Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Nadhani a weak CCM is exactly what Tanzania needs at this time.. Vyama vya upinzani hatuna. Viko dhaifu, vinaendeshwa na watu ambao wahuni na in many cases wanafiki.. as is with CCm. Tatizo moja ni kwamba Tanzania haina opposition due to the fact tht CCM is entrenched in the control and running of the Country.. Kikwete, albeit weak and struggling, is a blessing in disguise for Tanzania.. In the short term anasimamia inefficiency and corrupt practices lakini by weakening CCM ana creat a void or partial void intakayowapa wapinzani space to grow until we reach a point ambapo we are going to get a near 50/50 split in parliament and also in Presidential politics.. This is the only way in which democracy can function... albeit in an imperfect fashion...

CCM's blunders and current weakness is essential for the development of genuine multi-party democracy.. Something that could never have happened under Mkapa because he was an authoritarian leader...

Udhaifu is the way forward.. How ironic..!!
 
Baada ya kushindwa sasa anafutwa mchawi nani ,wakati alikuwa mmojawapo wa waliokuwa wanawanga kuua haki ya kikatiba ya watu kuchagua wanayemtaka.Nadhani Tinga tinga anawacheka sana,Nguvu nyingi akili sifuri.Bado sasa kule Jimbo la Biharamulo Magharibi,maana Phares KABUYE naye anawasubiri kwa hamu sana.Tangazeni uchaguzi

Huyu ana historia ya hizi taarabu zake, hata alipokuwa katibu mtendaji wa kwanza wa CCM aliwahi kusema maneno ya pumba kama haya dhidi ya Serikali na CCM, ndio Mwalimu akamuhaimishia Tabora haraka sana,

Sasa hapa kama kawaida yake yena, anajaribu kujifanya kuwa yeye hakuhusika na huo uchaguzi, ndio hata toka apewe umakamu hata kuhamia makao makuu ya chama cha CCM Dodoma hataki, anajificha Dar tu, na sasa nasikia the dataz ni kwamba yeye na mkewe wanajaribu kumsaidia Rita Mlaki kuwa mwenyekiti wa Wanawake mkoa wa Dar, it is just pathetic!
 
hivi uchaguzi mdogo biharamulo ni lini???...........maana wakati umefika...kwa utendaji wa kisanii wa jk ..mwaka 2010..wapinzani watapata zaidi ya asilimia 40 za viti vya bunge...

inatakiwa baada ya kushinda tarime wapinzani wangepata kausafiri wafanye ziara nchi nzima dubbed kumtambilisha mbunge wao mpya ...waanzie kanda ya ziwa ..up..

Mkuu PM,

Heshima mbele, jana nilikuwa ninaongea na Mkulu mmoja wa CCM aliyetoka Tarime, nilipomuuliza kuhusu majimbo ya Biharamulo na Mwibara, kwa furaha sana alinijibu kua "....kijana kumbe hujui kuwa bunge lilishapitisha muswaada wa kupiga marufuku chaguzi ndogo za ubunge miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu?..." akaniambia kuwa maana yake ni kwamba hakutakuwa na mbunge au uchagiz kwenye haya majimbo mpaka uchaguzi mkuu wa 2010,

Nilipombana zaidi, akaniambia "....kijana uchaguzi ukifanyika leo hatushindi CCM..., kwa hiyo hii sheria ni nzuri sana kwetu..."

Sasa hebu wakuu wanaojua vizuri je hiyo sheria ipo kweli au?
 
Date::10/15/2008
Chadema yamuunga mkono Msekwa kupinga matumizi makubwa Tarime
Na Kizitto Noya
Mwananchi

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa kwamba hakukuwa na lazima fedha nyingi kutumika katika uchaguzi mdogo jimboni Tarime na kubabinisha kwamba chenyewe kimetumia Sh60 milioni.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilibrod Slaa aliliambia gazeti hili jana kuwa haikuwa lazima sio tu kwa vyama vya siasa kutumia fedha hizo, bali pia serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuwapeleka askari 4,000, magari ya kifahari na magari ya maji ya kuwasha katika uchaguzi huo.

Licha ya chadema kuweka wazi kiasi cha fedha kilichotumia, CCM kimegoma kutaja fedha kilizotumia na kueleza kuwa hoja ya Makamu Mwenyekiti huyo, itajadiliwa katika vikao vya chama.

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli hiyo iliyotolewa na Msekwa siku moja baada ya kumalizika uchaguzi huo ulioupa ushindi Chadema.

Makamba, alisema suala hilo halilihusu gazeti la Mwananchi bali wana-CCM ambao watalijadili kwenye vikao vyao.

"Hii hoja inatuhusu sisi wana-CCM na tutaijadili kwenye vikao vyetu, hivyo sina cha kueleza leo," alisema Makamba na kukata simu.


