Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Hamjapewa nchi mnaanza kutuongopea seuze mkipewa si itakuwa balaa
 
Picha ziko wapi mkuu?, au ni mimi tu nashindwa kuzipata hapa JF?
Kama huoni picha ina maana wewe huitakii mema CHADEMA, mimi nimeziona kwi kwi kwi!!!!

Au ndio the Emperor's new clothes?
 
CCM wamekanusha habari hizo za kuzomewa, kwa uhakika wanaona aibu kukubali. Kazeni mwendo wana Busanda, tutafika tu siku moja!

Sijui watakana mpaka lini kwamba hawazomewi, ebu angalia hapa, Ngeleja imebidi atoroke ka mwizi baad ya kuwekwa kiti moto. Kwakweli Busanda Mungu awabariki sana. Ujumbe mnao utuma ni mkubwa kuliko mnavo dhani.
Kutoka mwananchi


Waziri Ngeleja awekwa 'kiti moto' Busanda
Mgombea Ubunge wa Chadema Finias Magesa akijinadi kwa wapiga kura katika mkutano wa chama chake uliofanyika Katoro jana na kuhudhuriwa na Zitto Kabwe.Na Frederick Katulanda, Busanda

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzongwa na kundi la wananchi waliomuhoji juu ya ahadi zake za umeme alipowasili katika mji wa Katoro wilayani Geita.

Tukio hilo mithili ya mdahalo lilitokea kati ya majira ya ya saa 9:30 hadi saa 10:15 muda mfupi tu baada ya Ngeleja kuwasili Busanda akitokea Mwanza.

Maswali yalianza baada ya Waziri Ngeleja kusalimiana na wananchi hao na akajibiwa kwa kuonyeshwa alama za vidole viwili.

Hali hiyo ilimfanya waziri huyo kuwauliza wananchi hao sababu za kuichukia CCM wakati imekuwa ikijitahidi kuwaletea maendeleo na ndipo walipoanza kumuuliza maswali huku akiyajibu wakati fulani kugeuka mabishano.

"Hatuwezi kuwashangilia nyinyi... mmetuahidi umeme siku nyingi na hatuuoni, leo mnakuja kutuambia nini. Alikuja hapa sijui (Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam) Malima akasema umeme utakuja, lakini wapi hatujaona lolote mpaka leo," alisema mwananchi mmoja.

Ngeleja alipotaka kujibu, mwananchi mwingine alidakia kusema: "Hata kwenye machimbo mmekuwa mkitunyang'anya maeneo yetu na kuwapa wawekezaji. Sisi mnatuona hatufai kama vile ni wakimbizi ndani ya nchi yetu."

Ngeleja alilazimika kuwatuliza na kuwaomba wapunguze maswali ili ajibu swali moja baada ya jingine, lakini kila mtu akataka kumuuliza swali na kukawa na msuguano kati yake na wananchi.

Alianza kujibu kwa kusema kuwa serikali ipo mbioni na kwamba kinachofanyika sasa ni kufuata taratibu kwa sababu mchakato wa suala hilo hauwezi kumalizika siku moja, hivyo akawaomba wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea.

Ngeleja alidai kuwa suala lao kuhusu umeme liko katika hatua ya kuridhisha na kwamba wanapaswa kutambua utaratibu wa kushughulikia miradi ya serikali umekuwa ukifanyika kwa hatua.

Majibu hayo yalipingwa na wananchi ambao walimwambia wamekuwa wakidanganywa kama watoto kwa sababu ya kutaka kura na wakishapata, hutoweka.

"Sikiliza basi nikujibu, wewe naona umetanguliza ushabiki tuu. Naomba unisikilize. Ni kweli tulipowaahidi umeme tulidhani mchakato ungekamilika mapema, lakini kuna mambo yametukwamisha, tunaomba mtuvumulie," alisema huku wananchi hao wakiendeleza maswali.

Wakati wakiendelea na mjadala huo, lilipita gari la mgombea CCM wa kiti cha ubunge cha Busanda, Lolensia Bukwimba na mara moja wananchi hao wakageuka na kuanza kuzomea msafara.

Wakati wakiendelea kuzomea ndipo Ngeleja alipopata mwanya na dereva wake akawasha gari na kuondoka.

Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited. CCM imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na Faustin Kabuzi Rwilomba ambaye alifariki akiwa nchini India alikoenda kutibiwa.





Halafu cheki nyomi hiyo anyo imwagia sera Magessa wa Chadema, si bure hapa operesheni sangara nimeikubali.
 
Hii triller kwanza ili kuwaweka watu tayari! Picha zenyewe kesho!

