upuuzi wa hali ya juu. Huwezi kusema kuwa unataka kuwatendea haki wananchi wa Tarime at the same time ukiwaita kuwa ni wanywa gongo.

Mtikila alikuwa wapi wakati wananchi wa Tarime wakiuwawa na kuburuzwa toka migodini ili wazungu wapewe? Alikuwa wapi wakati ukatili ukitumika dhidi ya waliojaribu kupinga mauzo ya migodi kabla mikataba ya kueleweka na ya maana haijasainiwa? Mtikila alikuwa wapi wakati Wangwe, Sasi na wengine wengi walipokamatwa na kuwekwa ndani bila sababu ya msingi? Kwa nini Mtikila hakuungana na Tundu Lissu kushughulikia kesi za wana-Tarime wote waliokuwa wakinyanyaswa na polisi na wazungu migodini?

Mtikila ondoa upuuzi wako Tarime, watu kama nyie ni aibu kwa ukristo na taifa la watanzania.
 
Kuweza kuhisi matokeo ya uchaguzi siyo kuangalia helikopta, mikutano ya watu n.k siri iko kwa nani atajitokeza kupiga kura. Turn out ya election kwangu ndiyo msingi wa mambo yatakavyokuwa.

a. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa zaidi ya au karibu ya asilimia 50 ya wapiga kura na nje ya Tarime (vijijini) ikawa chini ya asilimia 40 na zaidi basi Chadema itashinda uchaguzi mzima kwa kati ya asilimia 60 na zaidi.

b. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa karibu ya asilimia 50 lakini kule vijijini ikawa zaidi ya asilimia 50 vile vile CCM itaweza kushindwa kwa margin ndogo sana a little under 50.

c. Endapo hata hivyo vyama vingine vilivyosimamisha wagombea ukiondoa CCM na Chadema vikiweza kupata asilimia 10 ya kura zote (which I really doubt) basi CCM itashinda!


I get it right
 
HATARI:

KUna taarifa za watu watatu kukatwa na mapanga mbele ya polisi Tarime na watuhumiwa kutoroshwa na gari la kiraia linalojulikana. Polisi badala ya kushughulikia watuhumiwa, wakakimbia na gari lao.

Saa moja baadaye uongozi wa polisi unafika eneo la tukio na wakati wanaendelea kukagua, gari lililowatorosha watuhumiwa linafika, na wananchi wanapiga kelele kusema hilo! Hilo!, linageuza na kukimbia, mkuu wa polisi anaamuri gari la polisi liwafukuze, dereva wa polisi anacheka na kukaidi amri ya bosi wake. GAri linatokomea na polisi wanaendelea kubaki walipo.

MAONI:
-Hii ni hatari na matokeo yake huenda kukazuka mauaji ya kutisha.
-Jimbo moja lisiwe mwanzo wa maafa kwa Watanzania
-JK lazima atoe tamko la kukemea na kuwaambia watu wake waache UJINGA
 
Mtikila ni mpuuzi sana,ndiyo maana nasema kwa hali kama hii akipigwa mawe kesho au kabla ya uchaguzi sasa sitalaani hicho kitendo.

Idiot Reverend!
 
HATARI:

KUna taarifa za watu watatu kukatwa na mapanga mbele ya polisi Tarime na watuhumiwa kutoroshwa na gari la kiraia linalojulikana. Polisi badala ya kushughulikia watuhumiwa, wakakimbia na gari lao.

Saa moja baadaye uongozi wa polisi unafika eneo la tukio na wakati wanaendelea kukagua, gari lililowatorosha watuhumiwa linafika, na wananchi wanapiga kelele kusema hilo! Hilo!, linageuza na kukimbia, mkuu wa polisi anaamuri gari la polisi liwafukuze, dereva wa polisi anacheka na kukaidi amri ya bosi wake. GAri linatokomea na polisi wanaendelea kubaki walipo.

MAONI:
-Hii ni hatari na matokeo yake huenda kukazuka mauaji ya kutisha.
-Jimbo moja lisiwe mwanzo wa maafa kwa Watanzania
-JK lazima atoe tamko la kukemea na kuwaambia watu wake waache UJINGA


My God, unaona tulikofika sasa? sasa wananchi wa Tarime nao wakiamua kupambana na polisi itakuaje? Maanke inaonekana hawana kipaumbele cha kulinda amani ya raia badala yake wapo huko for political purpose.aah! Enough is enough,lazima kuna kitu more than that.
 
My God, unaona tulikofika sasa? sasa wananchi wa Tarime nao wakiamua kupambana na polisi itakuaje? Maanke inaonekana hawana kipaumbele cha kulinda amani ya raia badala yake wapo huko for political purpose.aah! Enough is enough,lazima kuna kitu more than that.

Hapa naisikiliza BBc dira ya dunia na wanatangaza mtu mmoja kawakata watu sita kwa panga, mkuu wa polisi wa mkoa anasema kuwa ni wafuasi wa chadema inakuwaje mara moja wanajua waliofanya mbmao kama haya ni chadema na wala sio NCCR, CUF au CCM?
 
Aaa wapi,huna msimamo wowote.Hata kichaaa husimama barabarani magari yanakopita,akiaambiwa toka anasema msimamo wake ni huo huo.Kwi kwi kwi!


Naona umekuja na jipya kukiri CCM ni wapuuzi.Tafadhali usiwasingizie CHADEMA,we are very strategic,si afadhali CHADEMA wanaokopa na kufanya kazi kulipa kuliko CCM wanaoiba kutoka hazina ya walalahoi? For you it seems it makes sense! CHADEMA NI CHAMA MBADALA kwa hiyo kutoka Kukataa chama cha mafisadi na wezi (CCM) na ku-opt chama cha wakopaji kama ulivyodai wewe (CHADEMA) ni hatua kubwa sana,wewe huoni hilo?