Hata hivyo, jana Msekwa aliendelea kusisitiza hoja yake ya kushangazwa na matumizi makubwa ya fedha yaliyojumuisha gharama za helikopta, magari ya kifahari na fedha yaliyofanywa na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani wilayani Tarime.

Alisema anaamini matumizi ya kiasi hicho cha fedha ni makubwa kuliko ilivyostahili na kwamba kitendo hicho hakikujali thamani ya matumizi ya fedha.

"Kama mwanasayansi ya siasa kwa kusomea ninaona kuwa kwanza chaguzi ndogo ni gharama kubwa. Hivi tunatambua kweli thamani ya kutumia fedha nyingi kiasi hiki ili kupata jimbo lililoachwa wazi, wakati Bunge lina zaidi ya wabunge 320 ikizingatiwa chama kinachoshinda hakibadilishi uwiano wowote katika uimara wa chama," alisema.

CCM ilitumia helikopta mbili zilizokodishwa kutoka nchi jirani ya Kenya kwa ajili ya kujiimarisha kwenye kampeni zake, baada ya Chadema kuendelza mtindo wake wa kutumia helikopta iliyouanza mwaka 2005 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Mbali na matumizi ya helikopta vyama vya Chadema na CCM, vilitumia magari ya kifahari na kupeleka ujumbe mzito wa viongozi wa juu na wakereketwa huku CCM ikidaiwa kutumia magari ya kifahari zaidi ya 40.
 
Mkuu PM,

Heshima mbele, jana nilikuwa ninaongea na Mkulu mmoja wa CCM aliyetoka Tarime, nilipomuuliza kuhusu majimbo ya Biharamulo na Mwibara, kwa furaha sana alinijibu kua "....kijana kumbe hujui kuwa bunge lilishapitisha muswaada wa kupiga marufuku chaguzi ndogo za ubunge miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu?..." akaniambia kuwa maana yake ni kwamba hakutakuwa na mbunge au uchagiz kwenye haya majimbo mpaka uchaguzi mkuu wa 2010,

Nilipombana zaidi, akaniambia "....kijana uchaguzi ukifanyika leo hatushindi CCM..., kwa hiyo hii sheria ni nzuri sana kwetu..."

Sasa hebu wakuu wanaojua vizuri je hiyo sheria ipo kweli au?

FMES, huyu jamaa anajidanganya CCM sasa hivi siyo chama cha wanyonge ambao bi wakulima na wafanyakazi bali ni chama cha mafisadi na mafioso, Watanzania taratibu katika kila kona ya nchi yetu wanaanza kufumbua macho na kufahamu kwamba kuna tofauti kubwa kati ya CCM ya miaka 20 iliyopita na CCM ya sasa. CCM inabidi wabadilike sasa na wabadilike kwa kiasi kikubwa sana, lakini muda nao unawapiga chenga maana toka sasa mpaka uchaguzi wa 2010 ni miaka miwili. Na wakati umefika wa Watanzania kusema sasa basi hatuwezi kuendelea kuwavumilia miaka nenda miaka rudi na kuona nchi yetu inazidi kuangamia.

Hivyo basi wasubiri kimbunga kikubwa kitakavyowazoa mafisadi hapo 2010. Kutakuwa hakuna wa kulaumiwa bali ni JK, Msekwa, Makamba kwa kushindwa kukisafisha chama na kupambana na mafisadi ndani ya chama na serikali bila woga wala kificho.
 
Poor Msekwa.

Hebu hapo ulipo piga picha ama mchungulie malecela na Mangura watakuwa wanasema nini hasa baada ya kumnyima mangura hata uenyekiti wa ccm mkoa tu.patamu hapo!!!!
 
they hired people to go to tarime to intimidate the voters this is a crime.
 
huu ni mwanzo tu... wembe uwo uwo utawanyoa 2010!!!!haaa....haaaa!!!!
 
Watajiju...
Walidandia train kwa mbele bila kujua sasa watakiona cha moto.
 
Wasubiri kimbunga. Na kabla ya kimbunga 2010,hapa katikati kutakua na migomo,maandamano,kuzomea,mgogoro ndani ya CCM,kuipaka matope CHADEMA lakini anguko kuu 2010!
 
Among 40 million Tanzanians, eti Makamba na Msekwa ndio wenye akili nzuri ya kutuongoza kwenye 21st Century?

Unajua mambo mengine hata kuyasema ni aibu!
 
Hayo matumbo yao ndiyo yaliyowaponza.

Hata hivyo,si ustaarabu na wala ubinadamu kumfanyia mtu huo unyama.Sasa hawa ndiyo viongozi,wanakua wahuni nanna hii sasa wana tofauti ghani na wavuta bangi?

Makamba,please and please,hawa watu hawausiani na wewe na chama chako kushindwa uchaguzi.Kama ni kweli tafadhali fanya ustaarabu na onyesha mfano na picha halisi ya kiongozi mwenye busara na mamlaka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom