Uchaguzi: Hii ndio Dira ya Mh. Samuel J. Sitta Kama mwenyekiti Bunge la Katiba

Uchaguzi: Hii ndio Dira ya Mh. Samuel J. Sitta Kama mwenyekiti Bunge la Katiba

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
935197_692096290854356_659691062_n.jpg


Leo saa 10,Bunge la katiba litamchagua mwenyekiti wa kudumu wa bunge la KATIBA,Wadau mnaombwa kuzingatia uzoefu,uadilifu,ujasiri na DIRA ya mgombea husika.
 
hii DIRA nimeikubali na kama ningekuwa ni mjumbe wa bunge la katiba basi kura yangu ingekwenda kwa Mh Samuel J.Sitta
 
Mzee sinashida naye nitamchagua mzee wa viwango samweli sitta.

mkuu,kama upo ktk bunge la katiba basi usiache kura yako ikapotea bure,endelea kusimamia hapo na mpe kura Mh Samuel J.Sitta kwa maendeleo ya Taifa letu
 
Mbona naona kama ametumia rangi za CCJ? Hilo litamsumbua mbele ya safari.
 
Mh.mwenyekiti wa bunge la katiba,mh.samweli john sitta.nianze kwa kukupongeza kwa kuchaguliwa katika nafasi hii muhimu na ya kihistoria katika nchi yetu,,,,,,, wamekuchagua kwa sababu wanayoimani kubwa na uwezo wako,ni matumaini ya wajumbe wa bunge hili,na watanzania walio wengi kwamba jukumu hili,kazi hii ya unahodha uliyokabidhiwa na kuaminiwa,utaifanya kwa weledi mkubwa,na chombo hiki utakivusha salama-can't wait the speech !!!!!!
 
935197_692096290854356_659691062_n.jpg


Leo saa 10,Bunge la katiba litamchagua mwenyekiti wa kudumu wa bunge la KATIBA,Wadau mnaombwa kuzingatia uzoefu,uadilifu,ujasiri na DIRA ya mgombea husika.

Akishinda, anatakiwa aache legacy, mimi nimsifu mwenyekiti wa muda mzee Kificho kwa alipotufikisha, japo kama binadam alikuwa na mapungufu yake.
 
Hongera sana una sifa zote. Kura yangu unayo kwa interest pana ya Nchi yangu.
 
namuomba Sita asimamie Serikali moja,mimi nawashangaa wanaosema serikali moja ni kuvunja muungano kwani hawataki tuwe wamoja?
 
Kwa bunge hili hata angekuwa nani mbele ya safari atalaumiwa sana" pengine hata mzee Sitta asipokuwa makini atakuja jiharibia sifa zake"
 
katika kinyang'anyiro cha kuongoza BUNGE LA KIHISTORIA LA KATIBA nadhani MH.SIX anatoshaaa kabisa na nadhani hadi sasa hana mpinzani hao wengine walikuwa wanatimiza haki zao tu za kidemokrasia huku nao wakijua wazi hawawezi kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwani tayari MH SAMUEL JOHN SITTA anaaminika sana na wananchi wote pamoja na viongozi wote wa vyama vyote vya siasa kama MZEE WA VIWANGO NA UBORA kama alivoonesha katika bunge kabla ya ANNE MAKINDA

KILA LA KHERI SAMUEL SITTA
WATANZANIA TUNA MATARAJIO MAKUBWA SANA NA WEWE
 
Watamchagua kwa kura ya siri au ya wazi.?
 
kuna habari zimezaga mtaani kuwa Mh sitta ameugua ghafla na sasa yupo hospital je ni kweli

mungu amuepushe na hizi dua mbaya kwake,bado hatujapata hizo taarifa,labda tuendelee kuulizia huko Idodomea.lakini upo uwezekano zikawa ni habari za kupikwa
 
Back
Top Bottom