Kesho yenyewe mbona imeisha fika?, ila hii inaonyesha watu kila mtu ana hamu ya kuangalia jinsi mwamko ulivo kutoka kila kona ya Tanzania. lakini kwakweli wana Busanda wamenikuna. Mungu awabariki, ujumbe walio utuma si mdogo. na hakika, hakuna siraha iliyo kubwa kupita ya kuzomea!,


Pale mtu mzima anapo fanya kampeni ya uchaguzi ndani ya nyumba kwa kuogopa kuzomewa? sijui yale mabomu ya machozi wameyaweka wapi? make hiyo ndo ilikuwa silaha yao kubwa ya kuwatishia wananchi. ila wanabusanda wamekuja na siraha kiboko ya mabomu.. watakimbia wenyewe mwaka huu?/ sbili sasa hiyo 2010
 
Tuwazomee, tuwanyime kura hata wakitupigia magoti

Salehe Mohamed

Tanzania Daima~Muungwana ni Vitendo
​

NIMEFURAHISHWA na vituko vya kuzomewa kwa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Busanda, mkoani Mwanza, na kitendo cha mgombea ubunge wa chama hicho, Loloncia Maselle Bukwimba, kupiga magoti kuwaomba kura waananchi.

Kuna jambo moja napenda kuliweka wazi hapa mapema - Bukwimba ameonyesha ‘ukabila' - tena mbele ya viongozi wa juu waliokuwa jukwaani wakati wakimnadi mgombea wao huyo. Mbali na kujidai kuopiga magoti, alikuwa akitumia lugha za Kisukuma na Kinyamwezi kuomba ridhaa ya wananchi. Pale wengine walikuwa ni watani zao Wadigo na Wazaramu, sasa Bukwimba aklikuwa anafanya nini? Atakayenikosoa kwa hilo shauri yake!

Nimekenua meno hasa kwa mgombea kuwapigia magoti wapiga kura bila kujali umri wao, kuwaomba ridhaa ya kumpeleka bungeni kwa vile ana imani atavuna vinono kwa kuwa tayari wabunge wameanza mchakato wa kutaka kujineemesha zaidi.

Kitendo cha mgombea huyo kupiga magoti binafsi nakiona ni sawa na kujidhalilisha, kuonyesha udhaifu mbele ya wapiga kura pamoja na kuonyesha kiu na uchu madaraka alio nao mgombea huyo, ambaye bila shaka ameshatambua kuwa siasa ni ‘dili'.


Naamini mgombea yeyote mwenye kujiamini, malengo mazuri na dhamira ya kuwatumikia wananchi hana sababu ya kuwapigia magoti wananchi kuomba kura kwa kuwa sera zake ndizo zitakazomuuza na si vinginevyo.

Watu wanaotaka kura kwa kupiga magoti ni wa kuogopwa sana kwani wanakuwa wakarimu wanapoomba kura, lakini wanapozipata hubadilika na kuangalia zaidi masilahi yao na ya chama bila kujali wananchi waliomuwezesha kuwa mbunge.

Nina mifano mingi ya wabunge ambao hapo awali walikuwa wakarimu zaidi kwa wananchi wao, lakini baada ya kuchaguliwa walihamishia makazi yao Dar es Salaam au kuwaponda wananchi kuwa wamezidi kuwaomba fedha na kuwafikishia matatizo yao mengine kila kukicha.

Watu wanaoomba kura kwa aina hii hukosa ujasiri wa kuisimamia hoja wawapo ndani na nje ya Bunge, na ndiyo maana hivi sasa kuna baadhi ya wabunge hawajawahi kuonekana wakizungumza bungeni kiasi cha kupewa jina la ‘mabubu'.

Sipendi Bunge liwe na wabunge wa aina hii kwa kuwa watachangia kukwamisha maendeleo ya wananchi, na kuifanya serikali iendelee kulala usingizi katika utekelezaji wa majukumu yake kama ilivyoahidi katika ilani ya uchaguzi wa mwaka 2005.

Waswahili wanasema ‘Nyota njema huanza kuonekana asubuhi' na dalili za kuchagua wabunge wasio na ujasiri wa kutosha tumeshaanza kuziona hivi sasa kwa mgombea kukubali kupiga magoti kisa ni kuomba kura.

Tukio jingine lilonivutia ni lile la kuzomewa kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe wa chama hicho John Malecela pale walimisimama jukwaani na kumnadi mgombea wao Lolencia Maselle.

