Ubutu wa Primera Liga waanza kuthibitika

Ubutu wa Primera Liga waanza kuthibitika

Halafu bado tu huyo mbilikimo angepewa Balon D' Amor mwaka huu kama mwaka jana pamoja na kutofanya lolote la maana kwa timu yake na timu ya taifa lake
Balon D' ni tuzo binafsi,uwezo wa mchazaji kufunga,Ku assist, dribbling, n.k, mi ni shabiki wa Madrid lkn messi bado namuona ni mchezaji bora kwa karne hii
 
Sitaki kuamini kwamba Laliga ilikua ikibebwa na umahiri wa Cr7 na andunje Messi.
 
Balon D' ni tuzo binafsi,uwezo wa mchazaji kufunga,Ku assist, dribbling, n.k, mi ni shabiki wa Madrid lkn messi bado namuona ni mchezaji bora kwa karne hii
Kwa vigezo hivyo ulivyovitaja basi hapana shaka hiyo tuzo angestahili kupewa Adama Traore
 
Balloon d or inatolewa kibaguzi,kupendelea wachezaji wa timu za spain tu
Mpira huchezwa kweupe kila mmoja huona, Messi & Ronaldo wote si waspain ila uwezo wao hata takwimu uwanjani haukuwa na mashaka kwa kipindi kirefu, kwa nn useme kumekuwa na upendeleo!!!
 
Mpira huchezwa kweupe kila mmoja huona, Messi & Ronaldo wote si waspain ila uwezo wao hata takwimu uwanjani haukuwa na mashaka kwa kipindi kirefu, kwa nn useme kumekuwa na upendeleo!!!
Kama ni kwa takwim tu basi mwaka jana angepewa Kevin Debruyne
 
Makombe ya Ulaya hayakauki La Liga, ingawa ubora wake umeshuka kidogo kwa misimu miwili iliyopita
 
Hivi kuna anayeziogopa timu za Spain kwa sasa ?
 
Kwa muda mrefu sana wapenda soka wa dunia wamedanganywa kwamba ligi ya Spain ndio ligi bora na ngumu kuliko ligi zote duniani , hata pale sisi wataalam na wachambuzi wa soka tulipopinga , tena kwa mifano iliyofanyiwa utafiti , tuliishia kusimangwa .

Kipigo cha Barcelona kutoka kwa vibonde PSG ni ushahidi mwingine kwamba soka la spain si lolote , jambo pekee lililojificha ni kwamba , ligi ya spain ina mkusanyiko wa wachezaji wazuri wa dunia ambao kucheza kwao kwa muda kwenye ligi mbovu kumedumaza uwezo wao.

Mifano ni mingi sana , ligi bora haiwezi kuwa na timu bora zisizozidi 5 tu kama siyo 3 , ligi bora ya dunia haiwezekani kuonekana bure bila malipo , ukiacha Tv duni kabisa duniani kama TBC , karibu Tv zingine zote zinaonyesha ligi ya Spain bure kabisa , Azam na Dstv Bomba ni mifano ya karibu .

Timu za Spain zitaendelea kuadhirika zaidi kuanzia sasa na kuvuliwa huo ufalme hewa waliovikwa .

....... Itaendelea ........

UPDATES
BARCELONA 2 - 8 BAYERN MUNIC
Chelsea 2 - 0 R Madrid
Tuendelee na mjadala...
 
Kwanini useme eti kwa muda mrefu dunia imekua ikidanganywa wakati ulikua unaona mwenyewe timu hizo ndio zilizokua zina washiriki wengi katika makombe yote ya ulaya na kuyanyanyua kuliko timu za ligi nyingine
Sasa hapo vipi inasema dunia imekua ikidanganywa?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Umesoma andiko lote na kuelewa ?
 
Back
Top Bottom