Uchache wa abiria na mizigo wafanya SGR nchini Kenya kuendeshwa kwa hasara. Je, Tanzania tutakwepa hali hii?

Uchache wa abiria na mizigo wafanya SGR nchini Kenya kuendeshwa kwa hasara. Je, Tanzania tutakwepa hali hii?

SGR tz itakuwa Na faida TZ kutokana distance ya kutoka Dar hadi Mwz Na wengi wa miji mikubwa njiani mfano Moro, Dom, SGD, TBR, Khm, Shy lakini pia IPO miji mingi midogo midogo kama Kilosa, Manyoni, Itigi, Puge, Bukene, Isaka, Tinde, Maswa, Malampaka, MALYA, Sumve nk.Bidhaa zitakazosafirishwa sio lazima za viwandani Bali mifugio, mazao ya mashambani Na abiria
 
Watu wangapi wanaenda Dodoma na mizigo ipi inaenda Dodoma🏃😂 Itafika kighoma naada ya miaka 20 maana Magu hata Moro tu haijafunguliwa
 
Maswali kama hili yalipaswa kujibiwa kwenye hatua za mwanzo za feasibility study kabla ya ujenzi kuanza.
Sasa ni too late!

Zaidi ya hivyo reli zitakuwa mbili, meter gauge na sgr zikiwa sambamba. Maana yake itafika wakati zatanyan'ganyana mizigo na abiria!
Ndiyo maana ya "kupanga ni kuchagua". Hatukupanga, kwahiyo tulipofika hatuna uwezo wa "kuchagua".
Hahahaha eti zitanyang'anyana 😅😅😅😅😅

JF kuna utitiri wa vichwa maji
 
watu wangapi wanaenda Dodoma na mizigo ipi inaenda Dodoma🏃😂 Itafika kighoma naada ya miaka 20 maana Magu hata Moro tu haijafunguliwa
Tenda ya ujenzi mpaka mwanza hujaona imetangazwa juzi?
 
hii sgr inajengwa first priority ni Congo rwanda burundi &Uganda kabanga nickel na ndo final destination ok kama italeta hasara it's ok!! tutaipanda sie maana ata kipindi ndege znanunuliwa mlisema pia watu hawata panda but nowadays mmejisahaulisha utunduwazi wenu...... mpanda kigoma dom li bombardier linajaza sa sembuse kitu cha umeme? masaa 9 mtu uko rock city?
😁😁😁😁
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Sikuhiz mpandaji mkuu wa bombardier zito kabwe
 
P

Hii SGR itakuwa na faida ya kijamii zaidi kuliko kiuchumi.Kiuchumi tutarajie loss tu.

Iko hivi bro, hii miradi mikubwa kama hii ni mara chache sana kuwa na faida za kifedha, ukipiga mahesabu lazima utaona unapata hasara, hali huwa mbaya zaidi pale ambapo mradi unakuwa umetekelezwa kwa mkopo tena kutoka benki za kibiashara.

Lakini tukija kwenye manufaa ya kiuchumi na kijamii, hayo hupatika punde tu mradi unapoanza kutekelezwa. Watu wanaajiriwa katika kazi mbalimbali, mf. wajenzi, malori ya mchanga, uuzaji wa cement, mama ntilie n.k. Hivyo miradi kama hii kiuchumi bado ina faida kwa nchi.

Ila cha kuzingatia ni kuepuka kuweka cha juu, maana husababisha gharama kuwa kubwa ambazo hatimaye hubebwa na mtumiaji wa mwisho.
 
Swali:Kama Kenya yenye viwanda vingi kutuzidi, wanakuwa na uchache wa mizigo na kupelekea shirika lao kujiendesha kwa hasara,sisi wenye viwanda vichache ndio tutamudu kuendesha SGR yetu kwa
kenya tatizo si uchache wa abiria wala mizigo
Tatizo mradi ulijengwa kwa gharama kubwa mno,marejesho ni madogo kuliko gharama za uendeshaji
Treni ya tanzania ni ya umeme,itakimbia 220km per hour,treni ya kenya ni ya kerosene inatembea 90km per hour
 
Kwa kutumia umeme watakuwa wamepunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana kwenye mafuta, kununua spare na service hasa ukizingatia injini za umeme hazina parts nyingi sana ukilinganisha na injini za diesel.
Ni kweli kabisa nakubali brother ila kwa ninavyofahamu kutakuwa na mchanganyiko wa Electric locomotives na diesel Electric locomotives. Lakini nina swali ukitazama nchi kama india wanatumia zaidi diesel electric locomotives kuliko hizi Electric locomotives, tukiangalia nchi kama USA makampuni makubwa ya usafirishaji kwa njia ya reli Kama SOUTHERN PACIFIC, BNSF, NOLFORK n.k wanatumia diesel electric locomotives na electrification imefanyika katika reli za mijini kwa ajili ya abiria. Rejea Sout h Africa, Australia n.k kwanini bado wanatumia diesel Electric locomotives zaidi kuliko Electric locomotives??
 