Tabia hii ya wananchi kuwazomea viongozi wa chama na serikali hivi sasa imeanza kupata nafasi katika vichwa vya wananchi na ni vema tukaitafakari kwa makini zaidi kuliko kuiona imepandikizwa na wapinzani. Hii si mara ya kwanza kwa wananchi kuwazomea viongozi wa chama na serikali kwani nakumbuka miaka miwili iliyopita mawaziri kadhaa walizomewa pale walipokuwa wakizunguka mikoani kuelezea uzuri wa bajeti.

Wananchi walikuwa wakiwaona mawaziri hao kama wamekosa kazi ya kufanya na wafujaji wa fedha za wananchi kwa kuandaa ziara ambazo hazina faida kwa Wananchi badala ya kufikiria kununua dawa, kujenga shule, zahanati na huduma nyingine kwa jamii.


Najua kuwa wananchi wana upeo mkubwa wa kutambua wapi ni viongozi makini na si tumeona michango ya wabunge na mawaziri waliozomewa na kukataliwa wakati wa kampeni za mwaka 2005 lakini zikatumiaka hila mapaka wakaingia madarakani?

Si ni hawa ambao hivi leo wanataka kuwadhibiti watu wanaovujisha siri za nyaraka za ufisadi kwa hofu kuwa vibarua vyao na vya wafadhili wao viatakuwa shakani?

Kuzomea ni hatua ya kutoridhishwa na jambo linalofanywa na serikali au chama fulani na kama hatua makini zisipochukuliwa na viongozi hao kuna kila dalili hali hiyo ikapevuka na kuwa ya hatari zaidi kuliko hata tunavyotarajia.

Ni vema kuanzia sasa wananchi tukaanza kuwa makini na kukataa ahadi hewa na vijizawadi vidogo vinavyotolewa na wagombea ili wachaguliwe, viongozi makini wenye lengo la kuwahudumia wananchi hawawezi kuwanunua wapiga kura bali hutumwa na utashi na dhamira yao.

Viongozi ‘wachumia matumbo' ndiyo ambao kila kukicha huangaika huku na huko kutafuta fedha za kuwahonga wananchi na kamwe hawawezi kuweka mbele masilahi ya wananchi bali watafikiria zaidi namna ya kurejesha fedha walizozitoa.

Sitanyamaza kukemea viongozi na wagombea wanaotumia mbinu za kuwapigia magoti wananchi kuwaomba kura na wanapofanikiwa huwatekeleza wananchi.

Najua kwa wakati huu wagombea ubunge wa jimbo hilo watakuwa wanahaha huku na kule kwenye kampeni lakini ni vizuri wakafanya kampeni zenye kulinda heshima yao, chama na familia kwa ujumla ili hata watakapokuwa mawaziri tusipate cha kuwatania.

 
Waziri Ngeleja awekwa 'kiti moto' Busanda
Na Frederick Katulanda, Busanda
Mwananchi


Mgombea Ubunge wa Chadema Finias Magesa akijinadi kwa wapiga kura katika mkutano wa chama chake uliofanyika Katoro jana na kuhudhuriwa na Zitto Kabwe.

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzongwa na kundi la wananchi waliomuhoji juu ya ahadi zake za umeme alipowasili katika mji wa Katoro wilayani Geita.

Tukio hilo mithili ya mdahalo lilitokea kati ya majira ya ya saa 9:30 hadi saa 10:15 muda mfupi tu baada ya Ngeleja kuwasili Busanda akitokea Mwanza.

Maswali yalianza baada ya Waziri Ngeleja kusalimiana na wananchi hao na akajibiwa kwa kuonyeshwa alama za vidole viwili.

Hali hiyo ilimfanya waziri huyo kuwauliza wananchi hao sababu za kuichukia CCM wakati imekuwa ikijitahidi kuwaletea maendeleo na ndipo walipoanza kumuuliza maswali huku akiyajibu wakati fulani kugeuka mabishano.

"Hatuwezi kuwashangilia nyinyi... mmetuahidi umeme siku nyingi na hatuuoni, leo mnakuja kutuambia nini. Alikuja hapa sijui (Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam) Malima akasema umeme utakuja, lakini wapi hatujaona lolote mpaka leo," alisema mwananchi mmoja.

Ngeleja alipotaka kujibu, mwananchi mwingine alidakia kusema: "Hata kwenye machimbo mmekuwa mkitunyang'anya maeneo yetu na kuwapa wawekezaji. Sisi mnatuona hatufai kama vile ni wakimbizi ndani ya nchi yetu."

Ngeleja alilazimika kuwatuliza na kuwaomba wapunguze maswali ili ajibu swali moja baada ya jingine, lakini kila mtu akataka kumuuliza swali na kukawa na msuguano kati yake na wananchi.

