Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Date::5/7/2009

Ndipo ilipofika zamu ya Msekwa kumnadi mgombea na baada ya kupanda jukwaani alimkaribisha mgombea aliyemsimamisha mumuwe, Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao.

These guys are not serious eeh??

Hv kauli hizo zinatoka kwa watanzania wenzetu?

Huyo wa SEDA naye vp? Anatishia nyau vimikopo vya kishenzi vya

shs 50,000/=? Kweli, kama Baba kama mtoto!

NI BORA KUKOSA UMEME NA HIZO SENTI UCHWARA ZA SEDA!

PUNDA AFE, LAKINI MZIGO UWASILISHWE KWA TAJIRI!
 
Mimi nafikiri kama wasukuma watasimama imara wakagundua kwamba wameibiwa mda mrefu na chama cha ccm basi Ukombozi kamili wa wa Tanzania imekaribia kwa sababu wako wengi.
Pia inatia haibu kwa hawa wazee ambao hawana haibu wameendekeza ubinafsi kuliko chochote .Hawa wangepigwa mawe kama mkoa wa Mbeya wangeacha kampeni za kijinga hizo ,Kwani siku zote ccm inatawala lakini hawajawekewa umeme.huyo jamaa anaye danganya kwamba anaweza kutoa mikopo naye ni mjinga kwelikweli mimi nafikiri wanainchi wawe na mawe mifukoni.au slaa ndogo inapotokea mtu anawadharau kwa kuwambia vitu visivyoeleweka apewe adhabu kwani hawa wazee ni wazoefu inatia uchungu sana.
Ni atua nzuri hiyo nimeipenda kuna haja ya kujikomboa sasa.unyonyaji imetosha jamani.Pia kudharau watanzania siku moja itawapa mafundisho tena makubwa siku zao zime hesabiwa watu kama hawa.
 
mwanzo wa ngoma ni lele.
kama wasipoiba kura ushindi hawaupati hata kwa dawa.
 
Ina maana bwana Malecela anataka kuwaambia wananchi kuwa masharti ya kuletewa umeme ni kumchagua mbunge wa CCM?

Ina maana wananchi wakimchagua mgombea asiye wa CCM serikali itaacha kuleta umeme kwa sababu hiyo?

Huyu Malecela vipi?
Matamshi ya viongozi wa CCM na serikali wakati mwingine yananishangaza!Wanashindwa kuelewa Rais,Mawaziri,wakuu wa mikoa,Wilaya n.k.ni viongozi wa watanzania wote nawanafanya kazi kwa niaba ya watanzania wote.Kauli kama hizi sio tu za kibagu na za kitoto bali zinasikitisha.Inamana inatoa masharti kwa wananchi kitendo amabacho ni rushwa na kinyume na katiba yetu.Sitashanga ya kua serikali hiyo hiyo ikawa inafanya hujuma za maendeleo kwa majimbo amabayo hawakuchaguliwa!Na katika hali ya uchaguzi katika jimbo la Busanda kauli za CCM zinachekesha kama ni umeme CCM WALIKUA madarakani nini kiliwazuia kufanya hivyo mpaka wasubiri wakati wa uchaguzi,mume wa mgombea alikua wapi kumwaga misaada na kusubiri kutoa ahadi za kufanya hivyo baada ya mkewe kuchaguliwa.Huku nikujaribu kuwanunua wananchi kwa porojo,walikua na nafasi ya kuleta umeme na kumwaga misaada hiyo hawakufanya hivyo kama wangelifanya hayo kampeni zao zingelikua lahisi kwani kampeni zao zengeliandamana na ripoti ya nini kilitimizwa na nini kitatimizwa 'chema ujiuza kibaya ujitangaza'WATANZANIA SIO WAJINGA TENA WAMEAMKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Wazee wetu naona hawataki kusoma alama za nyakati: (Mwananchi 08-05-2009)

KAMPENI za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda jana zilizidi kukumbana na upinzani mkali baada ya makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela, kujikuta wakizomewa wakati walipokuwa wakijinadi katika mkutano uliofanyika Nyarugusu wilayani Geita.

