Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Yamebaki masaa 48 muhimu kwa Chadema kuunganisha nguvu na CUF kuichukua Busanda. Kuna watu wa aina yangu, type ya kina Tomaso wa Biblia, hatuwezi kuamini kinachotarajiwa kutokea Busanda mpaka tukashuhudie kwa macho, Kesho natia timu Busanda kushuhudia na kuwajulisha.
Mpaka sasa, barua imekuja too late na there is too little to do.Busanda ni CCM asilimia 40% hiyo asilimia 60% CUF watagawana na Chadema na mshindi atabaki CCM.
Haya ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi wetu kwa kila mmoja kujiuliza kwa nini nisiwe mimi?, Busanda hiyoo....CCM.
Haina maana mimi ni mshabiki wa CCM, mimi ni mshabiki wa ukweli na hali halisi.
 
Nasikitika kuona ni rasilimali kiasi gani huwa zinapotea wakati wa uchaguzi wa majimbo ambayo yako wazi kutokana na wawakilishi wake kufa au kushindwa rufaa. CCM nzima imehamia kwenye jimbo moja. Juzi ilikuwa huko Mara, na kesho utasikia tena sehem nyingine. Mi nadhani kama jimbo lilikuwa chini ya chama fulani, basi ateuliwe mwakilishi toka hicho chama na kukaimu hiyo nafasi hadi wakati wa uchaguzi mkuu. kwa mtindo huu matumizi mabovu ya rasilimali yatadhibitiwa, pamoja na kadhalika nyinginezo. Nadhani hiyo ni hoja kamili.
 
Kabla ya kuwasili helikopita hiyo, mamia ya wakazi wa eneo hilo walikuwa wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa kampeni za Chama cha Wananchi (CUF), lakini baada ya kutua, mkutano huo ulishindwa kuendelea baada ya waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kusikiliza sera za chama hicho kukimbilia katika mkutano wa CHADEMA.
duh...hii sasa italeta wivu ndani ya upinzani. CUF wangekaa pembeni tu sasa, wabaki washabiki tu!
 
“Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang’anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali,” alisema Ngeleja.

huyu jamaa ni nanga? Mbona analeta vitisho vya kipumbavu? Hawa ndo wadhanio serikali ni kila kitu? Ngojea mabadiliko yaje, watu wajue kuwa serikali ipo chini ya sheria kama mimi na wewe. Na sio chombo kinachotumika kunyanyasa wananchi!
Kifungu numba 7 katika Katiba itabidi kwanza kibadilishwe.
 
Unaonekana wewe upo chama kimoja na mafisadi,

Huo ni mtazamo wako; nimeamua kusema ukweli ili ijulikane kwa watu wote kuwa Upinzani ukipigwa bao kusiwe na visingizio tuliibiwa kura au mengineyo wkt mazingira ya kuibiwa tuliyataka wenyewe

Wewe mwenyewe umeshindwa kujiandaa vyema kuleta habari iliyokamilika. Huenda walitakiwa kujulikana mapema nao waanze kupewa chumvi na magodoro.

Mimi si mwandishi wa habari; nimeandika vile nilivyoipata hiyo habari kutoka ktk chombo cha habari (TBC Taifa) wakati msimamizi anahojiwa na mwandishi wa habari. Jadili somo husika usinijadili mimi bainafsi, nimefikisha ujumbe kwa wadau wa siasa. Kama unaona huelewi kitu kaa kimya hujalazimishwa.

watu wako makini wakiwajua mapema wanaanza kuwasumbua narushwa ndo mana wanawataja dakika ya mwisho.

Kujulikana mapema kwa wasimamizi ni jambo muhimu sana ni ktk mikakati ya kujihakikishia maandalizi ya kulinda kura za chama chako. Ukiweka msimizi asiye muaminifu ni tatizo la chama husika kilichomuweka msimamizi huyo bomu asiyejua thamani ya ushindi kwa chama chake na kwa wapenda maendeleo wote kwa ujumla; si la chama cha mafisadi. Tunajua mafisadi kazi yao ni kufisidi; kwa hiyo lazima tutarajie watatafuta upenyo ili wapitishe ufisadi wao kwa huyo msimamizi ili lengo lifanikiwe nalo ni kuiba kura au kuweka kura zilizokwishapigwa.
Vile vile tujue uchaguzi una sheria na taratibu zake; kama wakichelewa kupelekwa ndio tumeliwa sisi; hizo kampeni na mengineyo yote itakuwa ni big zero

Hongera mkuu kwa kuliona hilo, nafikiri ndicho walichokuwa wanakitafuta hicho kuwajua mapema ili wawape ahadi kubwa na kuruhusu wizi wa kura huyo ndio CCM kubwa la maadui kwenye picha ya kihindi.

Muhimu kila chama hasa wapinzani kujenga msingi madhubuti kwa wanachama wao hasa UAMINIFU KTK CHAMA NA MAISHA YA KILA SIKU KWA UJUMLA, tuwaeleshe wanachama wetu thamani yao ktk chama na wao wanatakiwa wakithamini chama; na jengine wawajulishe umuhimu wa kuwa na uaminifu kwao wenyewe na kwa chama chao.
Kama mtu anajua thamani yake, utu wake na thamani ya chama chake kwake binafsi na jamii kwa ujumla, hata FISADI AJE NA MILIONI NGAPI HATAPOTEZA UAMINIFU WAKE KWA MAMBO YA KUPITA

AMANDLA!!!
 
Hatua ya Ngeleja kukimbiwa na wachimbaji hao ilitokana na kauli yake kuwa, kama watashindwa kuichagua CCM watanyag'anywa leseni na kufutiwa usajili wa vitalu vyao.

Katika mkutano huo ambao ulifanyika katika Shule ya Msingi Mwenge, Ngeleja alisema CCM ndiyo yenye wezo wa kuchukua hatua zozote zinazostahili kuwaendeleza wachimbaji, wakiwamo wa migodi mikubwa kama vile Mererani, North Mara na Geita Gold Mine.

"Napenda kuwaambia ndugu zangu, leo nimewaita hapa kutaka kuwaambia kwamba, tuna kazi moja tu ya kuhakikisha mnachagua CCM katika uchaguzi ujao, sasa nawaambia kama hamtafanya hivyo, tutahakikisha tunawanyang'anya leseni kwani CCM ndiyo yenye serikali," alisema Ngeleja.

Alisema wachimbaji wadogo wadogo wamekuwa na tabia ya kupinga sera za CCM eti kwa madai kuwa imekuwa ikiwakandamiza, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Katika hali inayoonekana kuwa vitisho, Ngeleja alisema kama CCM itashindwa kwenye uchaguzi huo, wachimbaji hao watashukiwa kwa nguvu zote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuona kama kweli wanalipa kodi ya serikali.

"Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali," alisema Ngeleja.

Kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wachimbaji hao ambao walianza kuondoka mmoja mmoja ndani ya ukumbi na kumwacha Ngeleja na viongozi wa CCM aliokuwa ameambatana nao kwenye kikao hicho.

Hii inadhihirisha kuwa wanasiasa tunaodhani ni wanasiasa hawajui siasa.

Inawezekanaje kumuomba mtu kura kwa kumtisha? Wananchi wanatakiwa kujua kuwa, hata wakiipigia CCM kura, kama nia yao ni kuwanyang'anya leseni watawanyang'anya tu. Wamefanya hivyo sehemu nyingi, na hakuna kinachoweza kuwafanya wasifanye hivyo sehemu nyingine.

Serikali haiwezi kuacha kutuma TRA kwenda kutafuta ukweli wa kodi inayolipwa na wachimbaji hao, eti kwa kuwa wameichagua CCM. Inataka pesa, tena inataka pesa hasa. TRA ikijua kuna wakwepa kodi huko Busanda watawakimbilia bila hata kujali Mbunge wao ni nani. Wasidanganye watu kama vile watoto wachanga. Hata watoto wadogo siku hizi hawadanganyiki kijinga hivyo.

Kauli ya Waziri Ngeleja, mtu ninaemheshimu, ninaemfahamu kwa siku nyingi zinasikitisha sana. Angeweza kukaa nao kwa heshima na kuwaomba wamsaidie kutafuta kura kwa wenzao. Angewasikiliza na kukubali (kama zuzu tu) ili apate anachotaka. Wahenga wanasema "mtumikie kafiri upate mtaji wako". Kwani angepungukiwa na nini kama angejishusha na kuomba msaada kwa wachimbaji hao? Wachimbaji hao wangeweza kumtafutia kura nyingi tu, ila baada ya kumkashifu, kumsimanga na hata kumlaumu kwa ahadi zake hewa. Lakini angeondoka akiwa ameisaidia CCM kushinda, na angeheshimika kwa watu hao, kuliko kuwatishia na kujivunjia heshima kwa watu wote (hata wasiopo Busanda).

Wanasiasa wa TZ wako wapi siku hizi? Hawajui kuwa heshima na utii hubomoa miamba bila hata kuigusa?

Sijui niingie kwenye ulingo? Joke, no time for that.
 
