Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Vp watapakiwa kwenye malori na kuzungushwa vituoni kupiga kura mara kadhaa kama inavyokuwa huko Zenji au...
 
Yaani polisi wa Tanzania, ndio kikwazo cha demokrasia nchini, yaani wao wanatumiwa tuuu.. hata bila kufikiri!

Ila hata wafanyeje, kama Ukombozi wa Mtanzania muda wake umetimu, hawawezi zuia. Mungu yuko upande wetu, tutashinda tu.

Polisi wetu watafilikije wakati akili yao imedumaa.Nadhani hivi karibuni ndo angalau wameanza kuajili wasomi maana zamani waliowengi wakipata cheti cha sheria pale Taasisi ya elimu ya watu wazima tayari alionekana msomi.
Historia ya jeshi letu inajulikana wengi wao ni vijana wa Tanu Youth League waliokuwa wakijitolea na hatimaye kuwa special constable na leo hii viongozi wao ni elimu duni hawajaandaliwa vyema.
 
Na inasikitisha polisi wanaotumika na CCM ndio waathirika wakubwa wa country mismanagement inayoongozwa na CCM! Hali zao duni, hawathaminiwi, mishahara yao kiduchu and yet wanasupport CCM. I wish polisi na wanajeshi wangeigeuka CCM...jeshi la kikoloni lol
 
Huu utawala wa sheria unauona kwenye mapikipiki tu, kwenye Ufisadi uko kimyaaaa......[/QUOTE]


Mkuu, hii umegongomelea penyewe palepale! Asante mkuu.. sheria kwingine tu, kwingine wee.. usiguse! mmm?? tutafika?
 
Dawa ya moto ni moto, wanatembea na manati, janjaweed wanatembea na marungu, mashoka na mishale
 
Date::5/14/2009
Kampeni: Mawaziri wawili, Mbunge Kilango pia wazomewa Busanda

Na Mwandishi Wetu, Busanda

Mwananchi
​

SAKATA la zomea zomea jana liliingia katika sura mpya baada ya kuwakumba mawaziri wawili, George Mkuchika na William Ngeleja, pamoja na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.

Mbali na viongozi hao, mwingine aliyekumbana na shubiri ya Busanda ni mkuu wa kitengo cha propaganda wa CCM, Tambwe Hizza, pia katibu wa CCM mkoani Kigoma, Salum Msabaha pamoja na mgombea wa chama hicho, Lolensia Bukwimba.

Mkutano huo ulianza kukumbwa na 'kasheshe' hiyo mapema baada ya CCM kugawa mashati na fulana, lakini baadhi ya watu waliokuwa wakigawiwa waliamua kuzichana na kujikuta wakikamatwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Watu hao walipelekwa kituo cha polisi, lakini baadaye waliachiwa. Hata hivyo kitendo hicho kilionekana kuwapandisha hasira wananchi hao ambao waliamua kuzomea viongozi hao katika mkutano huo.


Kutokana na kitendo hicho cha kuzomea, watu 11 walikamatwa na polisi, akiwemo kiongozi wa Chadema ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Tanga, Mwita Waitara. Wote walipandishwa ndani ya gari la polisi namba PT 1498 na kupelekwa kituo cha polisi cha Katoro. Hali hiyo ilisababisha wananchi wa mji wa Katoro kuandamana hadi kituo cha polisi na kutawanywa na FFU.

Mkuchika, ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM, alikumbana na adha hiyo ya kuzomewa na umati mkubwa baada ya kutamba kuwa vyama vya upinzani vinadai kuwa CCM haipendwi hapo Katoro na jimbo zima la Busanda na kwamba, ni uongo kutokana na watu waliojitokeza katika mkutano huo kuwa wengi.

Kauli yake ilisababisha kelele nyingi za kuzomea huku watu wakionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema. Mkuchika alitulia kidogo na baadaye kutoa kejeli kuwa hao wanaozomea ni mamluki wa vyama vya upinzani.

''Waache wazomee kwani hao ni watu walioletwa na wapinzani. Tuwasameheni kwa kuwa hawajui watendalo. Sisi tuna hakika mgombea wetu atashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu na vile vile ukimwona mtu anazomea jua kakata tamaa,'' alisema Waziri Mkuchika huku akizidi kuzomewa.

Wakati Waziri Mkuchika akimnadi mgombea wa CCM, Lolensia Bukwimba kuwa ndiye atayekuwa mshindi wa kiti cha ubunge cha Jimbo la Busanda, baadhi ya watu walioonekana kuwa ni wafuasi wa Chadema walipiga kelele wakimtaja mgombea wao Magesa kuwa ndiye mshindi kwa kuimba "Magesa, Magesa. Magesa".

Naye Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini, alijikuta akitumia muda wake mwingi kwa nyimbo za Profesa J katika kumnadi mgombea wa CCM, akitaja wimbo wa "Ndio Mzee" kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuahidi ahadi ambazo hazitekelezeki.

Naye Tambwe Hizza alisema kuwa wapinzani wanayatumia magazeti kukishambulia chama hicho na kwamba, wapinzani ni wahuni wanaposema kuwa CCM haijafanya kitu chochote cha maendeleo, lakini akajikuta akizomewa kila mara.

Anne Kilango, ambaye amepata sifa kutokana na ujasiri wake katika vita dhidi ya ufisadi, alijikuta akikumbana na adha hiyo wakati akimnadi mgombea wa CCM.

Kilango aliwataka wananchi kumchagua Bukwimba ili aweze kushirikiana naye naye, lakini akajikuta akizomewa sawa na wenzake.

Kilango alisema wanawake wana nafasi kubwa ya kuongoza vizuri iwapo watapewa nafasi hiyo kwa kuwa hata familia zinaongozwa na kina mama, hivyo anayemdharau mwanamke ana mdharau mama yake mzazi.

Kamanda wa polisi wa wilaya ya Geita, Shabani Kimea alithibitisha kukamatwa kwa wafuasi wa Chadema kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mkutano wa CCM.

Alisema watu waliokamatwa ni 11 na kwamba imebainikwa kuwa yumo Waitara, ambaye ni kiongozi wa Chadema.

Alisema watu hao wanashikiliwa kwa kufanya fujo katika mkutano huo wa CCM na kwamba, baada ya kuhojiwa na kuchukuliwa maelezo kesho watafikishwa mahakamani.

 
mhhhhh mwaka wa shetani.ccm hebu waachilieni hao watu wa busanda wachague wanachokitaka,nyie mafisadi ni kama nguo iliyochakaa watu wanataka CHANGE.
 
CUF: We'll win Busanda by-election By Patty Magubira, Mwanza

The Civic United Front secretary-general, Mr Seif Sharif Hamad, is expected to address his party's campaign inaugural rally ahead of the forthcoming Busanda by-election.

The party's secretary for Geita District, Mr Severine Magese, said other top CUF leaders would grace the occasion to be held at Katoro township.

However, Mr Magese would not state the date of the inaugural rally although campaigns had started since April 23.

Four political parties - CUF, CCM, Chadema and UDP are taking part in the by-election slated for May 24.

CUF has nominated Mr Oscar Primus to vie for the seat left vacant by former MP Faustine Kabuzi Rwilomba (CCM), who died of heart complications in India mid last month.

Mr Magese said his party is optimistic that it would win the by-election despite threats and possible rigging the ruling party.

The CUF district secretary boasted that his party had so far hooked 57 defectors from CCM and Chadema in the constituency since the campaigns took off.


 

Ni kweli watu walishakata tamaa na sasa wana matumaini kwa vyama vya upinzani. CCM walishalewa madaraka na kuwadharau wananchi. Na sasa ni wakati wa wananchi kuwaonyesha CCM kuwa wao (wananchi) si mabwege tena. Now it is time for change, YES WE CAN.
 
Ni kweli watu walishakata tamaa na sasa wana matumaini kwa vyama vya upinzani. CCM walishalewa madaraka na kuwadharau wananchi. Na sasa ni wakati wa wananchi kuwaonyesha CCM kuwa wao (wananchi) si mabwege tena. Now it is time for change, YES WE CAN.

Kama hadithi vile lakini yanatokea, taratiiiiiiibu.. nyota ina anza kun'gara, tumaini lina anza kurejea, Ama kweli Mungu mkubwa.
 

Mkuu, mbinu zote zinaelkea kugonga mwamba! Yaani huwezi amini, ni kama ndoto vile ila ndo hivo yanatimia. Kweli walisema waweza kuwadnganya watu kwa kipindi fulani, lakini huwezi kuwadanganya maisha yao yote..
 
Tusubiri Mkuchika aite Press Conference kukanusha kuzomewa, kwa kuwa yupo kwenye eneo la tukio!!
 

Hii inawatisha nyinyi sisiemu maana nyie ndio mtakuwa wa mwisho katika uchaguzi huu nyuma ya cuf au chadema. Usipotee hapa siku tunashangilia ushindi.
Maana kuingiza vyama viwili vya upinzani vimewafanya mfikiri hapo ndipo ushindi ulipo. Mnajidanganya! mmesahau Tarime?
Watu wameichoka sisiemu yenu jamani! fed up! hata jina hatutaki kusikia!
 
Mmmh hii kweli ngumu! Inaonyesha wananchi wa nchi yetu tukufu ya wadanganyika wameamka. Jee ni wakati muafaka kusema wadanganyika wamekua wajanja??
 
Kama hadithi vile lakini yanatokea, taratiiiiiiibu.. nyota ina anza kun'gara, tumaini lina anza kurejea, Ama kweli Mungu mkubwa.

Itakuwa raha sana kwenye kampeni za mwakani kama Viongozi wa chama cha mafisadi na mapapa mafisadi kila wanapotia mguu katika kila kona ya nchi yetu wanazomewa tena kwa vishindo vya hali ya juu na zomea zomea hiyo inaashia kwenye CCM kutoambulia kura za Watanzania waliochoshwa na vioja vya chama cha mafisadi.
 
Ukianagalia kwa umakini hii zomea n ya Chadema. Wao wanaenda kwenye mikutano ya CCM na kuzomea. Hata CCM wakienda kwenye mikutano ya Chadema pia watazomea tu.

Kama CCM haipendwi hao wananchi LUKUKI waliokuwapo hapo walifuata nini?

Swali dogo tu hilo.
 
Kama CCM haipendwi hao wananchi LUKUKI waliokuwapo hapo walifuata nini?

Swali dogo tu hilo.[/QUOTE]

Ndio kusema wewe hujui kinachoendelea Busanda sasahivi???
CCM haipendwi kabisa, kinachowafanya washinde chaguzi nyingi ni kwa kuwa wanatumia mbinu chafu!!!!
 
ni moja ya mkakati wa 2010, inasemekana wamekua impressed na kazi iliyofanyika Zimbabwe, kuna tetesi walipeleka waangalizi wa kujifunza-how to terrorize voters..tusubiri tuone,na tumuombe Mungu...
 




Pikipiki zisajiliwe ndio zitumike kwenye kampeni,let us practice a rule of law,tuache visingizio,polisi lazima wafanye kazi yao bila kujali wakati huu ni wa kampeni au la provided a law has been broken. Mtumie pikipiki zisizosajiliwa muachwe tuuu kisa itaonekana ni unyanyasaji wapinzani?hata kidogo,pikipiki zisajiliwe ndio zitumiwe kwenye kampeni!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…