Kuna tatizo lingine kubwa, Nathan Hili linamhusu Mheshimiwa mkuu wa Mkoa kwa Msaada, eneo LA gerezani, Kuna genge LA watu wanne na wanatembea na Bajaji na reflector Nyekundu!! Ila najua kuna taasisi imewatuma!! Eneo limevurugwa sana na biashara na hakuna parking!! Wameandaa maeneo kama sita (6) hapa Kariakoo Gerezani na kuchapisha vibao "taxii" parking na kukaa pembeni, Ukijikuta umeona ni kama parking ukikaribia kupark wanakuja na kukutisha na kukufungia gari na kudai Rushwa!! Jamani Tumefikaje hapa kuwaajiri hawa Majizi!? Ni rahisi kwenda pale na kuwakuta hawana hata tone LA aibu!! Mheshimiwa Makala (Mkuu wa mkoa) tuokoe na matapeli hawa wanatuharibia nchi!! Karibia na Shule ya Kisarawe maeneo hayo na wapo matapeli wanne!! Wanadai rushwa bila aibu