Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,323
- 67
Huyu jamaa hamumjui, ni bonge ya mbumbumbu. Aliishia darasa la 7 hivyo hesabu ya 65+35+5=100 kumpiga chenga tusishangae jamani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
fidel,
mimi sina tatizo na chama au historia ya Ngawaiya. Mambo ya unazi wa vyama ndiyo yanaturudisha nyuma kila siku Tanzania na Afrika kwa ujumla hivyo sina tatizo na alikotoa majibu ya utafiti wake.
Tatizo liko kwenye math ya Ngawaiya - asilimia 65 kujumlisha asilimia 35 na kisha kujumlisha asilimia 5 - jibu lake linakuwa asilimia 105.
Sijui kuna uwezekano gani wa Tarime kuwa na asilimia 105 na wapiga kura.
Kuna watu wanaugua ugonjwa wa chuki katika forum hii. Wanapoona CHADEMA inapata nguvu na kuikabili CCM vilivyo huko Tarime wananuna kwa sababu wenyewe walishapitisha hukumu kwamba vyama vya upinzani havina kitu. Inawezekana ni kweli nyie wenzetu kwenye huu mtandao hamjasikia sera kutoka kwa wagombea. Hata hivyo wapiga kura wa Tarime wamezisikia. Wamesikia jinsi uongozi wao wa halmashauri chini ya CHADEMA ulivyoboresha maisha yao katika kipindi cha miaka miweli na nusu, ikiwemo kutoa elimu ya sekondari bure. Wamesikia mikakati ya kuwabana wawekezaji wa machimbo ya madini ya Nyamongo ili kuhakikisha kwamba mali asili hizi zinawanufaisha wananchi wa Tarime, na ndio maaana wameamua kuchukua "risk" ya kupigania haki zao na kuiunga mkono chadema.
Nasema tena poleni sana maoundits wenzangu wa online forum. Nawataarifu tu kwamba sisi wenzenu tuliopata nafasi kidogo ya kuonana na wananchi, yaani wapiga kura, tunaona jinsi ambavyo wananchi wameamua kuikumbatia CHADEMA kama chama mbadala. Inawezekana nyie wenzetu katika internet hamtambui hilo, lakini habari njema ni kwamba wananchi wapiga kura na hata CCM wenye wametambua hilo vizuri sana.
Haya nyie endeleeni kupiga ramli na kutoa laana, ngoja sisi tuendelee kufanya kazi ya wananchi. Ngoja nisogee tukampokee kiongozi mwingine anayekabidhiwa kadi ya chadema leo katika hizi kampeni. Andaeni kejeli na laana zingine, lakini tunaendelea kukata mbuga hadi kitakapoeleweka!
Mpaka leo sijasikia jambo la maana linalozungumziwa kuhusu mwananchi wa Tarime kutoka pande zote zinazogombania uchaguzi huu. Wamebaki kutambiana na kuonyeshana ubabe.
Taarifa za leo kutoka huko Tarime zinasema Chiligati ameomba radhi kwa niaba ya CCM kutokana na wafuasi wake kucharanga watu mapanga jana
MN,
Kuomba radhi hakutoshi, lazima wachukuliwe hatua pia. Karne ya 21 bado watu wanafikiri watashinda hoja kwa mapanga? Serikali lazima iwe strict na ujinga kama huo.
Kuweza kuhisi matokeo ya uchaguzi siyo kuangalia helikopta, mikutano ya watu n.k siri iko kwa nani atajitokeza kupiga kura. Turn out ya election kwangu ndiyo msingi wa mambo yatakavyokuwa.
a. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa zaidi ya au karibu ya asilimia 50 ya wapiga kura na nje ya Tarime (vijijini) ikawa chini ya asilimia 40 na zaidi basi Chadema itashinda uchaguzi mzima kwa kati ya asilimia 60 na zaidi.
b. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa karibu ya asilimia 50 lakini kule vijijini ikawa zaidi ya asilimia 50 vile vile CCM itaweza kushindwa kwa margin ndogo sana a little under 50.
c. Endapo hata hivyo vyama vingine vilivyosimamisha wagombea ukiondoa CCM na Chadema vikiweza kupata asilimia 10 ya kura zote (which I really doubt) basi CCM itashinda!