Mbali na vigogo hao wa CCM, mgombea wa chama hicho katika uchaguzi huo mdogo, Lolencia Maselle Bukwimba na mumewe, Maselle Buziku walizomewa wakati walipotambulishwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
Tukio hilo limetokea siku moja baada ya chama hicho kujikuta kikiwa na watu wachache wakati wa kuzindua kampeni zake kwenye kata ya Kaseme, tofauti na mikutano ya vyama pinzani vya Chadema na CUF.
Dalili za hali mbaya katika mkutano huo zilianza wakati viongozi hao wakiingia eneo la Nyarugusu ambalo ni maalumu kwa wachimbaji wa dhahabu. Viongozi hao walipokelewa na alama ya vidole viwili kila walikopita. Alama ya vidole viwili hutumiwa na Chadema.
Zomea zomea hizo ziliwakabili viongozi hao wa CCM wakati walipokuwa wakimnadi mgombea wao. Hali mbaya ilianza kwa katibu mwenezi na uhamasishaji, Simon Mangelepa wakati aliposimama jukwaani na kuanza kuwatambulisha wageni walioambatana nao na kufuatiwa na mbunge wa viti maalum mkoani Mwanza, Maria Hewa ambaye alizomewa baada ya kuwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kutulia.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Clement Mabina alisimama jukwaani kabla ya kumkaribisha Malecela ili amnadi mgombea wa chama hicho na kuwaeleza kuwa anazo taarifa kuwa kuna watu ambao wamepangwa hapo kwa ajili ya kuzomea, naye kuzomewa.

Baadaye ikawa zamu ya Malecela ambaye baada ya kusimama jukwaani aliwaeleza wananchi kuwa shutuma za ufisadi hazina nafasi katika kampeni kwa sasa na kuwataka wenye ushahidi wa ufisadi kuupeleka polisi, kauli ambayo iliwafanya wananchi ambao walikuwa wametulia, kuanza kuzomea wakimtaka aondoke huku wakionyesha vidole viwili.

Hata hivyo, Malecela aliwatuliza na kuwaeleza kuwa hiyo ndio njia sahihi ya kushughulikia mafisadi na kuendelea kuwaeleza wananchi kuwa iwapo wataichagua CCM katika uchaguzi huo watapatiwa umeme pamoja na kutengewa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

“Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo," alisema lakini akakatwa kauli na kelele za wananchi ambao walisema miaka yote wameichagua CCM na kuahidiwa mambo hayo bila ya kufanikiwa.

Kutokana na hali hiyo Malecela aliamua kuwatuliza na kuomba Busanda isigeuke kama Tarime na kwamba wao CCM wanataka kampeni za amani na utulivu.

Ndipo ilipofika zamu ya Msekwa kumnadi mgombea na baada ya kupanda jukwaani alimkaribisha mgombea aliyemsimamisha mumuwe, Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao.

Hata hivyo zomea zomea hizo hazikuweza kuhatarisha amani katika mkutano huo na mgombea huyo alijieleza bila ya matatizo na kupiga magoti lakini alipoomba kura, naye akajikuta anazomewa.

Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amekiri kuwa kuna hali ngumu kwenye Jimbo la Busanda na kuwataka viongozi wa chama hicho kupigana kufa au kupona ili kuhakikisha jimbo haliangukii mikononi mwa upinzani kwa kuwa machungu ya kushindwa Tarime anayajua.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamba juzi mchana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika mkutano wa ndani kwenye ofisi za CCM wilayani Geita baada ya kuwasili kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni wa chama chake zilizofanyika juzi katika kata ya Kaseme.

Makamba alikiri kuwa hali ni ngumu na hivyo kuwaomba kila mmoja kuhakikisha mgombea wa CCM anashinda, akilalamika kuwa makali ya kushindwa alishayaonja Tarime.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa chama wilayani humo zimeeleza kuwa Makamba aliamua kufanya mkutano huo kwa lengo la kuwekana sawa kutokana na CCM kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wale walioenguliwa katika kura za maoni za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho.

Makamba amesema "jamani kushindwa ni kubaya, mwenzenu Tarime nilionja ubaya wake mpaka ilibidi nitoroshwe na Green Guard ili kuepuka kuzomewa, sasa tusiposhikamana mambo yatakuwa magumu tutoe tofauti zetu,'” alisema mmoja wa wajumbe waliokuwa kwenye kikao hicho akimnukuu Makamba.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo Makamba alishtuka na kuhoji iwapo walikuwemo waandishi wa habari ukumbini humo na kuonya utoaji wa taarifa hizo baada ya kujibiwa hawakuwemo.

