Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Makamba amehairisha safariyakutoka Mwanza ambako alikuwa akingojea kusafiri leo Mchana hii, habari nilizopata ameagiza VIJANA Geita kumsaka mwandishi huyo sijui kwa lengo gani, na kamtuma katibu wake kupiga simu kwa Mhariri mkuu wa Mwananchi na kutoa lugha kali za Matusi huku akisema imeandikwa habari ya uongo.
Hajakataa kuzomewa lakini anasema wamekosea Kumwandika Msekwa kwani hakuwepo katika zomeazome hiyo na anataka mwandishi huyoafukuzwe kazi.
Nimetafuta simu ya Mwandishi huyohaipatikani, nikimpta na kuongea naye nitawaletea habari kamili.
 
Nimesikia kuwa bwana mchonga njia/tingatinga kazomewa katika kampeni, hapa kuna mawili 1. watu wamechoshwa na uongo/ahadi hewa na ufisadi ndani ya chama tawala 2. Ni siasa chafu yaani kikundi cha watu kimeamua kuzomea tu ili kupigia kampeni chama kingine.

Ila kwa mwaamko huu natumaini uchaguzi ujao utakuwa wa kueleweka zaidi, kidogo kidogo mpaka kieleweke. Nafurahi haya yanatokea nje ya miji mikubwa ikianisha kwamba mjini watu watakuwa waelewa zaidi na kutoa hii FALME ya kifisadi madarakani.

  • Uwezekano wa siasa chafu unaweza kuwa mdogo, kwani tunasoma pia kuwa idadi ya watu katika mikutano yao ni ndogo sana.
  • Watu wa mjini tusiwategemee kabisa, kwani wengi ni maopportunist na wabinafsi, kati ya sehemu zote zilizoamka kwa kutaka mabadiliko, hakuna miji mikubwa, nina uhakika EPA ilitumika zaidi mijini. Wapiga kura wenye uchungu wapo vijijini, na huko ndiko tunakotakiwa kuanza kuelimisha zaidi.
  • Nasema pia jamii ya wasomi haijawahi kuamka kuleta mabadiliko nchi hii, labda tuanze sasa.
  • Napata shaka sana na namna tunavyoweza kutumia vyuo vikuu kwa ajili ya mabadiliko. Nilishuhudia uchaguzi uliopita CCM wakigawa fedha zilizohifadhiwa kwenye furushi la mifuko ya plastiki kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, hebu chunguza matokeo kwenye vyuo vikuu yaliyoenda tofauti na CCM.
 
Makamba amehairisha safariyakutoka Mwanza ambako alikuwa akingojea kusafiri leo Mchana hii, habari nilizopata ameagiza VIJANA Geita kumsaka mwandishi huyo sijui kwa lengo gani, na kamtuma katibu wake kupiga simu kwa Mhariri mkuu wa Mwananchi na kutoa lugha kali za Matusi huku akisema imeandikwa habari ya uongo.
Hajakataa kuzomewa lakini anasema wamekosea Kumwandika Msekwa kwani hakuwepo katika zomeazome hiyo na anataka mwandishi huyoafukuzwe kazi.
Nimetafuta simu ya Mwandishi huyohaipatikani, nikimpta na kuongea naye nitawaletea habari kamili.

''Watashindana lakini hawatashinda''.......Mch. A.Lusekelo
 
Tukubali sasa hivi CCM hawana hata chembe ya sababu kushinda uchaguzi hata kama malecela aseme nini!

Hapana, wana sababu elfu mia za kushinda - nitataja chache :-

1. Fisadi Rostam Aziz
2. Jaji Lewis Makame
3. Polisi Said Mwema
5. Shushushu Othman Rashidi
6. Rugaruga Tendwa
7. Mawaziri
8. Wabunge wa CCM
9. Magabacholi
10. Wakuu wa Mikoa na wilaya
11. Katiba
12. Kiranja Mkuu, JMK.

Wizi, hongo, utapeli, uwongo, uonevu na kila aina ya mchezo mchafu - vyote ruksa kwa CCM na ndiyo mitaji yao ya ushindi.
 
Mag3, ni kweli kabisa ila naongezea TAKRIMA
 
Bibi Lolencia Maselle Bukwimba, mgombea wa CCM, usikubali Makao Makuu au Ikulu wakupangie taratibu za kampeni yako. Jaribu kuji distance na wazee wasiokubalika, amua nani unataka aje kuku introduce na kukunadi kwa wananchi, sio Makamba na kina Msekwa wakupangie.