Kwa mara nyingine nimekufunga bonge la bao 7-0

Daa kumbe wewe unafanya LIGI .kwi kwi
Tatizo ni kwamba CHADEMA hawakopi kwa njia halali ila wanakopa kwa njia ya kifisadi hilo chopa lenu mmelikopa milioni ngapi?

Tatizo ndilo lilelile sio kwamba kununua RADA ilikua UFISADI bali gharama zake ndio ufisadi.
Ndivyo hivyo kukopa sio ufisadi Lakini BEI hiyo na makubalioni ya malipo ndio UFISADI .Hili marehem Wangwe aliliona akalipigia KELELE mkamtimua.Sasa leo kwenye kampeni mnapowadanganya wana Tarime kumhedhi Wangwe
Je
1.Ni kumhedhi kwa kutimiliwa?
2.Ni kumhedhi kwa kushirikiana na FISADI RA kuhihujumu chadema?
3.Ni kumhedhi kushirikiana na KAbouru?
4.Ni kumhedhi kwa kushirikiana na Mziray kuihujumu CHADEMA?
5.Ni kumhedhi kwa kusema chadema chama cha kikabila?
6.Ni kumhedhi makao makuu kufisadi fedha za posho
7.Ni kumhedhi wabunge wanawake kuteuliwa kutoka sehemu moja
8.Ni kumhedhi kwa kuwa alikua pandikizi maalumu la ccm kuifutilia mbali chadema
Ama mnamhedhi kwa lipi? mnaowadaganya wana wa Tarime kweli mnawapiga mabao ya visigino.
 
Taarifa zilizothibitika kutoka Tarime zinaeleza kuwa wananchi wanne wa Tarime wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga na watu wawili kwa sababu zinazoweza kuwa za kisiasa.

Taarifa zinaeleza kuwa watu hao wanne walikuwa eneo amabapo helkopta inayotumiwa na CHADEMA katika kampeni za ubunge na udiwani ilikuwa inasubiria kutua.Wakati wananchi na wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanasubiri kuwasili kwa viongozi wa chama chao,ilitokea gari ambapo walishuka watu wawili wakiwa na mapanga na ghafla wakawavamia watu hao kwa kuwakatakata kwa mapanga.

Akithibitisha kuwahudumia watu hao hospitalini, daktari (jina ninalo) amethibitisha na kueleza kuwa mmoja wa majeruhi ameshonwa nyuzi kumi na tisa (19) kwa nje.Hakutaja idadi ya nyuzi alizoshonwa kwa ndani.

Hali hii inajitokeza zikiwa zimebaki siku tatu tu wanatarime watumie haki yao kikatiba kumchagua mwakilishi wao.
 
Umh! nimeisikia pia bbc dira ya dunia, hii aibu kwa Taifa zima, tuliwanyooshea vidole Kenya na Zimbwabwe kumbe na sisi ni hivyohivyo. Kumbuka hili ni jimbo moja je 2010 kukiwa na dalili za wazi za CCM kushindwa itakuwaje? si bora ya yale ya Kenya na Zimbwabwe? Mungu iponye Tarime na uibariki Tanzania.
 
My God, wapone haraka casulities. Hivi hakukua na askari? Hilo gari namba zake ni wa wapi?


Naona inatafutwa sababu kuahirisha uchaguzi ili CCM wakajipange upya.
 
Daa kumbe wewe unafanya LIGI .kwi kwi
Tatizo ni kwamba CHADEMA hawakopi kwa njia halali ila wanakopa kwa njia ya kifisadi hilo chopa lenu mmelikopa milioni ngapi?

Tatizo ndilo lilelile sio kwamba kununua RADA ilikua UFISADI bali gharama zake ndio ufisadi.
Ndivyo hivyo kukopa sio ufisadi Lakini BEI hiyo na makubalioni ya malipo ndio UFISADI .Hili marehem Wangwe aliliona akalipigia KELELE mkamtimua.Sasa leo kwenye kampeni mnapowadanganya wana Tarime kumhedhi Wangwe
Je
1.Ni kumhedhi kwa kutimiliwa?
2.Ni kumhedhi kwa kushirikiana na FISADI RA kuhihujumu chadema?
3.Ni kumhedhi kushirikiana na KAbouru?
4.Ni kumhedhi kwa kushirikiana na Mziray kuihujumu CHADEMA?
5.Ni kumhedhi kwa kusema chadema chama cha kikabila?
6.Ni kumhedhi makao makuu kufisadi fedha za posho
7.Ni kumhedhi wabunge wanawake kuteuliwa kutoka sehemu moja
8.Ni kumhedhi kwa kuwa alikua pandikizi maalumu la ccm kuifutilia mbali chadema
Ama mnamhedhi kwa lipi? mnaowadaganya wana wa Tarime kweli mnawapiga mabao ya visigino.

hivi kumhedhi ina maana gani?
 
Ndugu zangu watnzania Tumekuwa watu wepesi wa kusahau kwani hamkumbuki mateso kama hayo huwakuta ndugu zetu kule upande wa visiwa zanzibar kupigwa mapanga visu ubakaji sasa watanzania Tutasikia vilio vya kila upande
 
My God, wapone haraka casulities. Hivi hakukua na askari? Hilo gari namba zake ni wa wapi?


Naona inatafutwa sababu kuahirisha uchaguzi ili CCM wakajipange upya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amekaririwa akithibitisha kutokea kwa tukio hili baya lakini hakueleza chochote kuhusu kukamatwa kwa wahusika ama details zaidi.Inasemekana ni watu walikuwa wametumwa kwa kusudi la kujeruhi kama siyo kuua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom