Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
Kampeni: Mawaziri wawili, Mbunge Kilango pia wazomewa Busanda
Na Mwandishi Wetu, Busanda
SAKATA la zomea zomea jana liliingia katika sura mpya baada ya kuwakumba mawaziri wawili, George Mkuchika na William Ngeleja, pamoja na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.
Mbali na viongozi hao, mwingine aliyekumbana na shubiri ya Busanda ni mkuu wa kitengo cha propaganda wa CCM, Tambwe Hizza, pia katibu wa CCM mkoani Kigoma, Salum Msabaha pamoja na mgombea wa chama hicho, Lolensia Bukwimba.
Mkutano huo ulianza kukumbwa na 'kasheshe' hiyo mapema baada ya CCM kugawa mashati na fulana, lakini baadhi ya watu waliokuwa wakigawiwa waliamua kuzichana na kujikuta wakikamatwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Watu hao walipelekwa kituo cha polisi, lakini baadaye waliachiwa. Hata hivyo kitendo hicho kilionekana kuwapandisha hasira wananchi hao ambao waliamua kuzomea viongozi hao katika mkutano huo.
Kutokana na kitendo hicho cha kuzomea, watu 11 walikamatwa na polisi, akiwemo kiongozi wa Chadema ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Tanga, Mwita Waitara. Wote walipandishwa ndani ya gari la polisi namba PT 1498 na kupelekwa kituo cha polisi cha Katoro. Hali hiyo ilisababisha wananchi wa mji wa Katoro kuandamana hadi kituo cha polisi na kutawanywa na FFU.
Mkuchika, ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM, alikumbana na adha hiyo ya kuzomewa na umati mkubwa baada ya kutamba kuwa vyama vya upinzani vinadai kuwa CCM haipendwi hapo Katoro na jimbo zima la Busanda na kwamba, ni uongo kutokana na watu waliojitokeza katika mkutano huo kuwa wengi.
Kauli yake ilisababisha kelele nyingi za kuzomea huku watu wakionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema. Mkuchika alitulia kidogo na baadaye kutoa kejeli kuwa hao wanaozomea ni mamluki wa vyama vya upinzani.
''Waache wazomee kwani hao ni watu walioletwa na wapinzani. Tuwasameheni kwa kuwa hawajui watendalo. Sisi tuna hakika mgombea wetu atashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu na vile vile ukimwona mtu anazomea jua kakata tamaa,'' alisema Waziri Mkuchika huku akizidi kuzomewa.
Wakati Waziri Mkuchika akimnadi mgombea wa CCM, Lolensia Bukwimba kuwa ndiye atayekuwa mshindi wa kiti cha ubunge cha Jimbo la Busanda, baadhi ya watu walioonekana kuwa ni wafuasi wa Chadema walipiga kelele wakimtaja mgombea wao Magesa kuwa ndiye mshindi kwa kuimba "Magesa, Magesa. Magesa".
Naye Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini, alijikuta akitumia muda wake mwingi kwa nyimbo za Profesa J katika kumnadi mgombea wa CCM, akitaja wimbo wa "Ndio Mzee" kwa kusema kuwa CCM haiwezi kuahidi ahadi ambazo hazitekelezeki.
Naye Tambwe Hizza alisema kuwa wapinzani wanayatumia magazeti kukishambulia chama hicho na kwamba, wapinzani ni wahuni wanaposema kuwa CCM haijafanya kitu chochote cha maendeleo, lakini akajikuta akizomewa kila mara.
Anne Kilango, ambaye amepata sifa kutokana na ujasiri wake katika vita dhidi ya ufisadi, alijikuta akikumbana na adha hiyo wakati akimnadi mgombea wa CCM.
Kilango aliwataka wananchi kumchagua Bukwimba ili aweze kushirikiana naye naye, lakini akajikuta akizomewa sawa na wenzake.
Kilango alisema wanawake wana nafasi kubwa ya kuongoza vizuri iwapo watapewa nafasi hiyo kwa kuwa hata familia zinaongozwa na kina mama, hivyo anayemdharau mwanamke ana mdharau mama yake mzazi.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Geita, Shabani Kimea alithibitisha kukamatwa kwa wafuasi wa Chadema kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mkutano wa CCM.
Alisema watu waliokamatwa ni 11 na kwamba imebainikwa kuwa yumo Waitara, ambaye ni kiongozi wa Chadema.
Alisema watu hao wanashikiliwa kwa kufanya fujo katika mkutano huo wa CCM na kwamba, baada ya kuhojiwa na kuchukuliwa maelezo kesho watafikishwa mahakamani.