Uchaguzi bora wa shule ya kumpeleka mtoto wako

Uchaguzi bora wa shule ya kumpeleka mtoto wako

Impactinglife

Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
41
Reaction score
99
Habari wakuu.

Leo ningependa tushirikishane jambo moja muhimu hususani kwa wazazi na walezi hasa wanapofanya maamuzi juu ya uchaguzi wa shule ya kumpeleka mwanafunzi au mtoto kwajili ya kupata elimu na maendeleo ya elimu kwa ujumla wa mwanafunzi.

Awali ya yote ni kiri au ku declare interest kuwa makala hii inatokana na uzoefu nilionao wa zaidi ya miaka 12 katika sekta ya elimu kama mdau wa elimu na mwalimu pia na yale niliyojifunza katika sekta hii ya elimu maana uzoefu ni moja ya mwalimu mzuri.

Nikiri pia tupo kwenye zama na jamii ambayo ina machaguo mengi sana (Choice oriented society) kiasi cha kwamba mtu anaweza kuwa kwenye DILLEMA OF DECISION katika kuamua nini afanye. Pia tupo kwenye wakati ambao taasisi nyingi binafsi zimetikisika na hivyo nyingine kutumia mbinu mbalimbali halali na zisizo halali katika kuvutia wateja huku AHADI NA HUDUMA inayozitoa hazilingani na uhalisia hivyo katika jamii kama hii ambayo karibia kila baada ya kilometa 5 hadi 10 unaweza kutana na Private school na wingi wa shule binafsi ni vyema ukawa informed vizuri juu ya mambo ya kuzingatia unapofanya uchaguzi wa SHULE AU TAASISI YA KUMPELEKA MWANAO kwajili ya kupata elimu na yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kabla ya kufanya uchaguzi huo.

1) USIISHIE KUANGALIA UKUBWA WA JINA NA HISTORIA YA TAASISI AU SHULE HUSIKA.

Tupo kwenye zama ambazo shule ni nyingi na zipo shule ambazo zilijijengea jina miaka mingi iliyopita na saizi zinaishi kwa kutumia jina au historia huku yaliyomo hayamo (JINA LA KITABU HALIAKISI YALIYOMO) na hivyo usipokuwa makini unaweza rubuniwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi na pia zipo shule ambazo HAZINA JINA lakini zimekuwa zikifanya kazi kubwa sana ya kuwapika na kuwaandaa wanafunzi wenye UELEWA TOFAUTI TOFAUTI ( SLOW LEARNERS AND FAST LEARNERS) lakini hazitambuliki kirahisi pamoja na kazi kubwa wanayofanya hawa ni wale ambao Ni (HAWAVUMI LAKINI WAMO).

Nimewahi fundisha katika shule moja mkoani Mbeya ambayo mwenye shule alikuwa yupo vizuri sana kwenye KUAJIRI WALIMU WENYE WEREDI NA DARAJA LA JUU na KUWASIMAMIA VIZURI ili kuhakikisha wanafanya vyema na kufaulisha na shule hii haijawahi kataa MWANAFUNZI WA UELEWA WOWOTE ULE na matokeo yake yalikuwa wakiwapika wanafunzi vizuri na kuwanoa hata wale ambao walikuwa wakiingia sekondari hawajui kusoma na kuandika Wanapohitimu kidato cha nne wanatoka na daraja la I hadi la III au IV tu kitu ambacho kwangu kilikuwa AJABU SANA (kuwafundisha wale ambao wengine waliona hawafundishiki).

Hapa ndipo nilipoamini ule msemo wa kimombo kuwa "sometimes big things can come in small package"
 
Uko sahihi sana kwa sasa private schools zimejijengea kadunia kao.most of them wanatoa huduma mbovu mno.wananyanyasa walimu haijapata kutokea,miezi sita bila kulipa mishahara na serikali ipo tu.sababu kubwa eti walimu ni wengi hutaki acha kazi.kweli wazazi fanyeni uchunguzi wa kina kabla ya kumpeleka mwanao shule flani.

Kuna shule moja ilikuwa na jina kibwa sana pale arusha akianza na herufi Muk.....Ma sasa wazazi wanaependa sana ila huduma yake kwa sasa ni mbovu mno.asante kwa uzi huu
 
Ni kweli kabisa,nami niko njia panda.Hizi shule usipokuwa makini unaweza kupoteza pesa bure.
 
Back
Top Bottom