Hengera sana CHADEMA! Jana nilikesha hapa kusubiria matokeo,leo nilikua na pepa lakini kimeeleweka.
Ushindi huu ni ushindi wa wapenda mabadiliko,wenye nia ya dhati na taifa letu tukufu,wachukia dhuluma,ufisadi,manyanyaso,fitina na vitisho.
Ni ushindi dhidi ya CCM na maluki wa upinzani,ni ushindi dhidi ya polisi wasio waadilifu,usalama wa taifa uliopoteza dira,tume isiokua huru ya uchaguzi,mfumo kandamizi usopenda demokrasia ya vyama vingi ishamiri na ni laana dhidi ya watumiao misiba kama kivutio cha wapiga kura,na ni ushindi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ili kuidhulumu haki na kiu ya mapinduzi.
Mungu awaponye wale waliomia na kudhalilishwa ktk mchakato huu,awaponye wenye majeraha ya Moyo na Mwili katika kusimamia kile walichoamini.Wanatarime kwa mara nyingine tena wamedhihirisha nguvu ya mabadiliko.
Ni mfano wa kuigwa katika taifa,nguvu wanazotumia polisi dhidi ya wanatarime wakati matokeo rasmi yakisubiriwa kutangazwa ni ishara nyingine ya kutokubali kushindwa.Hili jimbo lisiwe chanzo cha chuki,unyama na visasi.Hizo ni Rasha rasha kwa CCM,wasubiri nguvu kuu 2010.
Mungu Ibariki CHADEMA,wape uvumilivu wanatarime,Mungu Ibariki Tanzania