Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

mkuu kuna Pepo linaitwa CCM,hiyo ndo nasikia leo,sina pepo mimi ila ushindi kwa CCM ni wa lazima
Kama ulinisoma mapema nilisema kama Busanda wanachagua mtu, basi mbunge ni wa Chadema, wa CCM hamna kitu. Kama wanachagua chama, CCM ni kwa muujiza.
 
Kama ulinisoma mapema nilisema kama Busanda wanachagua mtu, basi mbunge ni wa Chadema, wa CCM hamna kitu. Kama wanachagua chama, CCM ni kwa muujiza.

Mkuu unaturusha roho hapa.....tuanze fungua Champagne zetu ? Kazi nzuri mazee....hatutali hadi kieleweke!
 
Mkuu Pasco, mimi sina uhakika kama Invincible ndio huyo huyo Invisible. Kama mmoja/wote wapo online ni vizuri watufafanulie, maana naona amepost mmoja na wewe ukamuunga mkono mwingine. Nadhani hii inawachanganya wengi humu, si wewe na mimi tu.

Wengi wanachanganya haya majina katika maeneo tofauti tofauti.

Bahati nzuri mimi na Invisible tunafanana, kama majina yanavyofanana.
 
bado jamani.. mbona kuna wasiwasi.. sasa hivi kulikuwa na mtu kakamatwa akituhumiwa kuiba kura... (ka nzi kako on the ground of course)..
 
Haya wana JF, yale masaa 48 muhimu kwa Wanabusanda ndio yame expire, kampeni zimefanywa, kura zimepigwa hivyo kilichofanyika Busanda, kimefanyika sasa tusubiri matokeo hivyo naomba kusign off kwa kumuomba mod aifunge hiii thread lengo lake limeisha.
Tukutane kwenye thread mpya ya 'Matokeo Busanda' .
Asanteni sana
Pasco.
 
Simon Mhina
Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Busanda, leo wanamiminika vituoni kupiga kura kumchagua atakayemrithi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Kabuzi Rwilomba huku wagombea na viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo wakitambiana kwa kila mmoja kuibuka mshindi.

Vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali, ni pamoja na Chadema, ambayo imemsimamisha Finias Magessa na CCM, iliyomsimamisha Lolesia Bukwimba kuwania kiti hicho.

Vyama vingine, ni CUF kilichomsimamisha Oscar Ndalahwa na UDP, ambacho kimemsimamisha Beatrice Lubambe.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya vyama hivyo kufanya kampeni kwa kipindi cha zaidi ya wiki tatu, kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu, kuwanadi wagombea wao.

Kampeni hizo zilihitimishwa jana kwa Chadema kufanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya Mnadani vilivyoko katika mji mdogo wa Katoro, ambako ni makao makuu ya jimbo.

UDP ilifunga kampeni za mgombea wake katika viwanja vya kituo cha mabasi, wakati CCM ilihitimisha katika viwanja vya CCM vilivyoko mjini humo na CUF kwenye viwanja vilivyoko katika Kata ya Nyarugusu, wilayani Geita.

Matukio, kauli na vitendo vingi, vimekuwa vikiripotiwa na vyombo vya habari kutokea tangu kuanza kwa kampeni hizo, vinavyolenga kuzua vurugu na kuhatarisha amani katika kuelekea uchaguzi huo.

Miongoni mwa matukio hayo, ni pamoja na kukamatwa kwa watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa baadhi ya vyama wakinunua shahada za kupiga kura kwa wapigakura.

Mengine, yalihusu wafuasi wa chama kimoja kuwashambulia kwa kuwapiga na kuwajeruhi wafuasi wa chama kingine.

Hata hivyo, hali chafu ya hewa kufikia jana, ilifanikiwa kudhibitiwa na Jeshi la Polisi, ambalo kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wake Mkoa wa Mwanza, Elias Kalinga limeongeza askari kutoka 113 hadi 183 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika uchaguzi huo.

Askari hao, wakiwamo askari kanzu na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa wamejiandaa na zana za kivita, yakiwa na magari ya kurusha maji yanayowasha mwilini, walifanya doria katika mji mdogo wa Wilaya ya Geita wa Katoro na vitongoji vyake kuanzia jana asubuhi na hali kuwa shwari.

Doria hiyo walikuwa wakiifanya kwa kutumia magari maalum ya polisi wakati huo wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM wakiwa kwenye pikipiki, baiskeli na wengine kutembea kwa miguu wakizunguka maeneo mbalimbali ya mjini Katoro kuhamasishana kuhusiana na uchaguzi huo.

Katika hatua isiyo ya kawaida, polisi wote wamevua namba zao, ambazo huwa zinabandikwa kifuani ili waweze kutambulika kirahisi. Mmoja wa Polisi aliyeulizwa, alisema kwa kawaida wakiwa kwenye oparesheni kama hizo huwa wanaamriwa kuvua namba zao.

Ukiachilia mbali hayo, mchuano mkali katika uchaguzi huo umetabiriwa kuwa kati ya vyama vya Chadema na CCM, ambavyo vimeonyesha mbwembwe kubwa katika kampeni zao.

Mbwembwe hizo, ni pamoja na matumizi ya helikopta yaliyofanywa na Chadema na pia vikundi mbalimbali vya burudani na hamasa, kikiwamo kile cha Tanzania One Theatre (TOT) kwa CCM, ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kutia chachu na hamasa kampeni za wagombea wao.

Katika kampeni zake, CCM ilikuwa na timu tano za kampeni zilizojichimbia katika Kata zote 13 za jimbo hilo kumnadi mgombea wake kwa siri na dhahiri. Timu hizo zilikuwa na watu wazito wa chama na serikali.

Hata hivyo, kulingana na tathmini ya hali ya siasa jimboni hapa na hali halisi ya CUF, lolote linaloweza kutokea kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Pia, ule muujiza wa Yesu Kristo wa kubariki mkate mmoja kuwa mingi ukitarajiwa kutokea kwa chama cha UDP, ambacho matumaini ya kushinda uchaguzi huo ni finyu sana.

Licha ya kampeni za kumnadi mgombea wake kutokuwa na mbwembwe, CUF inaweza kubadili hali ya mambo kwa kuibuka mshindi na kuwashangaza wengi kutokana na faida iliyonayo ya kujijengea mtandao wa chama kwa muda mrefu katika wilaya Geita.

Akizungumza na Nipashe mjini Geita, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wana matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo ingawa alisema hawezi kutaja asilimia za ushindi huo kwa vile huenda watu waliojiandikisha wasiweze wote kujitokeza kupiga kura.

Katibu Mkuu wa UDP, John Nkolo alisema wana matumaini ya kushinda katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, naye aliungana na Profesa Lipumba kwa kusema kwamba, hawezi kutaja watashinda kwa asilimia ngapi kwa vile vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ni vinne.

Mratibu wa Kampeni za CCM, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, George Mkuchika alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, mgombea wao, Rwilomba alishinda kwa asilimia 79, hivyo katika uchaguzi wa leo wana mategemeo ya kufanya vizuri zaidi katika uchaguzi wa leo.

Naye mgombea wa Chadema, Magessa alipoulizwa na Nipashe aliwataka wananchi kusubiri matokeo akisema kwamba, kwa sasa bado wangali kwenye mapambano.

Awali, Afisa Habari wa Chama hicho, David Kafulila alisema kulingana na utafiti walioufanya wana matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 78.

Katika kile kinachoonekana kama jumuiya ya kimataifa imeamua kufuatilia kwa karibu uchaguzi huo uliovuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi, imetuma waangalizi wake jimboni hapa kuangalia hali ya mambo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geita jana, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Lewes Makame, alitaja nchi zilizotuma waangalizi wao katika uchaguzi huo, kuwa ni Uholanzi, Marekani, Uingereza na umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

Katika kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa, wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa wamehamia Busanda, kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, uhuru na amani.

Tambo na vijembe vilivyokuwa vimetawala kwa kila chama jimboni Busanda jana jioni vilifikia tamati. Hata hivyo, tofauti na ilivyodhaniwa kila chama kilihitimisha mikutano yake kwa amani.

Wakati viongozi wa vyama vya upinzani bado wapo mijini Busanda, wale wa CCM waliondoka kuelekea mjini Geita kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

Viongozi hao wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, George Mkuchika, wako mjini Geita wakijipumzisha katika hoteli ya Tulo kujiandaa na safari kesho.

Habari zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinasema kuwa matokeo ya awali yanaonyesha kuwa CCM wanaongoza katika uchaguzi mdogo wa Magogoni baada ya kupata kura 2910 na CUF 1972, wakifuatiwa na chama cha SAU ambacho kimepata kura chache katika uchaguzi kati ya wapiga kura 5493, Mwinyi Sadallah anaripoti.

Kwa matokeo hayo, ni dhahiri kuwa CCM kimeshashinda katika uchaguzi huo na matokeo kamili yalitarajiwa kutangazwa saa tatu usiku jana.

NIPASHE JUMAPILI
 

Mkuu Pasco kwa nini usimuombe Mod abadili heading na kuwa masaa 54, yaani ongeza masaa sita ya kuhesabu kura?. hii iyasaidia kuendeleza mlolongo mzima wa Busanda kwa masaa 54
 
If they(CCM will win at Busanda nita conclude kuwa watz wooote ni wanafik

TUTAKE RADHI MKUU.....AMA WANAFIKI WALIO NJE YA TANZANIA WANAOPIGANIA TANZANIA???
 
If they(CCM will win at Busanda nita conclude kuwa watz wooote ni wanafik

Hey,ina maana Busanda ndio Tanzania yooote na watanzania woooote wanaishi hapo?Ebo!Mkuu vipi?Taratibu mazeee......your conclusion is/will be illogical.
 
kuweka kambi Busanda, kazi za serikali wanafanya aMawaziri kina nani?
Na Reginald Miruko
NILIPOANDIKA kwenye safu hii kuwa ‘Kampeni za Busanda ni jando ya kisiasa’ Jumapili iliyopita, nilipigiwa simu nyingi na wasomaji, wengine walinitumia ujumbe mfupi wa maneno. Wote waliowasiliana nami walionyesha kulielewa vema somo linalotokana na uchaguzi huu wa leo.

Walikubali kuwa mambo yanayotokea sasa katika kampeni za uchaguzi wa Busanda ni mafunzo maalumu kwa wanasiasa na wapiga kura—kwamba, kila upande unajifunza na kuelewa wajibu wake. Wapigakura wanaanza kutambua kuwa ukishamchagua mbunge au chama fulani, lazima aliyechaguliwa arudi kuleta maendeleo na kutimiza ahadi zake badala kuingia mitini na kusubiri uchaguzi mwingine.

Walielewa kwamba, wanaochaguliwa wanajifunza kuwa usipotimiza ahadi zako za kuondoa umaskini utapata cha mtemakuni wakati wa uchaguzi unaofuata—utasutwa, utazomewa, utahenyeshwa, utatumia pesa nyingi, utatunga uongo mwingi na utalazimika kupeleka misaada na huduma zilizochelewa ili kuwafuta machozi wapiga kura wako.

Lengo la makala ya leo si kurudia yote niliyojadili na wasomaji wangu, bali nitamtumia tu maoni ya mmoja wao. Huyu alijitambulisha kama John Simon wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Alihoji iweje mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wapige kambi kwenye Jimbo la Busanda kukipigia debe chama kimojawapo, kwa muda wote wa kampeni na kutelekeza majukumu yao ya kuhudumia wananchi wote.

Hoja ya msomaji huyu ilinichoma. Niliifikiria mno hasa kwa kuwa mawaziri kwa fedha zangu za kodi. Wanalipwa na wananchi wote ili wawatumikie wao. Hawalipwi mshahara na chama chochote cha siasa. Nimeamua kujadili hiyo hapa hapa leo kwa kuangalia mawaziri hao ambao hadi leo hii siku ya uchaguzi, bado wapo Busanda walipokuwa wanakipigania Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika kampeni hizo mawaziri waliokuwapo muda wote ni pamoja na George Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo aliyekuwa anaongoza kampeni za CCM na William Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini. Pia mawaziri wengine wa serikali ya awamu ya nne walipitapita huko Busanda kwa vipindi tofauti, akiwamo John Magufuli, Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.

Wanaolitazama juujuu suala hili, wanaweza kusema tu kwamba mawaziri hao wana haki ya kukinadi chama chao, au waziri kama vile Mkuchika ana nafasi zaidi kwa kuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, au kwamba mawaziri hao ni wanachama na wabunge wa chama husika, sawa. Swali langu kwao liko pale pale, kwamba kofia zao za uwaziri wakati wamepiga kambi Busanda wamezitumikiaje?

Kuna uwezekano mkubwa kuwa labda majukumu yao, yaliachwa kwa wasaidizi wao kwa mwezi mzima wa kampeni. Kama wasaidizi wanaweza kufanya kazi zote za mabosi zikaenda vizuri kwa muda wote huo, hao mabosi wanahitajika kufanya nini?

Mara nyingi huwa najiuliza kuna haja gani kwa rais kuwateua watu wenye majukumu ya juu kwenye chama kuwa mawaziri. Ni wakati gani hawa wanafanya kazi ya chama na muda upi wanarudi kuwa watumishi wa umma wote wa Watanzania. Bila shaka hapa panahitaji mabadiliko.

Mawaziri hao ni wanasiasa, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa ni watumishi wa wananchi wote bila kujali itikadi zao. Serikali ndiyo inawalipa mishahara yao kutokana na kodi za wananchi wake. Swali la kujiuliza ni je, kwa mwezi mzima waliokaa Busanda kupiga debe la chama wamelipwa mshahara kwa kazi gani?

Nitafurahi nikisikia kuwa CCM ndiyo ilikuwa inawalipa posho za kukaa Busanda mawaziri hao, lakini pia sitashangaa nikisikia kuwa serikali yetu ndiyo ilibeba mzigo huo kwa kazi za kukinadi chama. Itakuwa ni ajabu kama mawaziri hao walikwenda Busanda bila wasaidizi wao (waajiriwa wa serikali) wala madereva wanaolipwa mishahara na posho na serikali. Kama ndivyo, hapa haki iko wapi?

Hili la Busanda limetufumbua tu macho. Kama ambavyo mimi nashindwa kujua mpaka kati ya shughuli za chama na za serikali, mawaziri wengi pia hawafahamu. Ni jambo la kawaida sana kukuta waziri akitembelea jimbo lake la uchaguzi kwa magari ya serikali, akiendeshwa na dereva wa serikali, pamoja na msaidizi wake binafsi anayelipwa na waziri. Si hayo tu, inawezekana wote hao wanalipwa posho za serikali.

Ukiacha hili na kukaa Busanda na malipo yao, jingine ni kauli zao wakati wa kampeni. Kwa kipindi chote cha kampeni nimeshindwa kuona mipaka kati ya kiongozi wa chama na kiongozi wa serikali. Kauli za mawaziri hao zimeonekana zina uzito wa kulazimisha wapiga kura kukichagua chao.

Mfano kauli za Ngeleja kuhusu suala la kupeleka umeme Busanda na utoaji wa vibali vya wachimbaji wadogo wadogo wa madini; aliposema mgombea fulani (wa upinzani) hawezi kuwapelekea umeme wakazi wa Busanda, kwa kuwa vibali anavitoa yeye. Kauli hii ina maana nyingi, moja wapo ni kwamba, akichaguliwa mgombea mwingine, mbali na yule wa CCM, waziri atakwamisha juhudi zake za kuwapelekea umeme Busanda.

Kwa upande mwingine kauli hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa yeye (waziri) kwa nafasi yake ndiye aliyekwamisha kwa makusudi Busanda kupata umeme. Kwa maoni yangu haikuwa sahihi kwa kiongozi wa umma mwenye nafasi nyeti kama hiyo kutumia kauli za namna hii katika kampeni.

Pengine ndio maana wapinzani wa CCM wamebeza juhudi za watu waliojiita ni wafanyakazi wa Tanesco, waliosambaza nguzo kwenye jimbo hilo wakati wa kampeni.
Matamshi ya namna hiyo yaliwahi kutolewa mwaka 1996 na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati akimnadi mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, Cicso Mtiro dhidi ya Augustine Mrema.

Alikaririwa akisema wamchague mgombea wa CCM kwa kuwa ndiye atashirikiana naye kuleta maendeleo. Kauli hiyo ilikaririwa na vyombo karibu vyote vya habari, lakini siku iliyofuata rais ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM alitambua kosa lake akaikana kauli yake. Wananchi wa Temeke hawakumsikiliza, walichagua mtu wao Mrema.

Waziri Ngeleja hajaikana kauli yake, bila shaka aliikusudia. Katika kipindi hiki pia tumesikia Waziri Masha wa Mambo ya Ndani akiwaelekeza askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwamba ‘wafanye kazi yao’, mara baada ya helkopta ya Chadema kuwasili Busanda.

Hakufafanua kauli yake, lakini pia haijulikani aliitoa kama waziri au kama kada wa CCM.
Katika kampeni hizo yamefanyika mengi zaidi ya haya lakini nafasi hii haitoshi kuyaeleza yote. Cha msingi ni viongozi wetu wa umma kubadilika na kuweka mkazo kwenye shughuli za umma kwa manufaa ya wanancho wote.
 
* Diwani CCM akamatwa na polisi akituhumiwa

Waandishi Wetu, Busanda

VYAMA vinne vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Busanda wilaya ya Geita mkoani Mwanza, jana vilihitimisha kampeni kwa mbwembwe na shamra shamra za aina yake, huku viongozi wa Chadema wakijikuta wanaibiwa kompyuta ndogo yenye siri na mikakati ya ushindi.

Tukio hilo lilikikuta chama hicho usiku wa kuamkia jana wakati watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM waliwavamia viongozi wawili wa Chadema na kuwapulizia dawa isiyofahamika kisha kuwakamata na kuwapiga kabla ya kuwapora kompyuta ndogo (Lap top) iliyokuwa na nyaraka nyeti na kumbukumbu za mkakati wa ulinzi wa vituo vya kupigia kura.

Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kaimu wa Polisi mkoani Mwanza, Elias Kalinga, viongozi walioshambuliwa ni Bazir Lema ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya fedha na Himid Sabula ambaye ni mkurugenzi wa ulinzi na usalama.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 6: 45 usiku katika kata ya Kamena wilayani Geita wakati wakiwa chumbani kwao wamelala ambako waligongewa mlango na wavamizi hao wakiwataka kufungua, huku wakijitambulisha kuwa wao ni maofisa usalama.

Baada ya kugoma kufungua mlango huo walipuliziwa hewa mbaya ambayo bado haijatambuliwa, kisha wakavunjiwa mlango na kuwafunga kamba na kuanza kuwapiga na kuwapora nyaraka zao ikiwemo kompyuta.

Kamanda Kalinga alisema jeshi lake linawasaka waliohusika na tukio hilo. Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni ni kwamba, diwani wa CC Kata ya Kamena, ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Geita, Thobias Ikangala alikamatwa na polisi baada ya kutajwa na mtendaji wa kijiji hicho, akidaiwa kuhusika na tukio hilo.

Mkurungenzi wa uchaguzi wa Chadema, Singo Benson Kigaila alieleza kuwa tukio hilo limewasikitisha kwa vile CCM imekuwa ikiwatangaza Chadema kuwa na vurugu ilihali yenyewe ikifanya vurugu.

Viongozi wakuu wa Chadema, Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Dk Willibrod Slaa walimtembelea Lema katika hospitali alikolazwa na kumjulia hali.

Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM, Tambwe Hiza amekanusha chama chake kuhusika na shambulio hilo na kueleza kuwa walishambuliwa na wanakijiji kutokana na wao kuwalazimisha kuihujumu CCM katika kata hiyo.

Mbali na tukio hilo lililotia doa ufungaji wa kampeni, vyama vyote vya CCM, UDP, Chadema na CUF, vilihitimisha kampeni zake huku vikishuhudiwa na waangalizi kutoka nje ya nchi katika majukwaa tofauti.

Waangalizi hao kutoka ubalozi wa Marekani, Shirika la Millenium Challeenge Cooparation, Ubalozi wa Uholanzi, Jumuiya ya nchi za Ulaya (EU) na mwakilishi wa Ubalozi wa Uingereza, ambao mbali na kuangalia kampeni hizo jana, walizunguka maeneo kadhaa ya jimbo hilo kuona maandalizi ya uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali malalamiko ya CCM kupinga Chadema kutumia mawakala wanafunzi kusimamia kura zao katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kuwa malalamiko dhidi ya Chadema hayana msingi kwa vile hakuna sheria inayozuia kuwepo kwa mawakala ama kutoka nje ya jimbo au wanafunzi.

“Hili lalamiko siyo la msingi, hakuna sheria inayowakataza vyama kuweka mawakala wao kusimamia vituo kutoka nje ya Jimbo la Uchaguzi au kuwa wanafunzi, kila chama kinaweza kuleta mawakala kutoka popote ilimradi kinaona kinaweza kunufaika na hilo.

Jaji Makame amelaani vitendo vya ugawaji wa vyandarua, chumvi na nguo za ndani ambavyo vimeelezwea kutendeka katika kampeni na kuvielezea kuwa ni kosa sawa na makosa ya mengine ya rushwa.

Maadalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na kwamba vituo vitaanza kufunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni, hivyo kuwahimiza wananchi kufika mapema kupiga kura.

“Nawaomba wananchi wakishapiga kura watoke katika vituo warudi makwao, tunataka zoezi la uchaguzi huu liwe la amani na salama, hivyo nawaomba wadau wote wa uchaguzi wanaoshiriki uchaguzi huu kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi” alieleza.

