AGIZO LA MUNGU KWA BINADAMU 'KUSHUKURU KWA KILA JAMBO':
KAMA SI MAREHEMU WETU WA AJALI YA PEMBA KUMGOMEA RAIS KIKWETE KWA SAFARI ZAIDI UGHAIBUNI, MAMILIONI HAYA YA GHARAMA WALIPAKODI TUNGEJIOKOLEA WAPI?????
Vipi sasa jamani inamaana baada ya Mhe Kikwete kulazimishwa na huu msiba wa kitaifa kule Pemba, vipi sasa walau balozi wetu huko nchini Marekani ataweza kupata fursa yake stahiki kuwakilisha serikali yetu kwenye hiyo minuso miwili ya PEACE CORPS na kule kwenye mkutano wa DICCOTA na kutuokolea walipa kodi gharama kubwa ya hela za usafiri, chakula, malazi, na posho kwa ujumbe wa zaidi ya watu 50 sio????????????
Ama kweli kila baya na afadhali yake; pengine ndio maana Mungu Muumba wetu ametuficha ujumbe mzito sana nyuma maneno 'SHUKURUNI KWA KILA JAMBO' eeeehhhh??????????
Hakika siku zote sie viumbe dhaifu hukumbuka tu na kukubali KUSHUKURU katika jema lakini baya linapotokea watu hatukawii kuanza ubishi ndani ya kughairi kwetu kwenye ukimya wa KUTOKUTEKELEZA agizo hilo la Mola wetu.
Ni vema waumini wa dini zote tukajifunza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, zuri au baya, kama maandiko yanavyotuagiza. Kwa mara nyingine, Marehemu zetu AJALI YA PEMBA pumzikeni kwa amani!!!!!!!!!