Msekwa hawezi kuuza mtu Mwanza, yeye mwenyewe walimkataa katika timbwili lake na Mongella.

Malecela nae alishapoteza gravitas, hasikiliziki na mtu ndani au nje ya chama. Kama mzee wa chama, kaitisha mkutano kutoa wito wa dhati kuhusu malumbano ya hadharani ya wana CCM. Wamempuuza, wanapigana mabomu mpaka wanapelekana TAKUKURU na kwa majaji. Hasikilizwi hata na mkewe. Bwana Malecela mkimya, anasema shutuma za ufisadi zibakie ndani kwa ndani kwenye warsha za chama, Bibi Malecela anafurumusha makombora bila kusubiri makongamano ya sekretarieti za chama, mwendo wa taratibu wa Mzee yeye hawezi kumfuatisha. Hana mvuto hata nyumbani.

Watu wanaopuuzwa kama hao huwezi ukawaleta wakutambulishe kwa watu, utazomewa.

Hapana, wana sababu elfu mia za kushinda - nitataja chache :-

1. Fisadi Rostam Aziz
2. Jaji Lewis Makame
3. Polisi Said Mwema
5. Shushushu Othman Rashidi
6. Rugaruga Tendwa
7. Mawaziri
8. Wabunge wa CCM
9. Magabacholi
10. Wakuu wa Mikoa na wilaya
11. Katiba
12. Kiranja Mkuu, JMK.

Wizi, hongo, utapeli, uwongo, uonevu na kila aina ya mchezo mchafu - vyote ruksa kwa CCM na ndiyo mitaji yao ya ushindi.

Kweli kabisa ila tu umewasahau viungo muhimu kabisa "Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya majimbo yaliyomo." Wengine ni walimu hasa wa shule za msingi ambao ni wasimamizi wa vituo. Hao wa mwisho pamoja nakuwa wanadhalilishwa lakini ndio namba moja katika kusaidia kuiba kura
 
Date::5/7/2009
Malecela, Msekwa wazomewa Nyarugusu katika kampeni

Na Frederick Katulanda, Busanda

Mwananchi

1. KAMPENI za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda jana zilizidi kukumbana na upinzani mkali baada ya makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela, kujikuta wakizomewa wakati walipokuwa wakijinadi katika mkutano uliofanyika Nyarugusu wilayani Geita.

2. Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Clement Mabina alisimama jukwaani kabla ya kumkaribisha Malecela ili amnadi mgombea wa chama hicho na kuwaeleza kuwa anazo taarifa kuwa kuna watu ambao wamepangwa hapo kwa ajili ya kuzomea, naye kuzomewa.

3. Kutokana na hali hiyo Malecela aliamua kuwatuliza na kuomba Busanda isigeuke kama Tarime na kwamba wao CCM wanataka kampeni za amani na utulivu.

Ndipo ilipofika zamu ya Msekwa kumnadi mgombea na baada ya kupanda jukwaani alimkaribisha mgombea aliyemsimamisha mumuwe, Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao.

Hata hivyo zomea zomea hizo hazikuweza kuhatarisha amani katika mkutano huo na mgombea huyo alijieleza bila ya matatizo na kupiga magoti lakini alipoomba kura, naye akajikuta anazomewa.

- Unajua nilikuwa sijaiona hii, mbona big deal for nothing? Mimi nilifikiri uchaguzi umeshafanyika na upinzani wameshinda kumbe ilikuwa ni kampeni tu? Yaaani Chedama kuwapanda wazomeaji na CCM nao kuwapanda wazomeaji kwenye kampnei za Chadema, ni a big deal?

- Yaani all this pages ni kwa sababu ya shughuli za kampeni ambayo haijaisha? Au kuna something hakijasemwa au ni kwa sababu kipenzi cha JF Malecela amehusika?

Wakuu kampeni zinaendelea na CCM, tutashinda hiki kiti bila tatizo, kuzomea hakujawahi kuamua mshindi wa kiti, na ukiona chama kimoja kinaishia kuapanga wananchi wa kuzomea, ujue kimeshajua matokeo yatakuwaje, hapa CCM juu zaidi! Bwa! ha! ha!