Alianza kujibu kwa kusema kuwa serikali ipo mbioni na kwamba kinachofanyika sasa ni kufuata taratibu kwa sababu mchakato wa suala hilo hauwezi kumalizika siku moja, hivyo akawaomba wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea.

Ngeleja alidai kuwa suala lao kuhusu umeme liko katika hatua ya kuridhisha na kwamba wanapaswa kutambua utaratibu wa kushughulikia miradi ya serikali umekuwa ukifanyika kwa hatua.

Majibu hayo yalipingwa na wananchi ambao walimwambia wamekuwa wakidanganywa kama watoto kwa sababu ya kutaka kura na wakishapata, hutoweka.

"Sikiliza basi nikujibu, wewe naona umetanguliza ushabiki tuu. Naomba unisikilize. Ni kweli tulipowaahidi umeme tulidhani mchakato ungekamilika mapema, lakini kuna mambo yametukwamisha, tunaomba mtuvumulie," alisema huku wananchi hao wakiendeleza maswali.

Wakati wakiendelea na mjadala huo, lilipita gari la mgombea CCM wa kiti cha ubunge cha Busanda, Lolensia Bukwimba na mara moja wananchi hao wakageuka na kuanza kuzomea msafara.

Wakati wakiendelea kuzomea ndipo Ngeleja alipopata mwanya na dereva wake akawasha gari na kuondoka.

Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited.

CCM imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na Faustin Kabuzi Rwilomba ambaye alifariki akiwa nchini India alikoenda kutibiwa.
 
Adaiwa kukwama kupanda jukwaani
.CCM yafanya mikutano mafichoni

Reuben Kagaruki na Faida Muyomba, Busanda

NAIBU Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto amesema tingatinga la Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Bw. John Malecela limeshindwa kupanda jukwaani kwa kuwa limegeuka bajaj kwa kuanza mikutano ya mafichoni.

Alisema hayo juzi wakati akihutubia umati mkubwa wa watu kwenye mkutano wa kampeni katika mji mdogo wa Katoro, jimboni hapa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho Bw. Finias Magesa.

"CCM hawana ubavu wa kupambana na CHADEMA, hata wabunge wao wanaojidai wanapambana na ufisadi ni waongo wakubwa. Kama wanataka kupambana na ufisadi waondoke CCM kwa sababu hawawezi kupambana na ufisadi wakiwa ndani ya CCM," alidai Bw. Zitto.

Alisema CCM imekuwa na mazoea ya kumtuma Bw. Malecela kwenye uchaguzi unaokuwa na upinzani mkubwa na ndio maana akaletwa hapa kama tingatinga lakini amejikuta akikwama kupanda jukwaani.

Bw. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alidai moto wa CHADEMA jimboni hapa Bw. Malecela hauwezi kwa kuwa ni bajaj iliyochoka na ndio maana imeamua kufanya mikutano ya mafichoni na wanachama yenye lengo la kuiba kura.

Katibu huyo ambaye alikuwa akishangiliwa muda wote alisema hata kama CCM watapeleka viongozi wao maarufu wakiwemo wabunge kama akina Dkt. Harrison Mwakyembe na Bi. Anne Kilango jimboni hapa lakini akatamba kuwa ngoma
hawaiwezi kwa kuwa ni nzito.

Bw. Zitto aliwaomba wananchi wa Busanda kumchagua mgombea wa chama hicho ili waweze kupata nguvu zaidi bungeni ya kupambana na ufisadi nchini.

Naye Faida Muyomba anaripoti kutoka Busanda kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Wilfred Lwakatare na wabunge wengine sita wanatarajiwa kuwasili jimboni humo kwa lengo la kuongeza nguvu za kampeni kwa chama hicho.

Katibu wa Tume ya Uchaguzi wa CUF, Bw. Maole Kuchilingulo aliwaambia waandishi habari kuwa kufika kwa Mwenyekiti huyo na wabunge hao kutaongeza hamasa kubwa zaidi kwenye uchaguzi huo.

Aliwataja wabunge watakaoongozana na Prof. Lipumba ni Bw. Omari Ali Mzee (Jimbo la Pemba), Bw. Mohamed Mnyaa (Pemba), Bi. Mwanawetu Zaharani(Viti Maalum) na Bi. Magreth Sakaya (Viti Maalum).

Wengine kwa mjibu wa katibu huyo ni Bi. Nuhu Bafadhili (Viti Maalum), Bw. Salum Abdallah (Pemba) na Bi. Savelina Mwijage (Viti Maalum) na kwamba safu hiyo inatarajiwa kuingia Busanda humo wiki hii kwa ajili ya kampeni.

Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kudhibiti njama za wizi wa kura zinazodaiwa kutumiwa na chama tawala cha CCM.


