Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Jamani ikibidi tuwatie moyo kwa jinsi yoyote wawapeleke RA na mzee wa VIJISENTI ili idadi ya wabunge wa upinzani iongezeke bungeni.
wameshampeleka mmoja mkuu
na inasemekana alikwenda amepanda fisi na amerudi amekwea njiwa.
hakwenda kutawala jukwaa bali kutandika kapeti chini ya jukwaa
 
Busanda ni CCM hata bila ya RA. Hii ni kutokana na kugawana kura kati ya Chadema na CUF. Kwa wapenda demokrasia ya kweli, watapenda kuona Busanda inatwaliwa na upinzani ili kupanua wigo wa demokrasia ndani ya Bunge kwa kuongeza uwiano wa upinzani Bungeni haswa ukizingatia wingi wa CCM Bungeni.

Wala hiyo si lazima mkuu, Hata Tarime walizigawana! na bado CCM wanaweza kuwa wapinzani Busanda. tusiandikie mate, ni siku 5 tu zimebaki mkuu
 
oH! so bw. Roast Arm naye kashatia maguu huku na mm! kazi ipo wasije watu wa Bu sanda wakaacha yalobora wakafata yaloletwa na mtaaalamu wa maisha bora kwa kila mbishi katika kupiga kura, enh! si watamwaga mahelaa! na najua wengi wetu kule hatuna dili basi ni kuzikamata tu! liakini chonde wana Busanda chagueni Kiongozi bora na si Kiongozi Helaa! Roast Arm huyooo amewaletea!
 
Wala hiyo si lazima mkuu, Hata Tarime walizigawana! na bado CCM wanaweza kuwa wapinzani Busanda. tusiandikie mate, ni siku 5 tu zimebaki mkuu

Aisee Rwabu kule Tarime CUF hawakuweka mgombea ubunge, walisema wanamuunga mkono yule wa Chadema. Waliweka kwenye udiwani wa kata tu. watu waamke, kama vp wale pesa hizo za kifisadi ila wapigie wanayemtaka wao, si sababu ya pesa.

A strong opposition will make the Government accountable. Help make it happen.
 
Zikiwa zimebaki siku sita tu wananchi wa jimbo la Busanda kupiga kura kumchagua mbunge wao, huku CCM ikiwa imekabwa kisawasawa na upinzani kutokana na tuhuma za ufisadi. Zipo tetesi kuwa CCM inapanga kuwatuma makda wake mahiri Mhe Rosatam Aziz na Mhe Andrew Chenge kwenda kufanya ka,peni kuokoa jahazi la chama hicho.

Kwa mujibu wa watu walio karibu na viongozi waandamizi wa CCM, baada ya mafanikio makubwa aliypoyapata Mhe Anne Kilango katika kampeni hizo kwa wananchi kumheshimu kwa kutomzomea hata kidogo. Viongozi mbali mbali wanataka makada hao ambao kwa kiwango kikubwa ndio wanaongozaakuipaka matope CCM wajitolee kwenda Busanda ili kukutana na joto la wananchi na sio kujificha kwenye luninga na redio.

Sababu ingine inayofanya viongozi wa CCM kutaka RA na AC wapelekwe Busanda ni kutokana na wao kuwa vinara wakusambaza siasa za chuki kikanda kuwa sasa hivi ni zamu ya kanda ya ziwa. Ikiwa Mama Kilango kutoka kanda ya kaskazini kulimudu joto la Busanda iweje makada mahiri kama RA na Ac wapige chenga kwenda kufanya kampeni kwenye kanda yao.

Wana JF mnasemaje? Je tunawaunga mkono wanaotaka RA na AC waende Busanda? au hatuungi mkono

Waende tu ila si kwa staili ya RA ya kwenda sehemu na kutoa mishiko ya nguvu kimya kimya. Natamani Rostam asimame jukwaani ahutubie na kumuombea kura mgombea wa CCM. Wawapeleke pia Jeetu Patel, Somaiya, Karamagi, Lowassa, Manji etc...
 
RA aliingia kimya kimya Busanda na kumwanga fedha kufanikisha ushindi wa Bibie ambaye wengi wanasema ilipata ushindi wa kura za maoni kwa kupitia mngongo wa Katibu mkuu na kuwashinda Bwana Donald Max na yule kibaraka wa Dialo huku wengi wakitegemea Max ashinde akambulia nafasi ya pili.
RA ikabidi atumwe kwenda kumkatia Max ambaye tayari alishaweka makundi hivyo kuhatarisha ushindi wa CCM kama kipande hiki kinavyothibitisha

"Kutokana na makubaliano hayo CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye."

Hata hivyo RA alikuwa analalamika kuwa kuna baadhi ya viongozi wamemtenga sijajua kwanini (papa)?

news baadhi ndio hizo

Hivi RA ndio Mbunge pekee wa kanda ya magharibi na Mjumbe wa halmashauri kuu au ndio unataka kumuingiza mkenge??? Hebu tuweke wazi mkuu.

Hicho kipande ni ulichokikata ktk mwananchi; full news yake ni hii hapa chini : -

JK Aipa Pumzi CCM Busanda Amrejesha Aliyesababisha Mpasuko

* Helkopta ya Chadema kutua wiki hii
Frederick Katulanda, Busanda

ZIKIWA zimebakia siku saba kufanyika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelamba dume baada ya kufanikiwa kumshawishi kada wake aliyeshindwa kura za maoni, Donard Max ambaye atapanda jukwaani kuanzia leo, ili kusaidia kuokoa jahazi.

Kukubali kupanda jukwaani kwa Max ambaye anaanzia kampeni zake katika Kata ya Nyarugusu, kunaelezwa kunatokana na agizo la Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ambaye baada ya kuambiwa kuwa Max amegoma kusaidia kampeni, alimpigia simu na kumuomba kubadili msimamo wake kwa faida ya chama.

“Ni kweli Max leo ataanza rasmi kumnadi mgombea, lakini jambo hili ni siri kubwa, amepangiwa kata zenye hali mbaya ambako akiwa na timu yake atalazimika kupenya huko na kufanya vikao vya faragha na kambi zake,” kilieleza chanzo chetu na kudokeza kuwa amekubali baada ya juhudi za mwenyekiti wa chama.

Hatua hiyo inaelezwa na wachambuzi wa hali ya kisiasa jimboni humo kuwa ni muhimu kwa chama hicho ili kiweze kujinasua, kwa vile mgawanyiko unaokikabili kwa kiwango kikubwa ulisababishwa na kumeguka kwa kambi ya Max aliyeibuka mshindi wa pili katika kura hizo, nyuma ya mgombea Lolensia Bukwimba.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Propaganda, Tambwe Hiza zimeeleza kuwa baada ya kubaini kuwa chama kipo katika hali mbaya, CCM ililazimika kumuita Max ili aweze kurejesha uhai wa chama hicho, kilichokuwa kinakabiliwa na misukosuko ya viongozi wake kuzomewa na watu wachache kujitokeza kwenye kampeni zake.

Awali, ilielezwa kuwa Max amegoma kurudi Busanda na kutoa sharti la kuondolewa kwa hasimu wake, Anthony Diallo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, jambo ambalo lilifanyika. Pia Max alifanya mazungumzo na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Samwel Malecela na makada wengine bila mafanikio.

Diallo anadaiwa kumsaidia Sostenes Kulwa aliyeshika nafasi ya tatu kwa nia ya kumuengua Max, jambo ambalo liligawa kura zake na kuambulia nafasi ya pili.

Taarifa nyingine za ndani zilisema kukubali kwa Max kupanda jukwaani, kunatokana na makubaliano ya faragha baina yake na Malecela kwa niaba ya Kikwete ambaye aliagiza arejeshewe gharama zake za kampeni katika mchakato wa kura za maoni.

Kutokana na makubaliano hayo CCM kiliagizwa kusaka fedha za kumrudishia Max ambazo zililetwa na mbunge mmoja wa Kanda ya Magharibi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, ambaye imeelezwa aliingia Geita kimya kimya na kufanya mazungumzo naye.

Hata hivyo, Max alipozungumza na Mwananchi Jumapili jana, alisema ameamua kusaidia kampeni kama mwanachama na siyo kwa kuombwa na vigogo wa chama hicho.

Kauli inayofafana na hiyo pia ilitolewa na Hiza ambaye alisema kwamba, Max ni sawa na wanachama wengine wa CCM wa wilaya ya Geita ambao wamekuwa na jukumu moja la kumnadi mgombea wa chama hicho.

“Huyu ni mwanachama sawa na wengine, hatusemi anapanda jukwaani kwa sababu zenu ninyi waandishi, anapanda sawa na viongozi wengine wote wa chama wilayani, hakufanya hivyo tangu awali kwa sababu hakuwapo Geita, sasa amekuja, atapanda jukwaani,” alisema Hiza.

Kutokana na makubaliano hayo baina ya CCM na Max chanzo chetu kimedokeza kuwa tofauti kati ya kambi yake na Diallo imemalizika na hivyo mjumbe huyo wa NEC, kurejea Geita ambako tangu juzi ameonekana mitaani akiendelea kusaidia kampeni.

Kwa upande mwingine, CCM imepunguza idadi kubwa ya mikutano yake ya kampeni ya kumnadi mgombea wake katika miji na badala yake imeimarisha mikutano ya vijijini ambapo kwa siku imekuwa ikifanya mikutano mitatu hadi minne kila kata.

Hatua hii imekuja baada ya kukumbana na hali ngumu katika mikutano ya majukwaani ambayo imekuwa ikiishia kuzomewa kwa viongozi wake, hatua ambayo imeelezwa kuwa imekiathiri chama hicho kutokana na watu wengi kubadilika na kuisapoti kambi ya wapinzani wao na hasa Chadema.

Katika mikutano hiyo ya nje ya mji, viongozi na wabunge wa CCM wamekuwa wakizunguka kila kijiji kuzungumza na wananchi mbalimbali kwa makundi maalumu ambayo ni makundi ya wazee, vijana na viongozi wa dini.

“Hali yetu ni ngumu lakini siyo kama mnavyodhani, mkakati wetu wa vijijini ni mzito sana kutokana na kuonyesha mafanikio,” alieleza mmoja wa viongozi wa wilaya wa CCM ambaye amepangiwa kata ya Nyarugusu.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakizungumza na wazee kwa kuwaomba radhi kutokana na kushindwa kutimiza ahadi walizoahidiwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005 na kuwasii watoe nafasi kwa CCM kwa vile Rais Kikwete ameahidi kuyapa msukumo matatizo ya Busanda mara baada ya uchaguzi.

Wakati hayo yakitendeka, Chadema wameanzisha mkakati maalumu kwa ajili ya kusimamia na kulinda kura katika vituo ili kudhibiti upotevu wa kura zao.

Habari za ndani ya Chadema ambazo zimethibitishwa na Afisa Mwandamizi na Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Mwikwabe Waitara, zimesema kuwa kamati maalumu imeundwa kwa ajili ya kuratibu mbinu za usimamizi wa kura katika vituo jimboni Busanda ili kuhakikisha mgombea wao, Finias Magesa anaibuka mshindi.

Katika kufanikisha mkakati huo, kamati hiyo imetoa namba za viongozi ili wananchi waweze kutoa taarifa wakati wowote pale wanapoona masanduku yakiwa nje ya vituo au katika hali isiyo kawaida.

Akizungumza juzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, Waitara alisema wanatambua mikakati ya CCM, kwani baada ya kuzidiwa katika jukwaa wametulia wakielekeza mbinu zao katika wizi wa kura, jambo ambalo alisema watalisimamia kikamilifu kuhakikisha hawapati mwanya wa kufanikisha azma yao hiyo.

Sambamba na mkakati huo Chadema wamepanga kufanya kampeni za mwisho kwa kishindo huku wakitumia helkopta atakayozunguka nayo mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe ili kufikia vituo vingi kwa kipindi kifupi.

Vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo vimeendelea na mikakati yake ya kutumia majukwaa. CUF wameongeza nguvu kwa kumuita Mwenyekiti wake, Profose Ibrahimu Lipumba ambaye ataingia leo kumnadi mgombea wao, Oscar Ndalawah.

Kampeni za UDP zimeendelea kudorora kutokana na kutumia mbinu ya kutoa matangazo kwa njia ya vipaza sauti vilivyowekwa katika gari ambalo limekuwa likipita mara kadhaa katika mitaa kuwahimiza wananchi kumchagua mgombea wake, Beatrice Lubambe.

Katika hatua nyingine, Salma Said anaripoti kutoka Zanzibar kuwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM), Hamad Yussuf Masauni amewakemea wapinzani wanaowatisha na kuwazomea viongozi wa chama hicho katika kampeni zinazoendelea katika uchaguzi mdogo wa Busanda.

Akihutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Magogoni Visiwani Zanzibar, Masauni alisema Chadema kinaendesha kampeni chafu huko Busanda jambo ambalo ni kinyume na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi.

“Tumevumilia vya kutosha, sasa imetosha na sasa tunataka kuona mambo haya yanakomeshwa haraka…,” alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Masauni aliyasema hayo wakati Chadema wakimlalamikia mkuu wa polisi wilaya ya Geita kwa kupokea amri kutoka kwa CCM kuwakamata wanachama wake bila sababu na wengine kufikishwa mahakamani, huku akiwaachia huru makada wa CCM waliokamatwa wakinunua shahada za kupigia kura.
 
Ukweli ni kwamba huu uchaguzi kwenye sanduku CCM waliisha shindwa zamani, Kinachofanyika sasa ni kuhalalisha wizi utaofanyika siku ya uchaguzi. Watasema kuwa tulipeleka watu wazito, timu yetu ilikuwa na nguvu ndiyo maana tukashinda. steps wanazochukua sasa

1. wameongeza askari polisi 30 wapya na kufikia 110 ukiacha wale wa wilayani.

2. kupeleka vigogo ambao kwa wananchi si lolote si chochote zaidi ya kuwa kundi la waporaji na wanyonyaji waliowarubuni kwa kipindi kirefu sana kuhusu maendeleo.

3. CCM kwao amani ni second priority baada ya kushinda kwa kuiba kura kwanza, yaani nguvu zote hizi zinazotumika ni lazima CCM washinde kwa vyovyote ( waibe kura na kumwaga polisi kutuliza ghasia baada ya wiki mbili tatu wananchi watasahau kwani hali ngumu ya maisha itawafanya waachane na kufuatilia uchaguzi watafute riziki zao za kila siku)

4. Kwa kutumia polisi wananchi wataamrishwa watawanyike baada ya kupiga kura ili wizi ufanyike vizuri.

5. Vijijini ambako si dhani kama CHADEMA wanaweza fika baada ya kunyang'anywa pikipiki zao na polisi wa CCM ndiko utakapotokea ushindi, kwa kila kura moja ya mwanakijiji kuhesabiwa kama kura 1,000. na siku hiyo kama mvua haikunyesha basi magari ya tume ya uchaguzi yataharibika ama kuishiwa mafuta njiani katikati ya pori yakisafirisha masanduku kuja makao makuu ya wilaya kwa ajili ya kujumlisha, ambapo itachukua siku tatu mpaka nne watasema wanasubiri mafuta yanatoka Mwanza ili kuwachosha walinda kura wa CHADEMA na kuwapiga bao la tsunami.

6. Kwa kuwa wamebanwa sana watafanya ushindi wao uwe finyu kama 0.1% yaani CHADEMA 49.9% CCM 50.1%, wengi wape mchezo utakuwa umekwisha.
 
Last edited:
Kama RA kaenda Busanda, basi ni kujaribu kuiangusha CCM -- kwa kuipa misaada CUF. Kumbukeni: Kuna hii ya Rostam-Jussa connection. Inasemekana RA amekuwa anaisadidia sana CUF huko nyuma -- na ndio maana katika suala la ufisadi -- Profesa IL sasa anakuwa na kigugumizi cha kushangaza.

Habari zinasema kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti ya RA -- Muhingo Rweyemamu (aliyefukuzwa Mwananchi 2005 kwa kampeni chafu ya kughushi picha ya Dr Salim) amepelekwa Busanda -- pamoja na Manyerere Jackton, yule aliyemtukana Mengi kwenye makala ktk Mtanzania Jumapili iliyomfanya Mengi kumshitaki na kudai Sh 3bn/-.

Kama kugawa fedha, basi Muhingo ndiyo anaaminika zaidi na RA tangu wakati wa kampeni ya JK ya 2005 ndiye alikuwa mshika fedha -- hasa kwa kuwagawia waandishi wa habari.

Hali kadhalika kuna habari kwamba RA alimfuata JK kule Afrika ya Kusini wakati wa kuapishwa kwa Zuma. RA alichukua chumba katika hoteli hiyo hiyo na floo hiyo hiyo -- madhumuni yakiwa akutane naye kwa mazungumzo, angalau kwa dakika chache -- ripoti za uhakika zinasema.

RA aliwatumia akina January, Makalla na Mkuu wa usalama -- Othman kufanikisha mkutano huo lakini haikuwezekana -- JK alikataa kata kata kukutana naye na inasemekana alikasirika kusikia kwamba siyo tu RA alimfuata tu kule Bondeni, bali pia alikuwa na jeuri ya kupanga katika hoteli hiyo hiyo.

Haijajulikana RA alitaka kumwambia nini JK. Mwenye habari zaidi kuhusu hili azitoe humu JF.
 
..........................

.
Duh Mzee Punch hii kali!
Sasa tunaona mwanga ? au bado hakujapambazuka ?
 
Hali kadhalika kuna habari kwamba RA alimfuata JK kule Afrika ya Kusini wakati wa kuapishwa kwa Zuma. RA alichukua chumba katika hoteli hiyo hiyo na floo hiyo hiyo -- madhumuni yakiwa akutane naye kwa mazungumzo, angalau kwa dakika chache -- ripoti za uhakika zinasema.

RA aliwatumia akina January, Makalla na Mkuu wa usalama -- Othman kufanikisha mkutano huo lakini haikuwezekana -- JK alikataa kata kata kukutana naye na inasemekana alikasirika kusikia kwamba siyo tu RA alimfuata tu kule Bondeni, bali pia alikuwa na jeuri ya kupanga katika hoteli hiyo hiyo.

Haijajulikana RA alitaka kumwambia nini JK. Mwenye habari zaidi kuhusu hili azitoe humu JF.

Huu ni upotoshaji. Umedhihirisha kwamba huu ni uongo na udaku pale ulipomalizia kwa kusema 'mwenye habari zaidi azitoe'.

Rostam Aziz ambae mnasema ana connections na minguvu kama ya mizimu, amemweka mfukoni kila mtu, hawezi kuhitaji kwenda South Africa ili tu kupata audience na Kikwete. Kama nia ni kujificha, basi hata huko South Africa kuna wana CCM walikuwa kwenye msafara wa Rais, kwa nini Rostam asihofie kwamba hawa wataleta habari nyumbani kwa mahasimu wake? Hata kama ni mahotelini, Pretoria sio Las Vegas.

Habari za 'inasemekana' kaa nazo hadi hapo utakapopata ushahidi.

UDAKU!
 
So what if RA and Chenge joins the campaign? Actually for me they should join so as to understand the urban and rural politics divides!

I think we need to move beyond individual politics and focus on political context of tanzania. To me, RA and CHenge are reflection of their party and qualify for their position both with citizens and ccm eyes. If they are corrupt as they are claimed to be they should have not been member's of parliament up now. Until then both of them have all the rights to take part in ccm political campaigns.

If we don't like that we should do something about it, otherwise we better learn to swallow up!
 
Malecela: Busanda CCM maji shingoni

• Awaangukia wafanyabiashara kuiokoa

na Kulwa Karedia, Busanda

Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

MAKAMU Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, maarufu Tingatinga, amekiri kuwa chama hicho kinakabiliwa na upinzani mkali katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda na kwamba sasa maji yako shingoni.

Akizungumza na wafanyabiashara zaidi ya 50 katika soko kuu la mji mdogo wa Katoro, jana, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Busanda, Malecela alisema hali ya mambo si shwari na kuwaomba kuiunga mkono CCM.

“Nimewatembelea hapa kujua matatizo yenu pamoja na kuwaambia kwamba, tunakabiliwa na uchaguzi ndani ya jimbo hili, nawaomba mtumie fursa hii kuchagua CCM ili iweze kumaliza matatizo madogo madogo yaliyopo,” alisema.

Malecela ambaye alifika sokoni hapo majira ya saa 7 mchana akiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser, yenye namba za usajili T 509 AFZ, aliwataka wafanyabiashara kutobabaishwa na sera za vyama vingine.

Kauli ya Malecela ilionekana kuwa mwiba mchungu kwa wafanyabiashara hao ambao waligeuka na kumweleza kuwa umefika wakati wa kufanya mabadiliko.

“Tunasema kama CCM mnasema maji yamefika shingoni, tunasema ni haki yenu kwani sisi tukiingia humo tutazama, sasa kwanini tujitafutie matatizo hivyo,” alisema mmoja wa wafanyabiashara hao, Marando Mayalla.

Alisema kwa kipindi kirefu CCM imetumia mwanya wa kuwadanganya katika masuala mbalimbali ya kijamii, ikiwamo ahadi ya kupelekewa umeme, lakini imeshindwa kutimiza.

“Tumekuwa watu wa kudanganywa kila mwaka sisi… tumeahidiwa umeme hapa miaka mingi, leo tena mnakuja na sera eti ya kuwachagua, tunasema kila jambo lina mwanzo na mwisho wake,” alisema Mayalla kwa niaba ya wenzake.

Alisema hata kitendo cha CCM kumrejesha mmoja wa wanasiasa maarufu wa chama hicho, aliyegoma kupanda jukwaani, Donald Maxi, hakutasaidia kitu kwani mwenyewe amejimaliza kisiasa.

“Sisi tunasema hata huyo Maxi ambaye mmeamua kumrudisha CCM kwa ajili ya kusaidia kampeni, amechemsha kwani huko ni kujimaliza kisiasa... inakuwaje agome kupanda jukwaani mpaka rais aaingilie kati?” alihoji Mayalla.

Kutokana na kauli za wafanyabiashara hao, Malecela aliamua kuondoka eneo hilo, huku akinyonyeshewa vidole kwa alama ya V ambayo hutumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kupeana salamu za chama.

Tangu CCM ilipozindua kampeni zake, imekuwa na wakati mgumu kutokana na viongozi wake kuzomewa karibu mikutano yote inayofanywa hali ambayo imesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anatarajiwa kuwasili leo jimboni hapa na kuanza kutumia helikopta kumnadi mgombea wa chama hicho, Finias Magessa.

Ratiba inaonyesha kuwa, Mbowe anatarajiwa kufanya mikutano saba kwa siku moja ambapo ataanzia katika viijiji vya Rwamgasa, Kaseme, Katoro na Ibondo kwa nyakati tofauti.

Katika hatua nyingine, vijana wa CCM, maarufu kama Green Guard, jana waligeuza Kijiji cha Nyachilulula kuwa uwanja wa vujo baada ya kutembeza kipigo kwa baadhi ya wafuasi wa CHADEMA.

Tukio hilo ambalo limeonekana wazi kubadili sura ya kampeni, lilitokea majira ya saa 5:40 asubuhi kijijini hapo wakati CCM ilipokuwa ikimnadi mgombea wake, Lolencia Bukwimba, ambaye amekuwa na wakati mgumu kutokana na kuzomewa kila anapopanda jukwaani.

Tangu CCM walipofanya mkutano wao katika Kijiji cha Katoro wiki iliyopita, wamekuwa wakitumia vijana wa Green Guard kukamata na kuwapiga vijana wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa vyama vya upinzani, jambo ambalo limezua malalamiko mengi.

Wakati mkutano huo wa Nyachilulula ukiwa unaendelea, vijana watatu ambao wanasaidikiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, walipita karibu na eneo la mkutano, huku wakipeperusha bendera ya chama hicho.

Vijana hao wakiendelea na safari, walishitukia wakifuatwa na gari aina ya Toyota Prado, yenye namba za usajili T 718 na waliokuwamo ndani kushuka ghafla na kuanza kuwapiga.

Waliopigwa ni pamoja na Chacha Magabe na Lucas Tigamanya ambao baada ya kipigo hicho haikujulikana mara moja walipelekwa wapi.

Wakati tukio hilo linaendelea, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, alikuwa jukwaani akimnadi mgombea wa CCM.

Hata hivyo, lawama nyingi zimeelekezwa kwa Jeshi la Polisi kwani hawahudhurii mikutano mingi ya kampeni.

Mmoja wa wanakijiji wa Nyachilulula, Mabula Shijja alisema amesikitishwa na kitendo cha CCM kupiga watu kila wanapofanya mikutano.

“Hii ni tabia mbaya kwani CCM sasa wamekuwa na tabia ya kupiga watu kila wanapofanya mkutano, juzi tumeshuhudia pale Katoro watu walivyopigwa vibaya na kuswekwa ndani,” alisema Shijja.

Alisema umefika wakati hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti hali hiyo ambayo inavunja misingi ya demokrasia.

Akimnadi mgombea wake, Kilango aliwataka wakazi wa Kijiji cha Nyachilulula, kutumia fursa ya kuchagua kiongozi bila ya shinikizo lolote la kisiasa.

“Tumieni fursa yenu kuhakikisha kwamba mnachagua kiongozi ambaye mnamtaka, msibabaishwe na vita ya mafisadi inayoendelea ndani ya chama chetu.

“Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya chama changu kuna baadhi ya wananchama na viongozi wanaojihusisha na ufisadi, lakini si wote,” alisema Kilango.

Katika hatua nyingine, askari polisi zaidi ya 45 ambao wamepelekwa jimboni Busanda kwa ajili ya shughuli za ulinzi, wamelalamikia posho ya sh 1,000 ambayo wanalipwa kwa siku.

Wakizungunza jana mjini hapa, na kuomba majina yao yasitajwe gazetini, askari hao walisema kiasi hicho ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

“Hata wewe fikiria kwamba tumeacha familia zetu, ndugu yangu tunalipwa sh 1,000 kwa siku, unadhani inaingia akilini? Basi ndiyo hivyo tena, hatuwezi kulalamika kwa wakubwa,” alisema mmoja wa askari hao.
 
Huu ni upotoshaji. Umedhihirisha kwamba huu ni uongo na udaku pale ulipomalizia kwa kusema 'mwenye habari zaidi azitoe'.

Rostam Aziz ambae mnasema ana connections na minguvu kama ya mizimu, amemweka mfukoni kila mtu, hawezi kuhitaji kwenda South Africa ili tu kupata audience na Kikwete. Kama nia ni kujificha, basi hata huko South Africa kuna wana CCM walikuwa kwenye msafara wa Rais, kwa nini Rostam asihofie kwamba hawa wataleta habari nyumbani kwa mahasimu wake? Hata kama ni mahotelini, Pretoria sio Las Vegas.

Habari za 'inasemekana' kaa nazo hadi hapo utakapopata ushahidi.

UDAKU!

Chenge na Rostamu ndio vinara wa ufisadi wote tunajua, wakijipeleka Busanda itakuwa vyema, ili ile mahakama yetu ya wezi wa kuku, iwafikie na wao huko huko majukwaani!
 
"Tunasema kama CCM mnasema maji yamefika shingoni, tunasema ni haki yenu kwani sisi tukiingia humo tutazama, sasa kwanini tujitafutie matatizo hivyo," alisema mmoja wa wafanyabiashara hao, Marando Mayalla.

"Tumekuwa watu wa kudanganywa kila mwaka sisi… tumeahidiwa umeme hapa miaka mingi, leo tena mnakuja na sera eti ya kuwachagua, tunasema kila jambo lina mwanzo na mwisho wake," alisema Mayalla kwa niaba ya wenzake.

"Sisi tunasema hata huyo Maxi ambaye mmeamua kumrudisha CCM kwa ajili ya kusaidia kampeni, amechemsha kwani huko ni kujimaliza kisiasa... inakuwaje agome kupanda jukwaani mpaka rais aaingilie kati?" alihoji Mayalla.

Kutokana na kauli za wafanyabiashara hao, Malecela aliamua kuondoka eneo hilo, huku akinyonyeshewa vidole kwa alama ya V ambayo hutumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kupeana salamu za chama.

Heko wananchi wa Busanda, huku ndiko kumkoma nyani kisawasawa - ila angalieni tabia ya mafisadi, wanaiba kila kitu kuanzia fedha hadi kura. Siku ya uchaguzi lindeni kura zenu na msiruhusu wawaibie kwani kwa hilo wamebobea - wanajisifu kuwa nambari wani.
Kula kwa CCM, kura kwa Chadema.
​
 
Zote hizi ni tetesi tu - hakuna ukweli ndani yake. Nakuambia ccm siyo wajinga wapeleke mafisadi wanaopigiwa kelele na kila mtu kwenye uwanja wa vita. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamejimaliza, na wao hilo wanalijua. Si unajua hakuna mafia kama ccm.
 
Kama RA kaenda Busanda, basi ni kujaribu kuiangusha CCM -- kwa kuipa misaada CUF. Kumbukeni: Kuna hii ya Rostam-Jussa connection. Inasemekana RA amekuwa anaisadidia sana CUF huko nyuma -- na ndio maana katika suala la ufisadi -- Profesa IL sasa anakuwa na kigugumizi cha kushangaza.

Habari zinasema kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti ya RA -- Muhingo Rweyemamu (aliyefukuzwa Mwananchi 2005 kwa kampeni chafu ya kughushi picha ya Dr Salim) amepelekwa Busanda -- pamoja na Manyerere Jackton, yule aliyemtukana Mengi kwenye makala ktk Mtanzania Jumapili iliyomfanya Mengi kumshitaki na kudai Sh 3bn/-.

Kama kugawa fedha, basi Muhingo ndiyo anaaminika zaidi na RA tangu wakati wa kampeni ya JK ya 2005 ndiye alikuwa mshika fedha -- hasa kwa kuwagawia waandishi wa habari.

Hali kadhalika kuna habari kwamba RA alimfuata JK kule Afrika ya Kusini wakati wa kuapishwa kwa Zuma. RA alichukua chumba katika hoteli hiyo hiyo na floo hiyo hiyo -- madhumuni yakiwa akutane naye kwa mazungumzo, angalau kwa dakika chache -- ripoti za uhakika zinasema.

RA aliwatumia akina January, Makalla na Mkuu wa usalama -- Othman kufanikisha mkutano huo lakini haikuwezekana -- JK alikataa kata kata kukutana naye na inasemekana alikasirika kusikia kwamba siyo tu RA alimfuata tu kule Bondeni, bali pia alikuwa na jeuri ya kupanga katika hoteli hiyo hiyo.

Haijajulikana RA alitaka kumwambia nini JK. Mwenye habari zaidi kuhusu hili azitoe humu JF.
Mzee ngumimrudisho habari zako nyingi huwa na ukweli kwa asilimia nyingi unaweza kujulisha jamvi nini hasa sababu za Jk kukataa kuonana na RA? Je uswahiba wao ndio unaishia? au wanatunga habari hizi ili tuone rais wetu anaanza kuwachukia mafisadi?
 
"Mzee ngumimrudisho habari zako nyingi huwa na ukweli kwa asilimia nyingi unaweza kujulisha jamvi nini hasa sababu za Jk kukataa kuonana na RA? Je uswahiba wao ndio unaishia? au wanatunga habari hizi ili tuone rais wetu anaanza kuwachukia mafisadi?"
__________________

MawazoMatatu:

Hizi habari ni za ukweli -- RA aliumbuka huko Bondeni. Vidokezo vyangu vinasema huenda alitaka kumwambia JK "Vipi swahiba, nasikia kuna mipango ya kunipandisha kizimbani?"

Tusisahau kwamba hivi karibuni akina Hosea wametamka kuwa kuna kesi 5 za ufisadi dhidi ya vigogo, zile "za kutikisa ardhi" zinazotarajiwa kutinga mahakamani mwezi ujao. Mojawapo bila shaka ni ya RA -- Kagoda.

halafu pia tusisahau Budget ni mwezi ujao tu na habari zinasema kuwa pamoja na wafadhili wetu kuahidi mabilioni katika Budget, lakini wameshikilia kuwa hawatatoa hata senti moja hadi hatua za maana zinachukuliwa dhidi ya ufisadi, kwa kuzifikisha mahakamani kesi nyingine zilizobaki -- hususan Kagoda. Kwa hiyo serikali inahaha sasa.

Pengine RA alitaka kumwambia RA kwamba "ukimwaga ugali nami nitamwaga mboga" iwapo anayo jeuri hiyo -- ili kumtisha asimweke kizimbani.
 
lakini juzi tulikuwa na marafiki zetu wa Iran na saudi arabia, kwani nao wamegoma kutupa hela?
 
Nimesoma kuwa zawadi zinagawiwa na kwa wananchi wa Jimbo la Busanda; labda ndiyo uwepo wa RA in kind.
 
Back
Top Bottom