Aidha baada ya kujibiwa kuwa hakuna waandishi makamba alishtuka baada ya kubaini kuwa kulikuwa na mpiga picha wa chama na kumuagiza kuhakikisha mkanda huo anaukabidhi kwa katibu wa CCM wa mkoa.

Makamba alipoulizwa kuhusu suala hilo alijibu kuwa hajawahi kukiri kuwepo kwa hali ngumu kwa vile hana wasiwasi na uchaguzi huo na kusema alikuwa akieleza masuala ya kushikamana.

“Wewe unataka nikueleze mikakati yangu, kama nilikuwa nawahimiza watoto wangu kulima we unakutakia nini,” alihoji katibu huyo wa CCM alipoulizwa na Mwananchi kuhusu kikao hicho.

Sambamba na hatua hiyo Makamba alimtaka mjumbe wa halmshauri kuu ya chama hicho mkoani Mwanza, Anthony Diallo kutumia uwezo wake kuhakikisha kampeni hizo zinakuwa na hamasa ya kutosha ikiwa ni pamoja na kurusha taarifa zake katika vyombo vya habari.

Uchaguzi katika jimbo la uchaguzi la Busanda umepangwa kufanyika Mei 24 kwa lengo la kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Faustine Kabuzi Rwilombe.

Vyama vingine vinavyowania kiti hicho ni Chadema, CUF na UDP
 
na bado,
ccm haitoki huko!
chadema kama kawaida!
 
huyo ndo mzee cigwiyemisi mzee wa besidei majuzi hapa.
hawa wanasiasa wazee walishazoea kusema uongo miaka tele na sasa hawaoni soni kudanganya tena na tena.
 
nadhani kuna thread nyengie kama hii
MODS please
 
"Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo,"
"Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao."

Wadau = swali langu kwa hizo quote mbili from kyaka.

hivi kumbe umeme ni zawadi kwa wengine kwa kuwa wamechagua ccm? hawa wananchi si wanalipa kodi jamani?kwanini kiongozi anasimama jukwaani na kusema wakichaguliwa wao ndio watafanya majukumu yao?hivi haya si yanapaswa kufanya na serikali iliyoko madarakani regardless eneo hilo liliwachagua hao or not?

Na huyo mume anayeahidi kutumia seda kuwapa mikopo waliomchagua MKE wake?
hivi hizi taarifa SEDA wanazo? Huku si kuinsult intteligence ya watanzania? i am so sick of this? hebu mnisaidie jamani.
 
"Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo,"
"Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao."

Wadau = swali langu kwa hizo quote mbili from kyaka.

hivi kumbe umeme ni zawadi kwa wengine kwa kuwa wamechagua ccm? hawa wananchi si wanalipa kodi jamani?kwanini kiongozi anasimama jukwaani na kusema wakichaguliwa wao ndio watafanya majukumu yao?hivi haya si yanapaswa kufanya na serikali iliyoko madarakani regardless eneo hilo liliwachagua hao or not?

Na huyo mume anayeahidi kutumia seda kuwapa mikopo waliomchagua MKE wake?
hivi hizi taarifa SEDA wanazo? Huku si kuinsult intteligence ya watanzania? i am so sick of this? hebu mnisaidie jamani.

Mkuu una macho ya ndani kweli!.........hayo uliyoyang'amua hapo....ndiyo haswa huwa wanayatumia hawa jamaa wasisiemu kuwarubuni wananchi wawachague!

Laiti kama wananchi wote huko vijijini wangeweza kuyang'amua hayo, tungekuwa mbali sana!
 