Sio lazima Tanzania SGR ipate hasara kama Kenya, sababu ziko nyingi.
1. Imeshasemwa SGR ya Tanzania itatumia umeme ya Kenya Diesel. Hii kwa Tanzania itaokoa gharama nyingi za matengenezo, vipuri, uendeshaji, muda wa safari, nk.
2. Mkopo-SGR ya Kenya imejengwa kwa mkopo mkubwa wakati ya Tanzania imejengwa kwa asilimia kubwa kwa fedha za ndani. Hii inafanya Kenya waweke bei kubwa na nauli kubwa ya usafiri na usafirishaji ili waweze kufikia lengo la kulipa deni. Nauli na bei juu inawafanya wasafiri na wasafirishaji wasitumie SGR watumie barabara.SGR inakosa mzigo. Tanzania haitalazimika kuweka bei juu kwa sababu haitakuwa na deni kubwa la kulipa. Gharama zikiwa nafuu wasafiri na wasafirishaji watapunguza matumizi ya barabara watahamia SGR.
3. Idadi ya nchi zinazotegemea bandari ya tanzania ni kubwa kuliko Kenya. Tanzania inazungukwa na nchi nane ambazo zinategemea bandari ya Tanzania. Kenya nchi za karibu ziko kama tatu ambazo zina mbadala wa bandari. Hizi nchi zinaangalia unafuu na ubora wa huduma. Sasa vile bandari za Tanzania zinaboreshwa na SGR ya umeme asilimia kubwa ya mizigo ya nchi hizi itapita Tanzania. Hata Uganda mshirika wa karibu na jirani na Kenya, mizigo yake itagawanywa Tanzania na kenya.
4. Uongozi-Tanzania kwa sasa kuna uongozi imara ambao hauna maswala ya nenda uje kesho. Rushwa inapigwa vita sana. Hii itasaidia kuondoa urasimu na ukiritimba kwenye utoaji huduma. Hapa Mizigo ikitoka bandari ni kwenye SGR mpaka nchi husika. SGR itakapokamilika hata Congo itapata mizigo yake bila kupitia nchi nyingine.
5. Ukuaji wa sekta ya viwanda vya ndani-viwanda vya ndani vinakua kwa kasi na kuongezeka Tanzaniana. Hii itaongeza mzigo wa kulisha SGR , Kenya ambayo uchumi wake unasimamia uwekezaji. Inachoangamoto ya wawekezaji kufunga uzalishaji na kuhamia maeneo mengine. Hapa mzigo unaweza kupungua.
6. Malighafi- Tanzania ina mashamba makubwa ya kuzalisha malighafi za kuja kutumika viwandani. Na reli ya mkoloni ilijengwa hasa si kutoa mizigo bandalini kwenda mikoani bali ilikuwa inalenga kutoa malighafi mashambani kwenda bandarini. Mazao karibunyote makuu Tanzania uzalishaji umeongezeka. Hivyo tutashuhudia SGR Ikienda na kurudi na mzigo hii italeta faida. Wakati Kenya uzalishaji wa malighafi na mazao uko chini hivyo SGR inaweza beba mzigo one way kutoka mombasa na mabehewa yakarudi mombasa tupu.
7. Mifugo- Kuna wakati niliishi shinyanga pale, mbali na mafuta na pamba kuchukua mabehewa mengi lakini pia niliona wasukuma walivyokuwa wakigombania mabehewa kusafirisha ng'ombe kuja Dar ea salaam. Sasa Tanzania ina machinjio mbili za kimataifa. Mifugo itachukua sehemu kubwa ya mzigo kuja pwani.
8. Idadi ya watu-Tanzania ina idadi kubwa ya watu , na wanapapenda kwao. Maendeleo hayako Dar na dodoma tu. SGR itarahisisha usafiri na tiketi zitakuwa zinakuwa full booked. Wakati wakenya wanapambana kubaki nairobi. Volume kubwa ya safari iko december tu wakienda kuona maji mombasa. Tanzania december watu wako station wanatafuta usafiri wa kwenda mikoani kwao na wilayani kwao wakale sikukuu . Kwa hiyo mgawanyo wa safari utarahisisha SGR ya Tanzania kutemgeneza mapato.

Wakenya niendeleee.....

Wewe ukizama shimoni, sisi tunaokuja nyuma shimo tunaliona lazima tulikwepe. Na hapo ndipo anayeanza huwa anaachwa njiani!
 
