Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 189
Nimesikia kuwa bwana mchonga njia/tingatinga kazomewa katika kampeni, hapa kuna mawili 1. watu wamechoshwa na uongo/ahadi hewa na ufisadi ndani ya chama tawala 2. Ni siasa chafu yaani kikundi cha watu kimeamua kuzomea tu ili kupigia kampeni chama kingine.
Ila kwa mwaamko huu natumaini uchaguzi ujao utakuwa wa kueleweka zaidi, kidogo kidogo mpaka kieleweke. Nafurahi haya yanatokea nje ya miji mikubwa ikianisha kwamba mjini watu watakuwa waelewa zaidi na kutoa hii FALME ya kifisadi madarakani.
Makamba amehairisha safariyakutoka Mwanza ambako alikuwa akingojea kusafiri leo Mchana hii, habari nilizopata ameagiza VIJANA Geita kumsaka mwandishi huyo sijui kwa lengo gani, na kamtuma katibu wake kupiga simu kwa Mhariri mkuu wa Mwananchi na kutoa lugha kali za Matusi huku akisema imeandikwa habari ya uongo.
Hajakataa kuzomewa lakini anasema wamekosea Kumwandika Msekwa kwani hakuwepo katika zomeazome hiyo na anataka mwandishi huyoafukuzwe kazi.
Nimetafuta simu ya Mwandishi huyohaipatikani, nikimpta na kuongea naye nitawaletea habari kamili.
Tukubali sasa hivi CCM hawana hata chembe ya sababu kushinda uchaguzi hata kama malecela aseme nini!
Hapana, wana sababu elfu mia za kushinda - nitataja chache :-
1. Fisadi Rostam Aziz
2. Jaji Lewis Makame
3. Polisi Said Mwema
5. Shushushu Othman Rashidi
6. Rugaruga Tendwa
7. Mawaziri
8. Wabunge wa CCM
9. Magabacholi
10. Wakuu wa Mikoa na wilaya
11. Katiba
12. Kiranja Mkuu, JMK.
Wizi, hongo, utapeli, uwongo, uonevu na kila aina ya mchezo mchafu - vyote ruksa kwa CCM na ndiyo mitaji yao ya ushindi.
Hapana, wana sababu elfu mia za kushinda - nitataja chache :-
1. Fisadi Rostam Aziz
2. Jaji Lewis Makame
3. Polisi Said Mwema
5. Shushushu Othman Rashidi
6. Rugaruga Tendwa
7. Mawaziri
8. Wabunge wa CCM
9. Magabacholi
10. Wakuu wa Mikoa na wilaya
11. Katiba
12. Kiranja Mkuu, JMK.
Wizi, hongo, utapeli, uwongo, uonevu na kila aina ya mchezo mchafu - vyote ruksa kwa CCM na ndiyo mitaji yao ya ushindi.
Date::5/7/2009
Malecela, Msekwa wazomewa Nyarugusu katika kampeni
Na Frederick Katulanda, Busanda
Mwananchi
1. KAMPENI za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda jana zilizidi kukumbana na upinzani mkali baada ya makamu mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela, kujikuta wakizomewa wakati walipokuwa wakijinadi katika mkutano uliofanyika Nyarugusu wilayani Geita.
2. Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Clement Mabina alisimama jukwaani kabla ya kumkaribisha Malecela ili amnadi mgombea wa chama hicho na kuwaeleza kuwa anazo taarifa kuwa kuna watu ambao wamepangwa hapo kwa ajili ya kuzomea, naye kuzomewa.
3. Kutokana na hali hiyo Malecela aliamua kuwatuliza na kuomba Busanda isigeuke kama Tarime na kwamba wao CCM wanataka kampeni za amani na utulivu.
Ndipo ilipofika zamu ya Msekwa kumnadi mgombea na baada ya kupanda jukwaani alimkaribisha mgombea aliyemsimamisha mumuwe, Maselle Buziku, ambaye naye alipoeleza kuwa iwapo watamchagua mkewe atatumia nafasi yake SEDA kuhakikisha wanapata mikopo, lakini akazomewa na wananchi hao.
Hata hivyo zomea zomea hizo hazikuweza kuhatarisha amani katika mkutano huo na mgombea huyo alijieleza bila ya matatizo na kupiga magoti lakini alipoomba kura, naye akajikuta anazomewa.
- Unajua nilikuwa sijaiona hii, mbona big deal for nothing? Mimi nilifikiri uchaguzi umeshafanyika na upinzani wameshinda kumbe ilikuwa ni kampeni tu? Yaaani Chedama kuwapanda wazomeaji na CCM nao kuwapanda wazomeaji kwenye kampnei za Chadema, ni a big deal?
- Yaani all this pages ni kwa sababu ya shughuli za kampeni ambayo haijaisha? Au kuna something hakijasemwa au ni kwa sababu kipenzi cha JF Malecela amehusika?
Wakuu kampeni zinaendelea na CCM, tutashinda hiki kiti bila tatizo, kuzomea hakujawahi kuamua mshindi wa kiti, na ukiona chama kimoja kinaishia kuapanga wananchi wa kuzomea, ujue kimeshajua matokeo yatakuwaje, hapa CCM juu zaidi! Bwa! ha! ha!
FMES!
Dilunga;
Bibi Lolencia Maselle Bukwimba, mgombea wa CCM, usikubali Makao Makuu au Ikulu wakupangie taratibu za kampeni yako. Jaribu kuji distance na wazee wasiokubalika, amua nani unataka aje kuku introduce na kukunadi kwa wananchi, sio Makamba na kina Msekwa wakupangie.
Msekwa hawezi kuuza mtu Mwanza, yeye mwenyewe walimkataa katika timbwili lake na Mongella.
Malecela nae alishapoteza gravitas, hasikiliziki na mtu ndani au nje ya chama. Kama mzee wa chama, kaitisha mkutano kutoa wito wa dhati kuhusu malumbano ya hadharani ya wana CCM. Wamempuuza, wanapigana mabomu mpaka wanapelekana TAKUKURU na kwa majaji.
- There you go your true colors, yaani wewe kwani unasikilizwa na mkeo? Toka lini? Bwa! ha! ha! ah! sHasikilizwi hata na mkewe. Bwana Malecela mkimya, anasema shutuma za ufisadi zibakie ndani kwa ndani kwenye warsha za chama, Bibi Malecela anafurumusha makombora bila kusubiri makongamano ya sekretarieti za chama, mwendo wa taratibu wa Mzee yeye hawezi kumfuatisha. Hana mvuto hata nyumbani.
haha, unajua tatizo ni hizi dalili zinazojitokeza juzi juzi tu, before tulikuwa tunapeta tu, makofi nyimbo...mara wakaanza kupiga mawe magari, mara kuzomewa, 2010 wanaweza kututupia mavi wananchi tusipowaondoa hawa mafia...wameharibu
... siku zote hata siku moja huwezi kuwa na ukweli, zaidi ya logic tu ni lini Msekwa alikataliwa over Mama Mongella? Msekwa akiwa Spika, aligombea ubuneg Ukerewe na ksuhinda kiti, na kukikalia wka 5 years, ilipokuja tena uchaguzi akaamua kukiachia mwenyewe kwa hiari yake, huku akiendelea kuwa Spika, ndpo Mama Mongella akashinda kiti mpaka leo, sasa hizi habari zako za Msekwa kukatalwia umezitoa wapi? Ni uongo tena wa kitoto sana!
Hivi unajua Field Marshall kuna vitu fulani vidogo vidogo vinakupita?
Utawezaje kutamka kwamba Msekwa aliacha Ubunge halafu akaendelea kuwa spika?
Bila hata kuhitaji kuwa mtaalam wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba au Parliamentary Standing Orders Ibara ya 7(2), hivi huwezi tu kujiuliza mwenyewe, Spika atakuwaje sio Mbunge? Utaokotaje mtu mtaani aje kugombea u-Uspika? Ataingiaje?
Sasa kama hujui vitu vidogo vidogo kama hivyo utawezaje kujua timbwili la Msekwa na Mongella?
https://www.jamiiforums.com/habari-...mafisadi-papa-wananchi-wako-mwaka-1947-a.html
"Kuthibitisha ninachokieleza juu ya uelewa wa wananchi na msimamo wao ni rahisi sana; Mwombe Mama Sophia, Mkuchika au mtetezi yoyote wa mafisadi akatolee kauli za kuwabeza wanaopingana na ufisadi na mafisadi papa, kwenye majukwaa ya wazi ya wananchi na si kwenye semina za ndani apate maajibu" Omutwale