========
Habari nilizo nazo ni kuwa CCM wanawalaumu akina Rostam kwa kukwamisha kampeni zao huko Busanda. Magazeti yao (Mtanzania na Rai) yamekaririwa wiki hii yakichambua udhaifu wa CCM badala ya kuwatia moyo. Rai limeenda mbali na kusema timu ya CCM huko Busanda haina mbinu za kisasa.
Ukweli huu unadhihirishwa na kuondoka kwa Makamba huko ambaye akina Rostam wanamtetea kuwa anaonewa na kuchongewa kwa Mwenyekiti. Kitendo cha Kampeni za Busanda kuongozwa na Mkuchika (Hasimu namba moja wa Lowassa) hakiwezi kuruhusu Rostam aende Busanda. Kimsingi, akina Rostam wanasubiri jimbo liende ili wapate cha kusema ndani ya KAMATI KUU. Mzee Malecela anapigana kufa na kupona, si kuwashinda Chadema, bali kuwaonyesha akina Rostam kuwa bila anaowaita "mafisadi", ushindi unawezekana. Nao wanaoitwa "Mafisadi" wanataka kusema, bila wao, CCM inayumba.
Muungwana kaenda USA na kuwaacha wamalizane wenyewe.