FMES!
 
haha, unajua tatizo ni hizi dalili zinazojitokeza juzi juzi tu, before tulikuwa tunapeta tu, makofi nyimbo...mara wakaanza kupiga mawe magari, mara kuzomewa, 2010 wanaweza kututupia mavi wananchi tusipowaondoa hawa mafia...wameharibu
 
1.
Dilunga;
Bibi Lolencia Maselle Bukwimba, mgombea wa CCM, usikubali Makao Makuu au Ikulu wakupangie taratibu za kampeni yako. Jaribu kuji distance na wazee wasiokubalika, amua nani unataka aje kuku introduce na kukunadi kwa wananchi, sio Makamba na kina Msekwa wakupangie.

- Mgombea yoyote hawezi kuwa bigger than chama anachogombea, huu ushauri wako ni pure waste, kwa sababu kama huyu mgombea alikwua na ubavu wa kushidna bila CCM, basi asingembea under tiketi ya CCM, kwa hiyo kama anataka kushinda ni lazima awasikilize viongozi wa chama chake cha CCM.

2.
Msekwa hawezi kuuza mtu Mwanza, yeye mwenyewe walimkataa katika timbwili lake na Mongella.

- Kama kawaida yako, siku zote hata siku moja huwezi kuwa na ukweli, zaidi ya logic tu ni lini Msekwa alikataliwa over Mama Mongella? Msekwa akiwa Spika, aligombea ubuneg Ukerewe na ksuhinda kiti, na kukikalia wka 5 years, ilipokuja tena uchaguzi akaamua kukiachia mwenyewe kwa hiari yake, huku akiendelea kuwa Spika, ndpo Mama Mongella akashinda kiti mpaka leo, sasa hizi habari zako za Msekwa kukatalwia umezitoa wapi? Ni uongo tena wa kitoto sana!

3.
Malecela nae alishapoteza gravitas, hasikiliziki na mtu ndani au nje ya chama. Kama mzee wa chama, kaitisha mkutano kutoa wito wa dhati kuhusu malumbano ya hadharani ya wana CCM. Wamempuuza, wanapigana mabomu mpaka wanapelekana TAKUKURU na kwa majaji.

- Hiyo gravitas aliipoteza wapi? CCM haiwezi kuwa haimsikilizi halafu ikamuomba kama chama kwenda kusimamia uchaguzi huu wa ubunge, kama ilivyomuomba kusimamia Mbeya na CCM ikashinda, kwa hiyo again ni uongo wa mchana ambao hauwezi kuwasaidia huko Busanda, kama unaewza nenda uwasaidie upinzani, maana CCM tuko imaara sana na tutashinda huu uchaguzi bila matatizo, kwa sababu historia inajisema wazi anapokwenda Malecela kushiriki uchaguzi mdogo kama huu, hawezi rudi miono mitupu, haijawahi kutokea!

- Kuhusu malumbano again uko mbali sana na ukweli, Mengi sio kiongozi wa CCM kwa hiyo hana sababu yoyote ya kusikiliza mawazo ya viongozi wa CCM, na besides Malecela ni mstaafu kwa hiyo mawazo yake sio sheria au amri ka wananchama wa CCM, ila ni ushauri tu, sasa ushauri unaweza kusikilizwa au usisikilizwe, sio lazima, sasa unaona ulivyo mbali na ukweli? Aibuuu! Kiongozi mstaafu asiyesikilizwa na chama chake, lakini chama hicho hicho kikamuomba aende kusimamia uchaguzi wake, unahitaji kupuuzwa tu mkuu!

4.
Hasikilizwi hata na mkewe. Bwana Malecela mkimya, anasema shutuma za ufisadi zibakie ndani kwa ndani kwenye warsha za chama, Bibi Malecela anafurumusha makombora bila kusubiri makongamano ya sekretarieti za chama, mwendo wa taratibu wa Mzee yeye hawezi kumfuatisha. Hana mvuto hata nyumbani.
- There you go your true colors, yaani wewe kwani unasikilizwa na mkeo? Toka lini? Bwa! ha! ha! ah! s

- Sasa ya kusikilizana na mkewe wewe umeyajuaje? Malecela kama mstaafu anataka ya ufisadi wabaki ndani ya chama chake, mkewe ambaye ni kiongozi wa CCM anataka yasemwe wazi, meaning kwamba wanatimiza demokrasia inavyotaka kukubali kutokubaliana, ndio maana mke wa Dr.Slaa ni CCM na Slaa mwenyewe ni Chadema, ndio maana kule US James Carville ni Democrat na mkewe ni Republican, mkuu jaribu kupunguza chuki zisizo na mpango zinakupunguzia sana hadhi na kuelimisha wananchi hapa maana sio siri unayo elimu kubwa sana ambayo wananchi hapa wangenufaika nayo sana kama ungepunguza chuki za binafsi katika hoja zako, kwa sababu umejawa mno na chuki na wivu kwamba unashindwa hata kufikiria nje ya box lako, acha hizi haziwezi kuwasiadia wananchi hapa wala huko Busanda!