Source: Majira, Sunday, 10 May 2009
 

Nilitaka niachane nawe lakini ngoja nikujibu tu!

1. Kama RA ashikilii ccm kwa nini mnashindwa kumface na kumtimua kwenye chama chenu. Mtu mabaye image yake imeharibika hivyo hata kama anaonewa ni better ajkae pembeni lakini mmeshindwa kumtoa na anaendelea kukizamisha chama chenu. Sasa hhvi ili mptate ushindi ni lazima muibe tu na ndipo hapo umuhimu wake unapoonekana. Chama chenu tunajua kisipomtaka mtu huwa kinamwambia live, kumbuka John malecela alivyokemewa na mkapa kuwa aache kulilia kama ajakubaliana na matokea ahame chama. Unaona msipo mtaka mtu mnavyofanya kwa hiyo wewe bwabwaja tu lakini bado RA ni muhimu sana kwa chama chako.

2. Kutolewa uweka hazina hii nayo nimoja ya vioja unavyovirudia rudia humu mara kwa mara. Kwanza unataka kuonesha kuwa unamjua Jk mpaka rohoni kwa kusema kuwa amemtema uweka hazina RA kwa sababu unajuaje kama hawakukubaliana mapema kuwa atoke? hebu ona hili, hawa jamaa mwaka 2005 waliiba fedha za umma, na walijua kuwa wameiba fedha za umma inawezekana siku moja waka gundulika na wakigundulika wasipoteze image yao. nini wafanye ni kumtoa ni kumtoa mshiriki kwenye nafasi amabayo soo likigundulika haliwezi kukiweka chama chenu kwenye nafasi mbaya. Kwa hiyo RA alichagua yeye mwenyewe kutoka na ndiyo maana aliyebadili anachukua order kutoka kwake. Au unataka kusema kuwa mmeleta mtun mpya kwenye hiyo post?

3. Hii ya takukuru wewe subiri tu kwa nini unataka kuwahi hivyo? njisi alivyopokelewa tu inaonesha njisi mlivyo mpa nguvu kwenye chama chenu na serikali yenu. Kwa sasa kikwazo chake ni sisi wanachi tu kwani nyie (ccm na Serikali) tayari amewakamata pabaya sana, pale!

4. Kuhusu kutumia Jina la Yesu wewe niombee tu kwani nampenda sana na nitaendelea kumweka mbele. Naomba unieleze ila nijirekebishe kuhusu kulitumia vibaya jina lake kwani hiyo ni moja ya mambo ambayo ninakuwa mpole kabisa

5 Mimi sijifanyi chadema ila kwa sasa kura yangu inaelekea huko. Naona unatamani niwe ccm na nimtumikie nchimbi na chama chako. kwani kwa wewe bora ni ushindi kwa chama chako na sio maslai ya taifa. unachotaka hakiwez kutokea ni ndoto tu. ccm haiwezi hata siku moja kujisafisha kwani imeoza.

6. tafuta njia nyingine ya kumbana mwanachama mwenzio nchimbi na sio kupitia kwangu mimi. Mimi sian tatizo na wewe binasfi wala sikujui na siitaji kukujua ila ukileta mawazo yako hapa nakujibu.

7 Namalizia kwa kusema kuwa kama unataka ushindi wa chama chako no=i lazima umpende RA kwani ndiye ushindi wenu
 
Huyu Zitto sasa keshaanza kuboa. Sijapendezwa na matusi yake ya reja reja kwa mzee Malecela na kama anazo attacks ilitakiwa azielekeze kwenye policies za CCM na siyo Mzee huyu ambaye hakuna alichomkosea

Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu

Mbona yeye mama yake aliiba pesa za walemavu na kukimbia mji na hakuna aliyepanda jukwaani kumwambia kuwa ni mwizi?

Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi
 

Jana Arsenal kafungwa ngapi?
...... Yeyote mwenye namba za Zitto naomba!
 
Huyu Zitto sasa keshaanza kuboa. Sijapendezwa na matusi yake ya reja reja kwa mzee Malecela na kama anazo attacks ilitakiwa azielekeze kwenye policies za CCM na siyo Mzee huyu ambaye hakuna alichomkosea

Matusi gani?
 

Mkuu GT pole naona ni maji ya shingo jahazi linazama Busanda mtumeni JK aende akamnadi yule mama lasivyo pigo jingine hilo....hakuna tusi hapo mkuu
 
Sasa arsenal wanahusiana nini na huu mjadala?

Acheni upuuzi huu mnaotaka kuuleta

Issue hapa ni zitto kumtukana mzee Malecela na si arsenal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…