Hawa watu wanaojiita CCM wana vichwa vya ajabu sana, wanafikiri Watanzania bado analogu! Haki ya Mtanzania wanaitoa eti ni zawadi
 
NEXT LEVEL, nakubaliana na wewe asilimia 100. Pia napenda kuwaambia wananchi wa Busaga kwamba Wakati wa CCM umekwisha na kama tulikuwa watoto tunadanganywa kwa pipi sasa tumekua - tena tumekua sana KIAKILI, KIMWILI na KIROHO ? umeme siyo zawadi ni haki ya kila mtanzania pindi fungu la fedha likiwepo. Tumechoshwa na porojo za hao wazee wameking'ang'ania hicho chama kama vile cha kwao - wamekizaa wao. Let the Busaga people choose their leader in peace - afadhali kukosa huo umeme for life kuliko kuwachagua hao walaaniwa .....! AM FED UP with these people
 
Ila tu wasiicshie kuwazomea bali wawanyime kura. Kama wawazomea halafu wawape kura then haisaidii kitu kwa vile washazoea haya na wanaona kama vile ni kelele za mpangaji!!!
 
Wacha kuzomewa mwisho wataanza tena kurushiwa mawe na kunadiwa wezi ,we wacha tu wajipitishe pitishe kwenye anga za waliochoka na ufisadi watakiona kilichomfanya tembo awe na mwili mkubwa.
 
Hawa wazee wamekosa akili na hekima kwa kiwango hiki? Shwain

Vipi umeme haupo mpaka leo? Ni kwa sababu jimbo lilikuwa na linaongozwa na upinzani? Wanazeeka vibaya hawa.
 
mwanzo wa ngoma ni lele.
kama wasipoiba kura ushindi hawaupati hata kwa dawa.

Kinachotakiwa ni kuhakikisha kunakuwa na uangalizi mzuri kwenye zoezi zima la upigaji kura na kwenye kuhesabu kura. Hawa wazee wa SISIEMU leo wanakuja na sera ya kuleta umeme miaka yote hiyo walikuwa wapi?? Kinachotakiwa hichi Chama Cha Mafisadi kielewe kuwa watanzania ndio wana amka kutoka usingizini na wameshachoshwa na serikali ya kifisadi.

BUSANDA OYEEEEEEEEE!!!!
 
Malecela; Dume la Mbegu, Tingatinga, Urais sio kubeba Zege......and now umeme=CCM!
 
Malecela; Dume la Mbegu, Tingatinga, Urais sio kubeba Zege......and now umeme=CCM!

Huyu mzee nilikuwa namuheshimu sana, na hasa pale alipo mtia moyo Mkewe Mama Kilango kukandamiza kibara wale mafisadi wa Richmondi, pamoja na utulivu alio uonyesha baada ya kunyanganywa tonge la upresida kiaina!

Ila sasa huku anako elekea anaanza kujiondolea heshima yake taratiiiiibu, mwishowe ataanza kuimbwa mitaani na kuoneakana hafai.

Nawasihi tu walioko karibu naye, Hata hero wetu Mama K, msihi mzee atulie aache kujipaka matope.

By theway kuna mwenzetu humu JF anaitwa somebody malecera alitualika kwenye birthday ya 75yrs old, tafadhari kamfikishie ujumbe dingi arudi home apumzike!
 
Huyu mzee nilikuwa namuheshimu sana, na hasa pale alipo mtia moyo Mkewe Mama Kilango kukandamiza kibara wale mafisadi wa Richmondi, pamoja na utulivu alio uonyesha baada ya kunyanganywa tonge la upresida kiaina!

Ila sasa huku anako elekea anaanza kujiondolea heshima yake taratiiiiibu, mwishowe ataanza kuimbwa mitaani na kuoneakana hafai.

Nawasihi tu walioko karibu naye, Hata hero wetu Mama K, msihi mzee atulie aache kujipaka matope.

By theway kuna mwenzetu humu JF anaitwa somebody malecera alitualika kwenye birthday ya 75yrs old, tafadhari kamfikishie ujumbe dingi arudi home apumzike!
Mzee ni mwana-Siasa, yeye anatimiza wajibu wake kichama, kwa kusema anayoyasema which is an advantage kwa opposition kwa sababu wananchi hawakubali; nyie mlitaka mzee aseme mnayoyataka nyie? everything has a limit; ahadi nazo zikizidi bila kuzitimiza zinakuwa utapeli; hapo ndiyo wananchi wanarevolt, inakuwa rahisi kwa opposition kuchukua kiti. Tukubali sasa hivi CCM hawana hata chembe ya sababu kushinda uchaguzi hata kama malecela aseme nini!
 
Back
Top Bottom