Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mkuu Mwanakijiji,
Mawazo mazuri lakini sidhani kama CHADEMA wameshinda kwa sababu ya watu kuwakimbia CCM peke yake, ingawa inaweza ikawa moja ya sababu. Kwa maoni yangu ukosefu wa amani unaweza ukawa kigezo kikubwa zaidi kwenye haya matokeo.
Kutokana na ushiriki wa watu kuwa mdogo sana, (~50,000) ukilinganisha na 2005 (~90,000), inaelekea wazi kuwa watu waliogopa kushiriki hasa baada ya kuwepo kwa vurugu na watu kuchomwa visu. Ushindi wa CHADEMA ni pungufu kwa kura zaidi ya 30,000 ukilinganisha na 2005, kiasi ambacho ni kingi kuliko kura walizopata hivi sasa na hata kwa asilimia ni chini kwa karibu 10%.
Mwaka 2005, marehemu Wangwe alipata kura 57,331 au 64.2% (nyingi kuliko jumla ya kura zote za CHADEMA na CCM kwenye huu uchaguzi wa leo). 2005, marehemu Wangwe alikuwa ndiye mbunge aliyeongoza kwa kuwa na ushindi mkubwa zaidi ndani ya CHADEMA.
Kwa hiyo inawezekana kuwa waliopiga kura wengi wao walikuwa ni wakereketwa tu wa hivyo vyama na wengine wasio wakereketwa wa hizo siasa zao, walioona waepukane na vurugu na wakakaa nyumbani.
Hivyo haya matokeo yanatakiwa yaangaliwe kwa udadisi mkubwa zaidi na wahusika wote, CHADEMA, CCM na zaidi ya wote waandaaji uchaguzi kwani vurugu zinaweza zikawa ndio zilizoleta haya matokeo na hivyo yanaweza kuwa hayatoi picha halisi ya siasa hapo Tarime.
hoja yako ingekuwa na nguvu kama ungelinganisha na Kiteto. CCM walishinda Kiteto kwa namna gani ukiangalia namba?
MMJJ,
Mazingira ya hizi chaguzi ni tofauti kabisaa kulinganisha. Sidhani kama Kiteto kuna aliyechomwa kisu kwa kupigania uwanja wa kutulia Helikopta. Ukosefu wa amani Tarime ni wazi kuwa ndio uliowafanya zaidi ya 50% ya wapiga kura kuogopa kutoka nje siku ya uchaguzi. Analysis yoyote inatakiwa ianzie hapa.