Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
QAnaposema 'gharama kubwa' bila kutuwekea figure ni sawa na kutuuzia mbuzi kwenye gunia. Ni matarajio yangu kuwa CCM na Chadema wataweka hadharani haraka hesabu zao za matumizi wakati wa kampeni. hapo ndipo tutakapojua kama Msekwa anamaanisha nini anaposema 'gharama kubwa.'
Lakini, hakuyajua haya kabla hawajaingia kwenye kampeni ambazo yeye aliziongoza? nanusa harufu ya unafiki na kutaka kujiosha
 
Date::10/15/2008
Polisi wafurahia Chadema kushinda
Na Mussa Juma, Tarime
Mwananchi

POLISI ambao walionekana kuwa maadui wakubwa wa vijana waliokuwa wakiishabikia Chadema wakati wote wa kampeni za uchaguzi wa mbunge na diwani wa Tarime, jana walikuwa wenye furaha baada ya purukushani za uchaguzi kutulia.

Mji wa Tarime jana ulirejea katika hali yake ya kawaida baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi yaliyompa Charles Mwera ubunge wa jimbo la Tarime kwa tiketi ya Chadema, na John Heche udiwani wa kata ya Tarime Mjini kwa tiketi ya chama hicho.

Na matokeo hayo yalikuwa ahueni kwa askari polisi hao ambao walifanya kazi kubwa ya kudhibiti vijana wa Chadema waliokuwa kwenye harakati nyingi wakati wa kampeni kiasi cha wakati fulani kutulizwa kwa mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na hata risasi kufyatuliwa hewani.

"Sisi tumefurahi sana Chadema kushinda kwani kama wangeshindwa ingebidi tukae hapa kwa zaidi ya wiki mbili tena ili kulinda amani na lolote lingetokea kutokana na hali ya hapa Tarime," alisema askari mmoja toka mkoani Mwanza.

Askari mwingine kutoka mkoa wa Arusha alisema wamefurahia ushindi wa Chadema kwa kuwa utawafanya waondoke Tarime ambako usalama wao ulikuwa mdogo na hali yao ya maisha kuwa mbaya kutokana na kupewa posho ya Sh1,000 tu kwa siku.

"Bwana sisi kesho tunaondoka tutakutana Arusha... maisha ya Sh1,000 kwa siku yametushosha na kwa kuwa Chadema wameshinda hakuna kazi tena hapa," alisema askari huyo.


Karibu polisi 400 walipelekwa Tarime kusimamia usalama kwenye eneo hilo, ambalo kulipuka kwa vurugu wakati wowote ule ni kitu cha kawaida.

Baadhi ya askari walijeruhiwa kwa mawe wakati wakipambana na vijana waliokuwa wakiandamana mitaani wakati wa kutoka kwenye mikutano ya kampeni na wakati wa kushangilia matokeo.

Askari hao walipelekwa wilayani humo kutokana na kutegemewa kulipuka kwa vurugu.
 
Mapigano ya KOO yameisha baada ya uchaguzi; Tosi ajitiokeze sasa aseme undani wa swala hili kama alivyotangaza hapo kabla
 
Serikali isiwaondoe Polisi hao Tarime itakuwa ni kutowatendea haki wanaTArime na WaTz kwa ujumla. Serikali ikumbuke kuwa iliwaambia WaTz kuwa Askari wale wamepelekwa kutuliza mapigano ya Kikoo huko Tarime na si kwa ajili ya Uchaguzi.


Kwa maneno yako labda uwe umeishahau serikali yako ya CCM
 
Kwa kweli kama hawa askari walikuwa wanalipwa sh alfu moja kwa siku, sina neno jingine zaidi ya udhalilishaji! Labda ndio sababu walikuwa wanageuka vichaa na kutembeza virungu hovyo kumaliza hasira zao!
 
Msekwa ananichekesha anapoandika kama vile hakuwako katika sakata hili, kama vile hakushiriki kupanga haya yaliyotokea! Anataka kujitoa kama vile waliofanya hayo yote ni wengine na yeye alikuwa mtazamaji tu asiyekuwa na kauli ama mamlaka yoyote, ambaye alisubiri haya yatokee ndipo aje na "reflections" zake. Mtu aliyekwenda Tarime na kauli kama "nimetumwa na Amiri Jeshi Mkuu....." leo anaandika kama vile alikuwa mtazamaji tu! Kweli amechoka huyu, arudi tu nyumbani akabembelezane na mzee mwenzie Anna! Hizi sasa ni hekaya za kuwasimulia wajukuu zake, si kauli za kuongozea chama katika ngazi ya makamu mwenyekiti taifa, au 2-ic.
 
[/I][/COLOR]

Asubiri kufungua kesi mahakamani.

Mategemeo ya kesi hiyo kuisha haraka ni 2010!

Akakusanye ushuru TRA!
Akakusanye wapi ushuru sasa?inavyojua ukijiingiza kwenye siasa kwa inakubidi uache kazi yako jaman.kama nimekosea mtanirekebisha wakuu.na ndio mana yule jamaa aliyekuwa mbunge wa mwibara alilazimika kuacha kazi pale foreign affairs.sijui kwa sasa yuko wapi.
 
If a small election was such a disaster can we imagin e what will happen in 2010. Will they have to hire an army from where????? even the police force do not feel comfortable to beat people who are celebrating their freedom of expression.
 
Ipo simulizi ya sungura aliyeshindwa kuzifikia ndizi mbivu juu ya mkungu na kusema "Sizitaki hizo ndizi kwanza ni mbichi" Msekwa alipelekwa Tarime kama mratibu wa kampeni ya uchaguzi na badget ya shughuli alipanga yeye na Makamba, wakaomba msaada kwa Tosi akapata, akaomba msaada kwa Mtikila akapata, wakaomba msaada kwa Mbatia akapata, wakaomba msaada kwa Rostam akapata n.k. Waliompa msaada sasa wanataka mahesabu ya kazi waliyomtuma akafanye Tarime kama kuna faida au hasara.
 
Sidhani kama CCM waliweza kununua shahada 20,000 bila ya CHADEMA n.k. kutokupata habari. Hivyo vitisho vya watu kwenda kuchukua silaha zao na kuingia mitaani, ni lazima ziliwafanya wasio wakereketwa wa CHADEMA na CCM kukaa nyumbani.

Despite winning, CHADEMA have to be worried of 10% decrease in support. Kama upungufu huo ungetokea kwenye jimbo lingine lolote waliloshinda ubunge 2005, basi wangepoteza hivyo viti.

Wewe nawe na CHADEMA?!
 
Sorry!!
Kidding !!wajamani ni kuwapinda tu presha watu si kweli.

Naona presha itakupanda sasa vizuri kwa vile watu wa Tarime hawakupigana na kukatana mapanga kama vile ulikuwa ukitabiri hapa kila mara. Habari za TBC1 na za magazeti ya Rostam Azizi kuwa Tarime kulikuwa na mapigano na fujo dhidi ya Mbowe na wanachadema zimethibitika kuwa za uongo, sijui utaomba msamaha kwa yote uliyosema wakati ule?
 
Huyu Msekwa ni mnafiki. Kwanini hakusimama kidete kuzuia ufujaji huo wa pesa? Je, CCM wangeshinda si angetwambia CCM ilikuwa na haki kutumia pesa nyingi ili kuhakikisha wanashinda kiti cha Tarime.

Tutamuona kama ni mkweli basi atasimama kidete kuzuia ufujaji wa pesa katika uchaguzi wa 2010 ikiwamo matumizi ya mashangingi, helicopters, magari ya jeshi na FFU pasipo na ulazima wowote wa kufanya hivyo.
 
Msekwa ananichekesha anapoandika kama vile hakuwako katika sakata hili, kama vile hakushiriki kupanga haya yaliyotokea! Anataka kujitoa kama vile waliofanya hayo yote ni wengine na yeye alikuwa mtazamaji tu asiyekuwa na kauli ama mamlaka yoyote, ambaye alisubiri haya yatokee ndipo aje na "reflections" zake. Mtu aliyekwenda Tarime na kauli kama "nimetumwa na Amiri Jeshi Mkuu....." leo anaandika kama vile alikuwa mtazamaji tu! Kweli amechoka huyu, arudi tu nyumbani akabembelezane na mzee mwenzie Anna! Hizi sasa ni hekaya za kuwasimulia wajukuu zake, si kauli za kuongozea chama katika ngazi ya makamu mwenyekiti taifa, au 2-ic.

au analigi nawenzake?
inawezekana baada ya kushindwa wameanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe tehetehe mwambieni bado 2010 itakuwa ngumu ajiuzulu mapema kwanza keshachoka na vile vijimatusi vinaweza vikampandisha pressure bure.
 
Toka lini CCM ikawa restrained on the base of frugality?

Kitu ambacho Msekwa hakutaka kusema wazi (judging from the scanty report at least), ni kuwa kuna mentality ya "at any cost" na "money is no object" katika ranks za CCM. This mentality is further enforced by the knowledge that, after all, if push comes to shove, they feel confidently entitled to come up with another Kagoda and rake a few billions in the name of "national security". Some of these goons are so much in denial they actually start to believe that stuff.

So why is Msekwa trying to play the proverbial zeze to a goat? If Msekwa was not among the topmost echelon in CCM I would have been tempted to view this as a visibility and political ambition issue. Msekwa is putting a lot at stake by coming out publicly with a paper analyzing CCM outside of it's rigid politburo processes. For this he is to be applauded, the last CCM bigwig to attempt a similar brainstorm, albeit admittedly more controversial, was Kolimba.

The only logical line of thought to me, is that Msekwa is playing the "I told you so" game after unsuccessfully trying to persuade his fellow CCM stalwarts against an overly flamboyant and costly campaign in the heart of opposition land.

Now who am I to discount ambition? He is not even president yet!
 
Hii imekaa vipi?





Tarehe October 14, 2008 4:37 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

HONGERA sana makamanda. Waongoze vyema wapiganaji wa tarime, wapate maisha bora, na wawe mfano wa kuigwa na majimbo mengine yanayodanganywa kwa kofia, fulana na khanga. Ninapendekeza Tarime itambuliwe na kutangazwe na wapiganaji wote wa tanzania kuwa MAKAO MAKUU ya kampeni tutakayoibatiza "TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA". Ukiwekwa utaratibu mzuri tupo wadau wengi ambao tuko tayari kuchangia linalowezekana. Hii maana yake ni kwamba, vijana watatumwa kutoka majimbo yote tanzania kuja tarime kujifunza mbinu za kuendesha kampeni hiyo. Wapiganaji mnasemaje?​



Comment hapo juu imetoka kwa mdau, website ya Michuzi
Mrithi wa chacha wangwe



.
 
Ndugu Ladslaus,


Ufisadi ndani ya CCM sio 'way of life' kama ulivyosema bali ni wa baadhi ya 'wanachama' wachache kama walivyo mafisadi kwenye vyama vingine vya siasa hapa Tanzania (kwa sasa wakiongozwa na Mchungaji mwenzangu Mtikila).

Hawa baadhi ya wanachama wachache wameweza kuishi na kustawi ndani ya chama ambacho kamanda wake alisema hana ubia na mtu kwa namna gani. Je wanachama hao walio wengi wamewezaje kuvumilia huo uchafu kwa karibu miaka mitatu bila kuufagia. Hivyo nina kila sababu ya kusema UFISADI ndani ya CCM ni way of life.

Ni kweli kuwa Rais wetu (ambaye ni mwenyekiti wa CCM) ni MSAFI isipokuwa amezungukwa na baadhi ya washauri wanaompotosha

Kama unasikia uzuzu (samahani sikutukani) ndani ya CCM ndio huu. Mwenyekiti wa CCM ambaye tena ndiye Rais wa Tanzania alipewa mandate na asilimia karibu 80% ya wananchi ailinde na kuitetea katiba ya Tanzania. Aliapa kudumisha utawala wa kisheria halafu siyo tu amezungukwa na washauri wanaompotosha, anakuta hana ubavu wa kupambana nao. Anakula na MAFISADI sahani moja na hapo hapo aitwe msafi. Labda unipe tafsiri yako ya neno msafi.

Mie kuihama CCM kama Kijana Waitara haitawezekana maana hata Waitara tunamsubiri atarudi CCM muda mfupi ujao

Hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo na kuna wengi tu wamemtangulia. Swali ni kwa nini mtu anayetukana CCM leo kesho apokewe kwa shangwe na vifijo akirejea tena kama chama ni makini. Hii inaonyesha kuwa ndani ya CCM, the end justifies the means. Ni matumbo tu yanayowapeleka watu CCM na siyo maslahi ya taifa.

Napenda pia kukukumbusha suala la Zambia, ambapo Chiluba alikuwa fisadi lakini alipoingia Levy Mwanawasa (RIP) madarakani, ambaye alikuwa mtu wa karibu sana na Chiluba, alibadili chama na kuwashughulikia mafisadi wote akiwemo Chiluba

Huo ndio udhaifu wa JK kama kiongozi na CCM kama chama. Mwanawasa aliamua kufanya kweli, JK amesalimu amri na badala yake amebaki kutalii nchi za nje kuyakwepa majukumu ya nyumbani. What a shame.


Mwisho napenda ufahamu kuwa CCM bado ni Chama makini kuliko vyote hapa Tanzania; Karibu sana CCM uwe mmoja wa wanachama wake

Ni kweli CCM huwezi kuilinganisha na chama chochote hapa Tanzania kwa sababu ndicho kimepewa nafasi ya uongozi kikashindwa. Wala rushwa wanapeta, wezi wanatanua, wahujumu uchumi ruksa......looo dola imekwenda usingizi na kamanda anatalii. Hao CCM wenye uchungu wako wapi ? Ndugu zangu Ladslaus, Bibi ntilie, Gembe, Masatu, Mtanzania, Fairplayer na wengine wengi tu, mko wapi na haya hamyaoni. FMES ameweza kuyaona mengine lakini kasahau kimoja muhimu - the buck stops with the President.
 
Hii imekaa vipi?





Tarehe October 14, 2008 4:37 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

HONGERA sana makamanda. Waongoze vyema wapiganaji wa tarime, wapate maisha bora, na wawe mfano wa kuigwa na majimbo mengine yanayodanganywa kwa kofia, fulana na khanga. Ninapendekeza Tarime itambuliwe na kutangazwe na wapiganaji wote wa tanzania kuwa MAKAO MAKUU ya kampeni tutakayoibatiza "TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA". Ukiwekwa utaratibu mzuri tupo wadau wengi ambao tuko tayari kuchangia linalowezekana. Hii maana yake ni kwamba, vijana watatumwa kutoka majimbo yote tanzania kuja tarime kujifunza mbinu za kuendesha kampeni hiyo. Wapiganaji mnasemaje?​



Comment hapo juu imetoka kwa mdau, website ya Michuzi
Mrithi wa chacha wangwe



.

Mhh,

Hiyo comment inafurahisha sana. Kama mtanzania aliyezaliwa na kukulia Tarime, nimefarijika kuona Tarime ikipewa heshima kama hii. Nadhani wito sio kuwa na Tanzania bila ccm bali iwe ya Tanzania ambayo vyama vyote vina nafasi sawa kwenye ushindani.
 
Mimi bado nasheherekea kushindwa kwa CCM.
Imekuwaje tukasau kuweka picha ya hawa wapiganaji?


chadema_mwera_heche.JPG


Huyu ndiye mbunge mpya wa Tarime Mh. Charles Mwera (kushoto) akiwa na diwani mpya wa jimbo hilo Mh. John Heche




Picha ni kwa hisani ya Michuzi website
Mrithi wa chacha wangwe



.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom