Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

CONFIRM UFISADI WA CCM HADI KTK KURA

Diwani wa CCM anaswa akidaiwa kununua shahada

Na Frederick Katulanda,Busanda


WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Busanda zikiendelea kushika kasi, hali imekuwa mbaya kwa CCM, baada ya diwani na mabalozi wake wawili kunaswa wakidaiwa kuorodhesha majina ya watu wenye shahada kwa lengo la kuzinunua.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na msimamizi wa uchaguzi wa CUF, Maole Kuchilongulo kuituhumu CCM kuwa ilikuwa ikijiandaa kuendesha hujuma ya kununua shahada za wapiga kura kwa lengo la kupunguza kura za upinzani.

Tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji cha Shilungule, kata ya Busanda kati ya saa 2:30 na saa 3:00 usiku baada ya mwenyekiti wa Chadema wa kata hiyo kubaini kikao cha siri cha wajumbe wa nyumba kumi kilichokuwa kikiongozwa na diwani wa kata hiyo, Alphonce Matonange (CCM).

Inadaiwa kikao hicho kilikuwa na ajenda ya kuorodhesha shahada za wapiga kura.
Kamanda wa polisi wilayani Geita (OCD), Shabani Kimei alithibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema jeshi lake limewakamata kutokana na malalamiko ya Chadema na kwamba wanalifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo.

“Sisi kazi yetu ni kupokea malalamiko kama hivyo tumepokea na sasa tunafanya uchunguzi. Tumewaita watu wa Chadema wametoa maelezo na tunaendelea na uchunguzi ukikamilika tutawasiliana na msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuangalia sheria za uchaguzi zinasemaje juu ya hatua hiyo,” alieleza.

Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi wa oganaizesheni ya mafunzo wa Chadema ambaye pia ni kamanda wa kampeni za uchaguzi wa Busanda, Singo Benson Kigaila alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo, walituma gari na kuwasiliana na polisi ambao walifika na kumtia mbaroni diwani huyo na balozi mmoja huku wengine wakikimbia.

Sambamba na mjumbe huyo kukamatwa na diwani, mjumbe mwingine wa nyumba kumi amekamatwa jana asubuhi katika Kijiji cha Musasa kilicho kata hiyo ya Busanda akidaiwa kuendesha zoezi hilo la kuorodhesha majina ya wananchi wenye shahada pamoja na namba zake.

“Baada ya kupata taarifa hiyo tulipeleka timu yetu, wakati inafika tu diwani na wajumbe wengine ambao walikuwa katika zoezi hilo walikimbia baada ya kuona mwanga wa taa za gari, mjumbe mmoja ambaye alikuwa na shahada alinaswa na baada ya kuhojiwa alikiri kuendesha zoezi hilo,” alieleza.

Alisema akihojiwa na maofisa wa polisi mbele ya viongozi wa Chadema, mjumbe huyo wa nyumba kumi alisema walikuwa wakiorodhesha shahada hizo kutokana na maelekezo ya wakubwa wake ndani ya CCM ambao waliyatoa kupitia msimamizi wa chama chao ambaye alimweleza kuwa ni mwanamke kutoka wilayani Magu mkoani Mwanza.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Diwani Alphonce Matonange wa kata ya Busanda ambaye inadaiwa baada ya kukimbia usiku huo aliwahi kupiga simu polisi akidai kulikuwa na gari la Chadema ambalo lilikuwa limeenda kijijini hapo kwa nia mbaya na kwamba lilitaka kumgonga.

Mwingine ni mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina la Abdalah Ibrahimu ambaye inadaiwa alikutwa akiwa na karatasi iliyokuwa imeshaorodheshwa watu 20, ikionyesha majina na namba zao za shahada za kupigia kura.

Kigaila alisema kuwa hatua hiyo ni kosa la jinai kwa vile sheria inaeleza wazi kuwa ni kosa la jinai kuorodhesha namba ya shahada ya kupigia kura ya mtu mwingine awe mwanachama wako ama wa chama kingine na kusema hatua yao ya kwanza imekuwa ni kuwakamata na kuwakabidhi mikononi mwa polisi kuthibitisha walichokuwa wakieleza katika mikutano yao.

