Uchafuzi wa Sensa 2022

Mkuu hata mimi nilikuepo kivule, kinachouma zaidi ni kutupotezea muda kwenye hayo ma interview yao wakati wana watu wao tena hata kwenye usaili hawakwenda

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ndio maana sikujisumbua kabisaaa. Mungu wangu alinijaalia kuyafahamu yajayo mapema na kwa taarifa yenu hata hizo pesa baada ya zoezi la sensa kuna watu watadhulumiwa.
mbona hilo swala lipo wazi baada ya sensa lazima watu wapgwe panga alaf kauli mbiu itakua uzalendo
 
Nchi za Afrika zimejaa magenge ya wahuni ,walevi na wezi?

Jiulize ni Kwa Nini wakati ule Wa miaka baada ya uhuru Kodi ilikua inaongezwa Kwenye bidhaa za starehe kama Bia, soda na Sigara. Cha ajabu miaka hii bidhaa hizo ndio zinashuka Bei. Tozo zinaongezwa kwe vyakula na mazao ya wakulima na Kwenye miamala ya pesa ambazo tayari zimeshalipiwa Kodi?

Ulevi
Uzinzi
Wakwepa Kodi
Wafanyabiashara za Magendo
Na starehe zinginezo ni chanzo kikubwa cha rushwa kweye ofisi za umma.

Mfanyakazi mshahara mdogo Lakini anataka Kuwa na michepuko Kibao. Anataka kulewa pombe kila Siku Wakati huo huo anataka awe na maisha ya Juu. Matokeo yake ni kuwaza madili na rushwa tu.

Dawa ilikua ni moja kupandisha Kodi ya vilevi mara Kwa mara Ili wabaotafuta fedha za rushwa na wakwepa Kodi na biasha za Magendo wachangie Kodi Kwa kiwango kikubwa.
 
mbona hilo swala lipo wazi baada ya sensa lazima watu wapgwe panga alaf kauli mbiu itakua uzalendo
Mkuu lushoto washapigwa badala ya kupewa 50000 watapewa 45000 . Wakati maeneo mengine wamepewa 50000. Dah hii nchii hii. Mama Samia watu wanapiga hela huku kuwa mkali afu watu wakiharibu kazi mtalaumu?
 
Mkuu lushoto washapigwa badala ya kupewa 50000 watapewa 45000 . Wakati maeneo mengine wamepewa 50000. Dah hii nchii hii. Mama Samia watu wanapiga hela huku kuwa mkali afu watu wakiharibu kazi mtalaumu?
Mkuu maeneo mengine kama yapi? Ruvuma wote 40000 kwa siku zote 19 na sensa siku 6
 
Kwani huyo mtoto wa diwani hastahili kupata kazi kwa kuwa baba yake ni diwani?? Nafasi ni chache, waombaji ni wengi. Ni lazima wengine mkose tu hakuna namna. Hata ungepata wewe, wenzako wangelalamika pia kuwa umependelewa.
 
Mkuu maeneo mengine kama yapi? Ruvuma wote 40000 kwa siku zote 19 na sensa siku 6
Ukitaka kuthibitisha umaskini wa Watanzania fanya hesabu ya 50 × 25 = 1,250,000/=

Million moja laki mbili na hamsini elfu ndio kelele zote hizi.

Vijana tafuteni passport mkajae Marekani kama Waethiopia au Wanaigeria, huu ni ufukara.

Imagine pesa hiyo inawasumbuwa wasomi ni posho ya siku mbili tu ya kukalia viti vya bunge kwa mtu aliyeishia darasa la saba kama Kibajaj.
 
Ukweli Sensa bila connection huwezi kupata mchongo kirahisi, mimi sikuapply hizo kazi ila na dada yangu X alinipigia sim akaniuliza kama nili apply nikamwambia No. akaniuliza kama nitakua interested aniweke tena kitengo kizuri chenye pesa nikamwambia kzi Zimenibana. Hiyo dili nikampa mshikaji wangu yuko training now.
 

Kwa mtu ambaye hana ajira ni pesa ndefu sana kwake
 
Kwahiyo mtoto wa Diwani Nyasika asifanyiwe nongwa hata yeye ana haki ya kupata connection.
 
Wahitimu ni lazima waajiriwe?
 
Kwani sensa wanapata shilingi ngapi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…