Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Ccm kazi wanayo kama hawatajirekebisha na siasa zao za kulindana.....

Maswali ya kujiuliza: Kujirekebisha kwa CCM kuna maslahi gani kwa Watanzania? Hivi bila ya CCM yenye uhalali/mabavu ya kiutawala Tanzania iliyo njema kwa wote haiwezekani? Je kujirekebisha huko kutatokana na kutambua kuwa wafanyayo walio wengi miongoni mwao na sio sahihi ama kwa kutambua kuwa wanapaswa "kuonekana" wamejirekebisha ili waweze kuendelea kuhalalisha utawala wao? Jee ni kwanini wajirekebishe wakati hayo wengine mnayoyaona kama ni mambo maovu bado yanawahakikishia kuendelea kulinda nafasi yao kiutawala? Ni yupi huyo ambaye ana MORAL AUTHORITY na UJASIRI wa kuongoza marekebisho hayo?

omarilyas
 
Naomba kutoka nje kidogo ya mada, mnaojuwa naomba mnijuze. Hivi hawa mawaziri wakienda kwenye hizo kampeni nani analipia gharama ni chama au serikali ambayo hata mimi nisiye na chama ninaiendesha kwa kodi zangu? Halafu pia hizo siku wakiwa huko, I know yaweza kuwa hata mwezi, mshahara bado wanachukuwa kama kawaida au lah? Kama wanachukuwa huu si upuuzi jamani na wizi mtupu? Maana tunawalipa mshahara kulitumikia Taifa na c chama.

Mwaka jana nilikwenda Ghana. Jamaa niliwapenda sana, kwao waziri akiteuliwa kugombea urais hapo hapo anaresigh kwa sababu 2 kubwa. (1) Ili kwa namna yeyote ile aisiingilie mchakato wa uchaguzi kwani kwa kuendelea na kuwa mfanyakazi wa serikali wakati tume ni ya serikali pia wanahisi kwamba kunaweza kusiwe na independence ya tume na uchaguzi usiwe fair. (2) Siku nyingi sana zinatumika kwenye campaign so kuzunguka nchi nzima then uendelee kuchukuwa mshahara kwao ni wizi wa waziwazi. One thing I know ni kwamba JK aliendelea kuwa waziri mpaka siku ya uchaguzi. Ninajiuliza kwanini tulindelea kumlipa mshahara ilihali tulijuwa kwamba alikuwa hafanyi kazi na pia kwanini aendelee kuwepo serikalini na huo uchaguzi unasimamiwa na serikali? Are we hopeless kiasi hicho?
 
Mwaka jana nilikwenda Ghana. Jamaa niliwapenda sana, kwao waziri akiteuliwa kugombea urais hapo hapo anaresigh kwa sababu 2 kubwa. (1) Ili kwa namna yeyote ile aisiingilie mchakato wa uchaguzi kwani kwa kuendelea na kuwa mfanyakazi wa serikali wakati tume ni ya serikali pia wanahisi kwamba kunaweza kusiwe na independence ya tume na uchaguzi usiwe fair. (2) Siku nyingi sana zinatumika kwenye campaign so kuzunguka nchi nzima then uendelee kuchukuwa mshahara kwao ni wizi wa waziwazi. One thing I know ni kwamba JK aliendelea kuwa waziri mpaka siku ya uchaguzi. Ninajiuliza kwanini tulindelea kumlipa mshahara ilihali tulijuwa kwamba alikuwa hafanyi kazi na pia kwanini aendelee kuwepo serikalini na huo uchaguzi unasimamiwa na serikali? Are we hopeless kiasi hicho?

Mkuu Ghana wapo juu sana kidemokrasia ni vigumu kulinganisha na nchi yeyote ya Afrika. Demokrasia ya Ghana imejikita ktk utashi wa Chama Tawala kukubali matakwa ya wananchi hivyo kuweka ushindani sawa kwa vyama vyote ktk chaguzi. Pia wananchi wapo tayari kuyakubali matokeo ya aina yeyote. It will take time kuweza kufikia kiwango hicho hasa kutokana na ibara ya 15:1
 
Ccm kazi wanayo kama hawatajirekebisha na siasa zao za kulindana.....sidhanii huko tuendako hali itakuwaje maana naona kabisa 2010 uchaguzi ni mgumu sana kwa mazingira ya ccm waliojitengenezea na kukumbatia mafisadi wao......endeleeni tuu mtajashangaa
CCM lazima wabadilike, muda muafaka umefika na nina imani wamejifunza mengi kwenye Chaguzi ndogo? Ni wakati muafaka Mwenyekiti wa Chama, akapanga safu mpya itakayompa ushindi. Mathalani Makamu Mwenyekiti akiwa Fredrick Sumaye na Katibu Mkuu Kinana, Naibu Katibu Mkuu Adam Kimbisa, Katibu Mwenezi Kilango, na Mweka Hazina Monica Mbega
 
Kama CCM haipendwi hao wananchi LUKUKI waliokuwapo hapo walifuata nini?

Swali dogo tu hilo.

Ndio kusema wewe hujui kinachoendelea Busanda sasahivi???
CCM haipendwi kabisa, kinachowafanya washinde chaguzi nyingi ni kwa kuwa wanatumia mbinu chafu!!!![/QUOTE]

Hao wananchi Lukuki walifuata pesa, kwani huju kama CCM wanapokuwa na mikutano huwachukua wananchi kutoka katika kata nyingine na kuwasafirisha kuja mahaari kwa ajili ya kuonyesha wingi. Nao wakishaletwa hulipwa posho. Busanda walianza kugawiwa mashati na posho ya sh. 2000 na wengine wenzangu mimi waliambulia na viroba vya konyangi sh. 1000.

Jibu lefu kwa swali fupi hilo.
 
Simbamwene said:
CCM lazima wabadilike, muda muafaka umefika na nina imani wamejifunza mengi kwenye Chaguzi ndogo? Ni wakati muafaka Mwenyekiti wa Chama, akapanga safu mpya itakayompa ushindi. Mathalani Makamu Mwenyekiti akiwa Fredrick Sumaye na Katibu Mkuu Kinana, Naibu Katibu Mkuu Adam Kimbisa, Katibu Mwenezi Kilango, na Mweka Hazina Monica Mbega

Simbamwene,

..aren't you fed up with CCM?!!

..bila kuondolewaa madarakani, CCM hawawezi kupata akili za kujisafisha, na kujipanga upya.
 
CCM lazima wabadilike, muda muafaka umefika na nina imani wamejifunza mengi kwenye Chaguzi ndogo? Ni wakati muafaka Mwenyekiti wa Chama, akapanga safu mpya itakayompa ushindi. Mathalani Makamu Mwenyekiti akiwa Fredrick Sumaye na Katibu Mkuu Kinana, Naibu Katibu Mkuu Adam Kimbisa, Katibu Mwenezi Kilango, na Mweka Hazina Monica Mbega

Mimi nadhani ianze hivi kwa ushindi wa kimbunga tena!

Katibu mkuu: Rostam Azizi
Katibu Mwenezi: Yusufu Makamba
Mkuchika ahamie kitengo cha propaganda.
 
Date::5/14/2009
Kampeni: Mawaziri wawili, Mbunge Kilango pia wazomewa Busanda

Na Mwandishi Wetu, Busanda

Mwananchi
​

SAKATA la zomea zomea jana liliingia katika sura mpya baada ya kuwakumba mawaziri wawili, George Mkuchika na William Ngeleja, pamoja na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.

Mbali na viongozi hao, mwingine aliyekumbana na shubiri ya Busanda ni mkuu wa kitengo cha propaganda wa CCM, Tambwe Hizza, pia katibu wa CCM mkoani Kigoma, Salum Msabaha pamoja na mgombea wa chama hicho, Lolensia Bukwimba.

Mkutano huo ulianza kukumbwa na 'kasheshe' hiyo mapema baada ya CCM kugawa mashati na fulana, lakini baadhi ya watu waliokuwa wakigawiwa waliamua kuzichana na kujikuta wakikamatwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Watu hao walipelekwa kituo cha polisi, lakini baadaye waliachiwa. Hata hivyo kitendo hicho kilionekana kuwapandisha hasira wananchi hao ambao waliamua kuzomea viongozi hao katika mkutano huo.


Kutokana na kitendo hicho cha kuzomea, watu 11 walikamatwa na polisi, akiwemo kiongozi wa Chadema ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Tanga, Mwita Waitara. Wote walipandishwa ndani ya gari la polisi namba PT 1498 na kupelekwa kituo cha polisi cha Katoro. Hali hiyo ilisababisha wananchi wa mji wa Katoro kuandamana hadi kituo cha polisi na kutawanywa na FFU.

Mkuchika, ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM, alikumbana na adha hiyo ya kuzomewa na umati mkubwa baada ya kutamba kuwa vyama vya upinzani vinadai kuwa CCM haipendwi hapo Katoro na jimbo zima la Busanda na kwamba, ni uongo kutokana na watu waliojitokeza katika mkutano huo kuwa wengi.

Kauli yake ilisababisha kelele nyingi za kuzomea huku watu wakionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema. Mkuchika alitulia kidogo na baadaye kutoa kejeli kuwa hao wanaozomea ni mamluki wa vyama vya upinzani.

''Waache wazomee kwani hao ni watu walioletwa na wapinzani. Tuwasameheni kwa kuwa hawajui watendalo. Sisi tuna hakika mgombea wetu atashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu na vile vile ukimwona mtu anazomea jua kakata tamaa,'' alisema Waziri Mkuchika huku akizidi kuzomewa.

Wakati Waziri Mkuchika akimnadi mgombea wa CCM, Lolensia Bukwimba kuwa ndiye atayekuwa mshindi wa kiti cha ubunge cha Jimbo la Busanda, baadhi ya watu walioonekana kuwa ni wafuasi wa Chadema walipiga kelele wakimtaja mgombea wao Magesa kuwa ndiye mshindi kwa kuimba "Magesa, Magesa. Magesa".

Naye Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini, alijikuta akitumia muda wake mwingi kwa nyimbo za Profesa J katika kumnadi mgombea wa CCM, akitaja wimbo wa "Ndio Mzee" kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuahidi ahadi ambazo hazitekelezeki.

Naye Tambwe Hizza alisema kuwa wapinzani wanayatumia magazeti kukishambulia chama hicho na kwamba, wapinzani ni wahuni wanaposema kuwa CCM haijafanya kitu chochote cha maendeleo, lakini akajikuta akizomewa kila mara.

Anne Kilango, ambaye amepata sifa kutokana na ujasiri wake katika vita dhidi ya ufisadi, alijikuta akikumbana na adha hiyo wakati akimnadi mgombea wa CCM.

Kilango aliwataka wananchi kumchagua Bukwimba ili aweze kushirikiana naye naye, lakini akajikuta akizomewa sawa na wenzake.

Kilango alisema wanawake wana nafasi kubwa ya kuongoza vizuri iwapo watapewa nafasi hiyo kwa kuwa hata familia zinaongozwa na kina mama, hivyo anayemdharau mwanamke ana mdharau mama yake mzazi.

Kamanda wa polisi wa wilaya ya Geita, Shabani Kimea alithibitisha kukamatwa kwa wafuasi wa Chadema kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mkutano wa CCM.

Alisema watu waliokamatwa ni 11 na kwamba imebainikwa kuwa yumo Waitara, ambaye ni kiongozi wa Chadema.

Alisema watu hao wanashikiliwa kwa kufanya fujo katika mkutano huo wa CCM na kwamba, baada ya kuhojiwa na kuchukuliwa maelezo kesho watafikishwa mahakamani.


Bubu,

Huyu Mwita Waitara ndio Mwita Mwikwabe?Maana Mwita Mwikwabe ndiye aliyekuwa katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga kabla ya kuhamia Chadema.Je,yote ni majina yake?Au kuna makosa?Ama...
 
CCM warudi kwenye methali za wahenga,chenye mwazo hakikosi mwisho,Ngoma ikilia sana hupasuka.
 
Date::5/16/2009
JK aipa pumzi CCM Busanda amrejesha aliyesababisha mpasuko

* Helkopta ya Chadema kutua wiki hii

Frederick Katulanda, Busanda

Mwananchi
​

ZIKIWA zimebakia siku saba kufanyika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelamba dume baada ya kufanikiwa kumshawishi kada wake aliyeshindwa kura za maoni, Donard Max ambaye atapanda jukwaani kuanzia leo, ili kusaidia kuokoa jahazi.

Kukubali kupanda jukwaani kwa Max ambaye anaanzia kampeni zake katika Kata ya Nyarugusu, kunaelezwa kunatokana na agizo la Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ambaye baada ya kuambiwa kuwa Max amegoma kusaidia kampeni, alimpigia simu na kumuomba kubadili msimamo wake kwa faida ya chama.

"Ni kweli Max leo ataanza rasmi kumnadi mgombea, lakini jambo hili ni siri kubwa, amepangiwa kata zenye hali mbaya ambako akiwa na timu yake atalazimika kupenya huko na kufanya vikao vya faragha na kambi zake," kilieleza chanzo chetu na kudokeza kuwa amekubali baada ya juhudi za mwenyekiti wa chama.

Hatua hiyo inaelezwa na wachambuzi wa hali ya kisiasa jimboni humo kuwa ni muhimu kwa chama hicho ili kiweze kujinasua, kwa vile mgawanyiko unaokikabili kwa kiwango kikubwa ulisababishwa na kumeguka kwa kambi ya Max aliyeibuka mshindi wa pili katika kura hizo, nyuma ya mgombea Lolensia Bukwimba.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Propaganda, Tambwe Hiza zimeeleza kuwa baada ya kubaini kuwa chama kipo katika hali mbaya, CCM ililazimika kumuita Max ili aweze kurejesha uhai wa chama hicho, kilichokuwa kinakabiliwa na misukosuko ya viongozi wake kuzomewa na watu wachache kujitokeza kwenye kampeni zake.

Awali, ilielezwa kuwa Max amegoma kurudi Busanda na kutoa sharti la kuondolewa kwa hasimu wake, Anthony Diallo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, jambo ambalo lilifanyika. Pia Max alifanya mazungumzo na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Samwel Malecela na makada wengine bila mafanikio.

Diallo anadaiwa kumsaidia Sostenes Kulwa aliyeshika nafasi ya tatu kwa nia ya kumuengua Max, jambo ambalo liligawa kura zake na kuambulia nafasi ya pili.

Taarifa nyingine za ndani zilisema kukubali kwa Max kupanda jukwaani, kunatokana na makubaliano ya faragha baina yake na Malecela kwa niaba ya Kikwete ambaye aliagiza arejeshewe gharama zake za kampeni katika mchakato wa kura za maoni.

Kutokana na makubaliano hayo CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye.

Hata hivyo, Max alipozungumza na Mwananchi Jumapili jana, alisema ameamua kusaidia kampeni kama mwanachama na siyo kwa kuombwa na vigogo wa chama hicho.

Kauli inayofafana na hiyo pia ilitolewa na Hiza ambaye alisema kwamba, Max ni sawa na wanachama wengine wa CCM wa wilaya ya Geita ambao wamekuwa na jukumu moja la kumnadi mgombea wa chama hicho.

"Huyu ni mwanachama sawa na wengine, hatusemi anapanda jukwaani kwa sababu zenu ninyi waandishi, anapanda sawa na viongozi wengine wote wa chama wilayani, hakufanya hivyo tangu awali kwa sababu hakuwapo Geita, sasa amekuja, atapanda jukwaani," alisema Hiza.

Kutokana na makubaliano hayo baina ya CCM na Max chanzo chetu kimedokeza kuwa tofauti kati ya kambi yake na Diallo imemalizika na hivyo mjumbe huyo wa NEC, kurejea Geita ambako tangu juzi ameonekana mitaani akiendelea kusaidia kampeni.

Kwa upande mwingine, CCM imepunguza idadi kubwa ya mikutano yake ya kampeni ya kumnadi mgombea wake katika miji na badala yake imeimarisha mikutano ya vijijini ambapo kwa siku imekuwa ikifanya mikutano mitatu hadi minne kila kata.

Hatua hii imekuja baada ya kukumbana na hali ngumu katika mikutano ya majukwaani ambayo imekuwa ikiishia kuzomewa kwa viongozi wake, hatua ambayo imeelezwa kuwa imekiathiri chama hicho kutokana na watu wengi kubadilika na kuisapoti kambi ya wapinzani wao na hasa Chadema.


Katika mikutano hiyo ya nje ya mji, viongozi na wabunge wa CCM wamekuwa wakizunguka kila kijiji kuzungumza na wananchi mbalimbali kwa makundi maalumu ambayo ni makundi ya wazee, vijana na viongozi wa dini.

"Hali yetu ni ngumu lakini siyo kama mnavyodhani, mkakati wetu wa vijijini ni mzito sana kutokana na kuonyesha mafanikio," alieleza mmoja wa viongozi wa wilaya wa CCM ambaye amepangiwa kata ya Nyarugusu.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakizungumza na wazee kwa kuwaomba radhi kutokana na kushindwa kutimiza ahadi walizoahidiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005 na kuwasii watoe nafasi kwa CCM kwa vile Rais Kikwete ameahidi kuyapa msukumo matatizo ya Busanda mara baada ya uchaguzi.

Wakati hayo yakitendeka, Chadema wameanzisha mkakati maalumu kwa ajili ya kusimamia na kulinda kura katika vituo ili kudhibiti upotevu wa kura zao.

Habari za ndani ya Chadema ambazo zimethibitishwa na Afisa Mwandamizi na Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Mwikwabe Waitara, zimesema kuwa kamati maalumu imeundwa kwa ajili ya kuratibu mbinu za usimamizi wa kura katika vituo jimboni Busanda ili kuhakikisha mgombea wao, Finias Magesa anaibuka mshindi.

Katika kufanikisha mkakati huo, kamati hiyo imetoa namba za viongozi ili wananchi waweze kutoa taarifa wakati wowote pale wanapoona masanduku yakiwa nje ya vituo au katika hali isiyo kawaida.

Akizungumza juzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, Waitara alisema wanatambua mikakati ya CCM, kwani baada ya kuzidiwa katika jukwaa wametulia wakielekeza mbinu zao katika wizi wa kura, jambo ambalo alisema watalisimamia kikamilifu kuhakikisha hawapati mwanya wa kufanikisha azma yao hiyo.

Sambamba na mkakati huo Chadema wamepanga kufanya kampeni za mwisho kwa kishindo huku wakitumia helkopta atakayozunguka nayo mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe ili kufikia vituo vingi kwa kipindi kifupi.

Vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo vimeendelea na mikakati yake ya kutumia majukwaa. CUF wameongeza nguvu kwa kumuita Mwenyekiti wake, Profose Ibrahimu Lipumba ambaye ataingia leo kumnadi mgombea wao, Oscar Ndalawah.

Kampeni za UDP zimeendelea kudorora kutokana na kutumia mbinu ya kutoa matangazo kwa njia ya vipaza sauti vilivyowekwa katika gari ambalo limekuwa likipita mara kadhaa katika mitaa kuwahimiza wananchi kumchagua mgombea wake, Beatrice Lubambe.

Katika hatua nyingine, Salma Said anaripoti kutoka Zanzibar kuwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM), Hamad Yussuf Masauni amewakemea wapinzani wanaowatisha na kuwazomea viongozi wa chama hicho katika kampeni zinazoendelea katika uchaguzi mdogo wa Busanda.

Akihutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Magogoni Visiwani Zanzibar, Masauni alisema Chadema kinaendesha kampeni chafu huko Busanda jambo ambalo ni kinyume na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi.

"Tumevumilia vya kutosha, sasa imetosha na sasa tunataka kuona mambo haya yanakomeshwa haraka…," alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Masauni aliyasema hayo wakati Chadema wakimlalamikia mkuu wa polisi wilaya ya Geita kwa kupokea amri kutoka kwa CCM kuwakamata wanachama wake bila sababu na wengine kufikishwa mahakamani, huku akiwaachia huru makada wa CCM waliokamatwa wakinunua shahada za kupigia kura.
 
CCM lazima wabadilike, muda muafaka umefika na nina imani wamejifunza mengi kwenye Chaguzi ndogo? Ni wakati muafaka Mwenyekiti wa Chama, akapanga safu mpya itakayompa ushindi. Mathalani Makamu Mwenyekiti akiwa Fredrick Sumaye na Katibu Mkuu Kinana, Naibu Katibu Mkuu Adam Kimbisa, Katibu Mwenezi Kilango, na Mweka Hazina Monica Mbega


DU........

Na hawa ndio mbadala wa walikuwepo? Kazi kwelikweli...

omarilyas
 
Kansa ya CCM imeenea mwili mwili mzima


Confirmed......na mwili huu hauponyeki kamwe. Kinachoendelea ni kuendeleza kufilisi na kubomoa kabisa familia ya Tanzania .....

omarilyas
 

Kukubali kupanda jukwaani kwa Max ambaye anaanzia kampeni zake katika Kata ya Nyarugusu, kunaelezwa kunatokana na agizo la Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ambaye baada ya kuambiwa kuwa Max amegoma kusaidia kampeni, alimpigia simu na kumuomba kubadili msimamo wake kwa faida ya chama.
Pia Max alifanya mazungumzo na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Samwel Malecela na makada wengine bila mafanikio.

Taarifa nyingine za ndani zilisema kukubali kwa Max kupanda jukwaani, kunatokana na makubaliano ya faragha baina yake na Malecela kwa niaba ya Kikwete ambaye aliagiza arejeshewe gharama zake za kampeni katika mchakato wa kura za maoni.

CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye.


CCM imepunguza idadi kubwa ya mikutano yake ya kampeni ya kumnadi mgombea wake katika miji na badala yake imeimarisha mikutano ya vijijini ambapo kwa siku imekuwa ikifanya mikutano mitatu hadi minne kila kata. Katika mikutano hiyo ya nje ya mji, viongozi na wabunge wa CCM wamekuwa wakizunguka kila kijiji kuzungumza na wananchi mbalimbali kwa makundi maalumu ambayo ni makundi ya wazee, vijana na viongozi wa dini.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakizungumza na wazee kwa kuwaomba radhi kutokana na kushindwa kutimiza ahadi walizoahidiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005 na kuwasii watoe nafasi kwa CCM kwa vile Rais Kikwete ameahidi kuyapa msukumo matatizo ya Busanda mara baada ya uchaguzi.

Inavyoonekana hapa ni kuwa CCM baada ya maji kuwafika shingoni wameamua kula matapishi yao wenyewe wakiongozwa na Raisi. Sasa hebu tujiulize ni aina gani ya vishawishi vinavyotumika hapa ili CCM iweze kushinda. Kama kuna mtu anayefaidika hapa kuliko mwingine yeyote ni Max - sijui kafungiwa mamilioni mangapi za walipa kodi. The guy must be laughing his way down to the bank !!

Halafu hii mikutano ya usiku vijijini kwa kuogopa kuzomewa mchana inaashiria nini kama siyo silaha kubwa ya CCM kila uchaguzi - RUSHWA. Takrima, wizi na ununuzi wa kadi za wapiga kura zikisimamiwa na jeshi la polisi na tume ya uchaguzi ni vitendo vinavyoweza kufanyika tu usiku - vitendo vya giza. Safari hii tumeshuhudia what they can do when they are desperate, naogopa yajayo 2010.
Hizi ni rasha rasha tu, 2010 itakuwa piga ua🙁​
 
Makamba, Msekwa wayeyuka Busanda
Nipashe - Na Simon Mhina
17th May 2009

Wamtosa mgombea akiwa mkiwa
Wanaogopa lawama eti akishindwa
Wamwachia zigo Anne Kilango Malecela


zomea zomea, fimbo ya mnyonge, yaonekana inafanya kazi - kumtimua Makamba si mchezo. Sasa huyu mama Kilango mmh - kazi kweli kweli !!

Kwa habari kamili soma nipashe Mei, 19 http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=2222
index.php

 
Simon Mhina
Katika kile kinachoonyesha kuwa mambo magumu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Busanda, viongozi wakuu wa chama hicho wanadaiwa kuondoka kwenye kampeni za uchaguzi huo na kumuacha mgombea wao akiwa mkiwa.

Viongozi hao ambao ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa wameondoka Busanda tangu kampeni za Chama hicho zilipozinduliwa.

Wachunguzi wa mambo ya siasa, wamesema kutoweka kwa Msekwa na Makamba kuna lengo la kunawa mikono, na kukwepa lawama iwapo mgombea wao atashindwa.

Akizungumza na gazeti hili, Msekwa alikiri kujiweka pembeni mwa kampeni hizo. “Ndio nilikuwepo kwenye ufunguzi nimeondoka, lakini sio kwa kuogopa zomeazomea kama mlivyoandika,”alisema.

Alipoulizwa kisa cha kukacha kampeni na kumuacha mgombea ukiwa, Msekwa alisema hizo ndizo sera zake na utaratibu ambao ameuanzisha ndani ya CCM.

Msekwa alisema CCM ilikuwa na utaratibu mbaya wa kuwamwaga vigogo wa Chama hicho kwenye chaguzi ndogo na kuacha kushughulikia kazi nyingine.

“Utaratibu wangu ambao nimeupendekeza ni kwamba kila kiongozi awajibike katika eneo lake, kila mtu na lwake, siwezi kuacha ofisi ya Chama chenye mtandao nchi nzima na kushughulikia kajimbo kamoja ka Busanda,”alisema Msekwa.

Alisema mambo ya kumwaga vigogo wa Chama, yanatakiwa yafanywe na wapinzani kwavile hawana mtandao wa kutosha.

“Mimi Nimefungua kampeni inatosha, mengine yafanywe na mgombea pamoja na viongozi wa CCM ngazi ya Jimbo,”alisema.

Kwa upande wake Makamba alisema yeye amejikita zaidi katika Uchaguzi mdogo ….. visiwani Zanzibar.

“Mimi nipo Zanzibar kazi yangu ipo huku mambo ya Buchosa, mimi simo wala usiniulize,”alisema kwa njia ya simu.

Habari toka kwenye vikao vya CCM mjini Busanda, zinasema siku ambayo vigogo wa Chama hicho walizomewa, Msekwa na Makamba waliitisha kikao cha ndani kujadili hali hiyo.

Habari hizo zinasema katika kikao hicho Makamba alifoka akidai kuwa mara baada ya kushindwa uchaguzi mdogo wa Tarime, kuna watu walipendekeza atimuliwe.

Kufuatia madai hayo, habari hizo zinasema Msekwa naye aliamua kujiweka pembeni kwa sababu hizo hizo.

Hata hivyo, kiongozi ambaye anaonekana kupigana kufa na kupona ni Makamu mstaafu wa CCM, John Malecela (Tingatinga), ambaye hata hivyo kwa kile kinalichoelezwa kuwa amegeuka Bajaji hapa Busanda, hataki kuhutubia mikutano sehemu za mijini.

“Mimi sijaondoka naendelea na kampeni, ila nimeweka kambi yangu Nyarugusu na ninahutubia mikutano minne kwa siku,” alisema alipozungumza na gazeti hili.

Kinachozidisha ugumu wa kampeni za CCM ni kutokana na vigogo wakiwemo Mawaziri kushindwa kuelezea sera zenye lengo la kutatua matatizo sugu ya jimbo hilo, ambayo ni umeme, maji, elimu, afya na miundombinu.

Mathalani, katika mkutano uliofanyika eneo la Katoro Centre, wananchi wengi wakiwemo wapinzani waliofurika, baada ya kusikia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, atahutubia wakiwa na matarajio kwamba angezungumzia kero ya umeme. Jimbo hilo halina umeme.

Hata hivyo Waziri Ngeleja alijikita zaidi katika kuwapiga vijembe viongozi wa Chadema.

Katika vijembe hivyo, Ngeleja alikuwa akitumia miziki ya bongo fleva ya wanamuziki akina Profesa J. badala ya Ilani ya CCM .

Vilevile alishindwa kuwashawishi wananchi hao kumkubali, baada ya kutumia takwimu za mafanikio ya Wizara yake nchi nzima, bila kufafanua kwamba katika jimbo hilo kuna mafanikio gani na wanatarajia kufanya nini.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu, Tanzania Bara, George Mkuchika, ameonekana kukosa uvumilivu, kiasi cha kuamua kutukana kwa ishara.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4:03 asubuhi, alipokuwa anapita kwenye eneo ambalo kuna kambi ya Chadema.

Mkuchika akiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruser lenye namba za usajili T995 AGK alizomewa na wafuasi wa Chadema, kisha kwa hasira akafungua kioo cha gari, akawaonyesha ishara kwa vidole vitatu vikimaanisha aina ya tusi.


Juzi wakati akitokea mjini Geita Mkuchika alilazimika kuficha uso kwa kuvaa kilemba, ili kuepuka zomeazomea.

Vilevile Katika mikutano ya CCM makada hao akiwemo Hiza Tambwe na Salum Msabaha, wanatumia muda mwingi kukejeli familia za viongozi wa Chadema, badala ya kuelezea kitu ambacho watawafanyia wananchi wa Busanda.

Mathalani mmoja wa wapiga debe hao, Shaibu Akwilombe, alitumia muda wote aliopewa kumnadi mgombea wao kuzungumzia madai kuwa mke wa mwenyekiti wa Chadema ni mtoto wa muasisi wa chama hicho.

Hata hivyo, makada hao kila walipotoa kejili hizo, walikuwa wanazomewa.

Kada ambaye alitarajiwa kukiokoa chama hicho ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, lakini kutokana na hali kuwa ngumu, matarajio yamekuwa hafifu.

Kwa ujumla vigogo walioletwa na CCM kuongeza nguvu, wameshindwa kukiletea afya chama hicho kwenye kampeni. Hata hivyo, katika hali inayoonyesha mtafaruku ndani ya kambi ya CCM, Mkuchika alisema sio kweli kwamba CCM imemuita Kilango aokoe jahazi.

Alisema Kilango alipelekwa Busanda na Umoja wa Wanawake (UWT) kwa lengo la kumsaidia mwanamke mwenzao hakuitwa na CCM.
Uchaguzi wa Busanda unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.

NIPASHE
 
Zipo tetesit kuwa CCM ina mpango wa kutuma makada wake mashuhuri Mhe Rostam Aziz na Mhe Andrew Chenge kwenda kuokna jahazi la CCM katika kampeni za ubunge Jimbo la Busanda. Sifa yao kuu ni kwa kuwa wanatoka kanda ya Ziwa na ni matajiri wakuawa. Je itasaidia?
 
hata siku moja hawawezi kupelekwa busanda,
we unafikiri ccm ni wapumbavu kias hicho?!
 
Kama ni kweli, basi sikio la kufa....
 
Zipo tetesi kuwa CCM imepanga kuwatuma makada wake mashuhuri Mhe Rostam Aziz na Mhe Andrew Chenge Kwenda kuokoa jahazi katika kampeni za ubumge jimbo la Busanda. Sifa yao kuu ni kutoka kanda ya ziwa. wanafikiri kama Mama Anne Kilango ameweza kusikilizwa nao pia watasikilizwa. Wama JF mna maoni gani?
 
Back
Top Bottom