Yes Exactly. Hayo madarasa ndiko kuliko na kazi ngumu sana ya kumtoa mtoto hatua ya kutajua kitu hadi kuwa anajua kitu.
Huko sio eti mtoto ajue tu abechedeiefugi....... Hapana. Ni zaidi ya hapo. Mtoto aweze kuzoea kuwa bila mzazi, mtoto aweze kujisitiri e.g. kupenga kamasi, kukaa pamoja na watoto wenzake (kuishi katika jamii) n.k. Ni ngumu sana -wapo watoto watundu, wakorofi, wagomvi, wenye fujo n.k. hayo yote mwl. wa madarasa hayo ni lazima akabiliane nayo la sivyo kwenye madarasa hayo hapafundishiki kitu. Mwl ndiye Mzazi, ndiye Polisi, ndiye Hakimu, ndiye Msuluhishi na mtoa Taarifa kwa Wazazi (Parents). Nyie yasikieni tu hayo madarasa usiombe ukapangiwa kushughulika au kuwa Mkurugenzi wa "kampuni" hiyo. Hakuna rangi utaacha kuona.