Mkuu
andoza sijibu yanayomhusu
Paskali mwenyewe ila hoja zako ambazo kwa maoni yangu ni
vioja kwa sababu:
√ Miradi inayotekelezwa ni kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya CCM, 2015 ikipewa ridhaa na wananchi kuunda Serikali. Hivyo basi siyo miradi ya Dr Magufuli, M/Kiti na Rais wa JMT. Anapongezwa kwa sababu ya utekelezaji uliotukuka wa Ilani ya Uchaguzi wa chama chake, CCM;
√ Labda swali la msingi la kuuliza ni:
je,vipaumbele vya maendeleo vya Ilani hiyo ya CCM vinakidhi mahitaji ya Watanzania? Bila shaka yoyote, jibu ni ndiyo. Kuthibitisha hilo CCM itarejeshwa madarakani kwa kishindo;
√ Madai yako kwamba gharama za barabara za juu kwenye makutano Ubungo ni kubwa (overpriced) bila takwimu ni hisia zinazosukumwa na chuki ya kisiasa tu;
√ Kuhusu kampeni za JPM, hakuna ubishi ananadi, kwa ufasaha, Sera za CCM zilizoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2020. Anaidadavua, kwa umakini mkubwa, hali ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na teknolojia ya jana, leo na kesho. Anapenda kutumia maneno ya "Tulipotoka, Tulipo, na Tunapokwenda" kuelezea hali hiyo kwa wapiga kura (watoto, vijana, watu wazima, wazee, walemavu, jinsi zote, wakulima, wafanya biashara, waajiriwa, waliojiajiri, nk).