Mimi ntajuaje hakuna kina "mashibya" wakati mwandishi kasema "mashibya"? Na wale wanaosema Busanda hakuna kina "mashibya" wameuliza majina ya kila mkazi wa eneo hilo, wahamiaji, na wageni wengine ambao si wa asili wa miji hiyo? ubishi mwingine!
 
Huo ni mtazamo wako; nimeamua kusema ukweli ili ijulikane kwa watu wote kuwa Upinzani ukipigwa bao kusiwe na visingizio tuliibiwa kura au mengineyo wkt mazingira ya kuibiwa tuliyataka wenyewe

Mimi si mwandishi wa habari; nimeandika vile nilivyoipata hiyo habari kutoka ktk chombo cha habari (TBC Taifa) wakati msimamizi anahojiwa na mwandishi wa habari. Jadili somo husika usinijadili mimi bainafsi, nimefikisha ujumbe kwa wadau wa siasa. Kama unaona huelewi kitu kaa kimya hujalazimishwa.

Kujulikana mapema kwa wasimamizi ni jambo muhimu sana ni ktk mikakati ya kujihakikishia maandalizi ya kulinda kura za chama chako. Ukiweka msimizi asiye muaminifu ni tatizo la chama husika kilichomuweka msimamizi huyo bomu asiyejua thamani ya ushindi kwa chama chake na kwa wapenda maendeleo wote kwa ujumla; si la chama cha mafisadi. Tunajua mafisadi kazi yao ni kufisidi; kwa hiyo lazima tutarajie watatafuta upenyo ili wapitishe ufisadi wao kwa huyo msimamizi ili lengo lifanikiwe nalo ni kuiba kura au kuweka kura zilizokwishapigwa.
Vile vile tujue uchaguzi una sheria na taratibu zake; kama wakichelewa kupelekwa ndio tumeliwa sisi; hizo kampeni na mengineyo yote itakuwa ni big zero

Muhimu kila chama hasa wapinzani kujenga msingi madhubuti kwa wanachama wao hasa UAMINIFU KTK CHAMA NA MAISHA YA KILA SIKU KWA UJUMLA, tuwaeleshe wanachama wetu thamani yao ktk chama na wao wanatakiwa wakithamini chama; na jengine wawajulishe umuhimu wa kuwa na uaminifu kwao wenyewe na kwa chama chao.
Kama mtu anajua thamani yake, utu wake na thamani ya chama chake kwake binafsi na jamii kwa ujumla, hata FISADI AJE NA MILIONI NGAPI HATAPOTEZA UAMINIFU WAKE KWA MAMBO YA KUPITA

AMANDLA!!!

Mkuu tatizo kubwa ninaloliona ni umasikini walionao wanaoingia kwenye siasa za vyama. Wengi wao wanajihusisha na siasa ili kuganga njaa. Hivyo huwa rahisi sana kurubuniwa.

Kuhusu uwakilishi katika usimamizi wa kuhesabu kura, ni jambo la hatari sana kama chama chochote hakitakuwa na wasimamizi wazuri wenye nia ya kuhakikisha haki kwa chama chao inapatikana.

Kwa mtazamo wangu, mwakilishi huyo wa Tume ya Uchaguzi amefanya kosa kubwa sana kutamka kuwa kuna vyama (na kwa kutaja majina ya vyama hivyo) ambavyo havijapeleka majina ya wasimamizi wao katika zoezi zimala kuhesabu kura. Ni makosa kwa kuwa anatoa indication kuwa CCM inayo nafasi ya kurubuni matokeo hayo endapo itataka kufanya hivyo. Vile vile, amekosea kwa kuwa wananchi hawataamini matokeo yatakayotangazwa kuwa hayajarubuniwa hata kama yatakuwa sahihi. Nilidhani ingekuwa vyema akabaki na siri hiyo, huku akifanya jitihada za kuwasiliana na vyama ambavyo havijatumia fursa yao ya kupeleka majina ya wasimamizi wao ili wafanye hivyo haraka.
 
Ymeashaanza. technicalities kama hizi (kupeleka majina wiki moja kabla...) zinafanana na yale mambo yaliyotokea Mbeya. Ebu nikalale mie
 
Ymeashaanza. technicalities kama hizi (kupeleka majina wiki moja kabla...) zinafanana na yale mambo yaliyotokea Mbeya. Ebu nikalale mie

Sio kweli; hii sheria ipo miaka mingi tu. Sina hakika ni viongozi wa vyama kutokujua taratibu nzima za uchaguzi au ni kutokufuatilia taratibu na sheria za uchaguzi; kuanzia mchakato wa kutafuta wagombea hadi ktk kumpata mshindi wa uchaguzi.

DOKEZO: Naomba sana kwa wale wenye uwezo wa kuzipata na watuwekee humu jamvini sheria za uchaguzi za tume ya taifa ya uchaguzi ili tuzijue na pia tuongeze upeo wa kuzifahamu sheria hizo. (Nitaituma pia ktk jukwa la sheria)
 
Sio kweli; hii sheria ipo miaka mingi tu. Sina hakika ni viongozi wa vyama kutokujua taratibu nzima za uchaguzi au ni kutokufuatilia taratibu na sheria za uchaguzi; kuanzia mchakato wa kutafuta wagombea hadi ktk kumpata mshindi wa uchaguzi.
Si kwamba napingana na sheria, hapana. Kinachonichosha ni kuona yaliyotokea Mbeya Vijijini yanaweza pia kutoka na Busanda. lawama of course zitakuwa juu ya watakaoshindwa kufuata matakwa ya sheria na kanuni
 
CCM wameshazoea ushindi wa hila. Hii ni elimination tu, 2010 ndio fainali. Tusubiri tuone mwisho wake.
 
Mimi ntajuaje hakuna kina "mashibya" wakati mwandishi kasema "mashibya"? Na wale wanaosema Busanda hakuna kina "mashibya" wameuliza majina ya kila mkazi wa eneo hilo, wahamiaji, na wageni wengine ambao si wa asili wa miji hiyo? ubishi mwingine!

Angalia mtu aliyetoa kasoro hiyo halafu jumlisha 1 na 1 kisha utajua kama jibu ni 11 ama vipi!

BTW anayejifanya kujua majina ya huko kang'ang'ania machibya tu wakati inawezekana ikawa mashiba pia.
 
Mkuu AljuniorTz habari yako hukuifanyia utafiti wa kutosha tayari wasimamizo wapo tena wamejiandaa vy akutosha kulinda hizo kura zetu za za ushindi.Watu wapo hatua moja mbele yako mkuu.
 
Yamebaki masaa 48 muhimu kwa Chadema kuunganisha nguvu na CUF kuichukua Busanda. Kuna watu wa aina yangu, type ya kina Tomaso wa Biblia, hatuwezi kuamini kinachotarajiwa kutokea Busanda mpaka tukashuhudie kwa macho, Kesho natia timu Busanda kushuhudia na kuwajulisha.
Mpaka sasa, barua imekuja too late na there is too little to do.Busanda ni CCM asilimia 40% hiyo asilimia 60% CUF watagawana na Chadema na mshindi atabaki CCM.
Haya ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi wetu kwa kila mmoja kujiuliza kwa nini nisiwe mimi?, Busanda hiyoo....CCM.
Haina maana mimi ni mshabiki wa CCM, mimi ni mshabiki wa ukweli na hali halisi.

Mkuu Pasco,

Niko nyuma yako. Mawazo yako ni sahihi. Tusishangae kusikia CCM wameshinda kwa sababu ya mawazo mafupi waliyo nayo viongozi wa vyama vya upinzani. (kama ni wapinzani kweli.) I doubt very much kama kweli hawa ni wapinzani wenye upeo wa kutaka kuikomboa nchi hii. Kwa nini wasikubali kuwa kitu kimoja ili adui yao awe CCM na baada ya kuiondoa CCM madarakani then kila chama kisimame kivyake vyake? Kenya ilifanika kuiondoa KANU madarakani kwa mtindo huu. Kwa nini vyama vya upinzani havijifunzi?

Sitashangaa kusikia course instructor wangu Professor Lipumba yuko kwenye payroll ya CCM.

Tiba
 
Mkuu AljuniorTz habari yako hukuifanyia utafiti wa kutosha tayari wasimamizo wapo tena wamejiandaa vy akutosha kulinda hizo kura zetu za za ushindi.Watu wapo hatua moja mbele yako mkuu.

Ni kweli sikufanya utafiti wa kutosha; ila nimetoa taarifa nikiwa mpenda mageuzi ya kweli ktk nchi yangu hasa baada ya kupata taarifa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi. Sipendi tuwe ni wababaishaji ktk kuyaendea hayo mageuzi ya kweli, halafu baadae tuwe tunalalamika...
 
Asante mkuu, hata hivo kwa hali ya ujambazi wa kura wa CCM ulivo, pengine kuto anika majina hayo mapema ni vyema, kwani ukiyaweka wazi unaandaa mwanya wa hao majambazi kwenda majumani mwao usiku kuwahonga ili wakubali kubadili matokeo! Ni bora wasiwajue mapema.
 
Back
Top Bottom