Mambo ya kiongozi na mkewe, ndani ya nyumba zao hayahusiki na siasa za taifa, kama vile ambavyo ya wewe na mkeo yalivyo hayatuhusu hapa JF!

Respect Bwa! ha! ha! ah!

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

haha, unajua tatizo ni hizi dalili zinazojitokeza juzi juzi tu, before tulikuwa tunapeta tu, makofi nyimbo...mara wakaanza kupiga mawe magari, mara kuzomewa, 2010 wanaweza kututupia mavi wananchi tusipowaondoa hawa mafia...wameharibu

- Hapana kuwa mkweli, ya kuzomeana yameanza baada ya Zitto kusimamishwa ubunge na bunge, viongozi wa serikali ya sasa walipojaribu kuwaeilmisha wananchi what happened ndio wakaanza kuzomewa na since then imekua kawaida viongozi wa CCM na upinzani kuzomeana, wakati wa kampeni za uchaguzi, nakumbuka Kiteto walivyozomeana na bado CCM ikashinda anyways, kuzomeana kwenye kampeni siwezi kuipa umuhimu wowote kwa sababu uchaguzi haujaisha bado!

- Halafu kiustaarabu na kuheshimu wasomaji wengine ungeweza kutumia neno "wanaweza kutupiwa kinyesi" maana hilo neno ulilotumia ni very low kwa sisi wananchi wastaarabu!

Ahsante Mkuu.

FMES!
 
... siku zote hata siku moja huwezi kuwa na ukweli, zaidi ya logic tu ni lini Msekwa alikataliwa over Mama Mongella? Msekwa akiwa Spika, aligombea ubuneg Ukerewe na ksuhinda kiti, na kukikalia wka 5 years, ilipokuja tena uchaguzi akaamua kukiachia mwenyewe kwa hiari yake, huku akiendelea kuwa Spika, ndpo Mama Mongella akashinda kiti mpaka leo, sasa hizi habari zako za Msekwa kukatalwia umezitoa wapi? Ni uongo tena wa kitoto sana!

Hivi unajua Field Marshall kuna vitu fulani vidogo vidogo vinakupita?

Utawezaje kutamka kwamba Msekwa aliacha Ubunge halafu akaendelea kuwa spika?

Bila hata kuhitaji kuwa mtaalam wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba au Parliamentary Standing Orders Ibara ya 7(2), hivi huwezi tu kujiuliza mwenyewe, Spika atakuwaje sio Mbunge? Utaokotaje mtu mtaani aje kugombea u-Uspika? Ataingiaje?

Sasa kama hujui vitu vidogo vidogo kama hivyo utawezaje kujua timbwili la Msekwa na Mongella?
 
Hiyo ibara uunayotumia kaipitie tena. 2005 Msekwa aligombea uspika kupitia CCM akashindwa na Sita na hiyo ni baada yakuwa ameshasema hataki tena kuwa spika uchu ukamwingia akajaribu akaumbuka mzee mzima. Ubunge nao pia alijaribu akapigwa mweleka kwenye kura za maoni.
 
https://www.jamiiforums.com/habari-...mafisadi-papa-wananchi-wako-mwaka-1947-a.html

"Kuthibitisha ninachokieleza juu ya uelewa wa wananchi na msimamo wao ni rahisi sana; Mwombe Mama Sophia, Mkuchika au mtetezi yoyote wa mafisadi akatolee kauli za kuwabeza wanaopingana na ufisadi na mafisadi papa, kwenye majukwaa ya wazi ya wananchi na si kwenye semina za ndani apate maajibu" Omutwale

Tayari Sophia Simba na Mkuchika wapo Busanda na wanaendeha kampeni kusaidia kuokoa jahazi la mgombe wao. Nasikia mgombea huyu anamahusiano makubwa sana na Sophia.
 
Back
Top Bottom