Ni kweli kabisa nakubali brother ila kwa ninavyofahamu kutakuwa na mchanganyiko wa Electric locomotives na diesel Electric locomotives. Lakini nina swali ukitazama nchi kama india wanatumia zaidi diesel electric locomotives kuliko hizi Electric locomotives, tukiangalia nchi kama USA makampuni makubwa ya usafirishaji kwa njia ya reli Kama SOUTHERN PACIFIC, BNSF, NOLFORK n.k wanatumia diesel electric locomotives na electrification imefanyika katika reli za mijini kwa ajili ya abiria. Rejea Sout h Africa, Australia n.k kwanini bado wanatumia diesel Electric locomotives zaidi kuliko Electric locomotives??
Mkuu sababu kubwa ni hizi.
Electrification ni Teknolojia ya kisasa. Na hizo nchi waliwekeza kwenye reli zamani. Sasa kubadili mfumo kwenda kwenye umeme inakuwa changamoto sana. Ndio maana unaona wanatia Diesel. Hata hapa Tanzania hatukuibadilisha MGR iwe SGR na badala yake tukaja na SGR mpya kwa sababu kuweka mpya na kuboresha ya zamani gharama hazipishani sana. Hizo treni za mijini kwenye hizo nchi nyingi ni mpya zilizoletwa kutokana na kukua kwa miji na teknolojia ya electification of the line tayari ilikuwepo.
Sababu nyingine ni upatikanaji wa umeme wa kutosha kuendesha SGR. Baadhi ya nchi hazijafanya SGR ya umeme kutokana na kutokuwa na umeme wa uhakika kuendesha SGR.
Sababu nyingine ya kutumia treni zenye umeme na diesel kwa pamoja ninkwa sababu ya baadhi ya maeneo ya njia hayajawekewa umeme hasa maeneo ya kuingia kwenye baadhi ya station hivyo train inaweza kuingia hayo maeneo na kutoka kwa kutumia diesel.
Pia pale changamoto ya umeme kukatika au mifumo ya umeme kuharibika basi safari iweze kuendelea kwa kutumia diesel.
 
Jibu zuri, kwa kuongozea, Treni za Tanzani zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme kwa muda wa dakika 45 hivyo basi hata kama kukitokea hitilafu kwenye njia ya umeme bado kazi itaendelea hadi pale mambo yatskspo kaa sawa.

Pia SGR ya Tanzania imejengewa msongo wake maalum uliounganishwa na chanzo cha umeme wa Kinyerezi na chanzo cha umeme wa Kidatu na baadaye chanzo cha umeme wa Stieglers. Kwa hio suala zima la umeme wako vizuri sana.
 
Mkuu sababu kubwa ni hizi.
Electrification ni Teknolojia ya kisasa. Na hizo nchi waliwekeza kwenye reli zamani. Sasa kubadili mfumo kwenda kwenye umeme inakuwa changamoto sana. Ndio maana unaona wanatia Diesel. Hata hapa Tanzania hatukuibadilisha MGR iwe SGR na badala yake tukaja na SGR mpya kwa sababu kuweka mpya na kuboresha ya zamani gharama hazipishani sana. Hizo treni za mijini kwenye hizo nchi nyingi ni mpya zilizoletwa kutokana na kukua kwa miji na teknolojia ya electification of the line tayari ilikuwepo.
Sababu nyingine ni upatikanaji wa umeme wa kutosha kuendesha SGR. Baadhi ya nchi hazijafanya SGR ya umeme kutokana na kutokuwa na umeme wa uhakika kuendesha SGR.
Sababu nyingine ya kutumia treni zenye umeme na diesel kwa pamoja ninkwa sababu ya baadhi ya maeneo ya njia hayajawekewa umeme hasa maeneo ya kuingia kwenye baadhi ya station hivyo train inaweza kuingia hayo maeneo na kutoka kwa kutumia diesel.
Pia pale changamoto ya umeme kukatika au mifumo ya umeme kuharibika basi safari iweze kuendelea kwa kutumia diesel.
Sawa kabisa sikupingii. Lakini gharama pia ya transmission line unaizungumzia vipi? Maana wengi wao hicho kimewapa wakati mgumu.

Nilisoma report moja ilitolewa huko Marekani ilisema utumiaji wa vichwa vya diesel ufanisi wake ni 35% tu tofauti na vichwa vya umeme.

Lakini gharama ya kufanya electrification ndiyo kizungumkuti. Ndiyo inapelekea mpaka leo kampuni kama GENERAL ELECTRIC TRANSPORT DIVISION SYSTEM (GE) na ELECTROMOTIVE DIESEL (EMD) chini ya Progress Rail kuendelea kuzalisha vichwa vya diesel mpaka leo na kuviboresha zaidi kutumia mifumo ya kisasa mfano kuondokana na matumizi ya TRACTION MOTORS za DC na kutumia three phase AC induction motor kuongeza ufanisi na kuyauzia mashirika makubwa na makampuni duniani.

Sijapinga hizi harakati ila bado nahisi kuna hatua muhimu sana tumeiruka ya muhimu sana kabla ya hili. Yawezekana usinielewe nini maana yangu ila mfano mdogo tu 2014 tumenunua Locomotives toka Marekani kwa hao EMD ukiziona hali yake leo hii huwezi amini.
 
Back
Top Bottom