Well, hatupingi hatua za kupelekwa askari wa usalama kwenye sehemu ambayo kuna "possibility" ya fujo kutokea. Hatutaki baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa zitokee fujo na watu waathirike, then tulaumu kwanini serikali haikupeleka wanausalama wa kutosha. Nafikiri hoja hapa ni extent ya hao wanausalama. Lakini umuhimu wao tunautambua. Ndio, wote tunakiri kwamba kuna siasa ndani yake, lakini lazima wanausalama wawepo eneo lolote la uchaguzi hasa kunapokuwa na "possibility" ya fujo kutokea. Kampeni zimetawaliwa na fujo za hapa na pale. So, unaweza kuimagine matokeo yakilalia upande mmoja, basi upande wa pili unaweza kureact. They did that at Tarime by-elections, and still the opposition party won. So, tusiogope sana.
Hoja hapa iwe, je idadi ya askari waliopelekwa inaendana na mahitaji? Je, imepelekwa nguvu ya ziada? Na kama mmoja wetu alivyoainisha hapo juu, je, serikali haioni kwamba nguvu hii ingeweza kupelekwa sehemu nyingine kukabili vibaka na majambazi? Au kule Tarime kukabili vita za koo?