Ndugu zangu, binafsi nimetafakari kwa kina kile kilichofanyika kwenye kile kilichoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Yaliyofanyika ni zaidi hata ya kinachosemwa. Ni hatari kweli kweli.
Uchaguzi huu umeonesha ni kwa jinsi gani waliopo madarakani wanavyowadharau wananchi wao.
Ebu fikirini kidogo hapa:-
1. Mwananchi aache shughuli zake asafiri kwenda kituo cha kupigia kura tena kwa gharama zake.
2. Mwananchi huyo apange foleni kwa muda mrefu ili kupiga kura.
3. Mwananchi huyo huyo apige kura yake akimchagua anayemtaka kisha aanze kurudi nyumbani tena kwa gharama zake.
Mwisho wa siku wanatupilia mbali machaguo ya wananchi na kuweka machaguo yao tena kikundi cha watu wachache tu kinachoamua kufanya hivyo. Huku ni kuwadharau Watanzania kwa kiwango cha juu sana.
Kutokana na hali ilivyo:-
1. Kila Mtanzania mwenye nia njema na Nchi hii atoe Elimu angalau kwa Watanzania 10 hivi kuhusu uchafu huu.
2. Mimi binafsi na Watanzania wenzangu, tusikubali tena kuingia kwenye uchaguzi mwingine wowote tukiwa katika hali hii hii.
3. Tuunge mkono kwa nguvu na hasira kubwa hatua zozote zile zinazolenga kubadili ujinga huu. Tuache kulia lia tu, bali tuchukue hatua madhubuti kupinga vitendo hivi lakini kuzingatia kwanza amani ya Nchi. Ili kufikia malengo mahsudi, naomba nijielekeze kwa wafuatao:-
1. VYOMBO VYETU VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA.
Niombe vyombo hivi uzalendo wao uonekane katika kuwapigania Watanzania na si tu kutekeleza matakwa ya waliopo madarakani. Watanzania wanaviheshimu sana vyombo hivi. Wakati mwingine wakumbusheni watawala kwamba hili linalopangwa kufanyika si sahihi. Tena semeni hivyo bila ugomvi(politely). Mimi naamini majeshi yetu ni CHUMVI ya Nchi. Je, CHUMVI ikiharibika au ikiharibiwa kitu gani tena kitaifanya irudi hali yake ya awali?
2. TAASISI ZA DINI NK.
Kwa upande wa Taasisi za Dini, kuna uwanja mpana sana wa kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali. Naomba TEC, BAKWATA, CCT na WENGINEO turudi kwenye mstari ili kuiokoa Nchi hii. Tuweke maazimio kwamba kila siku ya ibada ni lazima anayeongoza ibada achopeke Elimu ya Uraia na kukemea vikali Mambo haya ya ovyo. Kama tulijisahau, basi tuamke kuanzia leo.
3. VYOMBO VYA HABARI.
Vyombo vyote vya habari Nchini veweke mkakati maalumu wa kutoa Elimu ya Uraia kwa Watanzania wote ikiwa ni pamoja na kukemea haya yasiyofaa.
Mimi naamini, kama vyombo hivi vingetumia vizuri platform zao, yaliyotokea yasingetokea na yasingekuja kutokea hata kidogo. Lakini bado hatujachelewa.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Amina.