Alisema sasa wanasubiri kuona polisi itawafanya nini ikiwa ni pamoja na viongozi wao waliowatuma kuendesha zoezi hilo.

Wakati huo huo, wanafunzi wa shule ya sekondari ya Butundwe iliyopo katika kata ya Nyakagomba wameadhibiwa kwa viboko sita kila mmoja baada ya kuzomea msafara wa mgombea ubunge wa CCM, Lolencia Bukwimba wakati ulipokuwa ukipita eneo la shule yao kutoka kwenye kampeni.

Tukio hilo hilo limetokea Ijumaa majira ya saa 10:00 jioni wakati wanafunzi hao walipoona msafara wa mgombea huyo ukipita eneo la shule na kuzomea, kitendo ambacho kiliwaudhi baadhi ya viongozi wa CCM na kuwaagiza viongozi wa kata kufuatilia shule hiyo.

Habari toka Nyakagomba zinaeleza kuwa katika maagizo hayo katibu mwenezi wa kata hiyo, Oscar Magori, ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nyakagomba, ndiye aliyekwenda kulalamika kwa mwalimu mmoja wa zamu ambaye aliamua kuwaadhibu wanafunzi wote wa kidato cha kwanza lakini baadhi ya wanafunzi waligoma na hivyo kuwaadhibu sita tu.

Mkuu wa shule hiyo Monika Mzungu alisema wanafunzi hao wameadhibiwa na mwalimu huyo kwa sababu binafsi na kwamba yeye kama mkuu wa shule hiyo hakutoa amri hiyo ya kuwachapa viboko wanafunzi.

“Mimi sikuagiza watoto hao waadhibiwe. Nilishauri wasijiingize katika siasa na waepuke kushabikia vyama bali wajitahidi katika masomo. Kama kuna mwalimu amewaadhibu amewaadhibu yeye kama yeye na sina habari na hilo,” alieleza mkuu huyo. 


 

We FMES acha mambo ya uchama na undugu.

Akiguswa malecela ndio inakuwa nongwa. huyo Mzee aliposema huko Busanda kwamba wananchi wasichague upinzani kwa kuwa hauwezi kuleta maendeleo na kuandikwa kurasa za mbele za magazeti wee ulioona poa. na aliposema wabunge wa upanzani hawana mchango bungeni kutokana na uwingi wa wabunge wa CCM weweee uliona sawa tu anavyowasema wakina Dr Slaa?
 

Wacha uwongo wako umezoea kusema uwongo na kutetea ufisadi na chama chenu cha kifisadi. Malecela alizaliwa 1934, Shelukindo 1938 na Kingunge ni kijana mdogo wa 1969 - kachoka tu na sababu zipo !!
 
Huyu Tinga Tinga sijui amelogwa, yeye sio Makamu Mwenyekiti wa CCM wala sio Mbunge wa kanda ya Ziwa. Nani kamwambia ajipendekeze kwenye uwanja wa vita huko? Akivuliwa nguo wakina FMES wanakuja kulia lia hapa. yeye anajua kuwa Magesa ni bora kuliko huyo mgombea wa CCM halafu akwenda kumuuza kwa sababu tu ya kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya taifa. Sasa unamlaumu vipi Zitto kuanika unafiki unaoendelea?

Asha
 
Wacha uwongo wako umezoea kusema uwongo na kutetea ufisadi na chama chenu cha kifisadi. Malecela alizaliwa 1934, Shelukindo 1938 na Kingunge ni kijana mdogo wa 1969 - kachoka tu na sababu zipo !!

Kingunge yupi mkuu unamsema hapa? yaani Ngombale Mwiru? Na umri wa kutosha nilio nao hilo jina Ngombale mwiru nime anza kulisikia sijafikisha hata 10, huyu lazima yuko above 80yrs
 
Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi

JARIBU UONE::::::::

Matusi gani? mbona mna ngangana matusi matusi yatajeni tuyaone basi.. mi sioni tusi lolote hapo zaidi ya lugha linganifu ya tinga tinga na bajaji, kwani yeye ndo alimbatiza tinga tinga? wacheni kumwonea Zitto.
 

