SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Uchaguzi wa ndani CHADEMA
Wabunge na Mameya CHADEMA wamuunga mkono Mbunge wa jimbo la Ndanda Mhe Cecil David Mwambe kuchukua fomu ya uenyekiti wa CHADEMA taifa kumrithi Mbowe.
Kwa taarifa kutoka moja ya wabunge wanaomuunga mkono anasema wamemchangia shilingi milioni 25.
Anasema katika kikao hicho kilichoongozwa na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mhe Anthony Momu ni meya mmoja tu aliyekataa kuchangia ambaye ni Mhe Boniface Jacob Meya wa Manispaa ya Ubungo ambaye alilazimika kutoka kikaoni na kuondoka.
Mhe Mwambe anaungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge, wenyeviti wa Halmashauri na Mameya pamoja na viongozi wa kanda 5 walioamua kusimama naye.

Mbowe15Imetosha
MBOWE HIZI PESA ZOTE ZINAKWENDA WAPI?
Chadema inapokea ruzuku ya takribani milioni 337 kila mwezi kutoka serikalini. Michango na makato kutoka kwa wabunge wa viti maalum kila mmoja anachangia milioni 1 kila mwezi Wabunge wakuchaguliwa kila mmoja anachangia laki 5 kila mwezi
Mameya wanaotokana na chadema wanachangia kila mmoja laki 5 kila mwezi. Mameya watokanao na chadema ni 7 hivyo kwa jumla yao kila mwezi wanachangia shilingi milioni 3.5. Wenyeviti wa halmashairi watokanao na chadema ni wanne na wanachangia laki 3 kila mwezi hivyo jumla kila mwezi ni shilingi milioni 1.2
Madiwani wa viti maalum wanachangia asilimia 15 ya posho zao kila wanapopokea. Madiwani wakuchaguliwa wanachangia 6% ya posho zao kila wanapopokea
AJABU SASA
Mpaka leo chadema inakodi Majengo kwa ajili ya matumizi ya ofisi kwa kulipa mamilioni. Ifahamike Sabodo amewahi kuchangia milioni 200 ili wanunue eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi badala yake haifahamiki pesa hizo zilikwenda wapi?
Chadema ina magari 5 tu aina ya pick up hilux ambazo kila baraza kuu na mkutano mkuu ukifanyika hupelekwa gereji kupigwa rangi na kufanyiwa ukarabati huku zikipewa namba kama vile 56 au 73 au 15 au 90 kuashiria zipo zaidi ya hizo ila ukweli hakuna zipo hizo hizo. Fedha za kununua gari hizi ilitolewa na chama rafiki cha conservative na CDU walitakiwa kununua gari 150 kwa matumizi ya kanda, mikoa, wilaya na makao makuu lakini hazikununuliwa. Subiri maigizo mkutano mkuu zitaletwa gari hadi za kukodi na kuandikwa M4C gari namba 45 nk
Tumuulize Mowe kweli kwa fedha hizi zote watendaji wa Chama kwenye mikoa na kanda wameshindwa kulipwa? Ofisi za kanda na mikoa za Chama zimeshindwa kulipiwa na chama?
Chama Cha siasa kuwa taasisi imara inahitaji pia rasilimali hususani vitendea kazi ikiwemo ofisi, magari, pikipiki, nguvu kazi yenye ubora nk chadema inakwama wapi?
Miaka 15 ya Mbowe inatosha. Chama hiki kina wanachama wengi ni aibu na ajabu kuona mwanachama mmoja kutaka kuongoza vipindi vinne wakati tunahubiri demokrasia na kupinga wasioheshimu ukomo wa uongozi.
Alipotaka Chacha Zakayo Wangwe ulichukia na mauti ukamtafutia....
Alipojaribu Zitto mara ya kwanza mwaka 2007 ukamtumia wazee atulie utapisha mbeleni.. Akatulia
Aliporejea tena Zitto mwaka 2014 kwa kuonesha nia akaundiwa zengwe kuwa ni msaliti na nyadhifa zote mkamvua hadi akawakimbia na kuanzisha chama chake cha ACT WAZALENDO...
*BASI SISI WAPENDA MAGEUZI TUNASEMA MBOWE MIAKA 15 IMETOSHA, PISHA FIKRA MPYA, BAKI KUWA MSHAURI. UKIONDOKA SASA WAKATI CHAMA KIMEPATA MAFANIKIO NI HESHIMA KWAKO.*