Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Nimetoka kuongea na Zitto Kabwe muda si mrefu nikitaka kujua matokeo ya kura pale Tarime, kifupi tu Zitto kasema "TUMECHUKUA!!!, TUMECHUKUA!!!!" akimaanisha Chadema imeshinda kiti cha Ubunge na Udiwani. HABARI NJEMA. Pole kwa wale wote waliokutwa na maswahib mbalimbali wakati wa kampeni na hatimaye sasa jibu limepatikana.
 
Naona hata magwiji humu wamewahi kujitangazia USHINDI wakati matokeo bado.

Kwa mujibu wa tume SISI ndo tunaongoza mpaka sasa!

Kidumu chama cha mapinduzi!

Nimetoka kuongea na Zitto Kabwe muda si mrefu nikitaka kujua matokeo ya kura pale Tarime, kifupi tu Zitto kasema "TUMECHUKUA!!!, TUMECHUKUA!!!!" akimaanisha Chadema imeshinda kiti cha Ubunge na Udiwani. HABARI NJEMA. Pole kwa wale wote waliokutwa na maswahib mbalimbali wakati wa kampeni na hatimaye sasa jibu limepatikana.

East=West.
Walisema subira yavuta heri?
 
tujiandae kwa yaliyotokea kenya na zimbabwe karibuni, nasikia harufu ya uchafu
 
Tume ya Uchaguzi wanatengeneza OMBWE ambalo linawapa wakati mgumu sana WANANCHI na POLISI kwa kuchelewa kutangaza matokeo haya.
 
Hengera sana CHADEMA! Jana nilikesha hapa kusubiria matokeo,leo nilikua na pepa lakini kimeeleweka.

Ushindi huu ni ushindi wa wapenda mabadiliko,wenye nia ya dhati na taifa letu tukufu,wachukia dhuluma,ufisadi,manyanyaso,fitina na vitisho.

Ni ushindi dhidi ya CCM na maluki wa upinzani,ni ushindi dhidi ya polisi wasio waadilifu,usalama wa taifa uliopoteza dira,tume isiokua huru ya uchaguzi,mfumo kandamizi usopenda demokrasia ya vyama vingi ishamiri na ni laana dhidi ya watumiao misiba kama kivutio cha wapiga kura,na ni ushindi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ili kuidhulumu haki na kiu ya mapinduzi.

Mungu awaponye wale waliomia na kudhalilishwa ktk mchakato huu,awaponye wenye majeraha ya Moyo na Mwili katika kusimamia kile walichoamini.Wanatarime kwa mara nyingine tena wamedhihirisha nguvu ya mabadiliko.

Ni mfano wa kuigwa katika taifa,nguvu wanazotumia polisi dhidi ya wanatarime wakati matokeo rasmi yakisubiriwa kutangazwa ni ishara nyingine ya kutokubali kushindwa.Hili jimbo lisiwe chanzo cha chuki,unyama na visasi.Hizo ni Rasha rasha kwa CCM,wasubiri nguvu kuu 2010.


Mungu Ibariki CHADEMA,wape uvumilivu wanatarime,Mungu Ibariki Tanzania
 
Wapinzani watu wa ajabu sana. Wanaanza mambo ya Zanzibar 1995..

Kazi ya kutangaza matokeo ni ya TUME sasa sijui kwanini mnatangaza wakati TAARIFA RASMI BADO.

Naona mnataka kuanza kulalamika mmeonewa hali ikiwa tofauti
 
Mbona huko Tarime kutamu,kwasisi ambao hatuna affiliation na chama chochote furaha yetu ni kuona kama demokrasia itakuwa imeachwa itendeke na hivyo wanatarime kwamaana ya wengi wape wakampata mbunge wao. Nitachukia kama kutakuwa na ripoti ya usanii kutendeka katika kumpata mshindi. Naamini akina Makamba,Tossi,NEC na wengineo wataheshimu maamuzi ya wakazi wa Tarime.
 
Naona hata magwiji humu wamewahi kujitangazia USHINDI wakati matokeo bado.

Kwa mujibu wa tume SISI ndo tunaongoza mpaka sasa!

Kidumu chama cha mapinduzi!
....Ndugu hayo mambo ya "SISI" safari hii Tarime hakuna ni kugaragazwa tu mchana kweupeeeeeeeee kudadadeki!!!!!!!
 
Vipi nasikia kuwa risasi zinarushwa kutawanya wananchi wanaokusanyika kwenye vikundi. Ni kweli?
 
Wapinzani watu wa ajabu sana. Wanaanza mambo ya Zanzibar 1995..

Kazi ya kutangaza matokeo ni ya TUME sasa sijui kwanini mnatangaza wakati TAARIFA RASMI BADO.

Naona mnataka kuanza kulalamika mmeonewa hali ikiwa tofauti

FP taarifa 2lizoleta jana usiku siyo batili.Hesabu ndivyo zilivyo kwa kuwa mahesabu yameshafanywa.

Kilichobaki ni kuyaabariki matokeo kwa kuyarasimisha tu.Hofu ya wanatarime kwasasa ni kuwa mara zote matokeo yanapocheleweshwa kutangazwa huwa kuna miundombinu flani.

Hata hivyo hali haitabadilika na wala hatukukosea kutoa taarifa mapema.Hii ndiyo JF Bwana!Habari zinaanzia nyumbani ati
 
Km hatutapigania Tume Huru ya Uchaguzi kuanzia hivi sasa (kwa nguvu zote!), mwaka 2010 tutakuwa tunajitangazia matokeo tu, km tufanyavyo hivi sasa, ambayo hayatakuwa na athari yoyote.
 
Nafurahi kwa sababu ndugu zetu Tarime wameonyesha kuwa inawezekana kabisa tukiamua.
 
.....Hatatoka katika hiyo ofisi mkuu!!! amini maneno yangu... Hata hao polisi hawatasimamisha msuli.

Safi sana.Akifanya mchezo tu,wamgeuze Goliathi ili iwe fundisho kwa chaguzi zijazo
 
Wakuu naona mshatangaza matokeo...! Nahisi yakitoka kinyume na matarajio kuna watu watazibamiza pc zao makofi. Yangu mi macho 🙂

Mkuu,

Tovuti yenu ina thread iliyoanzishwa na moderator wenu inayosema
"Chadema yaibwaga CCM Tarime, yachukua Ubunge, Udiwani!"

Sasa hapo huwezi kusema wewe yako macho. Nyinyi ndio mmeitangazia dunia matokeo.
 
bado official leo lazima wanioteshe kibarua hawa watu nashindwa ku Do work
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom