Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Hiyo ndo potilikis sasa jamani si lazima watu watumie kila mbinu ili kushinda?sioni ubaya wa kutumia kisukuma jimboni kwa wasukuma.

Ukiruhusu kutumia kila mbinu maana yake unakubali hata mbinu chafu za kununua shahada, kuhonga, kutisha nk vitumike ili mradi ushindi upatikane. Unatakiwa kuheshimu sheria, hivyo mbinu zilizoruhusiwa kisheria au zisizokatazwa kisheria ndio tu zitumike.
Kama unakubaliana na maelezo hayo, basi ujue kuwa sheria imekataza kutumika lugha hizo za kikabila. Dada tusikubali kuvunja sheria ili kupata ushindi, tukizoea hivyo, mwingine atatumia silaha ili kupata ushindi na hatutakuwa na uwezo wa kumpinga maana tumeanza kuruhusu uvunjaji wa sheria - Busanda si wote ni wasukuma; enzi hizo zimepita!!
 
Kwa watu wenye akili na waliopevuka kama CCM, sikutegemea kusikia upuuzi huo kwani tumarudihwa tulikotoka, Nyerere hakuwa mpuuzi alipopiga vita ukabila. Unataka kusema kuwa Busanda ni ya Wasukuma pekee na kila mpiga kura wake ni Msukuma?

Nadhani jukumu zito la CCM ni kuhakikisha kuwa wanaendelea kutawala kwa gharama yoyote! Hiyo ni hatari maana yaweza kuturudiha Tarime. Kwa uzoefu nilionao, kuhesabu kura za Busanda ni kitu rahisi ikiwa CCM watashinda lakini ikiwa kuna dalili za kushindwa itachukua siku kadhaa kutangaza matokeo hadi wananchi waandamane kushinikiza yatangazwe kama Tarime. Lakini kama CCM watashinda, matokeo ni baada ya siku moja (kesho yake tu) yatatngazwa.


- Mkulu Ibrah, wewe ni mtu makini sana sasa mbona unakuwa one sided, una maana kwamba Chadema huko Busanda wanashinda kanisani tu kusali? Au ndio njia za kutokea hizi iwapo mambo yatakuwa mabaya?

- Kuweni balanced basi japo kidogo tu, mtuwekee na upande wa pili, au?

FMES!
 
"Shahada zote ambazo wananchi wanazo kwa mujibu wa sheria ni mali ya NEC, sasa inakuwaje chama fulani kipite na kuandikisha upya majina na namba zake...hii ni kazi ya tume tu kwani hata mwongozo ndivyo unavyoonyesha," alisema Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo la Busanda, Dani Mollel kuhusu dai la kunaswa kwa makada wawili wa CCM wakifanya kazi ya kuandikisha shahada za wapiga kura.

"Jimbo ni mali ya CCM na tutalitetea kama Yanga walivyotetea ubingwa wao kwa kutwaa kombe kabla ya ligi kumalizika. Wanachama wakae mkao wa kugombea kiti cha jimbo hilo," alisema katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba.

"Huyo ni mganga wa kienyeji," alisema Dk. Slaa alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Makamba kuwa tayari jimbo hilo ni mali ya CCM

"Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….na kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo," alisema Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Samwel Malecela.

"Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya chama changu kuna baadhi ya wananchama na viongozi wanaojihusisha na ufisadi, lakini si wote," alisema Mama Kilango Malecela, mbunge wa CCM jimbo la Same Mashariki.

"Asiwadanganye mtu kwamba ndani ya CCM kuna kiongozi mwenye ujasiri wa kupambana na ufisadi. Maana wameanza kujitokeza baadhi ya wabunge wa CCM eti wakijifanya na wao wana uchungu na nchi hii. Eti na wao wanapambana na ufisadi. Waulizeni walikuwa wapi miaka yote hii nchi ikiuzwa?"
aliuliza Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

"Jamani kushindwa ni kubaya, mwenzenu Tarime nilionja ubaya wake mpaka ilibidi nitoroshwe na Green Guard ili kuepuka kuzomewa, sasa tusiposhikamana mambo yatakuwa magumu tutoe tofauti zetu," alisema Katibu Mkuu wa CCM, Ysufu Makamba.

"Baadhi ya mafisadi waliopo ndani ya chama chetu ndio wanaoeneza propaganda kwenye vyombo vya habari ili CCM ishindwe," amelalamika Makamu Mwenyekiti msataafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bw. John Malecela kuwa chama chake kinahujumiwa na mafisadi kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge na makada wake.

"Watakuja, kina Dk. Mwakyembe kuwaambia wao wanapambana na mafisadi, lakini hao ni wanafiki, na wao ni mafisadi tu, kwani huwezi kusema unapambana na ufisadi halafu ukiwa ndani ya CCM," alisema Zitto.

"CCM kwa kumteua Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Tanzania Bara, John Malecela, anayefahamika zaidi kwa jina la Tingatinga kuwa, ni kumdhalilisha kwa sababu kwa umri wake na wadhifa wake hapaswi kufanya kazi ya kugawa chumvi na magodoro kwa wapiga kura ambao wamekwishaonyesha nia ya kutokichagua chama anachokitetea," alidai Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

"Wale waliotoroka makwao na kukimbilia mijini wakidhani kuwa Serikali ya CCM itakuwa ikimwaga fedha barabarani na wao waokote ndio wanaolaumu na kuunga mkono upinzani lakini wale wenye shughuli zao bado ni wana-CCM.," alisema Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM , Bw. Tambwe Hiza.

"Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang'anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali," alisema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akiongea na wachimbaji wadogo wadogo. "Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali," aliongeza Ngeleja.

"Tumeshangazwa na kauli ya Ngeleja na ndiyo maana tuliamua kumkimbia ndani ya ukumbi, kwa sababu inaonekana wazi kwamba sasa anataka kutufanya Watanzania ni wajinga wa kutupwa, kwanini kaja wakati wa kampeni kututisha hivi?" alihoji mmoja wa wachimbaji hao, Swedi Mussa.

"Tumekuwa watu wa kudanganywa kila mwaka sisi… tumeahidiwa umeme hapa miaka mingi, leo tena mnakuja na sera eti ya kuwachagua, tunasema kila jambo lina mwanzo na mwisho wake," alisema Mayalla kwa niaba ya wafanya biashara wa Katoro.

"Nasikia kuna Chopa linakuja, sisi tunaondoka, lakini mjue kuwa sisi wana CCM tuna uwezo wa kuleta ndege Boeing hata kumi," alisema Salum Msabaha, Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma katika mkutano huo wa kumnadi mgombea wao, Bukwimba.

"Nawaomba mfanye kazi yenu vizuri," alisema Mbunge wa Nyamagana, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, akiwa ndani ya gari lenye namba za Ubalozi wa Afrika Mashariki, huku akiwa amevalia fulana ya rangi ya njano na kijani, akitoa agizo kwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa na silaha mbalimbali, zikiwamo za moto waliojiandaa kwa mapambano, wakiwa wamepiga kambi jirani na viwanja hivyo (kulikotarajiwa kutua helikopta).

"Usinione hivi sina raha, kwanza usiku silali wala sipati usingizi nafikiria Busanda, lakini nitahakikisha kampeni zinafanyika kwa amani kubwa na vurumai zitakoma tu," alisema Kaimu Kamanda wa polisi, Kalinga. ( Licha ya hivyo vijana wa CCM wameendelea kutembeza mkong'oto kwa wananchi bila wasi wasi)
"Haya ni machache tu kati ya yanayofanyika katika kugombea jimbo moja tu la uchaguzi, Busanda - sijui itakuwaje mwakani 2010 kwenye uchaguzi mkuu. Watanzania tuombe Mungu," Mag3.
​
 
Uchaguzi Busanda ni batili Chadema wameu haribu kwa sababu zifuatazo;

1. Mh Zitto Zubeir Kabwe akiwa mbunge Bunge la JMT amechoma batili cha chama cha mapinduzi hadharani.

2. Mh Zitto amekuwa akinukuriwa katika mikutano yake ya hadhara akichochea uvunjifu wa amani na kutoa kashfa akiwa pamoja na kumuita Waziri mkuu mstaafu na makamu wa Rais wa JMT na Mbunge wa Bunge la JMT Mh John Malecela kuwa ni kibajaji nk

3. Chadema wameingiza kutoka Tarime kundi la wafanya fujo ambao wamekuwa wakiendesha matukio ya kuhatarisha amani huko Busanda.

4. Chadema wamekuwa wakihamasisha wahuni kwenda kwenye mikutano ya CCM na kuzomea viongozi wa juu wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwarushia mawe.

5. NK

Naam, hayo ni baadhi ya vituko vyao, Lakini hapa chini kuna kituko kikubwa zaidi, badala ya kujibu hoja mtu anakimbilia kushambulia profile ya mtu! Hii ni dalili tosha ya uchovu wa kufikili na kukiri yaliyosemwa hapo juu ni sahihi!

No wonder your contribution! Hivi uthubutu wa wana CCM kuongea pumba hadharani hivi wanautoa wapi???
Masatu
user_online.gif

Masatu falling asleep
JF Senior Expert Member
Join Date: Mon Jan 2007
Location: uwanja wa fisi
Posts: 2,936
Thanks: 244
Thanked 1,413 Times in 809 Posts
Rep Power: 0
reputation_neg.gif

Credits: 55,777,420
 
Na vipi kuhusu hii hapa

“Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang’anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali,” alisema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akiongea na wachimbaji wadogo wadogo.

“Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali,” aliongeza Ngeleja.
Halafu Tume ya Uchaguzi inakaa kimya.
​
 
Nukuu toka upande wa CCM (wenye DOLA ) zimekaa vizuri, Hao wa upande wa pili zao ni kama wanalia vile!
 
Naam, hayo ni baadhi ya vituko vyao, Lakini hapa chini kuna kituko kikubwa zaidi, badala ya kujibu hoja mtu anakimbilia kushambulia profile ya mtu! Hii ni dalili tosha ya uchovu wa kufikili na kukiri yaliyosemwa hapo juu ni sahihi!

Masatu hapa umechemka.

Hoja zilizotolewa hapa ni kwamba, yanayofanywa na ccm ni kinyume cha sheria za uchaguzi. na ni mambo yaliyoripotiwa. kwa mfano. kitendo cha kununua shahada za kupigia kura, kuweka nguzo za umeme, na kupiga wanachaama wa vyama vingine. Unachoeleza wewe masatu ni blaa blaa zisizokuwa hata na ushahidi. kwa mfano, kuzomea si kosa la jinai na wala si kwenda kinyume cha taratibu na sheria za uchaguzi
 
Nukuu toka upande wa CCM (wenye DOLA ) zimekaa vizuri, Hao wa upande wa pili zao ni kama wanalia vile!

Mkuu Kibunango hebu jaribu kufafanua kidogo - nimeshindwa kabisa kukuelewa una maana gani.
 
Na vipi kuhusu hii hapa

“Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang’anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali,” alisema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akiongea na wachimbaji wadogo wadogo.

“Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali,” aliongeza Ngeleja.
​
Halafu Tume ya Uchaguzi inakaa kimya.​

Hivi kwa kiongozi wa serikali kuwatishia wananchi kiasi hiki, hawezi kushitakiwa kwa mjibu wa sheria? yaani waziri mwenye dhamana unasema tutawanyanganya leseni kama hamtatuchagua?
please wana sheria hii ikoje? Na je siyo kutumia madaraka vibaya?
 
Hivi hakuna hoja za maana hadi mtu ung'ang'anie kuwa wapinzani watashindwa kwa sababu CCM wametumia kisukuma kwenye kampeni? kueni jamani miaka 17 imepita tangu 1992 mnapaswa kujua mnajukumu zitto la kuwakomboa watanzania. Ipo siku mtakuja kuwajibu watanzania hiyo ruzuku mnatumiaje.

Kwani Luzuku yenu mwaitumiaje??
 
Uchaguzi Busanda ni batili Chadema wameu haribu kwa sababu zifuatazo;

1. Mh Zitto Zubeir Kabwe akiwa mbunge Bunge la JMT amechoma bendera cha chama cha mapinduzi hadharani.

2. Mh Zitto amekuwa akinukuriwa katika mikutano yake ya hadhara akichochea uvunjifu wa amani na kutoa kashfa akiwa pamoja na kumuita Waziri mkuu mstaafu na makamu wa Rais wa JMT na Mbunge wa Bunge la JMT Mh John Malecela kuwa ni kibajaji nk

3. Chadema wameingiza kutoka Tarime kundi la wafanya fujo ambao wamekuwa wakiendesha matukio ya kuhatarisha amani huko Busanda.

4. Chadema wamekuwa wakihamasisha wahuni kwenda kwenye mikutano ya CCM na kuzomea viongozi wa juu wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwarushia mawe.

5. NK

Tambwe Hiza would take that crap in his upopular, and especially self-destructive compaign.
 
Mkuu Kibunango hebu jaribu kufafanua kidogo - nimeshindwa kabisa kukuelewa una maana gani.
Kamanda Mag3,
Siku zote kampeni ni ushindani kuanzia wa sera hadi wa maneno ya dhihaka na vituko vya dhihaka vilevile. Umekusanya vizuri nukuu zako nami katika kuzisoma nimeona za CCM as wenye dola, kampeni zao zinaendana sambamba na wasifa huo, huku upinzani nukuu zao ni kama watu wanaolia lia katika kupiga kampeni zao, ili waweze kuonewa huruma!
 
You are wrong Madam, infact very wrong! Kisukuma si lughaya Taifa, sheria zinataka tutumie lugha ya Taifa, ndo maana nasema CCM wameharibu uchaguzi na uchaguzi umekuwa batili (ikiwa watashinda) maana wamevunja sheria za uchaguzi. Pili, Mama nakukumbusha tu kuwa CCM ndo wanaojidai kuwa wamejenga Utaifa na kufuta Ukabila; hii ni CCM ile-ile au tuitegemee nyingine! NAogopa sana Mama, mwendo huu si mzuri. Mimi siamini ushindi kwa gharama yoyote hata kwa kwenda kinyume na misingi ya umoja wetu ati Chama fulani kishinde hasa Chama Tawala. Ni hatari kubwa!
Ndugu Ibra
Kuna mwanasiasa alitamka hivi "CCM yenyewe hasa iko makabatini inajaa vumbi! Mpaka atokee mtu mwenye akili nzuri ya kwenda kuitoa kabatini na kuifuta vumbi hapo ndipo kutakuwa na matumaini kwa chama hiki!"
 
Invincible,
Mkuu ukitazama maeleoz yote ya Zitto ni mashambulizi kwa mgombea au chama kinachoshiriki ktk uchaguzi lakini maneno ya waziri Ngeleja ni vitisho kwa wananchi wapiga kura..Huu ni uvunjaji wa sheria zote za demokrasia kwani mashambilizi siku zote huwa kati ya vyama au wagombea..Huwezi kuwatishia wananchi wapiga kura hata siku moja kama sii Udikteta!

Mkuu labda umesahau kwamba serikali ya CCM walimuua mbwa akiyekuwa amevikwa Tshirt ya CCM huko Tarime...sababu haijulikani, lakini inaonyesha wazi kwamba CCM wachovu ktk semokrasia..Upinzani kwao ni uadui na kila kinachofanyika hata kama ni dhihaka wao wanachukulia.. Kisokorokwinyo!
 
Hekaheka Busanda

• Helikopta ya Mbowe yaivuruga CCM

na Kulwa Karedia, Busanda

Tanzania Daima~Sauti ya Watu
​

MWENENDO wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Busanda, unazidi kuonyesha kila dalili za kuzidiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuendelea kwa matukio ya viongozi wake waandamizi kuzomewa na kukimbiwa katika mikutano yao ya kampeni.

Sambamba na kuendelea kwa matukio hayo, kuwasili kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana na kuanza kampeni za lala salama dhidi ya chama chake, kumezidisha tambo na mikikimikiki ya kampeni hizo kwa chama hicho.

Mbowe ambaye aliwasili katika anga la Busanda kwa kutumia helikopta majira ya saa nane mchana, alifanya mkutano wake wa kwanza katika Kijiji cha Nyamigota ambako aliwataka wapiga kura kutomchagua mgombea wa CCM kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kutangaza janga la kitaifa dhidi ya Watanzania.

“Ndugu zangu wana Busanda, naomba niwaeleze kuwa kuichagua CCM ni sawa na kutangaza janga la kitaifa kwani kwa kipindi cha miaka 48 kilichokaa madarakani, kimeshindwa kupambana na umasikini, badala yake kimekuwa kikiuzalisha kila siku,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo.

Mbowe aliilaumu CCM kwa kumteua Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Tanzania Bara, John Malecela, anayefahamika zaidi kwa jina la Tingatinga kuwa, ni kumdhalilisha kwa sababu kwa umri wake na wadhifa wake hapaswi kufanya kazi ya kugawa chumvi na magodoro kwa wapiga kura ambao wamekwishaonyesha nia ya kutokichagua chama anachokitetea.

“Wabunge wa CCM siku zote wamekuwa mzigo, wameshindwa kusoma alama za nyakati, sasa masikini wangu wameamua kumtoa mzee Malecela kwa ajili ya kukiokoa chama chao… tunasema wamechelewa kwa hili.


“CHADEMA hivi sasa ina kazi moja tu ya kuhakikisha inarudisha heshima ya jimbo hili kwa vile ina uhakika wa kushinda katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.

“Nawaambia huyo Malecela waliyemleta hapa atavuna alichopanda na atabeba gunia lake la aibu… kwanini asitumie nyakati hizi kukaa nyumbani au kuwa mshauri wa chama badala ya kugeuka kuwa kinara wa rushwa?” alihoji Mbowe.

Alisema anachoamini ni kwamba, Malecela kwa uwezo alionao anastahili kuwa mshauri wa vijana wa chama hicho na kuwaachia vijana hao kazi ya kupambana na wanamapinduzi wa kweli wanaotaka kuing’oa CCM madarakani.

“Nilitegemea Malecela angekuwa kioo cha kukemea rushwa, ufisadi na matendo maovu ndani ya CCM, lakini sasa wameamua kumtupa vijijini kugawa magodoro… namheshimu sana kama mzee wetu, lakini sina budi kumwambia ukweli kuwa, wakati wa kupumzika umefika,” alisema.


Baadaye Mbowe aliruka kwa helikopta hadi Kijiji cha Lwamgasa, ambako baada ya kufika ilionekana dhahiri kubadilika kwa upepo wa kisiasa katika kijiji hicho ambacho wakazi wake wengi ni wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Kabla ya kuwasili helikopita hiyo, mamia ya wakazi wa eneo hilo walikuwa wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa kampeni za Chama cha Wananchi (CUF), lakini baada ya kutua, mkutano huo ulishindwa kuendelea baada ya waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kusikiliza sera za chama hicho kukimbilia katika mkutano wa CHADEMA.

Akiwahutubia wakazi wa eneo hilo, aliwataka kufanya mageuzi bila ya kushinikizwa na viongozi wa CCM.

Mbowe ambaye aliwasili kijijini hapo saa mbili baada ya mgombea wa CCM, Lolencia Bukwimba kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni, aliwasihi wananchi kutobabaishwa na vitendo vya CCM vya kupeleka nguzo za umeme kijijini hapo, kwani hiyo ni kutaka kufanya ujanja wa kuchaguliwa.

“Msibabaishwe na CCM kuwaletea nguzo za umeme hapa, huu ni uongo tu, wanataka kuwadanganya ili muwapigie kura katika uchaguzi ujao… mbona miaka yote hawakuja, leo hii ndiyo wanakuja hawa wakataeni,” alisema Mbowe.

Baadaye alikwenda katika Kijiji cha Kaseme ambako aliwataka wananchi kutobabaishwa na propaganda za CCM za kuletewa maisha bora.

Kuwasili kwa helikopita katika jimbo hili jana, kulisababisha hata baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwa katika Hoteli ya Zacharia Lodge kuungana na wana CHADEMA kuipokea.

Kitendo hicho kilifanya viongozi hao kushangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakiimba ‘Kamanda wa Pori ametua kuondoka na mbunge’.

Aidha, kuwasili kwa helikopta hiyo inayotumiwa na Mbowe katika kampeni hizo, kulisababisha kusimama kwa shughuli nyingi za kijamii na barabara nyingi kufungwa kutokana na wingi wa watu waliokuwa wakifika kumuona mwenyekiti huyo wa CHADEMA.

Katika tukio ambalo halikutarajiwa na wengi, licha ya helikopita hiyo kutua karibu na Kituo cha Polisi Katoro na kufunga barabara, polisi hawakuchukua hatua yoyote ya kufukuza wananchi waliokuwa wakiishangilia CHADEMA baada ya Mbowe kushuka katika helikopta hiyo.

Katika hatua nyingine, hali ya mambo ndani ya CUF imeonekana kuwa mbaya baada ya uongozi wa chama hicho kuwafukuza wafanyakazi wake wawili kwa madai kuwa wanavujisha siri za chama hicho.

Tukio hilo limetokea jana ambapo iliwafukuza Haroun Mikole ambaye ni fundi mitambo na dereva Mazoe Chidide kwa maadai kuwa walikutwa wakiteta jambo na viongozi wa CHADEMA usiku wa kumkia jana.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa vyama vya CHADEMA na CUF, kwa upande wa CCM, jana ilikuwa zamu ya kada wake kijana ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kukumbana na hasira za wapiga kura wa Busanda.

Kwa mara ya kwanza tangu alipowasili katika kampeni hizo kukiongezea nguvu chama chake, jana Ngeleja alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukimbiwa na wachimbaji wadogo wadogo katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliokuwa ukifanyika katika mgodi wa dhahabu wa Lwamgasa.

Hatua ya Ngeleja kukimbiwa na wachimbaji hao ilitokana na kauli yake kuwa, kama watashindwa kuichagua CCM watanyag’anywa leseni na kufutiwa usajili wa vitalu vyao.

Katika mkutano huo ambao ulifanyika katika Shule ya Msingi Mwenge, Ngeleja alisema CCM ndiyo yenye wezo wa kuchukua hatua zozote zinazostahili kuwaendeleza wachimbaji, wakiwamo wa migodi mikubwa kama vile Mererani, North Mara na Geita Gold Mine.

“Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang’anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali,” alisema Ngeleja.

Alisema wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa na tabia ya kupinga sera za CCM eti kwa madai kuwa imekuwa ikiwakandamiza, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Katika hali inayoonekana kuwa vitisho, Ngeleja alisema kama CCM itashindwa kwenye uchaguzi huo, wachimbaji hao watashukiwa kwa nguvu zote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuona kama kweli wanalipa kodi ya serikali.

“Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali,” alisema Ngeleja.

Kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wachimbaji hao ambao walianza kuondoka mmoja mmoja ndani ya ukumbi na kumwacha Ngeleja na viongozi wa CCM aliokuwa ameambatana nao kwenye kikao hicho.


Baadhi ya wachimbaji hao waliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa, huo ni unyanyasaji mkubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali.

Mmoja wa wachimbaji hao, Swedi Mussa alisema kama Waziri Ngeleja ataendelea na kauli hiyo, anaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya jamii inayozunguka machimbo na Watanzania ambao ndio wanayategemea kuendesha maisha yao ya kila siku.

“Tumeshangazwa na kauli ya Ngeleja na ndiyo maana tuliamua kumkimbia ndani ya ukumbi, kwa sababu inaonekana wazi kwamba sasa anataka kutufanya Watanzania ni wajinga wa kutupwa, kwanini kaja wakati wa kampeni kututisha hivi?” alihoji Mussa.

Aliongeza kuwa, hatua ya kuambiwa kwamba watanyang’anywa leseni inaonyesha wazi kwamba CCM imedhamiria kuongeza umasikini katika jamii tofauti na sera zake kwamba inaleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
 
Well..
Niiwasilishe kama ilivyo: Mjumbe hauwawi.


BARUA TOKA MWANA-CCM BUSANDA ​
“HII NI KURA YA MAONI”​
Salaam!
Nikiwa ni mwanachama mwaminifu wa Chama cha Mapinduzi ninaamini uchaguzi uliopo mbele yetu ni uchaguzi ambao ni sawa kabisa na kura ya maoni juu ya mwelekeo wa jimbo letu na hasa hali ya uongozi katika jimbo hili. Ni kura inayohusu hasa kuridhika na uongozi uliowahi kuwepo kwa muda mrefu na ambao unataka kuendelea kuwepo. Hii ni kura ya maoni yetu kuhusu wapi tunataka Busanda iende na ifike chini ya Mbunge ajaye. Uchaguzi uliopo mbele yetu basi ni uchaguzi unaozidi mtu, watu, chama au mwelekeo wa kisiasa. Ni uchaguzi unaotuhusu sisi na watoto wetu na wajukuu zetu. Ni uchaguzi ambao kwa mapenzi ya Mungu umetokea wakati huu na ni wajibu wetu kutambua maana yake.


..... i
 

Attachments

Attachment is password proteected, can you attached unlocked files please.
 
Msharika soma read only tu.

Mzee Mwanakijiji

Emmanuel Mashibya,

hakuna jina la mashibya huko busanda,Hapo ndipo ulipokosea!kuna kina machibya tu!

Spinning zingine bwana,ila ni barua nzuri kwa ajili ya propaganda
 
Back
Top Bottom