Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 Zanzibar: Prof. Mbarawa vs Dr. Mwinyi, nani namba zinambeba?

Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 Zanzibar: Prof. Mbarawa vs Dr. Mwinyi, nani namba zinambeba?

Wote wawili Mwinyi na Mbarawa ni waislamu, na siku zote watu wa dini hii ni waungwana, hata siku moja huwezi kusikia wanamuita anayewazidi umri 'mpumbavu' au 'mjinga' kama marais wakristo wenzangu wanavyorudia hii hulka mbovu ya kiburi.

Namuona Mbarawa akiwa anafaa zaidi kuliko Mwinyi, Mbarawa anaweza kuongea kwa sauti yenye mamlaka na ikaheshimika. Mwinyi namuona kama ni wa ofisi zaidi, asiyependa mikwaruzano.

Mbarawa amekuwa mtu wa field kuliko Mwinyi na jambo hilo limemuwezesha kuzijua hulka za wasaidizi wake, hivyo anaweza kuwa na mpango mkakati wa kikazi wenye kuheshimiwa na taifa.
 
Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais kwa sababu moja kuu anatokea Pemba ambako hawajawahi kutoa Rais wa SMZ. Hivyo Mbarawa atawaongezea CCM ushindi kuleni Kisiwani Pemba!

Nadhani Shein anatoka Pemba!!!! Nyie watajeni hao mnaowapenda mkikaa kwenye key board. Watu wa Zanzibar wamechoka kuchaguliwa watawala kutoka bara; safari hii wanamchagua kijana wao wanaeishi nae visiwani muda wote ndiye atakaepeperusha bendera, nae si mwingine bali Mheshimiwa THABIT KOMBO waziri wa utalii zanzibar. Huyu kule hana mpinzani.
 
Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais kwa sababu moja kuu anatokea Pemba ambako hawajawahi kutoa Rais wa SMZ. Hivyo Mbarawa atawaongezea CCM ushindi kuleni Kisiwani Pemba!
DR.Shein ni mpemba na anatoka pemba pia.
 
Mkapa,kikwete na Jiwe ndio wataamua nani awe raisi wa zanzibar baada ya shein na Tanzania baada ya magufuli.
 
Wote wawili Mwinyi na Mbarawa ni waislamu, na siku zote watu wa dini hii ni waungwana, hata siku moja huwezi kusikia wanamuita anayewazidi umri 'mpumbavu' au 'mjinga' kama marais wakristo wenzangu wanavyorudia hii hulka mbovu ya kiburi.

Namuona Mbarawa akiwa anafaa zaidi kuliko Mwinyi, Mbarawa anaweza kuongea kwa sauti yenye mamlaka na ikaheshimika. Mwinyi namuona kama ni wa ofisi zaidi, asiyependa mikwaruzano.

Mbarawa amekuwa mtu wa field kuliko Mwinyi na jambo hilo limemuwezesha kuzijua hulka za wasaidizi wake, hivyo anaweza kuwa na mpango mkakati wa kikazi wenye kuheshimiwa na taifa.
lakini hata mh. Amani Karume hana sauti yenye mamlaka kama usemavyo lakini amekuwa rais wa znz, kuhusu suala la field nadhani aina ya wizara aliyopo mh. mwinyi haina makeke hayo ya kutimua na kuweka ndani wakandarasi vinginevyo ungemuona hivyo.
 
Mwinyi anatosha ..aje kuwa wa Muungano 2025 kama baba yake ..CDM wakishindwa
 
Siasa za Zanzibar ni za kipekee...subirini muone suprise...Mbarawa si rahisi kuwa rais zanzibar coz ni Mpemba so ni ngumu kuwafuatanisha wapemba mfululizo (Shein n Mbarawa), Samia hawezi kupewa coz ni mwanamke (atapingwa na hata masheikh wakubwa visiwani) labda wafosi, Hussein Mwinyi pia ni Ngumu kwa sababu kuna fununu kuwa hakuzaliwa Zanzibar (alizaliwa Misri) na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ili uwe rais wa Zanzibar ni lazima uwe Mzanzibari wa kuzaliwa.

Atakaekua mgombea wa uraisi wa ccm Zanzibar ni chagua la magufuli. Yoyote atakae kuwa chagua lake ndio atakaeipita. Hizo hoja zake za upemba na mwanamke hazina nafasi kabisa. CCM zanzibar ni madalali tu wa CCM bara, hawana kauli yoyote mbele ya CCM bara.
 
Nadhani Shein anatoka Pemba!!!! Nyie watajeni hao mnaowapenda mkikaa kwenye key board. Watu wa Zanzibar wamechoka kuchaguliwa watawala kutoka bara; safari hii wanamchagua kijana wao wanaeishi nae visiwani muda wote ndiye atakaepeperusha bendera, nae si mwingine bali Mheshimiwa THABIT KOMBO waziri wa utalii zanzibar. Huyu kule hana mpinzani.

usiseme watu wa Zanzibar sema CCM wa Zanzibar.
Na kwa kifupi tu CCM Zanzibar hawana ubavu wa kumueka mgombea wao wanaomtaka. mgombea wa Uraisi kupitia CCM Zanzibar atakua ni chaguo la Makufuli tu.
 
Aliyemleta shein na Bilal ni mtandao wa Lowassa!! Chaguo la JK lilikua Nahodha!! Inaonekana huzijui siasa
Nasikia JK alimtaka yule mama shombeshombe aliyekuwa waziri was fedha ndiye awe makamu wa Rais
 
Yani Tz ni nchi yangu ila kuna watu zaidi ya takataka. Kama wangekuwa kuku basi pasaka wasingepita. Jitu linatetea Dr. Mwinyi eti sababu sio limbukeni!!!! Badala ya kumpima utendaji kz wake km waziri kwa muda mrefu eti sio limbukeni!!!
 
Kama tunavyojua kuwa 2020 Dr Shein atakuwa anafikia muhula wake wa mwisho wa uongozi visiwani Zbar, kinyang'anyiro cha kumpata mrithi wake kinaweza kikatawaliwa na 'wababe' hawa wawili yani Dr Mwinyi na Prof Mbarawa.

Sasa nimekuja kwenu wachambuzi wa maswala ya siasa mtoe uchambuzi wenu kuwa nani namba zinambeba na nani kati ya hawa wawili anaweza kuibuka kidedea?

Karibuni.
Hivi hakuna wazanzibar wengine wafia Nchi kuliko hawa wa kuungaunga ? , hakuna hata aliye hukohuko Zanzibar zaidi ya hawa walowezi wa Tanganyika ?
 
Ezekieli : Mlango 24
6 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Ole wake mji wa damu! Hilo sufuria ambalo kutu yake i ndani yake, ambalo kutu yake haikulitoka; litoe kipande kipande; maana hapana kura iliyoanguka juu yake.
 
Back
Top Bottom