Malunde-Malundi
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 1,288
- 131
Good News; Hii ni Zawadi ya Mwl Nyerere kwa wananchi wa Tarime ( by Zitto)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Belo, hakuna vita Tanzania, bali kuna ushindani, ingependeza kusema kuwa 'ingawa ushindani ni mgumu".
Nambari wani ni CCM.
Naona sasa JF inatumika kama chombo cha propaganda za CHADEMA. Iwapo moderators hawatakuwa macho juu ya hili credibility ya JF kwa jamii itashuka. Kichwa cha habari hii hakiko sahihi na kina ladha ya propaganda za CHADEMA, MODS mko wapi???
Kama ni kweli CHADEMA mmeshinda, basi 'hongereni zenu'.
CCM tulishasema kuwa tutakubali matokeo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kidumu Chama Tawala
Kwanza mods na mkuu invisible mmeniudhi sana leo hii!
Mbona mmebadilisha heading? Tafadhali rudisha heading "chadema yaibwaga ccm tarime"
au "ccm yaangukia pua tarime"
au "ccm yaona cha mtemakuni mbele ya chadema"
Kwanza mods na mkuu invisible mmeniudhi sana leo hii!
Mbona mmebadilisha heading? Tafadhali rudisha heading "chadema yaibwaga ccm tarime"
au "ccm yaangukia pua tarime"
au "ccm yaona cha mtemakuni mbele ya chadema"
Keep on dreaming. CCM ni nambari wani kwa kukumbatia mafisadi, kusaini mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa Watanzania, kama hutaki kuliona hilo utajiju. Kigumu chama cha mafisadi, kigumu!!!!
Ndugu yangu Ladslaus,
Hebu pitia thread ya Re: Zakaria ni nani huyu Tarime?.
I am not dreaming mkuu!
Nambari wani ni CCM
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kidumu Chama Tawala
(CCM itawale Tanzania hadi mwaka 2100).
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki CCM
Mwisho, niseme kwamba uchaguzi huu unaashiria mwisho wa siasa za ujanjaujanja. Siasa za akina Tambwe, Makamba na Akwilombe hazitawasaidia huko tuendako. Huko tuendako kinachotakiwa ni umakini, ukweli na uwezo.
...
Halafu as a nation imefika wakati wa kuliangalia tena suala la ruzuku in general, mimi ninafikiri umefika wakati wa ku- do away na ruzuku kwa sababu zinasaidia one thing only, nacho ni ku-off balance ushindani wa kweli wa kisiasa kwa taifa letu, na kudhoofisha kabisa upinzani wa kweli wa kisiasa nchini iondolewe au itafutwe njia nyingine ya kuleta balance haiwezekani chama kimoja kipate shillingi millioni 99, na vingine millioni 10, mpaka 30 halafu ukategemea kuwepo na ushindani ambao ni balanced na politically heathy kwa taifa.
......
maneno mzito sana mkuu fmes..lakini i beg to differ kuhusu ushiriki wa mwenyekiti wa chama.....mwenyekiti wa chama hangoji mwaliko ...kama amiri namba moja wa chama akisikia mbiu anaenda..ukizingatia safari ndefu alizokuwa nazo nje ..bado asingeshindwa kuchelewa mbeya kwa siku moja zaidi ili angalau afanye mkutano mmoja pale tarime...[mbona muda wa kwenda serengeti huwa anapata tena bila ratiba??]...
PM
Huyu anakwenda Serengeti kwenye mapumziko katika ile hoteli ileeee!
(ambayo wewe na mimi hatuwezi kuingia)
Wana ccm wenzako wengi wamekimbia forum kuanzia jana mkuu, Msekwa na wengine walikimbia toka Tarime kabla hata matokeo hayajatangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi. Anyway, ingawa huu ni ushindi mmoja tu kati ya viti vingi sana bungeni, ni vizuri ijulikane hapa kuwa wana-Tarime wamefanya la muhimu sana kwa demokrasia Tanzania.
Labda watanzania wengi sasa watajifunza hapa na kusema NO pale ambapo mambo yanakuwa yamewafikia shingoni huku ccm na mafisadi kama jambazi hili la Tarime - Zakaria wakiwaonyesha vipesa pesa vya wizi.