Kuna watu wanaugua ugonjwa wa chuki katika forum hii. Wanapoona CHADEMA inapata nguvu na kuikabili CCM vilivyo huko Tarime wananuna kwa sababu wenyewe walishapitisha hukumu kwamba vyama vya upinzani havina kitu. Inawezekana ni kweli nyie wenzetu kwenye huu mtandao hamjasikia sera kutoka kwa wagombea. Hata hivyo wapiga kura wa Tarime wamezisikia. Wamesikia jinsi uongozi wao wa halmashauri chini ya CHADEMA ulivyoboresha maisha yao katika kipindi cha miaka miweli na nusu, ikiwemo kutoa elimu ya sekondari bure. Wamesikia mikakati ya kuwabana wawekezaji wa machimbo ya madini ya Nyamongo ili kuhakikisha kwamba mali asili hizi zinawanufaisha wananchi wa Tarime, na ndio maaana wameamua kuchukua "risk" ya kupigania haki zao na kuiunga mkono chadema.
a. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa zaidi ya au karibu ya asilimia 50 ya wapiga kura na nje ya Tarime (vijijini) ikawa chini ya asilimia 40 na zaidi basi Chadema itashinda uchaguzi mzima kwa kati ya asilimia 60 na zaidi.
b. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa karibu ya asilimia 50 lakini kule vijijini ikawa zaidi ya asilimia 50 vile vile CCM itaweza kushindwa kwa margin ndogo sana a little under 50.
c. Endapo hata hivyo vyama vingine vilivyosimamisha wagombea ukiondoa CCM na Chadema vikiweza kupata asilimia 10 ya kura zote (which I really doubt) basi CCM itashinda!
CHADEMA wamejiandaa kukabiliana na jambo hili kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wananchi wa Tarime, wananchi wamejiandaa kulinda kura zao na haki zao .
TAARIME.
1. Kuna mabasi mawili ya Zakaria yanatokea jijini mwanza yakiwa yamewabeba wafanyakazi wa kiwanda cha Coca cola ambacho ni cha Gachuma na huku wakisindikizwa na escort ya magari mawili ya polisi moja nyuma na jingine mbele yanaelekea Tarime , kufanya nini , stay tuned.
2.Jana usiku ziliandaliwa hujuma eneo la mgodi kule Nyamongo na wamekamatwa vijana zaidi ya 120 , kwa kile kilichoitwa kuwa mgodi ulivamiwa .......
3.Usiku wa leo maeneo ya vijijini zimeandaliwa hujuma kuwa mifugo itaibiwa na haswa Ngombe ili kesho wanatarime badala ya kwenda kupiga kura basi wawe wanafuatilia mifugo yao na kata hizo zitakazohusika ni zile ambazo CHADEMA wananguvu kubwa na hilo ni kuhakikisha kuwa wapiga kura wanapungua.
4.Hujuma nyingine ambayo imeandaliwa kufanyika maeneo ya mijini ni kuwa CCM wamehimizana kwenda kupiga kura asubuhi na ikifika saa tano basi polisi watazua mtafaruku na kuanza kutumia nguvu kuhakikisha kuwa hakuna watu kwenda kupiga kura na hivyo kuipa CCM ushindi.
5.Mawakala wa NCCR NA DP wamekubaliana na wale wa CCM kuwa watoe tamko kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki , na hakuna kilichovuruga uchaguzi huo ,hata kama polisi watatekeleza mpango wa 4 hapo juu, .
CHADEMA wamejiandaa kukabiliana na jambo hili kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wananchi wa Tarime, wananchi wamejiandaa kulinda kura zao na haki zao .
kesho ntaweza kuwapa updates za kila wakati kuhusiana na upigaji kura , matukio kwenye vituo na kuhusu matokeo na hali halisi .