Jumla ya wapiga kura 135,160 wamejiandikisha na wanatarajia kupiga kura katika vituo 380 katika kata 13 za jimbo hilo. 


Katika hatua nyingine, Hemed Kivuyo anaripoti kutoka Arusha kuwa, Mwasisi na Mshauri wa Chadema, Edwin Mtei, ameitaka CCM kuwawajibisha viongozi wake, Makamu mwenyekiti bara, Pius Msekwa na mtangulizi wake John Malecela pamoja na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba , kwa kuchochea vurugu na kutishia usalama na amani katika jimbo la Busanda.

Mtei aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kwa madai kuwa CCM imekiuka taratibu na sheria za uchaguzi, na kuwa Chadema itapinga matokeo hayo mahakamani endapo haitashindwa.

Alisema kuwa viongozi hao walihamasisha kikundi kiitwacho ‘Green Guard’ kutoka Dar es salaam kuwapiga wananchi hasa wafuasia wa vyama vya upinzani na kwamba kitendo cha kupeleka askari wengi wenye silaha za kivita jimboni humo ni mbinu chafu ya kuwaogopesha wananchi wa Busanda.
 
Watanzania tunapaswa kuhusisha ripoti ya fedha zilizotumiwa katika uchaguzi kama sehemu ya matokeo ya uchaguzi. Kwanini swala la gharama haligusiwi kabisa.
Je, washindi wa Busanda CCM wametumia kiasi gani cha pesa?
Je, waliofuatia - CHADEMA, wametumia kiasi gani?
Pia ninaomba viongozi wa CHADEMA watupe gharama za kukodi helikopta.
Majibu ya maswali haya yatasaidia katika uchambuzi wa chaguzi za kisiasa nchini. Hatupaswi kuishia tu kwenye idadi ya kura, tuingie ndani zaidi na kuangalia pesa zilizotumika na pia tudadisi zilipotoka.
Nawasilisha.
 
Inaonekana wewe ni mgeni sana katika siasa za Tz, Masuala ya gharama za uchaguzi yalifikia kilele chake katika uchaguzi mdogo wa Tarime. Kwa pamoja viongozi wa siasa waliona kuwa wamekufuru katika hilo na Spika mstaafu, na makamu mwenyekiti wa CCM alitoa tathimini yake kuhusu hilo.

Anyway CCM waliifanyia kazi taarifa hiyo, na kuibuka na usemi wa vita. "Ushindi wa vita uletwa na askari wa ardhini na sio wa angani". Zaidi wameweza kutetea jimbo hilo. Jaribu kupitia bandiko la Tarime kwa kujua uvumbuzi wa gharama za Chaguzi.
 
Kibunango,
mbona bado sijaona connection kati ya gharama za Tarime na Busanda! Haya ni majimbo mawili tofauti na kampeni zimefanyika nyakati mbili tofauti, hivyo ni vyema kila uchaguzi ukawa na ripoti yake.
 
Kamanda ZeMarcopolo,
Katika chaguzi zilizo tumia gharama kubwa ni uchaguzi mdogo wa Tarime. Uchaguzi huu ulishuhudia zaidi ya pande mbili zikiingia gharama kubwa katika kampeni zake.

Hali hii ilipelekea watu kujiuliza umuhimu wa vyama vya siasa kuingia gharama kubwa kwa kampeni hiyo. Bahati nzuri vyama vyote vilikiri kutumia nje ya bajeti zao ili kufanikisha kampeni huko. Hapa nilipo sitoweza kukupa jibu la mija kwa moja ni kiasi gani kilitumika huko.

Hata hivyo ukiangalia kampeni za Busanda, haziwezi kufikia gharama za uchaguzi wa Tarime. Kwa sasa ni mapema mno kuja na jibu la moja kwa moja ni kiasi gani kilitumika huko. Jibu sahahi bado litabaki kwa vyama husika. Ila kwa kutizama mtililiko wake unaweza kupata picha kuwa safari hii gharama hazikuwa kubwa sana.

Zaidi ni kusuburi iwapo vyama husika vitaweka wazi matumizi yao katika uchaguzi huu, na wakifanya hivyo jaribu kulinganisha na Tarime.
 
Hichi ni kitu muhumi sana kujua. Gharama za uchaguzi zinasumbua sana hata nchi zilizoendelea. Na nyingi wako katika kurekebisha sheria zao katika ku-balance gharama na ushindani katika uchaguzi. Sema sisi tupo nyuma sana kiasi hata waelewa wako wachache sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…