Ubungo: Wanawake 36 wanaodai kukamatwa na kudhalilishwa kuwa "Dada Poa" kumfikisha mahakamani DC Hassan Bomboko na kumdai Fidia ya Tsh. Bilioni 36!

Ubungo: Wanawake 36 wanaodai kukamatwa na kudhalilishwa kuwa "Dada Poa" kumfikisha mahakamani DC Hassan Bomboko na kumdai Fidia ya Tsh. Bilioni 36!

Hakuna lengo hapo zaidi ya kutafuta sifa za kuteuliwa. Kuna shida ngapi za msingi za kushughulika nazo? Kwanza ni sheria ipi inazuia mtu kutumia viungo vyake kupata kipato? Nisaidie kifungu ndugu yangu.
Kwanza wahanga wale walikuwa maeneo yao ya Makazi na kuvamiwa na kudhalilishwa hii haijakaa SAWA!! Kisa mtu mmoja ajipatie sifa!! Hii haikubaliki mbele ya Taifa lenye utawala Bora na sheria
 
Wanawake 36 wa Ubungo waliokamatwa na Mkuu wa wilaya hiyo wakidaiwa Kuwa ni makahaba na kuwekwa lupango siku 5 sasa watamfikisha mahakamani Mkuu huyo wa Wilaya

Wakili Madeleka amesema Wateja wake 36 watamdai Mkuu wa Wilaya ya Ubungo fidia ya TSH 36 billion Kwa kuwadhalilisha

Ameandika Wakili Msomi Madeleka ukurasani X

Hii June ina mambo Sana 😂
Safi sana ,unadhalilisha watu Kwa sababu za ujinga wako
 
Katika hao wanaodaiwa kudhalilishwa trust me makahaba hawakosekani.Kwa kusema hivi simaanishi na-support usenge wa DC na pia sifurahishwi na biashara ya mbususu
 
Kweli angetusaidia kuondoa kwanza vibaka,madada poa unawapita
bila shida,simu yako na lap top vinakuwa salama lakini vibaka ukijifanya kutetea mali yako
utasikia wanasema ''mpe topaz'' hapo ujue kiwembe kinakuhusu
ah ah ah.
 
Tatizo liko wapi? Tambua ushahidi wa hili jambo ni mgumu sana,kuna loop holes nyingi sana za kumnasua mtuhumiwa,tushugulike na mambo muhimu,mfano kwa Dar huyo bwana apambane na vibaka kama ana morali ya kazi.

Kwa taarifa yako hachomoi,tanzania ya sasa sio ile ya mwaka 47
Kwa msing huo, kama Vyangudoa wataacha basi na vibaka nao waachwe wajitafutie riziki kwa njia waliyoichagua.
 
Back
Top Bottom