Ndio maana nawakatalia wote wale wanaojaribu kutetea CCM kwamba ni Safi isipokuwa viongozi wachache ndio wanakiharibu. Kansa ya CCM imeenea mwili mwili mzima na hakuna aliye afadhali humo kuanzia kiongozi wake mkuu hadi mjumbe wa nyumba kumi - shuhudia yanayotokea huko Busanda. Kinachonipa woga ni kuwa kama wako tayari kufanya umafia huu kutetea jimbo moja tu la uchaguzi, je tutegemee nini mwaka 2010.

Hakuna unafiki unaozidi kudai kwamba unapigana na UFISADI ndani ya CCM tena ukiwa kiongozi. Tusubiri vurugu na possilbly umwagaji wa damu mwaka 2010 kama ulivyotokea Zimbabwe kama wananchi wataamua kukiweka pembeni hiki chama cha wezi - ndio, wanakomba kila kitu iwe pesa, kura au mali za watanzania wote kwa ujumla wao. Sitashangaa wakereketwa wakijitoa mhanga na kujilipua kulinda mali hizo za wizi.

Hata hivyo kinacholeta faraja ni kuwa nguvu ya wananchi wakiamua kufanya kweli ni kama tsunami - haizuiliki na ukipambana nayo, umekwenda na maji. Walianza wana Tarime na nina imani wakifuata wana Busanda, ulaghai wa miaka 40 na ushee, utaporomoka kama minara ya Babeli.
Tarime waliwasha indiketa, Busanda fuateni njia.​
 

Na hapo kidogo ingefutia ile Mbeya vijijini, bahati yao walibahatisha kumuengua mapema, na unaona sasa wana ogopa kutangaza Biaharamlo make nako kunge wawakia tu!

Yaani wakuu.. tunako elekea ndiko.. ebu tukaze mguu tutafika. Inatia faraja kubwa kwamba huko nyarugusu machimboni watu wameisha wastukia hawa mafisadi.. yaani hapo ni pa tamu kuliko!
 
Kwani uwongo?

Zitto kamtukana mzee Malecela ambaye anaweza kuwa hata babu yake ... yeye kasahau kuwa mama yake mzazi ana tendencies za kifisadi fisadi baada ya kuwakimbia walemavu na pesa zao..ni kweli pia kuwa mama yake zito ni mlemavu

no secret there
 
Kingunge yupi mkuu unamsema hapa? yaani Ngombale Mwiru? Na umri wa kutosha nilio nao hilo jina Ngombale mwiru nime anza kulisikia sijafikisha hata 10, huyu lazima yuko above 80yrs

Kwi kwi kwi - labda tumuulize spika. Unajua tena sijui kalenda gani anatumia huyu Kingunge. Nachojua mtoto wake Kinjeketile ana miaka zaidi ya 34 hivi - sijui alimzaa akiwa na miaka 6? Hata hivyo ukweli ni kuwa Kingunge ni mdogo kwa Malecela.
 
Kwi kwi kwi - labda tumuulize spika. Unajua tena sijui kalenda gani anatumia huyu Kingunge. Nachojua mtoto wake Kinjeketile ana miaka zaidi ya 34 hivi - sijui alimzaa akiwa na miaka 6? Hata hivyo ukweli ni kuwa Kingunge ni mdogo kwa Malecela.

Mag3,
Hapana. Kingunge ni mzee zaidi ya Malecela. Ngoja aje hapa FMES atupe dataz.
 
mkuu sema tu umekosea kidogo.. hiyo mijitu inajua kuiba kura si kupiga kura!

Wow! CCM kwa wizi tu haijambo. Toka wizi wa rasilimali za taifa, mpaka wizi wa kura.

Baada ya muda kidogo wataanza kuibiana wao kwa wao.
 

Kumbe masanilo alikuwa sahihi hapa;

Madhara ya bangi bila kula ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiria....
 

- Sawa mimi nilifikiri unatishia kumtukana Mkulu wangu GT, otherwise Zitto ndiye hana jipya mkuu, maana sio siri na yeye ni CCM, sasa kama CCM imeoza basi na yeye ameoza au? Halafu hakuna mahali nimetukana Zito wala mama yake kwa hiyo hapo huna point mkuu!

- Halafu naomba nikuulize huko Busanda yupo Malecela tu? Mbona wengine hatuwasikii? Mema yako yaani ya Zitto kutetea Dowans huku DK. Slaa akikataa Dowans ile ile, maana yake ni moja kwamba mema yako sio lazima yawe na yangu, mimi ninaitetea CCM kama viongozi wengine wa CCM wanavyotetea huko Busanda, CCM tuna viongozi wachache wabovu so is Chadema, ya Zitto kuteeta Dowans kwangu ni uozo kwako ni sawa kwa sababu anayetetea ni Zitto, kwa hiyo hata kwenye hili la uozo huna point mkuu ni haki ya Malecela kama kiongozi mstaafu wa CCM kukitetea chama chake kama ilivyo haki yako kumtetea Zitto na Dowans ya Rostam.

- Otherwise hakuna anayetaka matusi ila wote tunaweza kuyarusha hakuna sababu ya kutishiana nyau! Na ninasema hivi Zitto zile dakika 15 za political fame zilishaisha, yeye sasa ni CCM the fact kwamba Chadema inaweza kumpeleka kwenye kampeni dhidi ya CCM ni dalili za Chadema kuishiwa mufilisi!, Chadema ninamuaminia DK. Slaa peke yake, wengine ni muflisi!

Respect

FMEs!
 
Mbona mie sioni hizo unazoziita hoja kutoka upande wako?
FMES, unakimbia kivuli? labda uende busanda ukatupe karata yako huenda ukapunguza shari japo kuwa nusu shari.

- Mkuu wewe acha hizi, nenda kwa bosi wako Nchimbi akusaidie upate ubunge wa Mwakaleli, nasikia ulikuwa unsaidia shule huko na unapeleka sana wazungu huko, sasa hapa unakwa Chadema, halafu in the really life kutwa kujikomba kwa wabunge wa CCM kina Nchimbi na Mwakyembe, kwa Mwandosya umejaribu umeshindwa maana hana muda na watu wa aina yako bwa! ha! ha! fanya kazi ndugu yangu ya siasa waachie wenyewe!

- Mkuu mimi sina shari, ila ukiileta kwangu ninakurudishia usoni yaani in your face na I love it!

Respect.

FMEs!
 

Mzee kapelekwa huko kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi ya kuiba kura za wananchi. Siwaonei haya watu kama hawa.

Katika uchaguzi wa 1995, ilibidi Mwenyekiti wa CCM wa wakati ule aibe mwenyewe kura. Sote tunajua alibadilisha matokeo ya uchaguzi Zanzibar (ambako CUF walikuwa wameshinda) na kwenye baadhi ya sehemu bara (ili kumnyima Mrema ushindi).

Ilipofika uchaguzi wa 2000, Mzee aliombwa asimamiye yeye uchaguzi kwa upande wa CCM. Alianza kwa kuwaasa vijana wa CCM wapigane na wapinzani kama ikibidi. Wale wasio na kumbukumbu fupi watakumbuka hayo.

Kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wana CCM dhidi ya ushindi wa Dr. Slaa Karatu iliwafungua Watanzania macho kuhusu jinsi CCM inavyodharau kura zao. Ulitolewa ushahidi wa wazi mahakamani jinsi viongozi wa CCM walivyojaribu kubadili matokeo ya uchaguzi katika sehemu mbali mbali. Yote hayo yaliwekwa hapa JF na tumeyaona.

CCM watajaribu kuiba kura Busanda. Hiyo ni kawaida yao. Wamemtuma Malechela kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi hiyo.

It is also my thesis that CCM is delaying the issuance of national identity cards for the simple reason proper identification could interfere with their usual methods of rigging elections. Prove me wrong if you can.
 

- Mkuu Asha, wewe ninakuheshimu na nitakujibu kistaarabu ni kwamba huko Busanda kampeni ni kali sana, na toka jana nimekubali kwamba CCM ina wakati mgumu sana kwa sababu moja kubwa wamechelewa sana kwenda huko, Chadema waliwahi, ninarudia tena kwamba baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa CCM walioko Busanda ninakubali kwamba chama changu CCM kina wakati mgumu sana kushinda huko,

- However, Malecela kusema hoja kwamba wapinzani hawawezi kuleta maendeleo huko Busanda, kwangu ni hoja je wamewahi kuleta maendeleo wapi? Ninajua for a fact kwamba jimbo moja tu la Ndesamburo ndilo lenye maendeleo ambayo hayakuepelekwa na CCM, ni kwa sababu mzee Ndesamburo mwenyewe hutumia hata hela zake kuwasadia wananchi, kwa mfano one time nilimuona kwa macho yangu majuu akinunua malori ya Fire akiyapeleka jimboni kwake, sasa kuacha hili jimbo mengine yote kama yana maendeleo yamepelekwa na CCM, kama hakuna basi wamenyimwa kwa sababu ya siasa za CCM Vs Upinzani, hizi siasa hata majuu kwenye demokrasia za kweli zipo.

- Wabunge wa upinzani hawana mchango mzito bungeni kwa sababu kwanza ni wachache na besides wengi wao ni CCM anyways, kwa hiyo hoja inasimama Republicans wamekataa Stimulus Bill lakini kwa sababu ni wachache wameshindwa na Democrats ambao ni wengi zaidi yao, sasa ukisema Republicans hawana effect yoyote Congress unakua unakosea? Au ukisema Upinzani hawana effect kwenye bunge letu kwa nini unakwua unakosea? Kushinda kwa Chadema au upinzani Busanda ni kuongeza ruzuku kwa chama, lakini not in anyway or shape kubadili upepo wa upitishwaji wa miswaada bungeni kwa ajili ya wananchi, no way! hii kwangi ni reality sio siasa au blah! balh!

- Umri mkubwa wa Malecela au umri mdogo wa Zitto, Rostam, na Manji bado hakuna scientific studies hapa bongo kuthibitisha kwamba kuna effect katika kuleta maendeleo ya taifa, ya jimbo, au kuwa sound politically, Kikwete amechaguliwa kwa platform ya ujana, sasa kama umri ni ishu then kwa nini tunamlilia sana hapa kwamba ameturudisha nyuma? Mimi sijawahi kusikia mtu mmoja akitajwa katika uchaguzi ambaye wala sio mgombea kama huu, maana yake ni moja tu kwamba ni threat na ataishia kushinda huko, na pia media inauza kutokana na jina lake, meaning kwamba majina mengine yalioko huko Busanda sio effective kama la Malecela, kuaniza kisiasa mpaka biashara ya media! Sasa kama all the attention huko Busanda iko kwa Malecela, then ni clear kwamba atashinda tu tena sina wasi na hilo!

Othwerwise, tupo pamoja mkuu!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMEs!
 

Wakuu JF.

Hivi huyu GAME THEORY yuko vipi? Au maana ya jina lake (GT) linaakisi na hoja zake? Maana komenti zake nyingi huwa naziona zinamaanisha tafsiri ya Game Theory. Mwenye ufahamu zaidi naomba anifahamishe au GT mwenyewe akikakaa na kuanza kuzitathmini hoja zake anaweza akawa kwenye nafasi nzuri ya kutuambia kuwa hoja zake zinazingatia maana halisi ya game theory.
 

- Acha vitisho mkuu kwenye siasa matusi kama ya Zitto yanakubalika, GT weka vitu mwanangu!

FMES!

Kama matusi ya zitto yana kubalika mbona GT huyo huyo kamlalamikia Zitto kwa "kumtukana" Malecela? Kumbe watu wana kubali matusi kwenye siasa yana kubalika sasa watu wana lalamika nini mzee aki tukanwa? Acheni mamboya double standards.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…